Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hoja ya dharura kuhusu kuongezwa kwa umri wa waombaji wa ajira za Serikali

Hon. Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hoja ya dharura kuhusu kuongezwa kwa umri wa waombaji wa ajira za Serikali

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Mimi nitaunga mkono hoja ya Mheshimiwa Kamani kwa ufupi sana, kwamba tumesikiliza hoja ya Mheshimiwa Mbunge na pia hoja na maelezo ya Mheshimiwa Waziri. Kama wanaweka vigezo vya umri, wanashindwa ku-consider vijana umri ambao wanamaliza Form Six na kwenda kwenye vyuo mbalimbali na kupata qualification kwa vigezo kwamba anaweza akashindwa kuruka vihunzi, kwanza siyo sahihi na siyo kweli kwamba ukiwa na miaka 30, 40 huwezi kuruka vihunzi.

Mheshimiwa Spika, kuna watu wana miaka 25 hawawezi kuruka. Mazoezi wanayoshindwa watu ambao wana umri mkubwa, tunatofautiana background. Wapo watu wengine ni watu wa mazoezi. Kwa hiyo, wao wangetoa free, watu wa-apply, kama ni kwenda kwenye mazoezi mtu ashindwe field. Akishindwa field atarudishwa site na hawezi ku-complain, lakini kwa sasa ilivyokaa ni kwamba unaweka limit, mtu anaweza kuomba ile kazi na hana ajira nyingine, yuko mtaani lakini umeweka umri, lakini anaweza aka-qualify.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba hii habari ya umri tuiangalie, iondolewe. Kama kuna mtu ataenda site kule akashindwa field, hawezi kulalamika, lakini kwa sasa itaonekana kazi imetengenezwa kwa kundi fulani na kwa umri fulani na wengine hawatakiwi kupata ajira, na kwa kweli wataendelea kulaumu mtaani bila kupata ajira.

Mheshimiwa Spika, ahsante, naunga mkono hoja ya Mheshimiwa Kamani. (Makofi)