Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024

Hon. Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, kwanza nami naomba niungane na Waheshimiwa Wabunge, Mawaziri wenzangu, kutoa pongeza kwa Kamati za Kudumu za Bunge ambazo zimefanya mawasilisho ya taarifa zake leo.
Mheshimiwa Spika, kipekee, napenda kutoa pongezi kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Timotheo Mnzava, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hii, Mheshimiwa Najma Giga pamoja na Wajumbe wote wa Kamati hii ambao wanafanya kazi kubwa ya kukuwakilisha wewe katika kuisimamia Serikali na kusimamia sekta yetu hii ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi.

Mheshimiwa Spika, niseme kwamba tunapokea maoni yote yaliyotolewa na Kamati. Tunapokea michango yote iliyotolewa na Waheshimiwa Wabunge leo humu ndani katika kuchangia Taarifa hii ya Kamati. Nami niseme kwamba, naunga mkono Taarifa hiyo ya Kamati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sisi kama Serikali tutakwenda kuhakikisha tunatekeleza maazimio yote yaliyotolewa kwenye Taarifa hii ya Kamati na kuhakikisha kwamba tunaleta Taarifa ya Utekelezaji wa Maazimio hayo. Kama ulivyojionea wewe mwenyewe, jitihada kubwa imekuwa ikifanyika katika kuhakikisha kwamba katika Sekta ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi tunatekeleza maazimio yanayotolewa na Bunge lako.

Mheshimiwa Spika, Maazimio hayo ya Bunge maana yake ni sauti za wananchi ambao wanaishauri Serikali nini kifanyike katika sekta hii. Tutaweka mkazo katika kuhakikisha mifumo inakuwa inasomana. Tunaenda kuweka mkazo katika kuhakikisha halmashauri zote 184 zinaenda kupata Mfumo wa Ardhi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile, ni kilio cha muda mrefu cha kuhakikisha kwamba vijiji vyetu vyote nchini vinapimwa. Tutahakikisha tunaweka nguvu kama ambavyo Kamati imeshauri na imeelekeza.

Mheshimiwa Spika, tutaweka nguvu kupima vijiji zaidi ya 330 mara moja, kwa sababu juzi tu tumefanya kikao cha Wizara ya Fedha, sisi Wizara ya Ardhi pamoja na Kamati hii ya Kudumu ya Bunge na kuna commitment hiyo ya kuhakikisha kwamba tunaenda kupima vijiji hivi mara moja. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mengine tutaendelea kupeana miongozo na maelekezo mbalimbali kupitia vikao mbalimbali vya Bunge na kupitia Kamati yako, nasi tuko tayari kuendelea kutekeleza maelekezo na maazimio yoyote yale ya Bunge. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, nashukuru sana kwa kupewa nafasi hii. (Makofi)