Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2023 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Katani Ahmadi Katani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tandahimba

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2023 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. KATANI A. KATANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nichukue fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu, lakini nimpongeze sana Waziri wa Fedha kwa bajeti hii ambayo ameileta ambayo matumaini yangu kama fedha hizi tutazipitisha, basi Watanzania wanaenda kupata neema ya Taifa hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee kuipongeza Wizara ya Fedha, lakini niipongeze na Wizara ya Kilimo kwa kuleta Finance Bill ya mabadiliko ya Sheria ile ya Sukari. Taifa hili tumekuwa mateka kwa muda mrefu kwenye sekta ya sukari, kwa zaidi ya miaka 25, miaka 50, tumekuwa mateka kwenye sekta ya sukari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati nzuri Mawaziri waliotangulia hapa kwenye Wizara ya Kilimo, Wabunge wenzangu waliokuwepo hapa watakubaliana nami, tumekuwa na Mheshimiwa Tizeba hapa, tatizo la sukari limekuwepo kwenye Taifa hili, bei zikiwa zinapanda na kushuka, tumekuwa na Mheshimiwa Hasunga, tumemekuwa na tatizo la sukari zikiwa zinapanda na kushuka, lakini hata Bunge lako hili Tukufu mwaka huu tunaosema, tumesimama Wabunge hapa tukiwa tunalalamikia bei kubwa ya sukari. Sisi Wabunge tutakuwa watu wa ajabu kwa Finance Bill hii inayokuja ya kufanya marekebisho kwenye suala la sukari, tukaja Wabunge tukafarakana wakati tunamtetea mlaji Mtanzania wa mwisho. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni juzi tu hapa Ramadhani ikiwa inakaribia, tukiwa Bungeni hapa Wabunge wamesimama sukari shilingi 8,000 kwenye majimbo yao. Wakuu wa Mikoa wanasema sukari shilingi 7,000 kwenye mikoa yao. Serikali inahangaika kwenda kufungua ma-godown ya watu kwa ajili ya suala la sukari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo itakuwa ni jambo la ajabu na la kusikitisha Serikali inachukua hatua Watanzania wapate sukari kwa bei nafuu, akasimama mjinga mmoja mimi simjui, akatetea jambo la bei inayopanda ya sukari na kuongea vitu visivyoeleweka. (Makofi) [Maneno Hayo Siyo Sehemu ya Taarifa Rasmi za Bunge]

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge, kanuni zinatukataza kutumia neno mjinga, ninaomba uliondoe kwenye Hansard.

MHE. KATANI A. KATANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nilisoma Kiswahili na kwa sababu wewe ni mtaalamu wa Kiswahili, daktari wewe, kabla sijaliondoa neno ungenipa fasili sahihi ya neno mjinga ili niweze kuliondoa vizuri na Watanzania wajue tafsiri ya mjinga