Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. NORAH W. MZERU: Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya kuboresha elimu katika Wizara ya Elimu. Pia nampongeza Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda na timu yake nzima kwa kazi nzuri wanayoifanya.
Mheshimiwa Spika, katika mpango wa bajeti ya Wizara kwa mwaka 2022/2023 ulijielekeza katika kutekeleza maeneo ya kimkakati ikiwa ni kuongeza fursa na kuimarisha elimu ya ufundi nchini, kuhimiza uandishi, uchapishaji na uchapaji wa vitabu nchini, kuongeza wigo wa shule za ufundi, na kuimarisha ujifunzaji kwa vitendo katika Taasisi za Elimu ya Juu kwa kuanza kujenga campus za vyuo zenye kujielekeza katika mafunzo kwa vitendo katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa maeneo hayo ya kimkakati ulienda sambamba na utekelezaji wa vipaumbele vifuatavyo: Serikali imeendelea kuimarisha mazingira, miundombinu ya kujifundishia na kujifunzia katika shule za msingi na sekondari katika kufikia azma hiyo.
Mheshimiwa Spika, aidha, Serikali kupitia Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mamlaka ya Elimu Tanzania imetekeleza yafuatayo: imejenga shule ya mfano ya sekondari Dodoma eneo la Iyumbu yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,000 na imejenga upya vituo vinne kwa ajili ya utoaji elimu ya sekonadari nje ya mfumo rasmi katika Mkoa wa Rukwa - Sumbawanga, Iringa Mjini, Pwani - Kibaha, na Manyara - Babati.
Mheshimiwa Spika, pia Serikali imekarabati vituo vinne katika Mkoa wa Dar es Salaam, Makao Makuu ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Morogoro Manispaa, na Ruvuma Songea. Miundombinu hiyo itaimarisha mazingira ya utoaji wa elimu ya ualimu na kuongeza fursa ya upatikanaji wa elimu ya walimu.
Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.