Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Eng. Ezra John Chiwelesa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Biharamulo Magharibi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. ENG. EZRA J. CHILEWESA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua nafasi hii kukushukuru kwa kunipa nafasi na mimi niwe mmoja wa wachangiaji katika hotuba ya Wizara ya Maji. Kipekee, namshukuru sana na kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa anayoifanya, hasa kwa visima hivi ambavyo vimeletwa kwenye majimbo yetu. Pia pongezi kwa msaidizi wake wa karibu anayemuwakilisha katika sekta ya maji, Mheshimiwa Jumaa Aweso, na wasaidizi wako wote katika Wizara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati mbaya sana mimi misemo ya pwani siijui, ningeweza kuchomekea kama ya kwako ile, lakini siijui. Kwa hiyo, mimi ninaenda hivyo hivyo na unielewe hivyo hivyo, lakini nasema tu wewe ni mtu rahimu sana. Ulikuja Biharamulo, mambo uliyoyakuta na ukaahidi, yote yameshatekelezwa mkuu. Kwa hiyo, mimi nakushukuru sana, tumepata gari, pesa na vitu vingine vyote tulivyokuwa tunavihitaji. Miradi hii miwili ya Usambazaji wa Maji Biharamulo Mjini na Nyarukongogo inaendelea, mmoja una 20% na mwingine una asilimia 65. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimepitia bajeti yako Mheshimiwa Waziri, iko vizuri, miradi yangu mingi inayoendelea na hii mipya ambayo imewekwa, ninakushukuru sana, naamini utekelezaji wake unaenda kufanyika. Ninaomba item 58 kwenye Mamlaka ya Maji Mijini, najua ndipo, nimeambiwa fungu hili ni kwa ajili ya mradi wa Ziwa Victoria. Mheshimiwa Rais alikuja Biharamulo na ahadi ikatolewa kwa hiyo, ninaomba utakaposimama Mheshimiwa Waziri, utakapokuwa unahitimisha, Wananchi wa Biharamulo wanakusikiliza na ninajua umekuwa ukinipa majibu, ningependa wananchi wa Biharamulo wajue kwa sababu, ni ahadi ya Rais, ni nini kinaendelea juu ya ule Mradi wa Maji wa Ziwa Viktoria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuyasema haya, mimi nina wazo tu. Ajenda ya maji ni ajenda ya Mheshimiwa Rais, maana ajenda zote ni zake, lakini ya maji ni yake zaidi. Ni yake zaidi kwa sababu, ni ajenda aliyoanza nayo tangu mwanzo na siku analihuitubia Bunge humu, Waziri aliyepewa maelekezo specific ni Mheshimiwa Aweso. Sasa bajeti ya maji inaporudi nyuma kwa kiasi kile, tunaifanya ajenda ya Rais au tunamrudisha wapi? (Makofi)

Mheshomiwa Mwenyekiti, kwa sababu Mheshimiwa Aweso nimemtaja kwamba, ni mtu rahimu. Mheshimiwa Aweso huyu ukimpigia simu muda wowote ukamuambia jimboni, kesho ataonekana, kesho kutwa ataonekana, ndiyo maana maisha yake yeye na Wabunge ndani ya Bunge hili huwezi kusikia amegombana na Mbunge yeyote. Ni kwa sababu, ni mtu anajinyenyekeza kupita kiasi na anawasikiliza Wabunge wote, lakini usikilizaji wake kama hapewi pesa hauna maana, unamuangusha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaomba kama inawezekana, tuone jinsi ya kufanya pesa hizi, Kamati ya Bajeti wako hapa, kwa maelekezo ya Kiti chako, waende wakaangalie jinsi ya kumuongezea pesa huyu bwana afanye kazi hii. Maji ni ajenda ya Rais, sasa msipompa pesa inaonekana kaiangusha wakati yeye na maisha yake na Wabunge humu ndani kila kitu anaenda nao vizuri. Tuombe Kiti chako kione jinsi ya kufanya, hatuwezi kuona bajeti ya maji mwaka jana imeenda juu, sasa hivi tunarudi nyuma, hicho kitu hakikubaliki. Naomba niweke hivyo, Kiti kiangalie tujue jinsi ya kwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nilikuwa na ushauri pia kwa Mheshimiwa Waziri. Wabunge wengi hapa tunatoka vijijini ndiyo maana mliunda RUWASA, ili wananchi wa vijijini waweze kupelekewa maji. Walau mjini unaona asilimia iko juu, lakini sisi huku tunaozunguka vijijini akina mama bado wanabeba ndoo na kuhangaika. Mijini kuna baadhi ya watu wana uwezo wa kuwa na visima, wana maboza na nini wanasaidiana, lakini vijijini facilities kama hizo hazipo na baadhi ya maeneo bado. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mimi ninaomba, ili uweze kuwa na mpango mzuri ni lazima ujipange pia katika utekelezaji na jinsi ambavyo watu wana-project cash flow yao. Ninaomba, pesa ya mfuko wa maji kama tunaweza tukaigawanya tukafanya kama wanavyofanya upande wa TANROADS; inajulikana kabisa kwamba, hapa ni vijijini TARURA, hapa ni TANROADS. Inakuwa inajulikana kwenye ile road fund. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, inakuwa ni rahisi zaidi hata mtu anapokuwa anapanga, anakuwa anajua kabisa mwezi huu, kuna bilioni hizi, mwezi huu kuna bilioni hizi. Hata unapo-project na hawa wakandarasi wa kusaidia kufanya miradi, it’s very easy, hata wewe ukawa unajua unawajibu nini. Sometimes tunakuwa tunakuonea huruma Mheshimiwa Waziri, atakuja mtu wa Maji Mjini, hujui unamjibu nini, atakuja mtu wa RUWASA, hujui unamjibu nini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tuone kama mtafanya projection, let say 60 percent, ikaenda RUWASA, labda 25 percent, ikaenda Mamlaka ya Maji Mijini, labda nyingine ndiyo iende kwenye mabonde; itakusaidia hata wewe unakuwa unajua kabisa kila mwezi nina 20 billion au nina 30 billion inaenda sehemu fulani. Kwa hiyo, hata wewe projection yako inaweza ikakaa vizuri ukaweza kuwasaidia wakandarasi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri lazima ukubali wakandarasi wamekubeba. Wakandarasi wa Kitanzania ni lazima tuwapongeze kwenye hili, maana hakuna Mkandarasi wa Kitanzania anayedai riba mpaka sasa, lakini pesa zao zaidi ya shilingi bilioni 200 unaelewa ziko zinadaiwa, lakini kwa sababu wewe ni mtu rahimu ukiwaambia wanakusikiliza, wanaenda kukopa wanaendelea kufanya hii miradi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tuiombe Wizara ya Fedha ikusaidie pia, usije ukapoteza ule uaminifu ambao umekuwanao, watu wanakusikiliza wanafanya, hatimaye sasa kesho wakaondoka site mambo yakaharibika. Kura za CCM na heshima ya Mheshimiwa Rais iko kwenye maji kwa sababu, ni ajenda yake. Sasa tuombe mjipange vizuri huko muweze kutusaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, liko suala la mita za pre-paid, hili suala nimelisema juzi, naomba kulirudia tena hapa, am talking of this as a professional, suala la mita za maji za kulipia kabla, mimi naliunga mkono 100 percent, sikatai, lakini ushauri wangu niliosema juzi, twende kwanza kwenye Mamlaka zenu za Serikali, Mamlaka za Serikali ndiyo zimekuwa hazilipi. Hayo madeni makubwa mnayoyasema yawekeni huko kwanza, kwa sababu experience yangu katika nchi nyingi ambazo nimefuatilia na kampuni nyingi kubwa ya mita duniani, hakuna kampuni inayozalisha hizo mita. Mita zimetokea China ingawa zimekuwa hazitumiki, tuone jinsi ya ku-rectify…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: …ili ziweze kutusaidia baadaye tusiingie mgogoro na wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nashukuru kwa ajili ya hilo, naunga mkono hoja, ahsante. (Makofi)