Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
House of Representatives
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
2
Ministries
nil
MHE. MWANTATU MBARAK KHAMIS: Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuimarisha sekta hii ya ujenzi kwa kuimarisha miundombinu mbalimbali ikiwemo ya barabara.
Mheshimiwa Spika, aidha nimpongeze Mheshimiwa Waziri, Katibu Mkuu na watendaji wote wa Wizara hii kwa kusimamia na kutekeleza vyema majukumu yao ambayo yanaleta matumaini kwa wananchi.
Mheshimiwa Spika, kazi kubwa imefanyika katika kuendeleza Mradi wa SGR, kujenga madaraja ndani ya wilaya, lakini pia kazi kubwa imefanyika katika kujenga barabara mbalimbali, licha ya kuwa miundombinu katika maeneo mengi yameharibika kutokana na mvua nyingi zilizonyesha.
Mheshimiwa Spika, ushauri wangu kwa Wizara hii, kuangalia na kufikiria kwa umakini namna ya kujenga barabara na madaraja ambayo yataweza kudumu hata kama kutatokea mabadiliko ya hali ya hewa basi yaweze kubaki salama na kuepusha hasara kwa Serikali na kupunguza kero kwa wananchi.