Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024

Hon. Amb. Dr. Pindi Hazara Chana

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, natoa shukrani za dhati kupata nafasi hii. Niungane na Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wenzangu kuendele kumpongeza Rais wetu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupewa dhamana ya kupeperusha bendera. Tunasema hongera sana Mheshimiwa Rais umetuheshimisha duniani, tunakushukuru sana.

Mheshimiwa Spika, sambamba na hilo, vilevile, nichukue nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Nchimbi pamoja na Dkt. Hussein Ali Mwinyi kule Zanzibar. Sisi Watanzania tunaunga mkono hoja hizi za chama tawala na tunasema tuko bega kwa bega kupeperusha bendera yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niseme tu kwamba naungana na michango mingi ya Waheshimiwa Wabunge, lakini nashukuru kwa maoni ya Kamati ikiongozwa na Mwenyekiti, Mheshimiwa Mnzava na timu nzima ya Kamati yetu ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Wabunge wote. Michango yote tumeisikia na hii ni Serikali sikivu. Tutahakikisha tunaleta ufafanuzi kwenye point moja mpaka nyingine.

Mheshimiwa Spika, tumeweza kufanikiwa kuongeza idadi ya watalii. Idadi hii ya watalii imeongezeka kuzidi hata ile ambayo ilikuwepo kabla ya UVIKO 19. Sasa hivi tuna watalii milioni 5.3 wanaoingia nchini na ndiyo maana tulikuja na ile plate number tukasema T503 USD. Hapa tulitaka tuwapongeze Watanzania, kwamba unaposema utalii, dereva tax anahusika, anapoenda kulala, muuza vocha, anayelima kule shambani mchicha tunahitaji pamoja na matunda.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ni Watanzania wote milioni 62 na zaidi kwa mujibu wa idadi ya watu wameshiriki kuhakikisha idadi ya watalii inaongezeka chini ya uongozi mahiri kabisa wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mheshimiwa Spika, ndiyo maana tukasema tunakuja na T503 USD tukimaanisha tumevuka zaidi ya idadi ambayo ilikuwepo kabla ya UVIKO, lakini hata upande wa fedha, sasa hii mapato yetu, ni Dola za Kimarekani bilioni 3.9 na chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kweli yajayo ni neema tele, tunamshukuru.

Mheshimiwa Spika, watu wanapoenda kutalii nchi fulani lazima wajihakikishie amani, utulivu, na uongozi bora; watu ambao tunawapokea na kuwahudumia. Kwa hiyo, haya yote yanachangia kuleta watalii wa kutosha. Siyo hilo tu, chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan tumekuwa na mikutano mikubwa sana. Utalii ni pamoja na kwenda kuangalia wanyama, utalii wa malikale na sasa hivi tuna utalii wa mikutano, tunaita conference tourism.

Mheshimiwa Spika, tumekuwa na mikutano mikubwa sana ya Waheshimiwa Marais, wamekuja hapa kwenye Mkutano wa Nishati. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais. Hivi sasa tuna mkutano mkubwa sana wa viongozi wakubwa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC. Hii yote ni chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mheshimiwa Spika, viongozi wameingia kujadili ili kutatua matatizo ya nchi mbalimbali ikiwemo DRC. Hii yote ni ishara kwamba Tanzania tuko imara chini ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na ndiyo maana tunasema mitano tena, Mheshimiwa rais wetu anastahili. Tunasema ahsante. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kutokana na hivyo vigezo vyote, 2027 tutakuwa wenyeji wa Mkutano wa Apimondia. Huu ni mkutano maalumu ambapo wadau wote wa masuala ya nyuki watakuja ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kamati imetupa ushauri na sisi tunashukuru.

Mheshimiwa Spika, Kamati imesema, ujenzi wa eneo la kufanyia Mkutano wa Apimondia tuukamilishe haraka. Tumelipokea na tuwahakikishie Kamati tayari eneo la ekari 48 pale Arusha limeshapatikana. Tunashirikiana na Foreign Affairs kumpata mkandarasi na kwa haraka sana structure itakwenda kuwepo mahali pale.

Mheshimiwa Spika, tunapozungumzia utalii ni pamoja na miundombinu. Waheshimiwa wamesema na wamesisitiza, tunasema ahsante. Miundombinu ni muhimu, masuala ya barabara, na masuala ya malazi lazima tuyape kipaumbele. Chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, niseme tu kwamba UNESCO tayari wameshatupatia kibali cha kuridhia tujenge barabara ya tabaka gumu kutoka Nabi hadi Fort Ikoma Eneo la Ngorongoro na tutaendelea kuhakikisha miundombinu tunaizingatia.

Mheshimiwa Spika, wewe mwenyewe tunakushukuru sana unatuheshimisha kama Rais wa IPU. Unapoenda kwenye mikutano ya huko unatuletea wageni wengi na hiyo sisi kwetu tuna package kama sehemu ya utalii na umeendelea kuwa balozi wetu mzuri sana wa utalii, tunakushukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja na masuala yote tutaendelea kuyafafanua, ahsante sana. (Makofi)