Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa fursa hii. Tunasikia kauli za Waheshimiwa Wabunge kwenye eneo hili, lakini ninachotaka kusema tu ni kwamba vigezo hivi vimewekwa baada ya kazi kubwa sana kufanywa na vyombo vyetu vya ulinzi. Lilikuwa ni zoezi shirikishi ambalo lilihusika katika kuandaa mitaala yetu ya kuwaandaa askari wetu wa Jeshi hili la Uhifadhi.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, matokeo ya ushirikishwaji ule wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ndiyo yalituletea vigezo hivi. Nimesikia mfano umetolewa kwa dereva, ndani ya majeshi yetu ya uhifadhi dereva kiuhalisia siyo dereva wa kawaida. Madereva wetu kwenye eneo la uhifadhi wanafanya kazi katika mazingira ya kiupekee sana. Unaweza kumkuta dereva wetu huko kwenye mapori akalazimika kuendesha gari kwenye sehemu hata haina barabara. Kwa hiyo, yale mafunzo ya utimamu anayopata ndiyo yanayotupeleka huko kwenye vigezo vya umri. Vilevile katika kukabiliana labda na majangili huko, inatupeleka kwenye vigezo hivyo.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, wataalamu wetu kwenye vyombo vya ulinzi waliona umuhimu wa kuwa na kada ya askari ambao watakuwa na muda mrefu wa kuendelea kupata mafunzo wakiwa ndani ya jeshi, umri ambao utawawezesha wao kuweza kushiriki mafunzo hayo.
Mheshimiwa Spika, sasa tumeyasikia mawazo ya Waheshimiwa Wabunge na sisi tunayachukua, tutarudi kwenye vyombo vyetu vya usalama tuyajadili tuone jinsi ambavyo tunaweza kuya-accommodate. Vilevile, tutakaa na wenzetu wenye instrument hii inayohusiana na mambo ya ajira, na Mheshimiwa Waziri ameeleza vizuri sana wakati anatoa maelezo haya, lakini kwa sababu ni ushauri, tunaupokea tunaenda kuufanyia kazi na Mheshimiwa Waziri atahitimisha. (Makofi)
SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Chuo cha Mweka kiko chini yenu au kiko chini ya Wizara gani?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, kiko chini yetu.
SPIKA: Chini yenu?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ndiyo.
SPIKA: Wastani wa mtu anayehitimu hapo Mweka, asome kitu chochote tu, wastani wa umri wa anayehitimu Mweka ni umri gani?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ni kati ya miaka 21 au 22.
SPIKA: Haya, watu ambao wanaenda kusoma hapo Mweka ni wale waliomaliza form four au wanafika form six? Yaani Mweka huwa mnachukua watu wa form six au mnachukua tu wa form four?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, wapo wa form six na wapo pia wa form four.