Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
2
Ministries
nil
MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia katika Mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo 2025/2026. Nimesoma mpango wenyewe, pia, nimesoma na kusikiliza hotuba ya Waziri wa Mipango na Uwekezaji, pia, nimesikiliza nakusoma hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Fedha, nimesoma taarifa ya kamati na nimefanya marejeo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa, ule wa 2024/2025. Kwa kurejea hizo zote na kusikiliza kila walichokizungumza kuhusiana na mpango huu wa mwaka 2025/2026 imenikumbusha na nikakumbuka kwa sababu, nafahamu unapoizungumzia Tanzania unazungumzia mambo matano au sita ya msingi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza, unapoizungumzia Tanzania, unazungumzia human development, unazungumzia maendeleo ya watu. Tunazungumzia Sekta ya Maji, Sekta ya Elimu na Sekta ya Afya. Tunazungumzia mazingira na masuala ambayo yanahusiana na watu kwa sababu, tumesema maendeleo ya vitu ni lazima yaende na maendeleo ya watu. Kwa hiyo, unapoizungumzia Tanzania, moja ya jambo la msingi ni hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili la msingi, siyo kwa umuhimu, lakini kwa kuyataja ni Sekta ya Utalii, tourism industry au tourism sector, lakini unapoizungumzia Tanzania unazungumzia agricultural sector, ndiyo sekta ambazo ni za msingi, zimeishika Tanzania. Huwezi kuweka miradi yoyote ambayo iko nje ya hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la nne ni extractive industry, sekta ya uziduaji, kwa maana ya uchimbaji wa madini. Huwezi kuzungumza maendeleo, mipango na uwekezaji wa Tanzania bila kuzungumza hicho.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tano ni logistics, usafiri na usafirishaji na kwingine tunakopambana sana ni viwanda na biashara. Bado tunaendelea kujipanga, lakini mambo ya msingi ambayo tunategemea katika kukusanya mapato, tunategemea katika kutawanya mapato ni katika mambo hayo matano ya msingi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu, nimesema nimesoma hayo yote na nimeeleza kwamba, Tanzania is about those five industries, basi niwapongeze sana Wizara ya Mipango chini ya kaka yangu Mheshimiwa Profesa Kitila Mkumbo, pia, kaka yangu Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba pamoja na, mmeongezewa kifaa kingine hapo, ndugu yetu Stanslaus Nyongo ambaye pia, ni Daktari, if I am not mistaken. Naibu Waziri pale, pamoja na timu nzima ya Wizara ya Mipango na Uwekezaji bila kuwasahau watendaji ambao najua wanakimbia sana kwa ajili ya kuhakikisha kwamba, Tanzania inapata mipango ya watu ambao wametoka kwenye mifupa ya watu wa Singida, akili zao zimekaa sawa, ndiyo wanaoongoza Wizara hizo mbili za msingi na kwa sababu, natoka huko ni lazima nijimegee hapo kipande, niwapongeze sana ndugu zangu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niwapongeze pia Kamati, wametu-direct. Wao waliupata mpango kabla na wakajadili mapendekezo, wametoa maoni, niwapongeze sana, wamefanya kazi kwa niaba yetu, lakini niwakumbushe. Moja, nasema nawapongeza kwa sababu, kama mtu amesoma mpango na amesoma nyaraka hizo ambazo nimezitaja, lazima ataona namna ambavyo watu hawa na watendaji wao wamehakikisha wanayashika yale maeneo matano ya msingi niliyoyataja na mapendekezo mengine. Hapo kuna maeneo sijayataja, kwa mfano TEHAMA na vitu vingine ambavyo ni cross cutting, vinapita katika hivyo vyote. Wamegusa karibu vyote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, angalizo langu ni moja tu; Mheshimiwa Waziri na timu yako, ukiangalia integrated labor force survey ya Tanzania, nimefuata ya 2021, mwisho utaona nguvukazi ya Taifa namna ilivyogawanywa iko pyramid. Namna tulivyogawanywa kwenye mfumo wa elimu, yaani kwenye level za elimu kwenye nchi, kwenye labor force utaona kwamba, ni pyramid. Tulisema pyramid juu kabisa ndiyo kwembamba ambako kuna wasomi wa vyuo vikuu asilimia 1.8, vocational training ni asilimia 1.3 na 16.5% ndiyo elimu ya sekondari.
Mheshimiwa Mwenyekiti, waliobaki wote ni elimu ya msingi. Kwa hiyo, kwa kusema hivyo ni kwamba, wanaoongoza uchumi, ambao ndiyo labour force ya nchi hii ni elimu ya sekondari na kushuka chini. Kwa hiyo, wakati tunapanga mipango yetu ni lazima tutafute namna tuta-address hilo suala. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi zote zilizoendelea walishika tertiary ambayo tunazungumzia kuwa ni vyuo, vocational training. Kwenye hilo sina mashaka kwa sababu, mimi niko Kamati ya Elimu, kuna namna ambavyo na sisi kule tunakimbizana kuhakikisha kwamba, upande wa kujenga ujuzi na wa vocational training tunakimbizana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niwaombe mipango yetu msiwe mnasahau hata siku moja kwamba, bado tunategemea mtindo huo katika labour force. Kwa hiyo, ni lazima tuhakikishe kwamba, tuna-address hayo mambo na tunayaweka katika mipango yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu nilizungumza yale mambo matano, leo nitachagua moja tu na nitajielekeza katika logistics, usafiri na usafirishaji. Mwaka 2004 nilipata kusoma na kusikiliza mahali, wakati huo sisi kwa umri wetu tulifanya marejeo, lakini niliwahi kumsikiliza Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamini Mkapa akizungumza kuhusu kiongozi shupavu na akamtaja kwa sifa kadhaa na nitatumia tatu kati ya hizo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, alisema, kwanza kiongozi shupavu ni lazima awe na maono na dira katika malengo yake aliyojiwekea. Ni lazima awe na malengo katika jambo lake kwa sababu, ni kiongozi, lakini la pili, alizungumzia kiongozi shupavu ni lazima awe madhubuti katika kusimamia rasilimali watu kuelekea malengo na dira ambayo yeye anaiona, kama kiongozi kwa sababu, ni lazima muwe na kiongozi kwenye jamii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu ni kuwa king’ang’anizi na madhubuti katika kuyasimamia malengo na maono ambayo yeye alikuwa nayo. Kwenye nukta hii na mimi nimeyarudia maneno hayo aliyoyasema Hayati Benjamini Mkapa kwa sababu, mimi ni miongoni mwa wanafunzi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika namna anavyoyaendea mambo yake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye hii nafasi ninaomba wote tumpongeze Mheshimiwa Rais kwa sababu, kwenye suala la logistics, usafiri na usafirishaji, mwaka jana tuliona namna ambavyo nchi iliingia kwenye mtikisiko, tukizungumza kuhusu uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam, DP World, na hakuyumba. Ninasema hivyo kwa sababu, hata mimi ningekuwa kwenye hiyo nafasi ningefanya kama alivyofanya kwa sababu, kila kiongozi mwenye maono anapoingia kwenye madaraka hakuna anayetaka kupita bila kuacha alama na kwa sababu, kulikuwa na mtikisiko yeye alisimama imara mpaka leo,
Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuwezi kushindwa kusema kifua mbele kwamba, kwa miezi mitano kuna mambo ambayo yamefanyika bandarini. Nitayataja kwa mfano kwa sababu, kwenye Wizara wamesema na mengine sisi tunayaona, mengine watayataja wao kwa vielelezo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mtikisiko ulikuwa mkubwa, lakini leo naomba niwaambie mambo yanayoendelea kwenye Bandari ya Dar es Salaam na niwapongeze sana watu wa Bandari ya Dar es Salaam pale TPA, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari ndugu yetu Mbosa. Kwanza, sisi kama vijana tunajiskia fahari sana kwa sababu, yule ni kijana mwenzetu na ana-perform vizuri kiasi kwamba, wengine tunaamini kama ameaminika na amefanya vizuri kuna vijana wengine wataaminiwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini, mtoto mdogo akinawa mikono vizuri anakaribishwa kula na wakubwa. Kwa hiyo, Bandari ya Dar es Salaam tunafanya vizuri kwa sababu, Mheshimiwa Rais alikuwa imara wakati tunapitisha DP World na hakuyumba. Sasa leo nasema hapa kwa sababu, mimi natoka Singida, nimeona kuna vitu vimefanyika pale Bandarini na kuna makusanyo yanafanyika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, kwa miezi mitano kuanzia Mwezi Aprili mpaka Septemba, Serikali imeweza kukusanya mapato takribani Shilingi za Kitanzania bilioni 325.3 ambayo sasa, Serikali kwa kuona namna hiyo na niwaambie hapa, Mheshimiwa Waziri inawezekana hizi statistics baadaye mwakani tukizirudia zitakuwa tofauti sana kwa sababu, nimwambie Waziri hiki kimefanyika wakati ule wanarekebisha mifumo. Yaani wakati wanafanya procurement, wakati wanaleta utaratibu mwingine mpya na haya yote yanaendelea kwa hiyo, wameweza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wangu hii five months mmeweza, lakini kwa sababu, Serikali kupitia TPA inapanga kufanya investment, inapanga kufanya uwekezaji wa takribani shilingi trilioni 1.922 kwenye miradi mitatu ambayo wameitaja hapa, ikiwemo ujenzi wa Bandari ya Kisiwa cha Mgao huko Mtwara, huo ni mmojawapo. Naamini tukiendelea hivi, hata sisi watu wa Singida tutapata mradi wa umeme wa upepo sasa, maana yake mambo yanaenda vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli, nilisema ni social development enthusiast, napenda mambo yaende na haijalishi nani atakuwa anasababisha yaende. Kama kuna mtu akikaa pale anafanya maamuzi ambayo sisi kama nchi tunatoka hatua moja tunaenda nyingine, mimi nitamuunga mkono. Ndiyo maana mwaka jana wakati watu wanajiuliza, hivi uwekezaji wa bandari unalenga kutatua nini au tunapata nini? Mimi nilijiuliza kama uwekezaji wa eneo kama bandari utakuwa unatusaidia kuongeza mapato kama Taifa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama utakuwa unatusaidia kuongeza ufanisi katika utendaji wa bandari, kama utakuwa unatusaidia kuchochea ukuaji wa uchumi, nitaunga mkono na niliunga mkono na leo ninaunga mkono na ninaomba wasiache kusema. Tafadhali wafuatilie vizuri wapate taarifa. Naomba waongee kwa sababu, ni lazima tu-set standard, lazima kama kiongozi akiamua kusimamia jambo lake hebu wampe benefit of doubt, kama mtu unaona kuna informed decisions, mtu anafanya maamuzi ambayo yamefanyiwa tafiti na wataalam na unaona kuna namna kwa sababu, mtu anayefahamu, ambaye ni mtaalam, kuna namna ambavyo anaweza akazungumza zikaonekana kama theory, lakini zikafanyiwa utafiti na wakaona kuna namna wanaenda, kwa nini wamkwamishe mtu kama huyo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hiyo ni sehemu moja tu nimesema ambayo naona hata sisi watu wa Singida tunaweza tukanufaika. Mpaka sasa hivi ninavyozungumza, haya yote ninayoyataja hapa, kwanza TRA wamekusanya mapato sana…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Mheshimiwa muda wako umeisha.
MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)