Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mahonda
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. ABDULLAH ALI MWINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia huu wasaa wa kuchangia katika mpango huu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, maendeleo lazima yawe maendeleo ya watu (people centered). Maendeleo ya vitu ni njia tu ya kutufikisha kule kwenye maendeleo ya watu. Infrastructure; barabara, umeme, maji, elimu, vyote vile ni njia ya kupeleka maendeleo kwa watu (people centered development). (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa huu ni mpango wa mwisho wa miaka 25 ni vyema tu tukaanza tukaangaza macho kama kweli tumepata people centered development katika hii miaka 25. Kwa hakika maendeleo makubwa yamepatikana. Ukiangalia kipato cha kila Mtanzania kimepanda mara dufu kwa kipindi hichi cha miaka 25. Ukiangalia kwenye afya (infant mortality) vile vichanga vilivyokuwa vinakufa kwa idadi kubwa sasa hivi vimepungua. Ukiangalia kwenye elimu, ukaangalia idadi ya watu ambao wamekwenda shule (access) kwa idadi ya namba na idadi ya percentage imekuwa mara dufu. Ukiangalia life expectancy, Mtanzania anatarajiwa kuishi kwa umri gani, umri umepanda mara dufu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hakika haya maendeleo na mpaka hapa tulipofika tumepata manufaa makubwa. Ni wajibu wetu kuhakikisha kwamba maendeleo yajayo yatakuwa makubwa zaidi na yatakuwa kwa haraka zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya utangulizi huo ningependa kuzungumzia mambo matatu: Elimu, mradi mkubwa wa kimkakati wa LNG na kama nitapata fursa nizungumzie ajira kama strategic bottleneck ya maendeleo ndani ya nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu ni mambo matatu. Elimu ni access, elimu ni quality, elimu ni relevancy. Mambo matatu, access; Watanzania wangapi wana fursa ya kwenda shule? Elimu la pili; quality. Elimu yetu ina kiwango gani? Suala la tatu, relevance. Katika ulimwengu huu tuliokuwa nao, elimu ile inatusaidia vipi? Is it relevant kwa leo? Sasa kwa hakika access kuhakikisha wanafunzi wetu wanakwenda mashuleni tumefanikiwa kwa kiwango kikubwa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali limebakia hapa kwenye quality na kwenye relevance. Kwenye quality; ulimwengu wa sasa elimu ya chuo kikuu haina umuhimu mkubwa sana kwenye ajira. Makampuni yote makubwa unayoyajua ulimwenguni wala hawatazami kama umekwenda chuo kikuu au la. Wewe kama una degree, kama una masters, kama una PhD na mwenzio aliyemaliza form six; yule kijana wa form six anaweza akapata kazi kabla yako. Hizo kampuni za google, Microsoft, apple; ile fortune 500 ya Marekani, degree yako si muhimu sana. Kama unayo unaweza ukaingia intern kama mwenzako aliyemaliza form five na form six. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maana hiyo nini kitu cha muhimu? Kitu cha muhimu ni skills. Skills tunazipata wapi? Katika ulimwengu wa leo university zote kubwa unazozijua hapo zinatoa kozi kwenye internet bure, tena kozi za elimu na study za leo (data scientist, coding) bure. Ivy League University, wewe ukiwa na bundle yako unaweza ukaingia kijana wako akajifunza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini naligusia hilo? Naligusia hilo kwa sababu moja ya msingi katika mitaala yetu ya elimu. Ni muhimu sana vijana wetu waweze kuzungumza na kufahamu Kiingereza vizuri. Kiswahili lugha yetu, Kiswahili tukienzi, lakini ili tusome tupate skills, lugha ya internet, lugha ya hizi kozi za kiulimwengu bure ni lugha ya Kiingereza. Ndiyo hoja niliyokuwa nazungumza ya tatu (relevance). (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ile emphasis yetu katika elimu lazima tufikirie hayo mambo matatu: la kwanza access, la pili quality, quality ya namna gani? Kulingana na ulimwengu wetu wa leo. Tatu, relevance; ndio haya. Tusifikirie maisha yana-revolve ndani ya nchi yetu; ajira ni global, ajira ni ya kimataifa leo hii. Lazima tuhakikishe Watanzania na vijana wetu wa Tanzania wanazungumza kwa umahiri angalau lugha mbili (bilingualism), Kiingereza na Kiswahili. (Makofi
Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi ya kimkakati tumeifanya mingi na impact yake ni kubwa sana, lakini mradi mkubwa zaidi mara dufu kushinda yote kabisa ni Mradi wa LNG ambao mpaka sasa hivi unasuasua. Mradi wa LNG kwa muhtasari, tuyazungumze tu. Hakuna mradi ndani ya Bara la Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara wenye ukubwa kama mradi huu wa LNG, utaongoza tukiweza kuukamilisha. Watanzania kwa kawaida yetu, mradi wowote ule, mabadiliko ya aina yoyote ya kiuchumi lazima maneno yawepo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kuwasihi Serikali yangu sikivu kuhakikisha mradi huu mazungumzo yanakamilishwa na unaanza. Hivi karibuni tumezungumza sana kuhusu dira na kwa miaka 25 iliyopita, uchumi wetu wa Tanzania umekua kwa kiwango cha asilimia sita mpaka saba. Wataalam wetu hapa wakasema, ili tufike kule tunakotaka kufika lazima kitokee kitu ambacho kinaweza kukuza uchumi into double digits, yaani 8,9,10 na kuendelea. Mwarobaini wa hilo ni LNG. (Makofi
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi wa LNG ukianza hapa Tanzania, ule mwaka wa kwanza directly kuingia katika Serikali ni dola bilioni saba kila mwaka. Hatujapata hiyo double digit growth tukiweza kukamilisha hilo? Sasa kwa hakika kabisa ningependa Serikali yangu kuweka mkazo na kuweka fikra zake zote kuhakikisha makubaliano yanakamilika. Kwa mfano maneno mengi, tatizo la LNG tofauti na wote tulivyokuwa tunafikiria (namalizia), kwamba, maliasili unaweza ukaitoa tu ardhini wakati wote, sio kweli.
Mheshimiwa Mwenyekiti, dunia ya leo mambo yanabadilika. Kuna teknolojia ambazo zinaweza kufanya kilichokuwa ardhini hakina thamani tena. Sasa muda unakwenda, kuna renewable energy ambazo zinatumika kwa kasi juu kubwa sana. Kuna technology inaweza ikafanya yale yaliyokuwa ardhini hayana thamani tukashindwa ku-access. Sasa tufanye haraka sana ili mradi huu wa LNG ukamilike.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkono hoja na ahsante sana. (Makofi)