Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Hon. Dr. Immaculate Sware Semesi

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa hii ya kutoa mchango wangu kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais na hoja yangu itakuwa upande wa Mazingira.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaanza kwa kutoa masikitiko yangu kuwa sekta hii ya mazingira imepewa kipaumbele cha chini sana, ukizingatia muda kwanza uliotengwa kujadili na hata sekta ya mazingira ilivyowekwa na Kamati ya Bunge imechanganywa na Viwanda na Biashara. Nataka tu nisisitizie umuhimu wa sekta hii ukiangalia hali ya nchi yetu ya Tanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania bado ni nchi maskini na tunategemea rasilimali tulizonazo ambazo ni mazingira katika sekta mbalimbali. Uvuvi huko kwenye maji, ukulima mashambani, ufugaji, yote haya ni mazingira. Ukiangalia Serikali kwa sasa mazingira imeipa priority ndogo sana, mfano tu mdogo, sasa hivi kuna harakati tukiongelea mazingira tunachokiona kwenye Vyombo vya Habari au harakati zinazoendelea ni kutoa warning kwenye viwanda au kufunga viwanda kwamba vinachafua mazingira ama tunasema kwamba tufanye usafi kwa kufagia au kupiga deki maeneo fulani. Kwa hiyo, hii concept nzima ya mazingira inakuwa sivyo inavyotakiwa iwe.
Mfano wa pili, kwenye mazingira ambavyo tumeipa priority ndogo sana na inashangaza, asilimia kubwa yetu, takribani asilimia 65 ya wananchi wa Tanzania ni wakulima. Ukulima uko wa aina gani? Ukulima huu uko katika kuvuna rasilimali au kupanda mazao kwenye haya maeneo, je, haya maeneo yanayolimwa yanafanya kazi vile inavyotakiwa kwenye kutunza mazingira ili huu ukulima wetu uwe endelevu?
Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia sekta ya mazingira pia katika shughuli za uvuvi, je hizi rasilimali tunazozichukua katika nchi yetu tunavuna vile inavyotakiwa? Sasa hivi kuna kesi kubwa sana mifano ya uvuvi haramu ambayo inaharibu hayo mazingira ya samaki. Hiyo ni mifano tu michache.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali yetu inaongelea kwamba, tunataka uchumi wa viwanda, lakini uchumi huu wa viwanda rasilimali zinatoka wapi? Ni kwenye haya haya mazingira. Hii ni sekta ambayo imeibeba nchi, lakini cha kushangaza ni sekta ambayo imepewa priority ndogo sana. Rasilimali zetu tunazitoa katika mazingira kwa nini hatuipi mazingira priority inayotakiwa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano mzuri ni katika hata hii Taasisi inayoshughulikia mazingira, National Environment Management Council (NEMC), imepewa bajeti kiasi gani ili kutekeleza majukumu ya kusimamia sera ya mazingira nchini, sifuri si ndiyo kwa mwaka huu wa bajeti? Je tutapitisha? Hilo ni suala la kuzingatia. Hapo nilikuwa naonesha tu umuhimu wa mazingira na jinsi ambavyo bahati mbaya hatujaipa sekta umuhimu katika nchi yetu vile inavyotakiwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza tu mifano michache kwa Wajumbe wengi ambao tupo humu ndani, tumepita njia ya Morogoro kufika hapa Dodoma. Katikati ya Morogoro na Dodoma nafikiri Wajumbe wengi wameona athari za mafuriko zilizotokea. Mfano mzuri ni Mto Mkondoa unao-flow kutoka Singida mpaka huko chini Morogoro, hapo katikati tunaona maeneo ya Kibaigwa wakazi wamepata madhara. Kuna reli ya kati eneo la Godegode, kila mwaka reli hii ya kati inatumia mamilioni ya pesa kurekebisaha na madhara ni nini? Ni kutokana na yale mafuriko yanayotokea katika Mto Mkondoa ambayo uharibu rasilimali hii muhimu ya nchi. Kwa hiyo, hela nyingi inatumika kugharamia hivyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano mwingine mzuri ni wale wananchi wanaoishi maeneo hayo, wanapata madhara makubwa. Wanapoteza mashamba yao, rasilimali zao nyingine zinaharibika, livelihoods zinakwisha, vyanzo vyao vya mapato pia vinaathirika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaanza lini kuchukulia umakini kwamba haya mafuriko tunayoyaona ni consequence ya kutokutunza mazingira kwa hali ya juu kwenye shughuli za kilimo au shughuli za mining, michanga inaingia kwenye mito, mito inakosa zile channel zake za asili, yanatapakaa maji all over the place. Mifano iko mingi hata kule Dar es Salaam, barabara ya Bagamoyo, maeneo ya Mbezi ni mafuriko maeneo ya Massana kila siku, kwa sababu ya miundombinu mibovu na mipango au mikakati ya kutunza hii mito haiko sawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano wa tatu ni Uvuvi. Uvuvi ni sekta muhimu sana ambayo bahati mbaya haitiliwi mkazo. Unapofanya uvuvi haramu, mfano wa kutumia mabomu, unaharibu rasilimali ya ile bahari, mazalia ya samaki. Hata hivyo, tukumbuke kwanza kule baharini, bahari siyo tu kwa ajili ya shughuli za uvuvi, bahari yenyewe ndiyo kiini ambacho kina-influence hali ya hewa. Sasa hivi tunaimba climate change, climate change. Climate change vyanzo ni vingi, mojawapo pia ni uharibifu wa sehemu kama za bahari. Namba mbili, hii climate change tunayolia na mafuriko tunayoyaona impact yake inazidishwa na kutotunza hayo mazingira. Mfano halisi ni hizi floods tunazoziona na kadhalika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nikibaki hapo kwenye mabadiliko ya tabianchi, mazingira yanagusa karibu sekta nyingi, kwenye mifugo, kwenye kilimo, kwenye uvuvi, kwenye mining na kadhalika, ukiangalia hata work plans za Wizara mbalimbali au Bajeti hamna kipengele kinachoonyesha kwamba hizi sekta mabalimbali zitakabiliana vipi na mabadiliko ya tabianchi, hamna bajeti, hatuna sera ya climate change, tuna strategy tu. Kwa mfano, ukiangalia huu Mkutano uliokwisha wa Climate Change Forum wa Paris, walichokubaliana, mbona hatujakiwekeza sisi katika nchi yetu?
Kwa hiyo, nafikiri ni muhimu sana kuangalia issue za mazingira kwa upana wake na umuhimu wake katika nchi yetu na katika uchumi wa nchi yetu. Tusiangalie tu kwa narrow set kwamba ni usafi, mazingira si usafi bali mazingira yamebeba kila kitu katika kila sekta ya nchi hii. Tunasema viwanda, rasilimali mnazozitumia viwandani zinatoka kwenye hayo mazingira au hata ukiangalia afya ya jamii inayohusika ambayo watafanya kazi kwenye hivyo viwanda au shughuli mbalimbali za uchumi, wasipokuwa na afya ya mwili na akili ambayo inakuwa influenced na mazingira, huwezi kuwa na Taifa imara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, issues za mazingira zinagusa kila Mtanzania, zinagusa issue za economy, zinagusa issue za afya, zinagusa issue za elimu, zinagusa sekta mbalimbali na hata nchi imeiona hii, lakini katika karatasi. Policies au sera katika environment zipo tu kwenye paper work lakini hatuoni katika utekelezaji. Naishauri Serikali iangalie tena kwa upya, iende ikaji-analyse kwa sababu tunatakiwa tu-report back kwa nchi nyingine ambazo zimekubaliana nazo nini tunakifanya kwenye kutunza mazingira na pia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni hayo tu kwa sasa. Ahsante.