Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Welezo
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua fursa hii kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri ambayo ameanza na anaendelea kuifanya. Vile vile pongezi kwa Waziri Mkuu na Mawaziri wake kwa kumsaidia Mheshimiwa Rais kutekeleza majukumu yake. Naomba kutoa mchango wangu kwenye hotuba hii kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Utalii; nimefurahishwa na kupata moyo kwa hatua ambazo Serikali itachukua kuimarisha utalli. Utalii ni sekta ambayo ina potential kubwa sana kwa uingizaji wa fedha za kigeni. Kwa upande wa Zanzibar, Sekta hii ni leading sector kwa mchango kwenye pato la Taifa. However, watalii wamekuwa wakilipia katika nchi zao na hivyo kukosesha pato kwa upande wa nchi. Uelewa mdogo wa changamoto hii kwa upande wa Kampuni za Kitalii kwa hapa nyumbani, umesababisha tabia hii kuendelea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati ambao utaandaliwa uhakikishe kwa kiwango kikubwa unashirikisha Makampuni ya Kitalii ya hapa nyumbani kuzungumzia changamoto hii na utatuzi wake. Vile vile kwa kuwa Zanzibar inategemea sana utalii, mkakati ushirikishe wadau wa Zanzibar kwa kiwango kikubwa cha majadiliano.
Mheshimiwa Mwenyekiti, UKIMWI; wakati tukiwa kwenye Kamati, imeonekana bajeti nyingi zimeweka eneo la mkakati wa kudhibiti UKIMWI, kama ni eneo ambalo linasubiri fedha kutoka kwa wafadhili. Hii ni hatari, afya za wananchi na matibabu yake, hayawezi kuwekwa katika mikono ya wafadhili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu ni kwamba, kwenye activities zetu ambazo tunazifadhili kwa fedha yetu ya ndani, issues za HIV/AIDS, Women, Climate change and environment, ziwe mainstreamed humo. Tusisubiri hadi fedha za wafadhili zifike.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Ukusanyaji wa Mapato; eneo hili ni gumu na lina changamoto nyingi, hata hivyo pongezi kwa Serikali kwa kulipa mtazamo maalum suala la ukusanyaji wa mapato. Matumizi ya mashine ya electronics (EFDs) ziambatane na mafunzo ya watu wetu katika matumizi hayo, hususan kwenye Halmashauri zetu. Eneo hili la ukusanyaji wa mapato ni eneo gumu sana, lakini ni muhimu kuliko yote. Maendeleo yetu bila ya mapato yatokanayo na vyanzo vyetu vya ndani yatakuwa ni magumu mno.
Mheshimiwa Mwenyekiti, approach ya utoaji wa elimu ibadilike now, ijielekeze sana kwa wananchi ili waelewe umuhimu wa ulipaji kodi kwa Serikali kwa kudai risiti wanaponunua bidhaa mbalimbali. Changamoto hii ikitatuliwa tunaweza kufika mbali zaidi. Vyombo vya habari vya Serikali na binafsi vione umuhimu wa jambo hili. Aidha, katika bidhaa za mafuta tuangalie jinsi gani tunaweza kupata fedha kwa kuongeza angalau shilingi mia ili tupate fedha ziingie katika Mifuko ya Maji na REA kama ilivyopangwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti,Viwanda; dhamira hii ni nzuri katika ujenzi wa Taifa na kiuchumi. Hata hivyo, viwanda vitakavyojengwa vitumie rasilimali zinazopatikana kwa wingi nchini ikiwemo rasilimali watu.
Mheshimiwa Mwenyekiti,karafuu ya Zanzibar ingepata viwanda vinavyohitaji, tuna hakika Zanzibar ingepata tija kubwa kuliko inavyopata hivi sasa. Liangaliwe hili kwa mapana yake.
Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja.