Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Mariamu Nassoro Kisangi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Spika, naomba kuongezea mchango wangu wa kuzungumza nikianza na TBA; nawapongeza kwa kazi kubwa wanazofanya, lakini naomba Mradi wa Temeke Mwisho utengewe fedha na ukamilike.

Mheshimiwa Spika, Temeke ni Wilaya ambayo hakuna nyumba nyingi za watumishi, hivyo tunatamani kuona nyumba zile zimekamilika. Rai yangu pamoja na juhudi za Serikali za kutafuta sekta binafsi kuungana na TBA, lakini wasitupandishie gharama za nyumba kwa kuwa mara nyingi sekta binafsi wanaangalia faida zaidi bila kujali hali za wananchi wetu/watumishi wetu.

Mheshimiwa Spika, ndani ya mradi wa ujenzi wa nyumba za TBA kuna Shule ya Msingi Mji Mpya ambayo ina mazingira magumu sana, haiwezi kuendelezwa, je, Serikali hawaoni umuhimu wa kusaidia kuendeleza shule hiyo kama sehemu ya mradi huo? Kwa sababu watakaokuja kuishi pale nao watakuwa na familia zao.

Mheshimiwa Spika, ninaunga mkono hoja.