Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 - Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa

Hon. Fakharia Shomar Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 - Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa
Mwenyekiti, ahsante. Kwanza sina budi kumshukuru Mheshimiwa Spika, Naibu Spika na Wenyeviti wote wa Bunge kwa kazi nzuri mnayoifanya humu ndani ya Bunge, kwa uweledi mliokuwa nao na kazi nzuri iliyotukuka, lazima mpongezwe.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sina budi kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Watendaji wake kwa kazi aliyotuletea hapa ametufahamisha, tumeelewa, lakini wenzetu wa upande wa pili walikuja na kashfa hawakuja na maelezo ya kuujulisha umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sina budi kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa sababu Zanzibar iko kwenye hali ya amani na utulivu, kuanzia uchaguzi uliofanywa wa marudio walikuwepo Wanajeshi wakaweza kuiweka hali ya salama na utulivu na hadi leo hali hiyo inaendelea ya usalama na utulivu, tunashukuru.

Mheshimiwa
Mwenyekiti, ahsante. Taarifa yake siipokei kwa sababu ilikuwa ishara tayari walishaonesha upande wa pili na walioweza kutuliza ni Jeshi waliofanya kazi na tukaenda kwa amani na utulivu. Polisi walikuwepo wakifanya shughuli zao na wao walikuwa wakiangalia amani na utulivu wa nchi yetu na hadi hii leo tunaendelea kuwa na amani na utulivu katika nchi yetu.

Mheshimiwa
Mwenyekiti, ahsante, nilindie muda wangu. Naomba kuzungumzia habari ya viwango vidogo vya pensheni wanavyolipwa askari wastaafu wa zamani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kila siku tunavyokwenda hali ya maisha inapanda na siku zinavyokwenda mishahara inapanda, lakini wale wastaafu wa zamani kiwango kinakuwa kiko kile kile, ambapo hakiongezeki. Sasa ningemwomba Mheshimiwa Waziri awe anaangalia, baada ya muda na wale askari wastaafu wa zamani viangaliwe viwango vyao. Kama kuna Koplo/Sajenti/Luteni Kanali wa sasa kastaafu basi na wale kiwango kile kile kwa mwaka ule waweze kuwapa wasiwaachie kile kiwango duni ambacho wanacho na kinaweza kuwapa maradhi, labda akapata sukari, pressure matumizi yake yatakuwa madogo wakati matumizi yako juu na yamepanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuja na suala lingine la JKT. JKT Mheshimiwa Waziri kaizungumza katika ukurasa wa
26 na amezungumza vizuri, tunakupongeza. Lakini ningekuomba Mheshimiwa Waziri idadi ya vijana wa Zanzibar wanaokwenda JKT utuongezee. Kwa sababu umesema kule wanapata elimu ya ukakamavu, elimu ya kujiajiri na elimu ya kuajiri wenzi wao. Sasa ukituongezea idadi ya vijana wetu wakaenda kule wakarejea tena kufanya kazi hiyo ya kwenda kujiajiri, wakawa wakakamavu watapata ajira nyingi za ukakamavu, watapata kujiajiri wao na wenzi wao. Naomba Mheshimiwa Waziri ulipokee ili uweze kutusaidia kwa upande wa Zanzibar. (Makofi)


Mheshimiwa Mwenyekiti, nazungumzia eneo la mambo ya kuingiliana baina ya majeshi na raia mitaani. Kuna maeneo kimazingira ni magumu, kuna maeneo ambayo wanayo jeshi lakini maeneo yale yalikuwa ya raia hapo wakati wa mabibi na mababu zetu, lakini jeshi sasa hivi imehodhi. Watu wa pale ilikuwa inabidi walipwe kwa kutoa viwanja vyao lakini huwa hawalipwi hivyo kunakuwa na mvutano baina ya raia na Jeshi. Sasa liangalie hili na kwa upande wenyewe tuangalie, kama upande wa Unguja Ukuu, Kisakasaka matatizo hayo yapo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuna mengine, wanajeshi wanawalipa raia, lakini baada ya kuwalipa raia hawaondoki sehemu ile na ninyi mnakuwa hamna uthibiti wa kuyazuia yale maeneo yenu; sasa kunakuwa mvutano mwingine mpya. Utayakuta haya kama kule Dunga, Mgeni Haji, sasa na hayo myaangalie. Kama mtu mmeshamlipa aondoke, kama hamjawalipa na wamekubali kuondoka itabadi muwalipe ili kuweka amani na utulivu uliokuwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo ya Jeshi lazima mfanye utafiti kwa sababu hivi sasa maeneo ya Jeshi yameshaingiliana na ya raia. Bila kufanya utafiti mkaweza kujua sehemu zenu ziko wapi na za raia ziko wapi hapo mwisho kutazuka mtafaruku baina ya Jeshi na raia. Mimi ninajua Ninyi Wanajeshi ni wasikivu, walinzi na pia mnawapenda raia wenu. Sasa naomba Mheshimiwa Waziri na hili mliangalie ili kuondoa mtafaruku. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hayo machache naunga mkono hoja, sina matatizo.