Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026.

Hon. Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026.

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niwe miongoni mwa wachangiaji jioni yetu ya leo. Ninaomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya na kuweza kusimama jioni hii. Mimi ni miongoni mwa Wajumbe wa Kamati ya Bajeti, nianze kwa kuwapongeza Waheshimiwa Mawaziri wote na Manaibu Waziri yale mawazo ambayo tulitoa kwenye Kamati yetu mengi wameya-accommodate, ninaomba niwapongeze sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpango wetu tunaenda kufanyia maboresho, lakini tukiwa bado tuna advantage ya baadhi ya mambo ambayo ninaomba niyataje ambayo yanatupa nafasi nzuri kama Taifa. Tunaenda kufanya maboresho ya Mpango sisi kama Taifa tukiwa na amani ya kutosha, lakini pia tunaenda kufanya maboresho kukiwepo SGR, lakini na TAZARA ni advantage kwetu kubwa sana kama Taifa, lakini tunaenda kufanya maboresho ya Mpango tukiwa na uhakika juu ya umeme baada ya uzalishaji kutoka Bwawa la Mwalimu Nyerere.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tunaenda kufanya maboresho katika Mpango ambao utakuja tukiwa na uhakika uwekezaji mzuri ambao umefanywa kwenye bandari yetu na efficiency kwenye bandari yetu imeongezeka. Pia tunaenda kufanya maboresho tukiwa na uhakika na tax calendar ambayo kwa vyovyote vile mwekezaji anapokuja ana uhakika wa uimara wa sera zetu ndani ya miaka mitatu. Vilevile, tunaenda kufanya hayo maboresho tukiwa na uhakika juu ya geographical position ya Taifa letu ambayo Mataifa mengine hawana fursa kama hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiwa na uhakika juu ya ukuaji wa uchumi ya Taifa letu pamoja na mitikisiko ambayo imetokea duniani uchumi wa Tanzania umezidi kuwa bora ukilinganisha na uchumi wa nchi nyingine. Tunaenda kufanya maboresho haya tukiwa na uhakika wa Soko la East Africa lenye idadi ya watu milioni 302 kwa hiyo tuna soko la kutosha, lakini miundombinu yetu ukilinganisha na nchi majirani zetu bado tuna miundombinu iliyo bora sana; lakini tunaenda kufanya maboresho tukiwa bado tuna fursa kwenye uchumi wa bluu. Vilevile, tunaenda kufanya maboresho tukiwa na uhakika wa food security, tuna chakula cha kutosha kama Taifa. Tunaenda kufanya maboresho kukiwepo na vivutio vya kiutalii huwezi ukalinganisha na majirani zetu wote. Tunaenda kufanya maboresho tukiwa na madini mengi ambayo huwezi ukalinganisha na Mataifa mengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nichangie maeneo ya changamoto ili mpango wetu uweze kuwa vizuri tukiwa na orodha ndefu hii, nimezitaja tu kwa uchache advantages ambazo tunazo kama Taifa. Uwepo wa SGR ni jambo jema, lakini SGR hii ili tuanze kupata matunda yake ni pale ambapo ujenzi wake utakamilika kwenda kufika Mwanza, Kigoma na huko kwingine nchi jirani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe katika Mpango tusije tukaingia kwenye ile wanayoita Dutch disease kwamba tunafika mahali ambapo tuna-concentrate eneo hilo tukaacha reli zetu zingine kwa maana ya Meter Gauge Rail tuhakikishe inaendelea kuwepo lakini kubwa zaidi ni uwepo wa TAZARA na maboresho ambayo yanafanyika ninaomba tushukuru waasisi walioona mbali. Tuhakikishe kwamba TAZARA tunaiboresha na niiombe Serikali katika Mpango ni wakati muafaka wa kuhakikisha kwamba tunakuwa na tawi ambalo linaanzia Tunduma kwenda Kasanga Border ili tuweze ku-access DRC kwa njia ambayo ni fupi kuliko njia zote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii itakuwa inasaidia Taifa kuhakikisha kwamba tunaenda huku ambapo mzigo upo mwingi ambao hautiliwi mashaka ambao ni Katanga kwa ya Lubumbashi na siyo kule Kalemie. Niombe wakati tunaendelea na ujenzi wa reli ni vizuri pia tukaendelea kufanya research tufanye utafiti hii reli yetu ya kisasa inapokuwa imekamilika inafika Mwanza, na Kigoma mzigo upi ambao tunategemea kwenda kuuchukua? Itakuwa si jambo jema mpaka tunamaliza ujenzi halafu hatuna uhakika juu ya mzigo kwa maana ya shehena tunaloenda kuchukua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vizuri pia waendelee kufanya utafiti; je, kwa kukamilika kwa ujenzi wa reli hiyo msongamano wa malori ambayo yapo Tunduma utapungua na utapungua kwa sababu zipi? Ni vizuri researchers wakatujia na majibu kwa nini mzigo ambao unaenda Tunduma kama kweli utapungua utahama utaenda Kalemie jambo ambalo sitaki kuamini. Kwa hiyo, ipo haja ya kuhakikisha kwamba tunaendelea kuboresha Reli yetu ya TAZARA ili iweze kusaidiana kuhakikisha kwamba Bandari yetu ya Dar es Salaam inaendelea kuwa competitive ukilinganisha na bandari za wengine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kasi ya kumalizia vipande hivyo ambavyo vimebaki iongezeke ili tuweze kunufaika na uwepo wa SGR pale ambapo hatutakuwa tunasafirisha abiria peke yake maana wachumi wanatuambia faida katika reli inapatikana pale ambapo unasafirisha mzigo. Sasa tunafurahia habari ya kusafirisha abiria, lakini ili tuweze kuona return on investment ambayo inaonekana ni pale ambapo tutakuwa tumekamilisha ujenzi wa vipande hivyo vingine na reli yetu ianze kuhudumia sheheni ya mizigo. Niiombe Serikali katika jambo ambalo tuna kila sababu ya kuhakikisha kwamba tunakamilisha kwa wakati ni ujenzi wa SGR pasi na kusita kwa sababu iwayo yoyote ile. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo naomba katika Mpango ni vizuri tukasititiza ni uwepo wa Sera za Kikodi ambazo zinatabirika. Ninaomba nimpongeze Mheshimiwa Rais kwa kuanzisha tume ambayo inaenda kufanya mapitio juu ya kodi zetu ili kama Taifa tupate kodi stahiki kwa sababu sasa hivi kile ambacho tunakusanya against GDP ni kidogo. Sasa hivi kwenye Mpango tunakusudia kwenda 13%, lakini tukifika 15% ya GDP hapo ndiyo tutasema tunakusanya kodi ambayo ni stahiki na tushindane na Mataifa mengine hicho ndiyo kiwango ambacho kinakubalika, 13% bado ni kiwango ambacho hakikubaliki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sera za Kikodi ziwe zile ambao zinatabirika. Mwekezaji anataka anapokuja kuwekeza hapa awe na uhakika kwamba kodi zake anaweza aka-plan hata baada ya miaka 10 anajua kiasi gani ambacho alikuwa analipa kama kodi kulikoni kila baada ya miaka miwili inabadilika kwa kweli haileti tija. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo ninaomba niongelee ni juu ya suala zima la upatikanaji wa mitaji. Mitaji inaweza ikapatikana ndani ya nchi au kutoka nje ya nchi. Kutoka nje ya nchi tunaweza tukapata either kwa kukopa, tukapata kama msaada, lakini tukapata wawekezaji ambao wanaweza wakawekeza kwa kutumia hisa kwa maana ya kununua shares kwa DSE ambayo ipo Tanzania. Vilevile, namna nyingine ya kupata mitaji ni kwa kutumia DSE kwa maana ya kwamba ndani ya Tanzania Watanzania ambao wangependa kwenda kununua shares wakienda DSE wakute shares zipo

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu niiombe Serikali wana misuli ya kutosha, wana uwezo wa kukopa nje ya nchi; ndani ya nchi waachie private sector ili wasiwe wananyang’anyana hicho kidogo ambacho kinapatikana kwenye benki zetu kiasi kwamba benki zinaona namna iliyo bora kwa sababu kwenda kuwekeza Serikalini kwa maana ya treasury bonds na bills ni sehemu ambayo unaenda kuwekeza na hakuna risk yoyote. Kwa hiyo benki yoyote janja au yeyote ataona bora afanye biashara na Serikali, kwa hiyo maana yake ni kwamba tunaiua private sector lakini hali kadhalika hata interest rate ambazo zinatozwa Serikali inatoa 16%. Kwa hiyo, kwenye benki inakuwa hiyo ndiyo kama benchmark hata unaposema tupunguze interest rate wanatazama je, ya Serikali tunapata ngapi? Kama Serikalini unapata 16% kwa nini akija Kandege usimwambie 20% ni vizuri Serikali ikatafakari ili Watanzania walio wengi ambao wanataka kuwekeza wapate interest rate zilizo chini ndani ya benki zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niunge mkono hoja na ninakushukuru kwa fursa. (Makofi)