Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Eng. Ezra John Chiwelesa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Biharamulo Magharibi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami ninashukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia kwenye maoni haya ya Mpango wetu wa 2024/2025. Kipekee kabisa ninawapongeza Mawaziri wote wawili na timu zao kwa mapendekezo haya ambayo wameyaleta, lakini kwa sababu tunatoa maoni, nitaenda moja kwa moja kwenye mambo hasa mawili makubwa ambayo yanabeba suala ya Kitaifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, cha kwanza, ninapenda kuongelea Mradi wa LNG kama mradi mkubwa wa kunyanyua Taifa, lakini pia nitaongelea mradi wetu ambao nimekuwa ninauongelea siku zote wa Liganga na Mchuchuma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Bajeti ya mwaka 2022/2023 wakati Wizara ya Nishati inawasilisha hapa, tuliongelea habari ya LNG. Kwa hiyo, ninapenda tu niweke mkazo hapa kwamba, miradi hii mikubwa ambayo inaleta sura ya Kitaifa na hasa ambayo inashindana na Mataifa mengine makubwa inapokuwa inataka kutekelezwa katika Taifa, si kusema wale wanaofanya miradi hii huwa wanafurahi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni miradi ambayo tuliaminishwa na tuliona kwamba inaweza ikatusaidia kama Taifa hasa kwenye uzalishaji wa nishati ya umeme, matumizi ya magari, ambapo tuta-compress hiyo gesi na kuwa compressed natural gas (NG) kwa ajili ya matumizi ya magari, lakini pia na kuuza gesi hii nje baada ya kui-compress tukaipakia katika meli zile kubwa na kwenda kuiuza huko nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa, tunaomba; tutakapokuwa tunapanga mpango huu, Wizara hizi mbili hasa Wizara ya Mipango, mje na a thorough analysis, ikiwezekana tupate take-off ya hili jambo. Kwa sababu wenzetu wanachofanya, kuna players kama watatu wanne watano ambao wao wanamiliki miradi hii mikubwa ya gesi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa, tunapozidi kuchelewa, uwezekano wa wao kuamua kufanya sehemu nyingine ni mkubwa na sisi tukabaki na hii gesi isitusaidie. Maana dunia inabadilika kila siku na visa vinakuwa vingi na hasa deals hizi kubwa zinapotokea, kila mmoja anaangalia advantage yake ambayo inamsaidia yeye kwenye kupata pesa, lakini pia kwenye kuzuia watu wengine wasinyanyuke. Kwa hiyo, ninaomba tulione na tuweze kulifanyia kazi

Mheshimiwa Mwenyekiti, huwezi pia kuongelea maendeleo ya Taifa kama hutakuwa na stable power supply, hasa umeme. Maana wote mnajua tunatekeleza miradi mikubwa ya Kitaifa na unapoongelea kukua, hasa ukawa na industrial packs kubwa, lazima uwe na stability ya umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninajua tunaingiza megawatts 2,115 kwenye Gridi ya Taifa kutoka kwenye Bwawa la Mwalimu Nyerere, lakini kwa mipango ambayo tunayo kama Taifa, nami bado ninaona huo umeme ni mdogo na hautoshi. Unajua leo umeme kwenye vijiji umefika maeneo mengi, ni zile centres tu za vijiji. Ukisema uusambaze uanze kuingia vijijini, huu umeme bado ni mdogo sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, bado nina-insist, kama Taifa lazima tujaribu kuangalia vyanzo vingine vipya vya umeme. Kwa sababu Taifa linalokuwa katika ushindani mkubwa namna hii, hatuwezi kuwa katika position hii ya umeme, bado tukajivunia. Fikiria tangu uhuru tulikuwa hatujafika megawatts 2,000; leo ndiyo tunaenda kuingiza hizi tunafika 4,000 na kitu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado umeme huu ni mdogo, kwa hiyo, tuangalie jinsi ya kuzalisha umeme hasa kutoka kwenye Project ya Liganga na Mchuchuma, kutoka kwenye Project ya LNG, ziweze kutusaidia kuingiza umeme mwingi kwenye Gridi ya Taifa, hatimaye hao wawekezaji ambao tunasema tunawavutia waje kuwekeza hapa, waje wakiwa na uhakika wa umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini ninayasema haya; wiki kama tatu zilizopita nilikuwa Uganda na bahati nzuri nikatembelea ile project yetu ya Bomba la Mafuta. Kwa kweli ukijaribu kuangalia presentations zilizokuwa zinafanyika pale, nami kama Mtanzania nilijisikia vibaya. Maana lile bomba linalotoka Hoima kuja Tanga, kiasili yale mafuta kwa sababu ni crude oils lazima yaendelee kubaki katika temperature fulani kwa ajili ya kuyasafirisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, unaangalia kwa upande wa Uganda pump stations mbili zinazojengwa Uganda, wao hawajaweka hata issue ya solar. Maana wanasema umeme uko stable, watatumia umeme wa maji (hydropower) kutoka Uganda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pump stations nne zinazojengwa Tanzania, iko package ya ku-include solar energy. Kwamba, kila pump station ya Tanzania wameweka solar na jamaa yule kipindi ana-present pale hakujua mimi ni Mtanzania. Kweli aka-insist kabisa, you know in Tanzania electricity is not stable, so, we have to include solar package here. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Mtanzania iliniumiza, nikawaza nikasema; hawa jamaa sehemu kubwa ya pump stations ziko kwetu, lakini bado hawatuamini. Wame-include solar package ili waweze kwenda kufanya ule mradi uweze kuwa stable. Sasa, nikaona hili jambo ni lazima kama Taifa tunaposema tunakuwa, tunasonga mbele, hata kama tunaingiza kwenye Nation Grid leo hii umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, ni lazima tuangalie vyanzo vingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nina-insist kwenye suala la Liganga na Mchuchuma, huu mradi ndiyo mradi wa kipekee ambao unaweza ukatunyanyua kama Taifa. Maana Uganda leo wana mafuta; wako mpaka kwenye Project ya kujenga refinery ndani ya nchi yao ile, kwamba mpaka watapata byproducts nyingine zinazotoka kwenye mafuta, ambazo zitakuwa zinatangaza Taifa lao kama byproducts za kutengenezea chemicals, byproducts za kutengenezea mabomba ya plastiki na vitu vingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa, tuombe hata sisi, huu Mradi wa Chuma, Serikali imelipa fidia, tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa zaidi ya shilingi bilioni 15 ambazo ameweka pale. Sasa, kwa sababu ya owning this project, tunaomba tuone kwenye Mpango huu wa mwaka 2025/2026, ni nini kinafanyika kwa ajili ya take-off ya mradi huu. Hatuna kitu kingine cha kujivunia kama Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais amesema habari ya Southern Corridor kwa ajili ya SGR. Sasa, kama huu mradi hauja-take-off, hiyo pesa tunayoenda kuwekeza huko chini itafanya nini? Ni lazima tuhakikishe huu mradi una-take-off, ili hatimaye kilio hiki cha Watanzania cha kuona tunasonga mbele tuweze kwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa dola bilioni tatu ambazo zinasadikiwa kama uwekezaji, deposit tuliyonayo, nilikuwa naangalia hapa napitia, deposit tuliyonayo kwenye iron ore peke yake, ni zaidi ya tani milioni 126, deposit tuliyonayo kwenye makaa ya mawe ni zaidi ya tani milioni 428.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia price ya leo kwenye iron ore, tani moja ni dola 118, ukiangalia kwenye makaa ya mawe, tani moja ni dola 141. Hii yenyewe uki-calculate tu ni zaidi ya dola bilioni 74, yaani unawekeza dola bilioni tatu, deposit uliyonayo itakuingizia zaidi ya dola bilioni 74. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa, sometimes unakaa unaangalia, ni nini, yaani tunakwama wapi? The think tankers of this country wanakwama wapi kutupeleka huku? Yaani kwa nini nishindwe kuweka dola bilioni tatu nika-recoup zaidi ya dola bilioni 74? Bado tunasema tunahangaika na vitu vingine, wakati huu mradi uko hapo muda mrefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona kwenye andiko, majadiliano yanaendelea na mtu yule yule aliyetukwamisha kwa muda mrefu. Inafikia stage kwenye mawazo yangu ninawaza hii ni hujuma, ni hujuma kwa sababu, tunapoelekea makaa ya mawe yanakuwa phased out na tutaanza kutumia nishati safi kama mnavyoelewa. Hata haya makaa ya mawe nilikuwa ninaongea na Mchina mmoja, anasema hawawezi kuingiza makaa ya mawe kwao yakiwa na state ya vumbi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtu yeyote anayetaka kuingiza makaa ya mawe China, wana mtambo wametengeneza wa kuyasafisha kwanza kabla ya kuya-export kwenda China. Kwa sababu wanaamini yanasababisha kansa, wanaamini yanaleta mercury na vitu vingine kama hivyo. Sasa, kipindi tunapambana na dunia, makaa ya mawe tumepata bei nzuri sana kwa sababu ya vita ya Russia na Ukraine. Energy supply kwa sehemu kubwa ya dunia ilisimama. Tunavyozidi kuchelewesha huu mradi tutakwama na haya makaa ya mawe tutabaki nayo. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba, kwa kumalizia ninajua kengele imegonga. Waziri wa Mipango uko hapa, lichukue hili mlifanyie kazi. Bahati nzuri umekuwa Waziri wa Viwanda na unalijua vizuri. Kwa hiyo, ninaamini kwenye mpango wako wa mwaka 2025/2026, tuone clear statement ya Serikali ya kwenye mpango huu. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, ahsante!

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana.