Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Spika, nianze kwa kuunga mkono hoja iliyoko Mezani.

Mheshimiwa Spika, naomba kuishauri Serikali, pamoja na kazi kubwa ambayo Serikali imefanya katika kuunganisha miundombinu ya barabara mkoa kwa mkoa na wilaya kwa wilaya katika mikoa mingi.

Mheshimiwa Spika, ninaomba Serikali ikamilishe miradi ambayo haijakamilika kwa muda mrefu. Changamoto kubwa ni kuwa wakandarasi wanapewa kazi na pesa hazitolewi kwa wakati. Naomba nitolee mfano barabara chache za Mkoa wa Mwanza ambazo moja ni ya tangu mwaka 2017 hadi leo kilometa 18.2 ambayo ina miaka tisa haijakamilika.

Mheshimiwa Spika, kwanza, Barabara ya Nyakato VETA - Buswelu - Igombe TX kilometa 18.2 tangu mwaka 2017 haijakamilika (Wilaya ya Ilemela). Pili, Barabara ya Airport - Igombe - Kayenze - Nyanguge kilometa 46 (ujenzi kilometa 10 na haujaanza tangu mwaka 2023/2024 (Wilaya ya Ilemela); na tatu, Isangula (Magu) - Ngudu (Kwimba) kilometa 50 (ujenzi kilometa 10).

Mheshimiwa Spika, nne, Mwamanga - Misasi - Salawe (Wilaya ya Misungwi) - Kahama (Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga) kilometa 150 (ujenzi kilometa tatu); tano, Ngudu - Jojilo - Mabuki (Wilaya ya Kwimba) kilometa 28 (ujenzi kilometa tatu); sita, Kamanga - Katunguru - Sengerema (Wilaya ya Sengerema) kilometa 32 (ujenzi kilometa tatu); saba, Bukoba - Nyakalilo kilometa 7.8 (ujenzi kilometa tatu); na nane, Nansio - Rugenzi kilometa 11 (ujenzi kilometa saba).

Mheshimiwa Spika, barabara ya pili hadi ya nane zabuni zake ni tangu mwaka 2023/2024, lakini kazi bado hazijafanyika. Aidha, kilometa zinazopangwa kujengwa, kwa nini ni kilometa chache tu zinapangwa kujengwa na bado hazijengwi?

Mheshimiwa Spika, hoja yangu kwa Serikali, kilometa ni chache sana ambako barabara hizi zimeelekezwa ujenzi ukamilike kabla haijatoa zabuni nyingine ili kumaliza hivi viporo.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja kwa kusisitiza ukamilishaji wa barabara hizi.