Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Mwantum Dau Haji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. MWANTUMU DAU HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, awali ya yote kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kunijalia kuwa na hali ya uzima na afya lakini sasa hivi nishukuru kuwa mzima na nimesimama nataka kuichaingia Wizara hii ya Ujenzi ni Mjumbe wa Kamati hii ya Miundombinu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwanza napenda sana kumshukuru Waziri wangu, Waziri Bashungwa pamoja na Naibu wake Kasekenya. Kwa kweli, hawa wanafanya kazi kubwa, wanafanya kazi kubwa tena nzuri na jitihada tunaziona sisi sote katika Wizara yake, maana tunatembelea maeneo mbalimbali katika Wizara hii. Lakini pia nimshukuru na Mwenyekiti wangu huyu wa Kamati, Mheshimiwa Selemani Kakoso kwa kutulea katika Kamati ile mpaka leo hii mimi naweza kusimama hapa sasa hivi na nikaweza kuchangia, namshukuru sana Mheshimiwa Mwenyekiti wangu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kwa kuendelea kuna suala hili kidogo nataka kuliwekea sawa kwamba kwa kuwa, mkakati wa kuwawezesha Wakandarasi wanawake na vijana. Mimi hili neno nilivyoliona katika mkakati wao mimi nilishukuru sana hili suala kwa sababu wanawake watapokuwa wao Wakandarasi pamoja na vijana wakawawezesha, wakajua kwamba hapa sasa hivi sisi tupo tunafanya kazi basi sisi wanawake tunafanya kazi kubwa sana kuliko wanaume. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vijana nao hali kadhalika kwa sasa hivi wanafanya kazi kubwa sana. Kwa hiyo, hili suala mimi naomba hawa wanawake pamoja na vijana wapewe kipaumbele waweze kufanya kazi zao katika ukandarasi wao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kwa kuongezea nazungumzia kuhusu ubora wa madaraja. Madaraja na ubora haya ndiyo tunayoyataka kwa sababu mimi nimetembelea katika barabara zetu tunazopitia nilishashuhudia kuna madaraja mengi sana yalikuwa yanakatika hasa kipindi hicho cha mvua mimi mwenyewe nilishashuhudia. Kwa hiyo, nilikuwa naomba Wakandarasi wanaojenga madaraja wayajenge madaraja yenye kiwango, madaraja yenye kiwango ambayo yanaweza angalau yakadumu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa sababu wanaweza kuifanyia hasara Serikali wakawa wanajenga madaraja ambayo hayana kiwango matokeo yake tunafika karibu ya madaraja magari yanasimamishwa mabasi tunaambiwa kule daraja limekatika kwa hiyo, Serikali pale imeishapata hasara.

Mheshimiwa Spika, lakini vilevile nizungumzie na hili kwamba mimi hapa nitasema sasa hivi ni mkazi wa Dodoma, Manispaa yangu ya Makulu ninakokaa mimi Mkalama. Nimshukuru Naibu Waziri wangu Biteko, kwa kazi kubwa anayoifanya katika barabara za Mkalama. Hivi sasa hivi kazisimamia madaraja yanafanya kazi na kesho kutwa karibu tutatembelea nini mgongo wa ngisi, maana ile barabara watazitia lami. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo namshukuru sana Waziri wangu Mheshimiwa Dkt. Biteko, afanye kazi kubwa ili tuweze kupita pale. Yule Mwenyezi Mungu katuletea kule aje akae ili na sisi Wanawake wa Mkalama tufaidike katika barabara zile pamoja na Wananchi wote wa Mkalama. Tunamshukuru sana sana sana na nikisema haya nikakosa kumshukuru basi mimi nitakuwa sina fadhila maana hili suala mimi nilimwomba na akaniambia Mheshimiwa taratibu, tutakwenda na tutafika. Ni kweli sasa hivi tumefika na tunamshukuru sana na naunga mkono hoja 100%, ahsante sana. (Makofi)