Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2023 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.

Hon. Asya Sharif Omar

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2023 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.

MHE. ASYA SHARIF OMAR: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Mimi namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia uhai na afya njema, leo nimeweza kusimama katika Bunge letu hili Tukufu. Binafsi nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia bajeti hii ya Serikali ya Mwaka 2024/2025. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naanza kwa kumpongeza Rais wetu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan. Pia, nampongeza Rais wetu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ally Hassan Mwinyi, kwa namna wanavyoendelea kuwaletea maendeleo ya kiuchumi wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi naanza mchango wangu kwenye bajeti hii kwa kumuomba Waziri wa Fedha, kaka yangu Mheshimiwa Mwigulu na Naibu Waziri wa Fedha kwa kumuwezesha Waziri wetu wa Maji, Mheshimiwa Jumaa Aweso, ili kupata fedha, kwa ajili ya kuwalipa wazabuni kuweza kutekeleza miradi ya maji kwa wakati. Tunaishukuru sana Serikali ya Awamu ya Sita ambayo inaongozwa na Mheshimiwa Dkt. Mama Samia Suluhu Hassan. Sisi wanawake na wanawake wenzetu wa vipato vya chini na vya kati tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa ile adhma yake ya kumtua mama ndoo kichwani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hii ni dhahiri na ni ukweli na kila mtu anafahamu; Mheshimiwa Dkt. Mama Samia amedhamiria kumtua mama ndoo kichwani, ili aweze kufanya shughuli zake za kujiletea maendeleo. Ni imani yangu Wizara ya fedha italizingatia hilo la kuiwezesha Wizara hii ya maji, ili wakandarasi watimize wajibu wao ikiwemo kutekeleza miradi hii ya kupatikana maji safi na salama kwa wakati. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mchango wangu mwingine utajikita kwenye masuala ya udhalilishaji wa kijinsia. Kama tunavyofahamu, hivi karibuni tumeshuhudia au tumesikia mauaji ya watoto wetu wenye ulemavu (ualbino). Jambo hili limetusikitisha sana, hasa sisi akinamama. Kitendo hiki hakikubaliki na ni cha kukemewa kwa nguvu zote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sana, Serikali yetu Tukufu iweze kuwachukulia hatua za kisheria wale wote waliohusika na vitendo hivyo vya kinyama. Tunalaani vikali na tunasema tutakuwa mstari wa mbele kuendelea kupambana na majanga haya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, namalizia kwa kumshukuru Mheshimiwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusogeza vituo vya afya karibu na sisi. Vituo hivi vimetusaidia sana kupata huduma hii ya mama na mtoto na vimetusaidia kujifungua katika mazingira safi na salama. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hakuna asiyejua mambo anayoyafanya Mheshimiwa Dkt. Samia, ni makubwa katika nchi yetu. Tutaendelea kumuunga mkono na kumsemea mazuri ambayo anayafanya na ambao hawaoni na hawataki kazi kwao, lakini sisi hapa tunasema 2025 ni Mheshimiwa Dkt. Mama Samia na Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha hoja. Ahsante.