Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tumbatu
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kukupongeza na kukushukuru wewe kwa kunipatia nafasi hii kutoa mchango wangu katika Wizara hii. Aidha, nampongeza Mheshimiwa Waziri wa Wizara hii pamoja na watendaji wake wote kwa utayari wa kuiwasilisha hotuba hii kwa umakini mkubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ni Idara ya Utalii. Sekta ya utalii ni sekta muhimu sana ulimwenguni. Azma ya kuendeleza utalii ni jambo jema angalau litatoa ajira za moja kwa moja na zile zisizo za moja kwa moja. Naiomba Serikali ichukue juhudi rasmi za kusimamia idara hii badala ya kuziachia sekta za wananchi jambo ambalo si zuri. Serikali iendelee kuwaelimisha wananchi na kuwahamasisha wajione kuwa ni sekta yenye manufaa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Serikali iweke ushawishi maalum kuwashauri watalii kutembelea sehemu zote za Muungano. Hivi sasa kumekuwa na mtindo ambao sio mzuri wa watalii ambao wanatembelea maeneo ya Bara kuishia huku tu, jambo ambalo linawanyima fursa Wazanzibar kuonesha vivutio vyao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ni mafunzo kwa Idara za Wizara hii. Wizara hii ina idara nyingi ambazo ni muhimu katika kuiendeleza Wizara. Kumekuwa na mtindo ambao si wa kuridhisha sana juu ya kuwapatia mafunzo wafanyakazi wa idara hizo. Mara nyingi nafasi za kujifunza zinapotoka huwa zinachukuliwa na viongozi na kuwaacha wafanyakazi wa chini ambao wao ndio wazalishaji wakubwa.
Naiomba Wizara kurekebisha mwenendo huu na kuweka mpango maalum (training program) ili wafanyakazi wa ngazi za chini nao wapate mafunzo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.