Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Edward Olelekaita Kisau

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kiteto

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi, nimpongeze Waziri, Naibu Waziri na timu nzima. Changamoto za wafugaji nchini tunahitaji maeneo ya malisho ya kutosha. Ilani ya Chama Cha Mapinduzi tulisema tutatenga maeneo kutoka hekta milioni 2,700,000 mpaka milioni 6,000,000, lakini kwa trendi ya mambo yanavyokwenda ni kama yanapunguzwa. Sasa wanaopunguza wanatumia Ilani ipi? Tunataka majibu hapo. Maeneo haya yakilindwa kisheria na ng’ombe wakapata sehemu ya kulishwa vizuri, hii sifa wanayosema kila wakati kwamba Tanzania ni Nchi ya pili kwa mifugo itapata tija. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la pili, tunataka mabwawa kwenye maeneo haya ili wafugaji waweze kutulia. Mheshimiwa Mnyeti wewe unafahamu Kiteto ni kame, Mheshimiwa Waziri ulikuja Kiteto tulipoteza ng’ombe karibu 25,000 lwa ukame. Kwa hivyo lazima tuweke pesa nyingi sana kwenye mabwawa; na Bwawa la Kaiwang Mheshimiwa Waziri anafahamu, tulitembelea na nimeona kwenye bajeti yao hapa, sasa lazima iishe.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatu ni chanjo za mifugo, maeneo yakishatengwa, tukapata mabwawa chanjo ziwepo na tunataka ruzuku ya Serikali tuione kwenye chanjo hizi. Ng’ombe wengi sana wanakufa kwa sababu ya kukosa chanjo za uhakika. Kwa hivyo it’s that time sasa nchi waanze kutuonesha kwamba chanjo za uhakika zinapatikana wapi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatu mnataka tuboreshe ng’ombe, hizi mbegu mnazoleta zinauzwa ghali sana. Tuuzieni 500,000, 1,000,000 tutanunua lakini kama hampunguzi hatubadilishi. T

Mheshimiwa Naibu Spika, tumezungumza kuhusu maeneo mengi sana ya wafugaji yanayochukuliwa na hifadhi na nyinyi mpo na Mheshimiwa Mnyeti wewe unafahamu, vurugu za watu wa hifadhi. Sasa inafika mahala inaonekana kwamba ng’ombe sasa sijui hata watoto wanaokuja sasa wanaanza kuona kama mifugo ni mbaya kufuga mifugo wakati ni uchumi kama ilivyo uchumi mwingine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hivyo Wizara i-promote ili wananchi wafahamu. Kumekuwa na tendency fulani watu wana-generalize vitu, wafugaji wanafanya hivi, sasa tukienda hivyo hatutajenga taifa imara ambalo kila mtu ana thamani. Kwa hiyo lazima tuwe careful na statement kama hizo. Hakuna shamba la ujamaa wala hakuna mifugo ya jamii nzima, Ole Kaita akiingiza ng’ombe shambani ni Ole Kaita na anayelima akilima maeneo ya kilimo ni Juma, kama ni Juma, kama ni Ally kama ni nani iwe hivyo. Lakini tukiseme tuki-generalize tukisema wafugaji, sijui wakulima, tunafanya nchi tu ionekane kwamba kuna mgawanyiko sio wa lazima sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu minada ya mifugo. Kiteto kuna minada mikubwa mitatu, Dosidosi, Kibaya na Sunya. Tunataka sasa muanze kutengeneza minada hii iwe na hadhi, ili wafugaji wapate sehemu ya kulishia mifugo. Hata leo wakati Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wanasema wakulima ukiwa na tani moja hautozwi faini, kuna wafugaji wananiandikia hapa; hivi tani moja ya ng’ombe ni ng’ombe wangapi, ili na sisi tufahamu? Kwamba, ukiwa na ng’ombe wangapi na wewe haulipi kodi?

Mheshimiwa Naibu Spika, lazima tuwe na system ambazo ni fair kwa kila mtu. Kwa hiyo, utatuambia baadaye rafiki yangu kwamba, tani moja ya ng’ombe ni sawa na ng’ombe wangapi, ili na sisi tufahamu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu BBT. BBT ni jambo zuri sana na tunawakaribisha hao wafugaji wapya, lakini msiwasahau wafugaji ambao tayari wako huko wanafanya hizi shughuli. Hebu tafuta pesa sasa za kuwasaidia wafugaji ambao tayari wanafanya hizi kazi za mifugo wakati unaendelea kuwafundisha hawa wapya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lipo suala la majosho na kwenye ilani tumesema hivi, ng’ombe wakiwa na afya watawezesha kufanya biashara hii tunayosema tuondokane na magonjwa. Leo majosho nchini, kwa mfano mimi Kiteto nina upungufu wa majosho karibu 40 na kitu, ni vyema Serikali iweke hela, ili majosho yapatikane ya kutosha kwa ajili ya mifugo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, watu wamezungumza kuhusu ng’ombe kwenda nje na mtu anasema sijui ni laki tatu sijui? Mahindi pia, yakivuka iwe ni bei gani? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nadhani, unajua hakuna mtu ana interest ya kupeleka ng’ombe huko nje. Masoko yakiimarika hapa na bei ikiwa nzuri kila mtu atauza hapa, lakini haiwezekani tuseme mahindi yapelekwe halafu mifugo sijui tufanye nini? Na tuwe careful na lugha kama hizi kwa sababu, zinaleta mkanganyiko ambao siyo wa lazima sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mifugo katika nchi hii ni uchumi kama ulivyo uchumi mwingine wowote. Mheshimiwa Ulega, sijui siku moja na wewe utaanza kutengeneza mazizi tukamate wanyama pori tuwaweke kwa sababu, wanakuja huku wanakula nyasi. Wao wakiondoka hivyo halafu mifugo hakuna mwingiliano. Ahsante sana. (Makofi)