Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Oliver Daniel Semuguruka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa naomba kumpongeza Mheshimiwa Rais wetu kipenzi kwa kazi kubwa anayoifanya ya kujenga nchi.

Mheshimiwa Spika, nampongeza Waziri wa Ujenzi na Naibu wake kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Mheshimiwa Spika, sasa naomba nijielekeze moja kwa moja kwenye hoja zangu. Kwanza naiomba Serikali kuwalipa fidia wananchi wa Tarafa ya Rulenge, Wilayani Ngara ambao walifanyiwa tathmini ili kupisha ujenzi wa barabara inayopita maeneo hayo kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, kuna ahadi ya kipindi kirefu tangu Awamu ya Nne, Barabara ya Nyakahura – Murusagamba – Murugarama - Tembo Nickel hadi Rulenge. Naomba majibu ni lini ujenzi wa barabara hii ambayo ni ya muhimu sana kwa wananchi wa Ngara inayoleta uchumi katika wilaya yetu na mkoa wetu.

Mheshimiwa Spika, pia naomba malipo ya wakandarasi yapewe kipaumbele kwa sababu wanategemea mikopo ya mabenki na wanapocheleweshewa malipo riba inazidi kupanda mwisho wa siku wanaishia kufa na pressure kwa sababu ya madeni.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja na naomba kuwasilisha.