Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2023 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Dorothy George Kilave

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Temeke

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2023 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. DOROTHY G. KILAVE: Mheshimiwa Spika, namshukuru Mungu kwa wema wake kwa uhai huu, lakini pia napenda kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa sana na nzuri kwa kuiweka nchi yetu katika maendeleo ya kitaifa, yapo mambo makubwa ya kiafya, elimu, miundombinu, maji na kadhalika kwani kila sekta amegusa kwa uwezo mkubwa sana, hakika ameziweka zile 4Rs vizuri.

Mheshimiwa Spika, niwapongeze Mawaziri wote, Waziri wa Fedha na Waziri wa Mipango na Uwekezaji pamoja na Naibu Mawaziri wao pamoja na jopo zima la wasaidizi wao kwa bajeti hii nzuri na hasa pale nilipoona wanavyopambana kuongeza mapato ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, nimesoma na kuona jinsi gani nguzo ya rasilimali watu na hasa kwa utekelezaji wao tuangalie watumishi wa umma kwa maendeleo hasa kwa kutowahamisha hamisha bali waangaliwe na kuwaweka pale ambapo mtumishi ana uwezo napo na kuweza kushauri kwa manufaa ya nchi.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa viwanda ninashauri tuwe tunafanya tathmini kwa sehemu ambazo viwanda vinaweza kujengwa kwa maoteo ya lengo husika mfano viwanda vya mzao vijengwe sehemu ya ulimaji wa zao husika au madini na kadhalika ili viwe na tija na faida kwa nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, niipongeze Serikali kwa uamuzi wake ambao ni bora na lengo lake la kuwezesha upatikanaji wa sukari nchini na hii ni nzuri kwani itawaondolea wenye viwanda kuhodhi bila kuathirika kwa dhamira ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, naipongeza Serikali kwa hatua ya kutoa idhini ya kuingiza sukari tani 410,000 kupitia NFRA na natambua dhamira nzuri ya Serikali na pia Serikali kufanya marekebisho ya kanuni ya NFRA na kuiweka sukari kuwa sehemu ya usalama wa chakula.

Mheshimiwa Spika, kwa kumalizia napenda kusema kuwa dhamira ni nzuri, lakini NFRA inategemewa na wakulima kununua mazao yao hivyo wasisahaulike.

Mheshimiwa Spika, niishauri pia Wizara ya Viwanda na Biashara inaposema inachochea uchumi basi waweke mahusiano mazuri na walipakodi ili kuona wanatendewa sawa na sheria zinzosimamia taratibu za biashara. TRA wawatembelee wafanyabiashara na kusikiliza hoja zao.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.