Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Iringa Mjini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na ninaomba kuchangia katika Wizara yetu hii ya Utamaduni. Niwapongeze kwa ajili ya mafanikio ambayo yamefanyika katika Wizara hii. Kwa ajili ya maslahi ya muda nitaomba niendee moja kwa moja kwenye hoja zangu tatu.
Mheshimiwa Naibu Spika, hoja ya kwanza itakuwa katika kuendeleza sana katika nchi yetu ikiwepo umuhimu wa viwanja tunaomba sana Wizara hii iweke msisitizo kwenye kusimamia masuala ya viwanja vya michezo nchini. Kuna mwamko mkubwa wa watu kufanya michezo lakini ukiingia kwenye viwanja vyetu vingi bado havipo kwenye menejimenti ya kuweza kuruhusu watu kufanya michezo ukiwepo Uwanja wetu wa Taifa. Tunaomba sana hii tabia ya kwamba Uwanja wa Taifa umefungiwa inaonekana hatuna menejimenti nzuri sana katika kuendesha ule uwanja wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kama ni hivyo itafutwe menejimenti ya uhakika kama ni vipi basi waweze kuona wanaongea vipi na sekta binafsi kuona namna gani tunafanya menejimenti, lakini kushirikiana na wale ambao wana viwanja katika Taifa letu ili kuona viwanja vile vinakuwa active kwa ajili ya ku-accommodate michezo katika nchi yetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, pale Iringa tuna Uwanja wa Samora pia mna maandalizi ya AFCON sasa. Tuna uwanja mzuri sana na lile ni lango la utalii Kusini. Tunawaomba kwa kuwa Kamati imetoa mapendekezo kwamba waangalie na viwanja vingine wanavyoweza kuviendeleza, basi tunawakaribisha sana Iringa na watu wakija pale wataweza kutembelea vivutio mbalimbali vya Mikoa 10 ya Nyanda za Juu Kusini ikiwepo Ruaha National Park. Sisi tumejiandaa vizuri uwanja wa ndege upo tayari, ndege kubwa zinatua pale vyakula vipo vya kila aina na ambavyo huwezi kuvipata sehemu nyingine katika Tanzania. Kwa hiyo, karibuni sana Iringa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ambalo nilitaka niliongelee ni kuhusiana na masuala ya utamaduni na kabla sijaenda utamaduni, ninaomba niongelee Kiswahili. Mheshimiwa Khadija ameongea, tunaomba sana Mheshimiwa Waziri umesema hatuwezi kukikuza Kiswahili bila kuangalia changamoto tatu: kubagaza, kubananga na kufubaza Kiswahili, lakini inaonesha kabisa kwamba katika ufubazaji huo, ubanangaji huo na ubagazaji huo inawezekana hata kabisa hata Baraza letu la BAKITA linabagaza kwa kutupa maneno magumu magumu ambayo hatuyaelewi. Yaani unaamua kutengeneza neno, kwa mfano, kishikwambi yaani mpaka mtu aje alewe apate coordination ya hilo neno na kile kinachoongelewa inachukua muda sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ukitaka kuja kuongelea maneno mengi kwa mfano; humu kuna maneno mengi wameyatumia, ‘kongoo’ vitu kama hivi yaani unakuta ni vigumu. Mheshimiwa Khadija ameelezea vizuri sana, wakati kuna maneno mazuri au laini tu. Kwa mfano, unaniambia Akili Mnemba, hasa mimi nikianza kuanza kutafuta lile neno mnemba na correlation ya artificial silipati. Kwa nini, usiniambie Akili Bandia, kirahisi? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba sana uwepo mjadala wa Kitaifa kukubaliana kama singeli itakuwa ndiyo mchezo au utamaduni wa Taifa letu kwa nyimbo zake, maneno yake, uvaaji wake na uchezaji wake. Je, tutakubaliana? Kwa kuwa ni suala la Kitaifa basi ni vizuri tukubaliane kwa pamoja tunakubaliana kwa pamoja, tunakubaliana singeli ndiyo ituwakilishe Watanzania? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, juzi nilituma kitu fulani kwenye group la Wabunge jinsi michezo ile inavyochezwa wakati mwingine; kama Wizara ndiyo wasimamizi basi mwone namna ya kudhibiti na nidhamu maneno yanayotamkwa na uchezaji wake. Nilituma juzi kitu ambacho siyo kizuri kwenye group, lakini watu wamebanwa na utamaduni wana mihemko, wanacheza hiyo singeli wapo uchi, wananing’inia kwenye daladala wanacheza uchi, lakini wakienda kucheza, kwenye kuvaa kwenye matamasha mbalimbali wanavaa nguo nyingine ambazo zinaonesha kabisa. Sasa tukubaliane kama tunakubaliana kama Watanzania ile ndio representation yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa ni suala la Kitaifa tusikubaliane kirahisi wamesema watafanya Tamasha la Kitaifa la Utamaduni huko ndiko wakatoe namna gani Watanzania watakuwa represented…
MHE. TASKA R. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, Taarifa.
NAIBU SPIKA: Taarifa.
TAARIFA
MHE. TASKA R. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kumpa taarifa Mzungumzaji kwamba hatujaona Kamati iliyokaa kupitisha singeli kama ndiyo ngoma inayowakilisha Tanzania. ahsante. (Makofi)
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Jesca, haichezwi kwenye daladala na hicho ulichokiona wala sicho, umeona kitu kingine na wala hawavui nguo. Ni mchezo ambao unaburudisha na hasa kwa watu wa Pwani. Kwa hiyo, haya mambo uliyoyaona, sitaki kutaja ni nani, kwa sababu sitaki kuwa implicated, lakini singeli haina kabisa mambo hayo na muda wako umekwisha vilevile.
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, Kiti chako ni kikubwa sana, sasa siwezi kusema chochote kwenye hilo.
NAIBU SPIKA: Muda wako umekwisha vilevile.
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye opinion yako, lakini kwa kuwa nilikuwa nimepewa taarifa, ninaomba niikubali taarifa Mheshimiwa Taska Mbogo, lakini ya kwako ibaki imeelea hivyohivyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba tukubaliane tutafute mjadala wa Kitaifa kukubaliana kama singeli itatu-represent. Ahsante. (Makofi)