Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninamshukuru Mwenyezi Mungu na nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na timu yake yote kwa utendaji wao.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunamshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuletea fedha za ujenzi wa shule na sekta ya afya, lakini bado tuna changamoto za barabara jimbo la Kalenga. Tunaomba barabara kutoka Kata ya Wasa hadi Mauninga Kata ya Tungamalenga katika Jimbo la Isimani ifunguliwe, itasaidia sana uchumi wa Wanakalenga. Barabara kutoka Ihemi hadi Ihimbo Kata ya Magulilwa kupitia Mgama - Lipembelwasenga ikifunguliwa ingesaidia sana uchumi kwa Wana-Kalenga.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu TARURA fedha hazitoshi Mkoa wa Iringa, tunaomba ziongezwe, watendaji ni wachache, tunaiomba Serikali iweze kutenga fedha kwa ajili ya kuajiri ma-engineer.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia tuna maboma ya zahanati katika Jimbo la Mafinga, Rungemba na Kitelewasi wananchi wamejenga tunaomba yamaliziwe na Serikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika Kata ya Wasa Jimbo la Kalenga zahanati za Ikungwe na Ufyambe tunahitaji waganga na vifaa tiba.
Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wa jumla; wakurugenzi wawe wanapewa ajira za mikataba ili waweze kupimwa utendaji wao na waweze kuwa committed kwa majukumu yao na kuhusu watumishi hasa walimu na watumishi wa afya waongezwe.
Mheshimiwa Naibu Spika, watumishi wanalalamikia kikokotoo kiboreshwe, mboreshe kikokotoo mkishirikiana na Wizara ya Utumishi. Aidha, walimu wapandishwe madaraja kwa wakati na kulipwa stahiki zao na watu wenye ulemavu wazingatiwe sana kwenye ile asilimia 10 itakaporejeshwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, niwapongeze kwa utendaji kazi wenu nyote Mheshimiwa Waziri, Naibu Mawaziri na watendaji wa Wizara.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.