Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na ukiukwaji wa sheria za barabarani kwa kasi sana. Hivi pikipiki kubeba watu watatu mpaka wanne ni ruksa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, magari ya Serikali hasa STL/STK bado speed zao siyo nzuri na uendeshaji wa hovyo hasa ku-overtake na kupita upande usiostahili unaendelea. Dodoma inaongoza kwa fujo za bodaboda. Pia magari mabovu yenye kelele na moshi yanaendelea kupita barabarani bila woga wowote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu vibaka na wabakaji wameendelea kuumiza watoto na wanawake. Kila mwezi taarifa za ubakaji zinatolewa na vyombo vyetu. Serikali iongeze nguvu ya ulinzi kwa watoto.