Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manyoni Mashariki
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nichukue nafasi hii kukushukuru kwa kunipatia hii nafasi ya kuchangia kwenye taarifa hizi mbili za Kamati zetu. Vilevile, nawashukuru Wenyeviti wetu wawili ambao wamewasilisha hizi taarifa muhimu sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kipekee namshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kazi kubwa ambayo ameifanya hususan katika Jimbo la Manyoni Mashariki. Nikisema nianze ku-mention miradi yote ambayo ameifanya, naweza nisimalize, lakini nskiri kwa kusema kwamba sisi watu wa Manyoni mwaka huu ni Mwaka wa Uchaguzi na tumepeana ahadi kwamba, tutahakikisha Mheshimiwa Rais tunampatia heshima kubwa kwa kazi kubwa ambayo ameifanya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nina maeneo mawili ambayo ningependa kuchangia kwenye Taarifa ya Kamati, hususan kilimo na upande wa mifugo. Upande wa kilimo, kwanza nampongeza Waziri pamoja na timu yake, kaka yangu Mheshimiwa Bashe. Kwa kweli, Mheshimiwa Bashe hajasomea kilimo, nadhani tunatakiwa tum-award Ph.D ya kilimo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa taarifa niliyonayo, najua Mheshimiwa Waziri amesoma Mzumbe, mambo ya administration, lakini kimsingi ame-master sana hii Wizara ya Kilimo. Ukiacha hilo, Mheshimiwa Bashe umekuwa very aggressive, very innovative, very strategic na nina mifano kwa nini ninasema hilo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wa Tume ya Umwagiliaji, wote ni mashahidi, huko nyuma Tume ya Umwagiliaji kimsingi ilikuwa imekufa, lakini kwa ushawishi wake kwa Mheshimiwa Rais, akamshawishi pamoja na Wizara yake, wakaongezewa fedha za umwagiliaji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakumbuka tulikuwa na shilingi bilioni 42 wakati tumeingia. Sasa hivi anachezea shilingi bilioni 500 na kitu. Hii ni kwa sababu, yupo aggressive, innovative na yupo result based. Ndiyo maana Mheshimiwa Rais amemwelewa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kule kwangu kuna mradi mmoja wa Umwagiliaji wa Mbwasa. Kila Ilani ya Uchaguzi huwa unawekwa. Mimi tangu nimeanza kukua nasikia tu unatajwa, Mradi wa Mbwasa Irrigation, Mradi wa Umwagiliaji wa Mbwasa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2024, Mheshimiwa Rais ali-commit ile tender ya zaidi ya shilingi bilioni 18 ikatangazwa, na mkandarasi ameshapatikana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii nimepewa taarifa, next week mkandarasi anaenda kukabidhiwa site na watu wa Manyoni wameniomba wakasema kwamba, Mheshimiwa Bashe kwa sababu, hii historia ameiweka mwenyewe, tunaomba yeye mwenyewe aje awe mgeni rasmi kwenye kumkabidhi site huyo mkandarasi, tarehe 13. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa heshima hii ambayo anaenda kuiweka. Ule ni mradi mkubwa sana wa kihistoria, tangu Mzee Chiligati akiwa Mbunge, akiwa Waziri, for 15 years alikuwa akipigia kelele, lakini ndani ya hii miaka minne ya Mheshimiwa Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anaenda kuweka historia nyingine kubwa sana ya kilimo cha umwagiliaji kwenye eneo letu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mbali ya hiyo, kuna mradi mwingine wa Udimaa. Nao mwaka 2024 ulitangazwa, ambapo kimsingi tunasubiri mkandarasi naye asaini contract, kwa ajili ya kuanza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, haya ni mafanikio makubwa sana upande wa kilimo, nami nimekuwa mdau wa Kilimo cha Umwagiliaji. Mara nyingi ninam-challenge Mheshimiwa Bashe, namwambia, kama hauta-focus kwenye suala la umwagiliaji, kilimo cha Tanzania tutakuwa waongo. We have to transform our agriculture, twende kwenye umwagiliaji kwa sababu, mvua hazitabiriki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mbali ya hayo kuna maeneo ya umwagiliaji, Mheshimiwa Bashe ni shahidi. Kule bondeni kwetu, Tarafa ya Kintinku, kuna maeneo ya umwagiliaji ambayo kimsingi yanahitaji kuwa developed.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, Scheme ya Walak, Scheme ya Msemembo, Scheme ya Udimaa, Scheme ya Ziale, Scheme ya Makanda na hata Ngaiti na kwingine. Haya ni maeneo ambayo kimsingi naomba ayachukue kama changamoto, in the future tuangalie ni jinsi gani tunaweza tukaendeleza?
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Tume ya Umwagiliaji, nimekuwa nikichangia mara nyingi. Ukiangalia sasa hivi haina investment ambayo tume ina-manage, is a very huge investment. Halafu bado tunadili na tume. Scope imeongezeka, lakini bado tuna-deal na tume. Ushauri wangu ni kwamba, kwa nini tusi-transform hii tume, tukatengeneza a very giant institution, mamlaka ambayo itaenda sasa kusimamia huu uwekezaji ambao tumeshauweka kwenye maeneo mengi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii shilingi bilioni 18 siyo Manyoni tu, mimi ninajua kule Mkalama kuna mradi mkubwa sana wa umwagiliaji, na Iringa kuna mradi mkubwa sana wa umwagiliaji. Nashauri, na ninaona hapo Mheshimiwa Waziri yupo karibu na Spika, naye ndiyo anahusika kwenye kushawishi hivi vitu, naomba tuletewe sheria ya kutengeneza Mamlaka ya Usimamizi wa Umwagiliaji Tanzania, ili tuweze kuipa nguvu Tume ya Umwagiliaji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la pili ni suala la korosho. Kwa kweli, ninamshukuru Mheshimiwa Rais, na pia namshukuru Mheshimiwa Bashe. Watu wa Mtwara na Lindi walikuwa wanatudharau Manyoni kwamba, ninyi Manyoni hamwezi kulima korosho. Frankly speaking, sasa hivi Kilimo cha Korosho Manyoni kime-peak. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka huu tumeenda kuuza korosho zaidi ya tani 100,000 kwa shilingi 3,167/=. Mimi wakati ninaingia Ubunge, nakumbuka tuliuza korosho kwa shilingi 1,600/= na mwaka 2024 tuliuza kwa shilingi 1,300/=, lakini mwaka huu wakulima wameuza kwa shilingi 3,167/=, ndani ya wiki hii iliyopita. Kwa hiyo, haya ni mafanikio makubwa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiacha hilo, Mheshimiwa Rais ametujengea ghala kubwa sana la kisasa pale. Watu wa TARI wamewekeza kwenye huu Mradi wa Korosho. Tuna zaidi ya ekari 22,000 ambazo tumeweka kule kwenye Mradi wa Korosho na tumejenga nyumba mbili za watumishi kule kwenye site za korosho. Haya ni mafanikio makubwa sana upande wa korosho. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nina changamoto chache ambazo ningeweza kumshauri Mheshimiwa Waziri, kwanza, ni vile viuatilifu vya ruzuku wanavyoleta, hawaangalii ukubwa wa ekari ambazo mtu anazo. Mwenye ekari 10 anapewa the same quantity na mwenye ekari mbili. Sasa wakulima wangu wanalalamika. Nadhani iangaliwe, kama mkulima ana ekari 50, idadi ya viuatilifu atakavyopewa iendane, iwe proportional na idadi ya ekari ambazo anazo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la pili ni kuhusu mnada. Tulifanya mnada last week, lakini kuna wakulima wengi bado wanaendelea kuvuna. Wanashauri, ni kwa nini tusiwe na minada mitatu? Kwa mfano, tukawa na mnada wa kwanza mid-February, mnada wa pili end of March na mnada wa tatu end of May, ili angalau tuweze ku-capture wakulima wote kulingana na vipindi tofauti tofauti vya uvunaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la tatu ni magunia. Gunia moja la kuhifadhia korosho linauzwa shilingi 10,000/= Manyoni. Najua kule kwenye tumbaku Mheshimiwa Bashe anatoa magunia ya ruzuku. Anawakopesha wakulima, wanachukua, then anakuja kuwakata wakati wa kuuza, kwa sababu sisi tunauza kwa kutumia Stakabadhi Ghalani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu ni kwamba, kwa nini tusitoe haya magunia kwa kuwakopesha, then wakati wanauza kwenye ule mnada wa Stakabadhi Ghalani wakatwe? Ile bei ya shilingi 10,000/= is very expensive. Kwa hiyo, wakulima wengi wanalalamika. Ningeshauri hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, tembo wanasumbua wakulima wa korosho. Sasa, hili siyo la Mheshimiwa Bashe, namwona kaka yangu hapo Mheshimiwa Kitandula ananiangalia. Tembo wanasumbua wakulima wa korosho, ninaomba nisaidiwe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ni Wizara ya Mifugo. Nampongeza Waziri wa Mifugo. Honestly speaking, Wizara ya Mifugo sasa hivi ina a very significant contribution kwenye uchumi wa Taifa. Mimi natoka kwenye ukanda ambao tuna mifugo wengi sana na nimekuwa nikilisema hili. Kama nilivyosema kwenye suala la Tume ya Umwagiliaji, Wizara ya Mifugo imekuwa mtoto yatima. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia tuna-deal na vitu vikubwa; majosho, malisho, sijui chanjo, masoko, mabwawa na kadhalika, lakini yapo ndani ya Wizara kama vi-unit tu. It is a high time sasa, tunahitaji vilevile kutengeneza an authority (mamlaka) ambayo itasimamia Sekta ya Mifugo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Sekta ya Mifugo ni sekta ambayo kimsingi kama tutaitengenezea a very giant institution, kama ilivyo TANESCO, TARURA, LATRA, RUWASA, nina uhakika mkubwa sana Sekta ya Mifugo ita-develop na inaweza ikawa na a very significant contribution kwa uchumi huu wa Taifa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niliona niliseme hilo na ninamwona pale daktari, Waziri wa Mifugo. Najua yeye ni Mchumi na Sekta ya Mifugo kimsingi ni ya uchumi perse. Kwa hiyo, najua kabisa ataenda kuitendea haki. Hebu tuanzishe hii mamlaka, then tuone ni jinsi gani itaenda ku-transform Sekta ya Mifugo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema haya, nirudie kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa ambayo ameifanya katika Taifa letu la Tanzania. Sisi watu wa Manyoni tunamwahidi ushindi wa kishindo mwaka huu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema haya, ninaunga mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)