Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Singida Magharibi
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
2
Ministries
nil
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii ya kutoa mchango wangu katika Wizara hii ya Fedha.
Mheshimiwa Spika, ninataka niwaambie kwa heshima yako kama Spika wetu, ninataka niwaambie Watanzania na kupitia Bunge lako hili Tukufu maneno machache yafuatayo katika sekta ya uchumi ambayo Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wetu ameisimamia kwa kipindi cha miaka minne toka amekuwa Rais, ili kusudi waone kwa nini Wajumbe wa Mkutano wa Chama Cha Mapinduzi wamempendekeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan awe mgombea wao kupiti tiketi ya Chama Cha Mapinduzi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, hakuna mashaka kwamba Waziri Dkt. Mwigulu na Naibu wake wamefanya kazi kubwa sana katika Wizara hii ya Fedha, na ni watu wanyenyekevu sana na ni watu wasikivu sana. Kaka zangu ninawapongeza sana, sana, sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha miaka minne Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Fiscal and Monetary Policy ya nchi yetu, Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanikiwa kutekeleza kwa vitendo Fiscal and Monetary Policy ambayo imepelekea Taifa letu kuweza ku-maintain inflation kwa kiwango cha 3.5% mpaka 3.7%. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nataka nikwambie, hii ni rekodi iliyovunjwa katika Mataifa yote ya Afrika Mashariki. Ukiangalia Inflation Rate katika mataifa ya East Africa sitaki kuyataja, ina-range kuanzia 6.3%; kuna mataifa ya inflation rate ya 17% na kuna mengine mpaka 45%. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhihirisha kwa vitendo kwamba Serikali anayoiongoza imeweza kuwajali Watanzania kuhakikisha consumption power ya umma walionayo na kipato walichonacho, mambo ya mahitaji ya goods and service kwenye Taifa letu, Serikali yake imedhihirisha uwezo mkubwa sana katika kulinda stability ya uchumi wa Taifa letu. Pongezi nyingi ziende kwa Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kama hiyo haitoshi, ukuaji wa uchumi katika Taifa letu, ukiangalia kutokana na shock kubwa iliyopo ya kiuchumi duniani ambayo ilisababishwa na Covid–19, lakini pia ikaendelezwa na vita vilivyopo katika mataifa yenye nguvu ambayo ni wasambazaji wakubwa wa mafuta duniani, lakini Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweza ku-maintain ukuaji wa uchumi kwa 5.6%, jambo ambalo rekodi hii pia imeendelea kuvunja rekodi katika mataifa ya East Africa. Nani kama Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya uchumi? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, hali hiyo imepelekea ndani ya kipindi cha miaka hii na kupita mwaka uliopita, Kituo cha Uwekezaji cha TIC kimeweza kurekodi miradi yenye value ya shilingi bilioni 9.3. Kiuchumi hii ina tafsiri gani? Hii ina tafsiri kwamba sera zinazotekelezwa za Fiscal and Monetary Policy ambazo zimeweza ku-regulate mambo ya taxation, ambazo zimeweza kuchochea suala la employment, ndiyo maana umeona kasi kubwa ya wawekezaji kutoka nje wameingia katika Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, impact yake ni nini? Katika utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi tumetengeneza ajira zisizopungua milioni nane. Tafsiri yake ni kwamba pasingekuwa na mazingira mazuri ya sera za kiuchumi za Fiscal and Monetary Policy ambao watekelezaji wake wakubwa ni Benki yetu Kuu ya Tanzania, na kwa muktadha huu niruhusu nitoe pongezi zangu za dhati kwa Gavana wetu Ndugu Tutuba wa Benki Kuu kwa ujasiri na uzalendo mkubwa alioufanya katika kusimamia mabenki Tanzania. Kwa sababu stability ya utoaji wa mikopo imeendelea kuendana na kasi ya ukuaji wa uchumi, jambo ambalo lime-stabilize microfinance za uchumi wetu, jambo ambalo limepelekea makusanyo ya mapato kuongezeka katika Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nikiri kwamba nitumie nafasi hii kukipongeza sana Chama Cha Mapinduzi, chama kilicho na Serikali madarakani. Juzi tulipokuwa kwenye vikao vya chama tumeona wamekuja na ilani ambayo inapelekea kutoa maelekezo ya ku-digitalize uchumi wa nchi na nimekuwa mchangiaji mzuri sana ambaye nimekuwa nikipingana sana na mambo ya cash economy katika Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mahali popote duniani, Serikali zozote zinazotaka kuongeza tax base katika nchi zinasisitiza sana mambo ya cashless economy. Tukiweza ku-digitalize uchumi wetu tutaweza kuzi-monitor transaction katika nchi, tutaweza kujua nani anafanya shughuli gani na nani halipi kodi. Serikali itaweza kuongeza tax base ya kukusanya kodi katika Taifa letu, na hivyo kuongeza mapato katika Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nitoe mfano mmoja kwa nia njema, mimi ninapokuwa sina dereva sometime hapa Dodoma, transaction ninazozifanya kwenye taxi za hapa Dodoma natumia zaidi ya shilingi 60,000 kwa siku. Niulize swali Mheshimiwa Waziri wa Fedha, ni taxi ngapi zilizopo kwenye nchi yetu zinzofanya kazi ambazo zina device za kielektroniki ambazo mtu akilipa pesa anapewa risiti na Serikali inapata kodi?
Mheshimiwa Spika, kuna mambo madogo sana ambayo kama Taifa letu tunayadharau lakini yanaweza yakawa tax base ya kuwasaidia TRA kuweza kuingiza mapato. Kama mnashindwa kuwatambua, twende mfano mdogo taasisi ya Uber ambayo imesajili Uber kwa malaki na malaki katika Taifa letu. Tunashindwaje kuchukua statistics za waendeshaji wa magari haya ya taxi kupitia watu wa Uber? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nenda katika Taifa la Uingereza, utapanda taxi utachanja kadi Serikali itapokea kodi. Nenda kwenye Taifa la Ukraine, nenda mataifa yoyote duniani. Kwa takwimu nilizozifanya kwenye kodi ya haya ma-taxi peke yake, tunaweza tukapoteza zaidi ya shilingi bilioni 24 kwa mwaka, fedha ambazo zingeweza kupatikana zikawasaidia Watanzania katika sekta za maji, kilimo na sekta zingine katika Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kama hiyo haitoshi, nataka nitumie Bunge lao Tukufu kumpongeza sana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na economic setback ya dunia, bado Taifa letu limeweza kufanya strategic investment ya miradi ambayo imekuwa financed na Wizara ya Fedha na fedha zimetoka. Miradi ambayo imekuja ku-spillover impact chini na kuchochea ukuaji wa Uchumi, kwa mfano kukamilika kwa Mradi wa SGR.
Mheshimiwa Spika, leo Dodoma kwa siku inaweza ikapokea wageni wasiopungua 2,000 mpaka 3,000, jambo ambalo linapelekea mapato kwenye hoteli, mapato kwenye vyakula, mapato kwenye viwanja vya ndege, mapato kwenye taxi ninazoziongelea. Lazima tumuunge mkono Rais wetu na tumtie moyo kwa kazi kubwa ya kizalendo aliyoifanya ya ku-stabilize uchumi wa Taifa letu na kufanya uchumi wetu uweze kukua kwa kasi katika nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, jambo la pili ninalotaka kushauri; tunaye Mtanzania ana kampuni inaitwa Diversity Health and Social Care Limited iko Uingereza, anaitwa Paschal. Mtanzania huyu uliponipa kibali cha kwenda Uingereza miezi miwili iliyopita, mimi pamoja na Wizara ya Afya tulienda kumtembelea Mtanzania huyu kwenye ofisi yake.
Mheshimiwa Spika, nataka niliambie Bunge lako Tukufu, Mtanzania huyu akiwa Uingereza kampuni yake imeweza kuwa one of the best kampuni katika Taifa la Uingereza katika ku-recruit watu kwenye sekta ya afya. Wastani kwa mwaka, kila mwaka analeta idadi ya kuchukua watu 200 kutoka Tanzania katika sekta ya afya kwenda kufanya kazi Uingereza na ni kazi rasmi kwa sababu ana vibali vya Serikali ya Uingereza. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ninasema haya kwa sababu gani? Wapo Watanzania ambao wameshindwa kwenda kufanya kazi Uingereza kwa kukosa mitaji midogo midogo. Ninatoa wito kwa Wizara ya Fedha, Waziri wa Fedha, Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imetoa maelekezo kwenye ilani, tuchochee na kukuza ajira za vijana na ndivyo agizo hili linatekelezwa na vyuo vyetu kuzalisha vijana wengi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ni aibu, Taifa letu tunaletewa nafasi vijana wakapate ajira Uingereza, wanashindwa kwenda kisa wameshindwa kuwa na fedha za visa, wameshindwa kuwa na fedha za tiketi. Kwa nini Waziri wa Fedha usizungumze na mabenki vijana hawa wakasaidiwa fedha na mabenki, wakienda kupata ajira Uingereza watakapolipwa mishahara wakalipwa hizo fedha tukasaidia kupata ajira kwenye Taifa letu?
Mheshimiwa Waziri ninakuomba, utakapokuja ku-windup, kama hutatoa maelekezo kaka yangu, mimi bwana sitakushukia shilingi lakini wewe tunakwenda njia moja. Tutakuja kuzungumza nyumbani na nitakusema kinyumbani, kwa sababu tutakuwa tumewasaidia watoto wa Kitanzania kuweza kupata ajira. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kampuni hii ninayoizungumza annual tan over yake kwa Uingereza ni karibia bilioni 160. Mtanzania huyu ameajiri watu wengi na tulipokutana alitwambia anashindwa kuwachukua Watanzania kwa sababu wanakosa hata hela za kulipa tiketi ya ndege.
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naomba nimalize kwa kuwaomba wananchi wa Uyole huko Mbeya, chonde chonde wananchi wa Uyole, tunawaomba sisi Wabunge wote, Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi na Wabunge kutoka vyama rafiki vya upinzani, Spika huyu ambaye ni dada yenu kutoka huko Mbeya na sisi ni dada yetu, amefanya mambo makubwa kwa Bunge, amefanya mambo makubwa kwa nchi. Chonde chonde Wana-Uyole, turudishieni dada yetu. Tunawapa kila kitu kinachostahili katika mustakabali wa maendeleo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nakushukuru sana. Wana-Uyole wamenisikia, tunaomba waturudishie wewe. Sisi tuna kazi na wewe kwa miaka mitano ijayo, ahsante sana. (Makofi)