Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Maryam Azan Mwinyi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Chake Chake

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kuchangia hutoba ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ya makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka 2024/2025.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, kwa kuendelea kuliongoza vyema Taifa letu ikiwa na utulivu na salama pamoja na kusimamia amani mshikamano. Pia ninapenda kumpogeza Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, minapenda kumpogeza Waziri na Naibu Waziri pamoja na watendaji wote wa Wizara hii kwa kazi nzuri ambazo wanazifanya katika Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ukaguzi wa malori makubwa barabarani, polisi ni lazima kuweka vituo maalumu kwa ajili ya ukaguzi wa malori hayo kwa sababu hivi sasa imekuwa kero kubwa kwa madereva ambao wanaenda safari ndefu hapa nchini na nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaishauri Serikali iweke nembo (sticker) maalumu ambayo itaonesha kwamba tayari gari hiyo imeshakaguliwa ili kuondoa usumbufu huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Vituo vya Polisi ambavyo vinajengwa hivi sasa, tunaomba Wizara kuimarisha zaidi ili kujenga vituo vya kisasa vya polisi kwa ajili ya sasa na baadae.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu vyombo vya usafiri hasa kwa Idara ya Usalama Barabarani, tunaomba Wizara kwa kitengo hiki iwapitie vyombo vya usafiri, kina ukosefu wa vitendea, kwa sababu idara hii ndio inayotoa huduma barabarani pale zinapotokea ajali inachukua muda mrefu, askari huchelewa kufika kwenye matukio hayo. Hata wale DTO hawana kabisa vyombo vya usafiri. Tunaomba Wizara katika mpango wake wa kuleta magari hayo iwakumbuke Idara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu wastaafu wa polisi, tunaomba maslahi yao ya kustaafu wasicheleweshewe mafao hayo wakati wa kustaafu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na ninaunga mkono hoja.