Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2017/2018

Hon. Rev. Peter Simon Msigwa

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Iringa Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2017/2018

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi siwapongezi Wizara hii kwa sababu kwanza wanatimiza majukumu yao na pesa wanazozitumia ni kodi ya wananchi. Ila ninachoweza kusema Jimbo langu limekaa vizuri kwenye miundombinu ya maji na umeme tuko vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kusema kinachofanyika humu ndani ya Bunge ni sawa na baba ambaye anaenda sebuleni anajisaidia halafu watoto na mama wanamchachamalia kwamba atoe uchafu aliojisaidia sebuleni, halafu anapoutoa anasema mnishangilie nimefanya kazi kubwa. Hiki ndio kinachofanyika na nyie Wabunge wa Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka jana, Bunge la Kumi.......

TAARIFA ....

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Naibu Spika, Bunge la 10 wakati wa saga la Escrow tulikaa katika Bunge hili mpaka saa sita za usiku na Waheshimiwa Wabunge wote tulikubaliana kuhakikisha Mheshimiwa Profesa Muhongo na watu wengine waondolewe. Pamoja na Mheshimiwa Kigwangalla wote mnajua kwenye kumbukumbu alisema hajawahi kuona Profesa muongo kama Mheshimiwa Muhongo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Wabunge wa CCM na sisi hapa kwa wingi wetu wote mkapiga makofi mkashangilia Mheshimiwa Profesa Muhongo aondoke na kwa sababu, Mheshimiwa JK alikuwa anaheshimu maamuzi ya Bunge, Mheshimiwa Profesa Muhongo na wenzake waliondoka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, alivyokuja Mheshimiwa Magufuli, alivyoanza kuteuwa Baraza la Mawaziri hakujali kwamba Bunge liliona nini, lilifanya nini, akasema hapa kazi, mnamuonea wivu, namchagua Mheshimiwa Muhongo; mkapiga makofi mkasema jembeee! Huko ng’ambo huko, kwa sababu ya wingi wenu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, juzi baada ya huu mchanga amemtumbua, tena mnashangilia mnasema jembee! Ninyi, ninyi! Hebu tufike mahali tuone wajibu wetu wa Bunge ni nini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, amezungumza Mheshimiwa Tundu Lissu ambaye walau katika Bunge hili ana historia ya migodi na jinsi ambavyo watu wameonewa, amefungwa mpaka ndani na mikataba iliyowekwa. Kweli, amekuwa akitetea na hajaacha kutetea wachimbaji wadogo, lakini leo tunaanza kujitoa ufahamu! Wataalam wanasema when you are lost speed is useless; ukipotea spidi haina maana! Ukipotea unarudi unasoma ramani....

T A A R I F A ......

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Naibu Spika, this is just a joke, tunazungumza Bunge hatuzungumzi mambo ya Lowassa hapa. Tunazungumza Bunge na wajibu wa Bunge, na tunaowazungumzia humu ndani ni wale waliopewa madaraka ya kuongoza nchi hii. Leo mnajitoa ufahamu mnashangilia Magufuli utadhania ni Columbus anagundua kisiwa cha Australia huko bara la Australia. Anachokifanya Magufuli si kitu cha kwanza.

MWONGOZO.....

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba unitunzie muda wangu. Ninachokisema alichokifanya Mtukufu Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli si kipya, maana mnashangilia hapa utadhania ni Columbus amugundua Bara la Australia. Tume ya akina Maige hapa wapo akina Zito. Haya mambo waliyazungumza. Alipoingia Ikulu tulitegemea angeona mafaili, kitu gani kifanyike kuhusiana na matatizo ya tasnia hii na kwenye Baraza la Mawaziri naye alikuwepo. Sasa hapa mnabeba ngoma mnashangilia kama tumevumbua bara lingine wakati ni mambo yenu wenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ninyi CCM ni waungwana mngewaomba radhi Watanzania, kwamba tumechafua sebule. Sebule tumeiweka katika hali mbaya ya hewa tunawaomba radhi tumewakosea. Sasa mnazunguka hapa kwa mlango wa nyuma kama vile sisi wote ni watoto. Eti tumpongeze Mheshimiwa Rais, hii nchi ni ya wote. Siku zote mnasema hapa ndiyo!, iweje nchi ya wote hapa kwenye mambo yasiyokuwa na maana? Tunajitoa ufahamu, ndiyo. Tume ya akina Maige hawa walienda walizunguka nchi nyingi duniani na walilipwa hela nyingi sana Tume na wenzake walizunguka dunia mzima, sasa leo mnakuja hapa tumpongeza Mheshimiwa Rais na nataka niwaambie Watanzania, hizi lugha tunazozungumza hapa kuhusu investors unajua kuna mtu mwingine anadhani investors hawa wa madini wana–invest kama kibanda chako unachouza mkaa huko nyumbani.

Mheshimiwa Naibu Spika, wengi hapa mnazungumza kwa sababu hamjaenda kwenye migodi mkaona heavy investments walizoziweka kule ndani. Kwa hiyo si kitu cha dakika moja; unadhani kwamba unaweza ukawaambia toka leo ingia leo? It is a heavy, ni hela nyingi. Muwaulize wenzenu waliotangulia tulifanya nini kwenye Dowans tulivyojaribu kutaka kuwapeleka mahakamani. Mnasimama tu hapa mnasema tuwapeleke mahakamani, sawa tutaenda lakini hiki tunachocheza nacho hapa si kitu kidogo; na kuwapoteza investors si kitu kidogo. Hakuna mtu wa upinzani anayetaka tuibiwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi tunachozungumza ni juu ya method iliyotumika na namna ya kufanya haya mambo. Tumezungumza miaka mingi tangu wakati wa Mheshimiwa Rais Ally Hassan Mwinyi; kwamba watu wanaingia vibaya mkabisha na ndiyo tabia yenu. Tulivyokuja na suala la Katiba, likiwa linatoka kwetu mkalivamia mkashindwa kulimaliza; tulipokuja na suala elimu bure mkashindwa kulimaliza; tuliwaambia haya madini nayo mnakosea, narudia, narudia tena, When you are lost speed is useless; ukipotea huongezi accelerator, hukanyagi mafuta bali unasoma ramani na ramani pekee ambayo mngechukua ni ile ya Tume ya Bomani, soma anasema nini, ndicho ambacho tungetakiwa kukifanya ndugu zangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunawatukana wawezekaji kama vile invaders kama vile wametuvamia. Hawa watu tukiwaambia kesho tu wanaondoka. Leo tunawaambia wezi hii mikataba tumefanya wenyewe, Sheria tumetunga wenyewe, leo tunawaita wezi eti tumekamata makontena mia saba, kwani yameanza kusafiri leo? Vyombo vya usalama havikuwepo? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunachokisema sisi kama Watanzania mbinu mnayotumia si sahihi. Njia mnayotumia si sahihi kwa sababu inatuingiza chaka zaidi. Niwaombe kama Bunge, tunachotakiwa kufanya hapa ni kuiomba Serikali i-engage, tuingie kwenye majadiliano badala ya kufikia kwenda mahakamani. Kwa sababu nawa- guarantee, kama wakitupeleka Mahakamani we are going to lose big time, whether you like or not. Cha msingi Bunge tungetoa ushauri badala ya kuwafukuza investor na kuwatuna. Ma- investors wale wanaweka heavy money…

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Kama tumehongwa hela nyie mikataba mliingia wenyewe na mmeifanya hii nchi ya trial and error halafu leo mnasema eti tuwe wazalendo. Katika Bunge liloisha kuna mikataba mingi Sheria nyingi zimetungwa kwa hati ya dharura na hizi Sheria nyingi tumekuwa tukizipinga tukijaribu kuwashauri lakini huwa hamsikii. Niwaombe Waheshimiwa Wabunge hebu tuache kujitoa ufahamu. Wengi wenu hapa mnapiga kelele hata hiyo Sheria ya Madini hamjasoma, hamjui hata hiyo migodi, mmekuwa washangiliaji tu kama Mheshimiwa Tundu Lissu anavyosema mmekuwa washangiliaji hamjasoma hata Sheria unakuja hapa hufanyi research huwezi kuuliza maswali, wewe walichosema tu unashangilia shangilia tu hapa, hili ni Bunge la aina gani? Hebu tuache kujitoa ufahamu turudi kwenye nafasi, tuache kujitoa ufahamu; na wengi wenu mnapiga kelele tu kwenye majimbo yenu hakuna lami, maji, umeme mnatetea mambo ya ovyo tu. Tunachozungumza hapa tunazungumza mustabali wa Taifa letu siyo ushabiki. Siyo ushabiki wa kupiga piga makofi hujaletwa kupiga piga makofi hapa. Kasome Sheria za madini chimba visima hakikisha unatetea maslahi ya nchi yako.

Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani hii dozi inatosha nitarudi kidogo kwenye ufahamu.