Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira

Hon. Dr. Immaculate Sware Semesi

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Nitatoa mchango wangu katika sekta ya mazingira katika Wizara hii, ningependa tu tukumbushane na kusisitiza kwamba mazingira ni suala mtambuka, mazingira ni uhai, mazingira ni kila kitu. Mazingira haya ni ardhi, ni hewa, ni maji, ni kila kitu ambacho kinatufanya sisi kama Watanzania tuishi au kama binadamu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, inasikitisha kwamba mazingira ukiangalia kwenye mfumo mzima wa Wizara zote hizi tulizonazo hata ukiangalia katika bajeti kipaumbele chake kipo kidogo sana. Hii iko dhahiri kabisa hata kwenye masuala ya maendeleo bajeti ya maendeleo ilivyo finyu au mfuko wetu wa maendeleo ulivyofinywa, hii inachanganya kidogo. Sasa hatuwezi kukuza sekta za kiuchumi au za kijamii tukiweka mazingira kando.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia suala la ardhi, ardhi tunaitumiaje katika masuala ya madini, ukulima, ufugaji, kila kitu kinatoka ardhini lakini ardhi yetu ukiangalia kwa Tanzania karibu asilimia 61 ya ardhi yote ina mmomonyoko wa udongo, hali ya ardhi ni duni. Sasa kama una ardhi duni ina maana hata misitu haifanyi vizuri, mazao hayafanyi vizuri, na hii hali inaendelea namna hii na hatuna mipango mikakati au madhubuti ambayo iko-reflected kwenye bajeti ya kutunza ardhi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia kwenye masuala ya bahari na mambo ya mwambao, bahari yetu ina matumbai karibu ukubwa wa hekari 3,580 za mraba, tuna misitu katika mwambao wetu yenye karibu hekari 70,000 inakatwa hovyo, matumbai yanapigwa mabomu kwenye uvuvi wa haramu tunaharibu mazingira. Effect yake tunakuja kuiona pale tunapoharibu mazingira baharini na misitu ya mwambao, hii yote inakuja kuleta madhara kwenye hali ya hewa. Tunaongelea mafuriko, tunaongelea mabadiliko ya tabianchi, hii inatokana na sisi kuharibu mazingira yetu ya baharini na hata kwenye ardhi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nigusie suala la misitu nchini kwetu. Kuna uvunaji holela na ukataji wa holela na uuzaji holela wa misitu. Misitu ndiyo hii inayofanya tupate maji kiasi gani au hali ya hewa iendeleeje, kwa hiyo kunahitajika kuonesha reflection kwamba kuna haja ya kutunza mazingira ukiangalia hasa katika sekta ya misitu. Mfano Tanzania tunapoteza karibu hekari laki tatu na sabini kwa ukataji holela wa misitu, je, tunai-replace vipi? Mikakati madhubuti hatuioni ikiwa reflected kwenye sekta hii ya mazingira. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili nataka niligusie kwa urefu kidogo na hili ni kuhusu usimamizi wa taka, taka ngumu, taka kwenye maji na taka za kielektroniki. Kwa mfano, Mji wetu wa Dar es Salaam una-potential ya kuwa mji popular duniani ni mzuri na wenye kuvutia, lakini takwimu na information za mwaka 2010 inaonyesha Mji wa Dar es Salaam umeshika namba nane dunia nzima kwa uchafu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuangalii tu mandhari ya uchafu lakini zile impact na effects zinazoletwa na uchafu. Kwanza ni magonjwa, karibu asilimia 80 hapa nchini kwetu hatuna mfumo mzuri wa ukusanyaji wa taka na kuzitenga zile taka. Taka ngumu, taka ambazo haziwi degraded biologically, zote zinachanganywa na ukiangalia kwa Mji mkubwa kama Dar es Salaam ambao unaongoza kwa idadi ya watu tuna sehemu moja tu ya dumping site- Pugu ambayo ina eneo karibu la hekta 75.
Mheshimiwa Mwenyekiti, zile takataka zinazotupwa kule Pugu jinsi ambavyo zinakuwa treated haziendani sawasawa na utunzaji wa mazingira. Zinatupwa, hamna mechanism maalum ya kuzuia uchafu ule wenye sumu usisambae katika mifumo ya maji, hakuna njia ya kuzuia kwamba unapochoma moto ule moshi una madhara gani kwenye hali ya hewa na hata kwenye afya za binadamu. Kwa hiyo, kunahitajika kuwe na mfumo madhubuti wa kuchanganua taka na jinsi ya kuzi-treat hizo taka. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi tuna vifaa vya simu, tuna computer, fridge, television, lakini hakuna mfumo madhubuti wa kuhakikisha kwamba taka za aina hii ya elektroniki zinatunzwaje au zinatolewaje katika mazingira ili zisilete madhara yoyote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitagusia pia kwenye Mfuko wa Mazingira. Tumejiwekea mkakati, tumeweka mfumo mzuri lakini kwa bahati mbaya hatujawa serious au makini na mfuko huu. Ni kwa sababu pia hatuja-reflect umuhimu wa kutunza mazingira na kusimamia mazingira. Sasa hivi Serikali yetu tunataka kuwa na mfumo wa viwanda lakini huoni ile link ya hii system mpya kwamba tuwe na mfumo wa viwanda au uchumi wa viwanda ina-link vipi na mazingira. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu hatujajua au hatujachanganua kwamba hivi viwanda vinatumia rasilimali gani na rasilimali hizi tunazozivuna na zinazoenda kuwa treated huko kwenye viwanda zitakuwa zina effect gani kwenye mazingira. Mfuko huu hauna fedha, kwa mfano kwenye kitabu hiki cha maendeleo ya bajeti, zimetengwa milioni mia tatu tu na chenji, utafanya nini na milioni mia tatu kwenye suala la mazingira ambalo ni mtambuka? Je, mta- address nini? Issues za hewa, za maji, za ardhi au issues zinazotokana na uharibifu wa mazingira kutokana na viwanda. Je, mikakati ni ipi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfuko huu unaweza ukawa na sources nyingi za kujipatia fedha, mfano TRA wanavyoweka extra charges kwenye magari chakavu au yaliyozeeka na kadhalika hela hizi zinatumikaje? Kwa hiyo, kuna umuhimu wa Serikali kuweka kipaumbele kwenye mfuko huu kwa ajili ya utunzaji wa mazingira na usimamizi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna National Environment Action Plan yetu ya 2013-2018. Hii imekaa kimaandishi tu lakini action plan yetu hii haina budget line na haina indicators au indicators zilizopo ni chache. Hii inaonesha dhahiri kwamba hatujawa waangalifu au hatuoni uthamani wa mazingira, mazingira ambayo yanayotufanya tuwe tumesimama hapa tukiwa tuna afya. Kwa hiyo, naomba hili liangaliwe upya. (Makofi)
Mheshimwa Mwenyekiti, kuna msemo ambao unasema kwamba kama huna information au data then huna right ya kuongea. Sasa ukiangalia research ambayo inasimamiwa na taasisi yetu ya NEMC haina hela ya kufanya tafiti. Sasa tunapokaa tunasema kwamba kuna mafuriko, kuna mabadiliko ya tabianchi, hali ya hewa haieleweki, mvua za masika hazieleweki, hatuwezi kusema kwa confidence, tunakuwa tu tunahisi au tunafikiria itakuwa hivyo lakini hatuna data ambazo zina back up kwamba hali ya hewa inakuwaje, ardhi yetu tuitumiaje, sasa tutafanyaje hizi kazi kama NEMC haipewi hela ya research? Yote yanakuwa batili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niishie hapo kwa kusisitiza kwamba, mazingira ndiyo yanayoshika rasilimali zetu tunazotumia, natural resources, tusiidharau, tutazidi kulalamika kwamba hakuna maendeleo endelevu kwa sababu kutwa tunaharibu mazingira yetu na mazingira yetu hatuyatunzi wala hatuyapi kipaumbele katika kuyafanyia research, katika ku-disseminate hiyo information, awareness raising haipo wala usimamizi wake ambayo iko reflected kwenye bajeti haupo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni hayo, nashukuru.