Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
2
Ministries
nil
MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia bajeti kuu ya Serikali Mwaka wa Fedha 2024/2025.
Mheshimiwa Naibu Spika, nitaanza kwa kujikumbusha na kutukumbusha wote kuhusiana na 4R’s za Mheshimiwa Rais, reconciliation, rebuilding, resilience na reforms. Kwa maana ya Mheshimiwa Rais wakati anaingia madarakani alitangaza muelekeo wa uongozi wake katika miaka yake atakayokaa madarakani na akazitambulisha 4R’s hizo akimaanisha mageuzi, ustamilifu na kujenga upya Taifa letu, kwa maana ya hizo 4R’s.
Mheshimiwa Naibu Spika, leo nitajikita katika reforms. Naipongeza sana Serikali na Wizara ya Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Fedha na Serikali kwa ujumla. Wamejitahidi sana kuonesha nia na dira ya Mheshimiwa Rais kuhusiana na reforms, upande wa reforms tu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna masuala kadhaa. Ukipitia Finance Bill unaweza kuona namna ambavyo mtazamo wa Mheshimiwa Rais umeonekana katika reforms. Nitataja maeneo ambayo kwa kweli, mimi kama Mbunge na sisi kama Waheshimiwa Wabunge, kuna mambo ambayo tumekuwa tunashauri ambayo sasa hivi kutokana na hii Finace Bill iliyoletwa mwaka huu tunaona namna ambavyo Serikali imejaribu ku-incorporate kuyaingiza katika Finace Bill.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli, pamoja na kwamba, nimesoma mapendelezo ya Kamati, nimesoma Hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Fedha na nimesoma Mpango wa Maendeleo wa Wizara ya Mipango na Uwekezaji, lakini nimeenda moja kwa moja kwenye Finace Bill kwa sababu, huku kwingine kote unaweza ukawa umezungumza mambo mengi, lakini kama hujaleta utekelezaji wake kwa kurekebisha na kutunga Sheria, unakuwa tu ulipiga stori. Kwa hiyo, nimeeda moja kwa moja kwenye bill na kuna baadhi ya vitu ambavyo vimewekwa na ninaomba nivitaje, kwa maana ni sehemu ya reform ambazo mimi naamini lengo lilikuwa ni hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tumejadili sana kuhusu sugar industry, ukipitia Finace Bill utaona marekebisho ya Sheria ya sekta ya sukari na wameleta vipengele viwili ambavyo nitavitaja mahususi. Tukipitisha Finance Bill hii hapa itakuwa dealers na manufacturers, wazalishaji na wasambazaji wa sukari, watalazimika kuwatangaza hadharani wasambazaji wa sukari na mawakala wao kila Mkoa. Kila Mkoa tutakuwa tunajua, kama ambavyo watu wa Cocacola wanatangaza kila Mkoa nani ni msambazaji wao pale kwenye Mkoa husika kwa hiyo, watu wa sukari pia, watakuwa wanalazimika kufanya hivyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia, wazalishaji na wasambazaji wa sukari nchini watakuwa wanalazimika kutangaza hadharani gharama ya uzalishaji. Vipengele hivi ni kwenye kutatua tatizo la monopoly katika sekta ya sukari, naona tukipitisha Finance Bill hii, kwenye kipendele hiki ni sehemu ya amendment ambazo ninaamini ni reforms ambazo Mheshimiwa Rais amekuwa akizizungumza. Hilo ni eneo moja wapo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna sehemu nyingine ambayo mimi, kama Mbunge ambaye nimekuwa nikizungumza masuala ya value chain kwenye sekta ya madini, Serikali imeleta amendment kwenye Sheria ya Madini na inatutaka kabla ya kutoa madini nje, asilimia 20 kila mtu ambaye anashiriki katika mnyororo wa thamani wa madini, asilimia 20 lazima ichakatwe ndani ya nchi, smelting, refining na trading ni lazima, imeletwa kwenye Sheria. Yani, hivi nikisema imeletwa kwenye Sheria, maana yake ni utekelezaji wake unaanza kuuona, tofauti na tukiongea bila kuona kwenye Finance Bill. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, napongeza kwenye hili. Ni sehemu mojawapo ya reform, lakini mimi pia, kama Mbunge ambaye nawakilisha kundi la vijana, nimeona Serikali imeweka kwamba, italeta venture capital fund (Mfuko wa mitaji). Lengo la mfuko wa mitaji ni kutoa mitaji kwa biashara ndogo ndogo, startup na SME’s.
Mheshimiwa Naibu Spika, hili naliomba kwa dhati kabisa litekelezwe. Yani Serikali watekeleze hili kwa sababu ni jambo zuri. Litasaidia vijana kuongeza ubunifu na kuweza kuanzisha biashara zao ndogo ndogo kwa sababu wanatoa mitaji kwa kupitia e-key na e-key ipo kwenye Finance Bill. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pia, nimekuwa nikizungumza kuhusiana na digital services tax na ukisoma Hotuba ya Wizara na Mpango unaona namna ambavyo Serikali inajaribu kupambana kutafuta vyanzo vipya vya mapato. Nimepitia sana na kuna namna unaona sehemu nyingine inaleta mushkeli, lakini unaona wanapambana kutafuta vyanzo vya mapato kwa sababu, wanajaribu kufuata ushauri wa Waheshimiwa Wabunge kuongeza wigo wa walipakodi.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimeona leo katika Sheria ya Finance Bill wameweka content creation capital gain tax. Kwa hiyo, hii inaonesha kwamba, wanasikiliza maoni ya Waheshimiwa Wabunge wakati mwingine, lakini nikipata nafasi mbele nitaendelea kushauri ni kitu gani zaidi cha kufanya.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia, wameleta kipengele ambacho kinahusu online data services. Lengo pia, ni kulinda taarifa binafsi za watu, lakini pia, wameweka tax kwa hiyo, Serikali itaendelea kupata kodi kwenye upande huo, lakini ningependa katika Sheria waweke tafsiri ya watoa maudhui mitandaoni (digital content creators) ni akina nani, ili tuone urahisi wakati tunaendelea kuchakata. Tuone kwamba, watu wanaelewa tunawazungumzia akinanani.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna sehemu moja ambayo hatujafanya vizuri, ni lazima tuseme. Kwanza, ninaunga mkono kuweka shilingi 382 kwenye compressed natural gas na ninaomba ieleweke kitu hiki kimoja, kwanza mtambue kwamba, lengo siyo kuumiza mtu yeyote, lengo ni kuongeza wigo wa walipakodi na kuongeza kodi.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi kilo moja ya gesi inauzwa shilingi 1,550 tukiongeza shilingi 382 inakuwa ni shilingi 1,932 tu kwa kilo moja ya gesi, ambayo ni gharama ndogo sana ukilinganisha na diesel na petrol. Mimi ni mwanamazingira, hiki kitu ni kitu ambacho naona ni sahihi kwa sababu, hizi fedha Waheshimiwa Wabunge mkumbuke zinaenda kwenye road fund. Sisi wote hapa, akikaa Mheshimiwa Waziri anayezungumza masuala ya barabara wote humu ndani tunainuka. Hii fedha inaenda road fund na inawezekana ikaonekana kwamba, kwa sababu bado hili suala la natural gas ni changa, tukaona kwamba, tumewahi sana ku-tax, lakini ni vizuri tukaanza kujipanga.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, mimi nimepitia Hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati na nimeona wale watu wamejinga na ninakwambia very soon tutaona impact ya hiki kitu. Waheshimiwa Wabunge, nawaomba tafadhari tupitishe hii kwa nia njema ila at the same time Wizara ya Fedha ninaomba muachane na tozo ya asilimia mbili kwa wakulima wa hii nchi. On the other side tuwapitishie hii shilingi 382, ili tuendelee ku-tax huku na tuendelee kujipanga kwenye natural gas na asilimia mbili ya wakulima, lakini tafadhali naomba muwaache wakulima.
Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi. Hao mnaowataja ndiyo watu wanaoenda kutupigia kura, maana yake ni vitu vingine mpaka tuambiane kwenye camera. Huyu mkulima mnaeenda kumtoza hii asilimia mbili, niwakumbushe, hiki kitu tulipitisha Mwaka 2021 tukakileta kwenye miscellaneous hapa.
NAIBU SPIKA: Ahsante.
MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba muachane na hii biashara, hamtoboi. Achaneni na biashara ya wakulima asilimia mbili...