Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kibakwe
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa nafasi. Natambua na kuheshimu sana michango ya Waheshimiwa Wabunge, lakini nataka tu niweke vizuri kwamba imeonekana kama vile tumeweka sharti ambalo linawaondoa vijana. Hatujawaondoa vijana kwa sababu hata hao wanaopewa hii fursa ni vijana. Maana tumesema limit isizidi miaka 25, siyo maana yake kwamba hii limit ambao hawajazidi 25 ni wazee, hapana.
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kamani ana hoja yake ya miaka mingi, hataki ile experience ya miaka mingi kwa sababu ilikuwa inawa-exclude vijana kwenye haki ya kupata ajira. Sasa hiki ni kitu tofauti. Hii ni kwamba hawa wanaopewa hizi ajira ni below 25. Kwa hiyo, hawa ni vijana, ni kundi la vijana hao hao, tena hapa sana sana hii hoja inawatetea wazee kwa sababu ukisema above 30 kwenda juu ni wazee.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hawa ambao Serikali tunasema position yake ni vijana, tena hawa tunawachukua vijana kwa sababu vyombo hivi vina asili yake. Ninukuu maneno ya General Mwamunyange aliwahi kusema kwamba, “Ni ngumu sana raia kujua nini kinatokea kwenye jeshi.” (Makofi)
SPIKA: Sasa Mheshimiwa unajua mwanzo nilikuuliza tofauti. Hebu tuondoe kwenye hiyo dhana, kwa sababu ukitaka kuifanya TAWA, kwamba na yenyewe ni Jeshi la Wananchi, duh! Sasa jamani hawa watu mbona itakuwa shughuli hapa nchini sasa, kwa sababu kila mtu ni mwanajeshi.
Yaani hili neno ‘jeshi’ nalo itabidi tuje tulitazame vizuri kisheria maana kuna mambo tulifanya marekebisho hapa Bungeni wenyewe. Maana kila mtu kama ni wa jeshi la ulinzi labda kama TAWA na wenyewe wanaitwa jeshi la akiba, lakini kama ni la wanyamapori na wenyewe tukawapa hadhi kama ya Jeshi la Wananchi, mbona itakuwa kazi.
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, ninachotamani kieleweke ni kwamba, hawa wanaopewa hizi ajira ni vijana. Nataka tu hicho kieleweke. Siyo kwamba, ni wazee, ni vijana na ndiyo kusema limit ya umri isizidi miaka 25. Sharti hili limekuwepo katika Jeshi la Polisi, Magereza na Uhamiaji kumekuwa na sharti hili hili la umri. Kwa nini umri?
Mheshimiwa Spika, ni kwa sababu, vyombo hivi na majeshi haya wakati mwingine hata kustaafu hawatumii Sheria yetu ya Utumishi ya miaka 60. Kwa mfano Polisi...
SPIKA: Mheshimiwa Simbachawene, lugha ya mazungumzo yako mimi nakuelewa kabisa, lakini nakuomba sana tafadhali, watenganishe TAWA na haya majeshi unayoyataja. Mbona ni kama vile TAWA na wenyewe wako kwenye orodha ya vyombo vya ulinzi na usalama? Mbona naanza kupata wasiwasi kama ndiyo picha tuliyoijenga?
Yaani wewe hoja yako ya msingi mimi nimeielewa kabisa, kwamba hata hawa ni vijana, lakini ukisema tena kwenye majeshi yetu, na hawa nao wamo kwenye ile orodha? Yaani TAWA wanalingana na Jeshi la Zimamoto, Jeshi la Magereza na Jeshi la Wananchi? Wanalingana? Mimi sijui, nielimishe. (Makofi)
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, wanapolingana ni pale kwenye eneo la uhitaji wa ukakamavu kwa sababu ndiyo tunaingiza training ya jeshi hata kama hatusemi ni jeshi na ndiyo maana kwa Kiingereza labda inaeleweka, ni paramilitary. Kwa hiyo, ni ujeshi ndani ya mtu ambaye siyo mwanajeshi ili a-behave na afanye majukumu yanayofanana na ya kijeshi.
Mheshimiwa Spika, kwa mfano, hawa kwenye Kiingereza wanaitwa Conservation Ranger. Conservation Ranger ni kazi ya field kwa hiyo, aina ya unayemhitaji pia inaweza ikatakiwa. Hata kuna ajira nyingine ambazo zimeshatangazwa tukahitaji wenye umri mkubwa kwa sababu ya speciality au fani walizonazo. Kwa mfano, huwezi kumhitaji mtu ambaye ni mbobezi katika fani, hata hii ya uhifadhi ambaye atakuwa na umri mdogo wa miaka 25, hapana.
Mheshimiwa Spika, uzoefu wa wengi hapa, tunao watoto. Watoto wetu wanaomaliza degree, kama ameenda moja kwa moja kwa mfumo wa elimu ya Tanzania, akifika miaka 24 tayari ni graduate ana degree. Kwa hiyo, siyo kwamba, imewa-exclude sana kwamba, hapa ni jambo kubwa la kiasi hicho. Hata hivyo, mimi nimebeba tu kutetea hoja ya Serikali, lakini mambo haya yana michakato yake ambayo inatoka mbali sana. Kwa haraka haraka hapa tutasema sasa tunaridhia au vipi. Nipo tayari kusikiliza Bunge linasema nini na baadaye Serikali tutasema kwamba position hii ikoje au tufanye nini. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, isije ikaonekana kwamba, Simbachawene ni mbishi, anabisha tu, aah ah. Hii ni hoja ya Serikali, kwa hiyo, wazee wangu nawaheshimu sana Waheshimiwa Wabunge, lakini nataka niseme kabisa kwamba, hatukufika hapa hivi hivi, ni kwa sababu ya vigezo na Serikali ina utaratibu wake. Ahsante sana. (Makofi)