Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024 Na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024

Hon. Vita Rashid Kawawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024 Na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024

MHE. VITA R. KAWAWA – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naomba nishukuru kwa kunipa fursa hii kuja kuhitimisha hoja ya Kamati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, waliochangia hoja ya Kamati katika eneo langu wapo tisa, na kati yao Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Daniel Sillo, akiwa mmojawapo. Pia, yupo Mheshimiwa Zahor, Mheshimiwa Kunti Majala, Mheshimiwa Mkundi, Mheshimiwa Balozi Mulamula, Mheshimiwa Vicent Mbogo, Mheshimiwa Grace Tendega, Mheshimiwa Advocate Swalle, Mheshimiwa Mkenge, Mheshimiwa Njau, Mheshimiwa Mathayo Manyinyi na Mheshimiwa Daniel Sillo, kama nilivyosema hapo awali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kiujumla wachangiaji wamesisitiza mlemle, maeneo yote ambayo Kamati tuliyotolea taarifa. Kwa hiyo, naamini Serikali imesikia msisitizo wa Waheshimiwa Wabunge na pia, imesikia ushauri wa Kamati. Vilevile, naomba niseme kwamba, kama Kamati, tumepokea ushauri uliotolewa na Wabunge na tutasisitiza kwa Serikali waifanyie kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kiujumla maoni yetu ya Kamati na Mapendekezo ya Maazimio kwa Bunge yamesheheni yote ambayo Waheshimiwa Wabunge wameshauri leo hapa. Hivyo, tunawaomba mtuunge mkono kupitisha maazimio haya ili Serikali ikayafanyie kazi na kuongeza ufanisi katika kuleta tija kwa maeneo ambayo Kamati yetu ya Ulinzi na Usalama tunasimamia kwa niaba ya Bunge letu Tukufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo naomba kutoa hoja ili Bunge lako Tukufu liweze kukubali mapendekezo yawe maazimio. Naomba kuwasilisha. (Makofi)