Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Shabani Omari Shekilindi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lushoto

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nimpongeze Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutuletea miradi mingi katika jimbo letu la Lushoto. Wananchi wa Lushoto wanaendelea kumwombea dua na Mwenyezi Mungu ampe siha na afya njema ili aendelee kuwatumikia Watanzania.

Mheshimiwa Spika, Jimbo la Lushoto lina kilometa 52 ambazo zinahudumiwa na TANROADS na kilometa zote 52 ni za changarawe na barabara hizi zina changamoto hasa wakati wa mvua zimekuwa hazipitiki na barabara hii kila mwaka ninaisemea. Kwa hiyo, naiomba Serikali katika kipindi hiki cha bajeti iweze kupatiwa bajeti ili zianzwe kutengenezwa kwa kiwango cha lami. Kilometa 34 zimeanzia Mkuzi hadi Mlola na kilometa 18 zimeanzia Nyasa kupitia Gare hadi Magamba.

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali iniangalie kwa jicho la kipekee na la huruma iweze kujengwa kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.