Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024 Na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024

Hon. Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024 Na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitumie nafasi hii kwanza kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya na kufika wakati huu. Pili, nianze kwa kuunga mkono hoja iliyoletwa Mezani na Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, nitumie nafasi hii kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote na niwahakikishie maoni na mapendekeo yote ambayo wamekuwa wakitushauri kama Serikali tutaendelea kuyafanyia kazi na tutayaweka katika mipango ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kubwa kabisa, nitumie nafasi hii kumshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa dhati. Kama Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana ya Kilimo, haikuwa rahisi kuhangaika na changamoto za wakulima wetu, ambao wengi ni wakulima wadogo ambao ndio wameshikilia uchumi na usalama wa nchi hii, lakini amekuwa tayari kutoa fedha kwa ajili ya kuwa-support.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawahakikishia Waheshimiwa Wabunge kuwa wakulima wadogo wa nchi hii wataendelea kuwa kipaumbele cha Taifa hili na mipango ya Serikali mpaka pale tutakapofika eneo lingine ambalo tunatarajia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, namshukuru sana Mheshimiwa Deo na Kamati nzima. Pia, nawashukuru Waheshimiwa Wabunge kwani hapa leo wamekuwa wakitoa pongezi. Pongezi hizi mbele ya Mwenyezi Mungu wanaostahili ni Mheshimiwa Rais wa nchi hii na Bunge hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunazungumzia mafanikio ya sekta ya kilimo ambayo ukuaji wake umefika 4.2%, tunakimbilia asilimia tano kutoka 2.7%. Ni reform na mapendekezo ya Bunge hili. Leo tunazungumzia export value imefika zaidi ya dola bilioni 3.5 kutoka dola bilioni 1.2, ni Bunge hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tumezungumzia ukuaji, kwamba sisi ni nchi ya pili leo Afrika kwenye uzalishaji wa zao la mahindi. Kama siyo Bunge hili na Mheshimiwa Rais kuridhia kuanza schemes za kutoa ruzuku kwenye mazao ya chakula, leo tusingekuwa hapa. Wakati tunaanza kutoa ruzuku ya mbolea kwa mara ya kwanza, kelele zilikuwa nyingi na changamoto zilikuwa nyingi, lakini Bunge hili liliendelea kusimama imara kwa maslahi ya wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2021, mbolea yote iliyokuwa inatumika katika nchi hii ilikuwa ni tani 360,000; per capital consumption. Kwa hekta, ilikuwa ni kilogramu 15. Kwa msimu huu uliyokwisha juzi tumetumia jumla ya tani 840,000, per capital consumption, imefika kwa hekta kilogramu 24.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo letu ni kufika kilogramu 50 ambayo ndiyo standard ya nchi za SADC. Hii ni kazi ya miaka mitatu. Productivity per hectare ya mahindi imefika tani mbili, lengo tulilojiwekea ni kufika tani tatu msimu ujao wa kilimo. Hizi ni hatua, na Bunge hili limekuwa sehemu ya reform hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti na Waheshimiwa Wabunge wameongelea issues za mazao kama mpunga (mchele), tumetoka uzalishaji wa tani milioni 1.6 kwenye zao la mpunga, leo kama nchi, tumefika zaidi ya tani milioni tatu. Tanzania ni nchi ya nne Afrika kwenye uzalishaji. Kwa hiyo, tupo kwenye mwelekeo sahihi, ni mwelekeo ambao unahitaji commitment ya muda mrefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeanza kuwekeza kwenye umwagiliaji. Serikali ya Awamu ya Sita Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati anahutubia Bunge hili hapa, tulikuwa na mtandao usiozidi hekta 500,000. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ilani ya Uchaguzi na ninashukuru aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama, mimi nikiwa Naibu Waziri tunapojadili juu ya mtandao wa irrigation aliniagiza kuandika paper maalumu ya kuomba maeneo ya priority, yule pale Mheshimiwa Dkt. Bashiru akasema kama hatutawekeza kwenye eneo la umwagiliaji, hatutafanikiwa. Leo sisi kama nchi ilani inatupa target ya hekta milioni 1.2.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Awamu ya Sita, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan alipomaliza kusoma hotuba hapa, tulikuwa na hekta zisizozidi 500,000. Hivi sasa tunatekeleza miradi 780 ambayo tukiikamilisha yote, tutafikia hekta milioni 1.2 msimu wa 2025/2026.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatekeleza jumla ya mabwawa 100. Maji haya yanayosambaa kati ya mabwawa 100 ambayo tunaendelea kuyafanyia feasibility study mabwawa 14, tayari yana wakandarasi, na kati ya hayo 14, mabwawa matatu yapo zaidi ya 90%. Hizi ni hatua, na ni safari, hatuwezi kumaliza kwa siku moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawaomba Waheshimiwa Wabunge, matamanio yetu ni makubwa, na matarajio ni makubwa. Tunatakiwa kupiga hatua, lakini ni lazima tuendelee kuwekeza. Leo kwenye kahawa tumetoka tani 55,000, leo tupo tani 85,000 kwa mwaka huu. Serikali inatoa ruzuku ya miche bure, kwa mwaka, zaidi ya miche milioni 20 tunaigawa kama Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu korosho, Waheshimiwa Wabunge wote mnafahamu, Mfumo huu wa Stakabadhi ya Ghala, Mfumo huu wa Ushirika ambao tumekuwa tukiuhoji, umetufikisha mahali kwa miaka mitatu Serikali imekuwa ikigawa pembejeo na miche bure kwa wakulima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaenda kuvunja rekodi ya korosho kwenye nchi hii, tunaenda kufikia tani laki tano. Minada ilimekwisha hivi karibuni katika mikoa minne tu, bado mingine inaendelea. Nimwambie Mheshimiwa Dkt. Chaya kwamba tumepokea mapendekezo yake ya kuwa na minada zaidi ya mara mbili, mara tatu. Tuta-reform mfumo wa Manyoni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo wakulima wa Lindi, Mtwara, Ruvuma na Pwani wamepokea zaidi ya shilingi trilioni 1.5 kwenye mifuko yao, na huu ni mfumo wa ushirika. Kwa hiyo, nilitaka niwaambie tu wakulima wa chai, hili ni fundisho kwa Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikimjibu ndugu yangu Mbunge wa Hanang’, tulifanya maamuzi kama Taifa, kufanya kitu ambacho mimi naita, Blind Privatization. Tumejifunza, tumeona, tumewapa watu mashamba wameyaacha mapori, wamekopea fedha benki. Tumewapa watu mashamba hawayatumii na viwanda wameua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inafanya nini? Namshukuru Waziri wa Ardhi kwamba timu yetu ya uthamini imemaliza kazi yake, wametuletea draft ya kwanza. Hawa wawekezaji wanayo commitment ya mikataba ambapo kama hawatatekeleza, tumefanya tathmini ya value ya yale mashamba na hali ya viwanda walivyovitelekeza, tumeangalia thamani yake, tutayachukua kwa mujibu wa sheria na kuwagawia wakulima wadogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni suala la muda, nawaomba tuwe na patient, tusije tukaonekana ni Taifa ambalo haliheshimu sheria. Tutafuata utaratibu wa sheria kuweza ku-reclaim zao la chai. Kwenye parachichi tunaenda vizuri. Dada yangu nimekuelewa, tatizo lililopo Rungwe tunalifahamu wote, tutalichukulia hatua. Tumeshaanza kutatua na tunaamini kama Serikali, tutaendelea kutatua matatizo yaliyopo kwenye parachichi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, nataka niseme jambo moja. Taifa hili huwezi kuongelea kilimo kama hutamwongelea Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Huwezi kuongelea kilimo kama hutaongelea Azimio la Iringa. Ndiyo msingi wa reform ya kilimo. Anachokifanya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan leo, ataandikwa katika rekodi ya nchi hii, Mwenyezi Mungu akijalia, kwani Hatua anazochukua ni investment kwenye basic. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo 71% ya mbegu zinazotumika nchi hii zinazalishwa ndani ya nchi hii. Tumepunguza importation by 50%. Kwa hiyo, nawaomba Waheshimiwa Wabunge tuendelee kuwa na hii root kama Taifa, tusitoke kwenye mwelekeo huu tulionao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, irrigation is a direction; research and development are directions; seed multiplication ndiyo uelekeo; siyo uwekezaji wa muda mfupi, ni wa muda mrefu na sekta hii itabebwa na wakulima wadogo. Ndiyo transformation itakapotokea, na hatutaondoka katika mwelekeo huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawashukuru sana. (Makofi)