Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nominated
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Naibu Spika, nami nikushukuru kwa kunipatia hii nafasi, nimshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema ambaye ametujalia kuwepo hapa tukiwa na afya njema.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Rais kwa kuchaguliwa kwa kishindo kwenda kugombea akiwa mwanamke peke yake, Mwenyezi Mungu azidi kumbariki, ampe afya njema na ninasema Mwenyezi Mungu ana kadari zake na ndiyo maana aliweka Adamu na Hawa.
Mheshimiwa Naibu Spika, hii maana yake ni zamu ya wanawake na Watanzania wote tumuunge mkono Mheshimiwa Rais kwa vile kazi aliyopewa anaifanya kwa ufanisi na hakuna mjadala wa watu aliye na macho haambiwi tazama, Mheshimiwa Rais anafanya kazi kubwa Mwenyezi Mungu ambariki.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, nitoe pole za dhati kwa familia ya Makamu Mwenyekiti wangu wa Malaria, Mheshimiwa marehemu Faustine Ndugulile, kwa kweli Kamati au caucus yetu ya malaria tumeondokewa, Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi na familia yake ipate faraja kwa kuwa kila nafsi dhaaikatul maut, hakuna nafsi itakayobakia duniani, wote tutaondoka.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, nitazungumzia kwanza mikopo. Kwanza tumshukuru Mheshimiwa Rais amehangaika amepambana mpaka sasa hivi zimepelekwa fedha Benki ya NMB kwa ajili ya kuwakopesha vijana, wanawake na walemavu.
Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo tulilonalo ni mkanganyiko mkubwa hata pa kuanzia hawa watu hawapajui. Sheria iliyopo bado haijawafanya watu hawa kujua wanazipataje zile fedha, tukichukulia sasa hivi vijana wengi wanamaliza vyuoni hawana ajira, akisema aende maendeleo ya jamii bado hakujakaa vizuri, akisema aende NMB nako inakuwa ni vurugu kiasi ambacho vijana hawa hawajui waende wapi.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tuisimamie na tuangalie sheria hii kwa umakini, pale kwenye mapungufu tufanye marekebisho mara moja ili kuwawezesha vijana na wanawake hawa kuweza kupata mikopo kwa urahisi na kuweza kujishughulisha katika shughuli zao. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, riba ipo chini, hivyo kama kweli tungesimamia hawa vijana ambao wanahangaika sasa hivi bila kuwa na kazi, tumemsikia Mheshimiwa Mbunge anasema wengi wamemaliza vyuo hawana shughuli, wameamua kuingia katika shughuli za ulevi na wale wengine baada ya kuona maamuzi yao kwa vile vichwa vyao havijatulia wameamua kuingia katika ushoga kitu ambacho si afya ya Watanzania katika suala hilo.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika upande huo huo wa mikopo vilevile kuna usajili. Nimefanya tathmini mara tatu sioni majibu. Kuna usemi usemao “likupigalo ndilo likufundishalo”. Leo tunafundishwa Waafrika na tunabezwa kwa vile hatujakuwa serious katika utendaji wa baadhi ya mambo.
Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania tunayo population ya watu milioni 61, lakini vijana au wanawake wangesajiliwa milioni tatu kwa shilingi 20,000 tungekuwa na bilioni 60. Narudia tena hapo, tungesajili watu milioni tatu tungekuwa na bilioni 60, hivi kulikuwa na haja ya kukopa hapo? Ina maana fedha tunayo lakini hatutaki kuzichezesha brain zetu, tunangojea kukopa, lakini kukopa ndiyo kunatudhalilisha sasa hivi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nilitamani Waziri wa Fedha angekuwa hapa maana yake linamuhusu. Ninaomba timu ya Wizara ya Fedha, Wizara ya TAMISEMI na Wizara ya Wanawake na Watoto ikishirikiana na Kamati tukalifanyie kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, utajiuliza Dar es Salaam, Temeke peke yake, kuanzia Temeke mpaka Mbagala na wafanyabiashara wale tungekuwa tunao watu wengi sana ambao wamesajiliwa, jambo la kusikitisha mpaka sasa hivi wamesajili watu 45 lakini waliolipa ni watu 15,000. Hivi ni kweli tupo serious katika kuhakikisha haya mambo yanafanikiwa?
Mheshimiwa Naibu Spika, watu 15,000 Tanzania nzima ndiyo waliojisajili na leo kama wamejisajili watu 15,000 zile hela benki zimekaa tu, zitachezewa tu. Ninaomba, imefika mahali Mheshimiwa Rais kama anaweza kutoa fedha sisi tumeshindwa vipi kusajili watu milioni tatu, hiki si kitu cha kawaida. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, leo kama Wizara zote tatu zitashirikiana hasa TAMISEMI, kila Halmashauri ikaonesha ilifanya kazi gani pale alipofeli Mkurugenzi kuonesha hawa watu tunaweza tukafanya hivi vitu, lakini tukitegemea leo mkopo tumeshazuiliwa kule, hela ya makusanyo ya ndani ya kawaida imetushinda, nani wa kumlaumu? Tujilaumu wenyewe kwa vile hatupo serious.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa sijui niseme nini, hii ni mara ya tatu ninazungumzia suala hili, hakuna ufanisi unaoingia au mtu akasema angalau tukae chini tuone tunafanya nini! Tupo tayari kujadiliana, kama mtu haelewi hata mkifanya calculation mara moja mtaona kuna hizi fedha zimekaa nje hazitumiki, zinachezewa tu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, uratibu ni Wizara ya Maendeleo ya Jamii, ukusanyaji ni Wizara ya TAMISEMI, hela inakwenda Hazina, kiasi gani kila mmoja ajue kinakwenda wapi. Sasa kwa nini tusibomolewe nchi kuwa hatujitambui katika makusanyo ya fedha wakati tuna fedha ma-billions of billions hazina mwelekeo, hazina mpangilio.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba wewe ni msikivu tuifanyie kazi. Imefika muda iwe mwisho! Tulikwenda Uganda na Kamati ya Bajeti kama miaka mitano nyuma, Uganda kila mfanyabiashara ana kitambulisho shingoni, huwezi kufanya biashara yoyote pale Uganda - Nakivubo bila kuwa na kitambulisho. Sisi tunavyo vitambulisho? Watu wanauza biashara hawana vitambulisho! Sasa kama hajajisajili unategemeaje kupata mapato? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo naomba, kwa kweli ninampongeza Donald Trump kwa hili atatufanya Waafrika tuamke. Tunaonekana nini, unajua kila siku ukidhalilishwa lazima utapata akili ya kuweza kujitegemea, hiyo tuifanyie kazi kama kweli tupo serious, tuna uwezo wa kukusanya mapato zaidi ya bilioni 100 katika mwaka huu na tukipata bilioni 100 Wizara hii haitakuwa tena na mikopo wala nini, vijana wanaweza wakajiendesha katika hela yao kwa revolving fund. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu ajira za nje, nimewasikia wenzangu wanaongea. Tanzania tuna vijana ambao wanasoma…
NAIBU SPIKA: Ahsante Mheshimiwa.
MHE. RIZIKI S. LULIDA: Eeh! Haya bwana. (Kicheko)