Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Ilemela
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Spika, naleta mchango wangu kuhusu sekta ya milki katika ukuaji wa uchumi Tanzania na nianze kwa kuunga mkono hoja.
Mheshimiwa Spika, napongeza wawasilishaji wote wawili, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba na Mheshimiwa Profesa Kitila Mkumbo kwa mawasilisho yao katika Bajeti Kuu ya Serikali na mpango wa Serikali uliowasilishwa.
Mheshimiwa Spika, sekta ya milki ni sekta muhimu katika uchumi, ni sekta mama kuchochea ukuaji wa uchumi katika sekta nyingine (multiplier effect) hasa ikisimamiwa vizuri na kuwekewa utaratibu nzuri unaolenga kuchochea ukuaji wake. Sekta inaweza kuchangia kwa kiwango kikubwa kupunguza umaskini na kuleta ukuaji wa uchumi endelevu mijini na vijinini. Mchango wa sekta ya milki upo katika maeneo mengi kwa kuwa inagusa kila eneo la kiuchumi.
Mheshimiwa Spika, utulivu wa kiuchumi (economic stability); soko la mali isiyohamishika linalofanya kazi vizuri na bei thabiti hutoa uhakikisho kwamba uchumi unafanya vizuri. Mali isiyohamishika hutumika kama dhamana ya ufadhili na ni nyenzo muhimu ya utulivu wa kiuchumi.
Mheshimiwa Spika, ukuaji wa sekta zingine za kiuchumi (other sector economic growth); sekta zote za kiuchumi ambazo ni uzalishaji wa viwandani (manufacturing), kilimo cha kibiashara (mechanized agriculture), usafirishaji (transportation), tourism (utalii), arts and sports (sanaa na michezo), makoso ya rejareja (retails) na kadhalika zinahitaji sekta ya milki inayofanya kazi vizuri ili kuweza kupata mahali na ardhi kwa ajili ya uzalishaji wake.
Mheshimiwa Spika, uwekezaji wa mitaji ya ndani na nje (attraction of domestic and foreign capital); soko la milki thabiti ni kivutio kikubwa cha mitaji hasa ya nje (foreign capital). Pia linaleta fursa ya uwekezaji wa mitaji kutoka soko la ndani na hivyo kuchochea uchumi zaidi. Hii pia inasaidia kukuza na kuongeza upatikanaji wa fedha za kigeni kwa kuwa wawekezaji wengi kutoka nje watatakiwa kuja na mitaji yao kutoka katika masoko ya fedha ya nje na siyo ya ndani.
Mheshimiwa Spika, kupatikana kwa teknolojia na ubobezi (technology and expertise); sekta ya milki thabiti na yenye kufanya kazi vizuri inavyovutia wawekezaji ndivyo wanavyoleta teknolojia katika ujenzi (construction), vifaa vya ujenzi vinavyotumika (building materials), ujuzi wa ujenzi (construction knowledge) na kusaidia ukuaji thabiti katika maeneo hayo.
Mheshimiwa Spika, ukuaji wa uchumi (wealth creation); usimamizi mzuri wa soko la nyumba na ardhi (real estate) kutakuwa kivutio kikubwa kwa wawekezaji, wajenzi na wamiliki wa nyumba na ardhi (investors, developers and property owners). Soko la nyumba na ardhi linakuwa na thamani inaongezeka kila wakati, faida ya mauzo inayopatikana inaweza kuwekezwa tena kuendeleza milki au kutumika kwenye maeneo mengine ya kiuchumi.
Mheshimiwa Spika, kuongeza ajira (job creation); uwekezaj kwenye majengo na ardhi kunatoa fursa nyingi za ajira katika ujenzi (construction), ubunifu wa michoro (architecture), uhandisi (engineering), usimamizi wa ujenzi (project management), uuzaji wa majengo na ardhi (real estate brokerage), usimamizi wa majengo na nyenzo (property management) na ukarabati (maintenance). Pamoja na ajira ambazo siyo za moja kwa moja nyingi zinazozalishwa kutokana na ukuaji mzuri, thabiti na tulivu wa soko la nyumba na ardhi.
Mheshimiwa Spika, haya ni maeneo machache kati ya mengi ambayo usimamizi mzuri wa sekta ya milki (nyumba na ardhi) inaweza kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa Taifa letu la Tanzania.
Mheshimiwa Spika, kuna usemi unaosema, “when spider webs unite, they can tie up a lion." Hii ina maanisha usimamizi mzuri wa sekta ya milki ni mtambuka ni jambo la pamoja (collective action) kwenye taasisi na idara zote zinazosimamia ardhi na nyumba. Kuanzia upangaji, upimaji, utoaji wa ardhi, ujenzi na usimamizi (utumiaji).
Mheshimiwa Spika, baada ya mchango huu, naomba kuwasilisha.