Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. ZULFA MMAKA OMAR: Mheshimiwa Spika, awali ya yote nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kunifikisha leo nikiwa mzima.
Mheshimiwa Spika, pili, nampongeza Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa anayoendelea nayo kwa kujenga nchi, kwa kweli Tanzania ya Mama Samia ni ya maendeleo makubwa sana.
Mheshimiwa Spika, nianze kuipongeza Serikali kwa kutoa fursa katika kampuni binafsi kuweza kuwekeza katika vivuko vya kwenda Kigamboni kwani jambo hili limesaidia sana kupunguza changamoto ya usafiri kwa wananchi wanaoishi huko na wale wanaoenda kwa matembezi. Pili, hili linaenda kuwashawishi wawekezaji kuweza kwenda kuwekeza huko bila ya hofu ya miundombinu.
Mheshimiwa Spika, pia nampongeza Rais kwa kuweza kujenga madaraja mbalimbali katika nchi yetu, kwani madaraja haya yanaunganisha watu kuweza kuvuka na kuvusha biashara mbalimbali kutoka nchini kwetu na kupeleka nchi Jirani. Pia nitoe pongezi kwa kumalizwa Daraja la Kigongo - Busisi kwani madaraja haya yatazidisha chachu ya maendeleo nchini.
Mheshimiwa Spika, mwisho naunga mkono hoja hii.