Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Priscus Jacob Tarimo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. PRISCUS J. TARIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru kwa nafasi hii ya kuchangia hotuba hii ya Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, tena wa kwanza kabisa mchana huu. Nichukue nafasi ya kipekee kabisa kuwapongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri ambaye ni mchezaji wangu ndiyo mambo yanavyokwenda, ni captain wake wa basketball, lakini pia Katibu Mkuu pamoja na timu nzima. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nina section mbili; kwanza nina maombi ambayo nimeshayawasilisha formally, lakini ni vizuri yawe registered hapa. Kwenye hili suala la AFCON. Sisi Moshi Mjini ndiyo tumeshikana na Arusha na inajengwa stadium kwa ajili ya michezo yenyewe. Sasa viwanja vya mazoezi kwa kudodosa nasikia vinatakiwa vijengwe kama vitano,

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nimeleta ombi hili formally, nilishamwomba Mheshimiwa Waziri aliyepita alipokuja kwenye Kili-Marathon mwaka 2024, lakini nilimwomba Mheshimiwa Waziri wa sasa mwaka huu 2025 tukaenda kulitembelea eneo la Memorial ambalo lina hekta 50, kuwaomba sasa ili kugawanya haya manufaa ya michezo au manufaa ya AFCON basi na Moshi Mjini ambapo ni kilomita 75/80 hivi kutoka pale Arusha, lakini iwe pia ni mwanzo wa kuboresha michezo kwenye Mkoa wa Kilimanjaro hasa pale Moshi Mjini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hili la kwanza ni ombi pale Memorial Stadium, lakini pia kwa sababu tuna facility zote, hotel za kitalii zipo za kutosha kwenye Mkoa wa Kilimanjaro, tuna uwanja wa ndege ni karibu, lakini ukivuka tu barabara kuna uwanja wa gofu, kwa hiyo, ninaomba hilo ombi la kwanza kwamba, katika vile viwanja kwa ajili ya mazoezi basi watuangalie sana pale Moshi Mjini – King George Memorial Stadium.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la pili, ni uwanja wa kwanza wa gofu Tanzania ni Moshi Club, ambao upo Moshi Mjini. Huu uwanja ulijengwa tangu mwaka 1920. Nilikuwa naomba na hili, najua Wizara wameshaanza kuangalia namna ya kuboresha na kuhakikisha kwamba unalindwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, niendelee kuwaomba kwa sababu Mheshimiwa Waziri wewe ni encyclopedia inayotembea. Sasa uwanja wa kwanza wa gofu ni ule wa Moshi Club wa mwaka 1920. Ni vizuri uangaliwe kwa upekee yaani tusiachie tu members, hata wakiwa wachache wakishindwa ku-maintain ushindwe kuendelea kutunzwa. Ni mashimo 18, ni uwanja mkubwa upo located sehemu nzuri, kwa hiyo, ninaomba pia hilo mlipokee.

Mheshimiwa Naibu Spika, ombi la tatu, nilishalileta tena huko nyuma kwamba, ni vizuri tuhakikishe sasa hii michezo tunaisogeza yote kwa pamoja. Riadha Tanzania hatujawahi kuwa nyuma sana, tumeshaonekana sana hasa kwenye marathon; na hata juzi Boston Marathon tuliwakilishwa vizuri sana na Simbu.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nilishaleta ombi kwamba ni vizuri tuangalie sehemu za kujenga zile kambi za wanariadha kama ilivyo ile Iten kule Kenya Home of Champions. Kule West Kilimanjaro kwa sababu wanapenda sehemu ya high altitude ni sehemu nzuri sana ya kutuingizia kipato. Pia kwa sababu tukishakuwa na zile kambi tunaweza tukawapa sekta binafsi wakaja wakajenga, maeneo ambayo ni suitable.

Mheshimiwa Naibu Spika, kule West Kilimanjaro ni eneo zuri, lakini pia maeneo ya Karatu, na Rift Valley lote ambayo ni maeneo ya high attitude, unaweka ile kambi hata kujenga hayo mabweni tusijenge kwa sababu watu wanavyokuja wanalipa fee, ila watu waende wanalipa halafu wana-train.

Mheshimiwa Naibu Spika, kule Kenya ipo hiyo Iten tunaweza kwenda kuitembelea halafu tukapata namna ya kukuza huu mchezo wa riadha. Kwa upande mwingine tukawa tunaingiza kipato kwa watu kuja ku-train kule. Kwa hiyo, kambi za riadha West Kilimanjaro na maeneo yote ya Rift Valley. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nilishaongelea sana suala la kuunganisha michezo na utalii na hili linahitaji juhudi za makusudi kwamba ni lazima tuangalie namna ya kuviunganisha ili viweke tija. Kwa hiyo, sababu ya muda, napenda kuendelea kushauri sana tuangalie namna ya kuviunganisha hata kwa kutumia desk la michezo pale kwenye Wizara ya Utalii.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru sana, ni mchango wangu huo. Ninaunga mkono hoja. (Makofi)