Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Singida Mashariki
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. Mimi nimepinga sera za uwekezaji za Chama cha Mapinduzi kabla sijawa CHADEMA, kabla sijaja Bungeni toka mwaka 1999. Yaliyofanyika na Mheshimiwa Rais Magufuli juzi ni ya hovyo, nitayapinga kama ambavyo nimepinga sera zote ambazo zimetufikisha leo hapa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme kwa kifupi. Hoja iko hivi, kwa haya ambayo yametendeka, sahauni kabisa diplomasia ya kiuchumi. Suala siyo Acacia watafanya nini? Suala ni kwamba watu wote tunaohusiana nao kiuchumi, Wachina ambao ndio the biggest investors in the world today na ndiyo biggest proponents wa free trade na globalization today. Fikiria Wachina watafanya nini?
Mheshimiwa Mwenyekiti, fikiria EU watafanya nini? United States, ile North America Economic Group itafanya nini? Japan, all the major economic blocks of this world fikiria zitafanya nini kwa sababu ya kitendo kimoja tu cha kunyang’anya michanga ya dhahabu kwa hoja ambazo, kwa wanaojua; sizungumzii wasiojua, washangiliaji hawa, kwa wanaojua, ni hoja za kijinga.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ni kwamba leo hii kiuchumi dunia hii ni multipolar, mwanadiplomasia wetu ataelewa nikisema multipolar wengine wote hawa ni wapiga debe tu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kitu kinaitwa Silk Road Economic Belt, kuna kitu kinaitwa The 21st Century Maritime Silk Road, these are the biggest economic initiatives in today’s world economy. We are not a member! Kenya ni member wa 21st Century Maritime Silk Road yaani Kenya ya leo ndiyo marafiki wakubwa wa kiuchumi wa China kuliko sisi ambao tumekuwa marafiki wa China wa miaka yote, kwa sababu tunazungumza economic diplomacy, we don’t know nothing about the economic diplomacy. Ndiyo maana tunafanya haya tunayoyafanya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, ni mwanadiplomasia, anafahamu haya, asikubali hizi kelele, nchi yetu sasa hivi ina hali mbaya kidiplomasia kwa sababu tumefanya kitu ambacho kisheria ni makosa kwa mujibu wa sheria zetu, kwa mujibu wa mikataba ni makosa, kwa mujibu wa Sheria za Kimataifa ni makosa na gharama tutakayolipa ninyi Wabunge mnaopiga kelele, gharama tutakayolipa ni kubwa kuliko huo mchanga wa Acacia. We will become an economic busket case kama Zimbabwe. Tusishabikie maamuzi ya kijinga kwa sababu tu yamefanywa na Mheshimiwa Rais.
Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, kazi za Mawaziri ni kumshauri Rais. Our economic diplomacy and our economic development is on the brink kwa sababu tumeharibu mahusiano. Kwa hili tu, tumeharibu mahusiano ya kiuchumi kila mahali. Siyo na Acacia. Suala siyo kupelekwa mahakamani tu, suala ni kwamba mwekezaji gani atakayetaka kubakisha hela zake hapa? Mwekezaji gani atakayetaka kuleta hela zake hapa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema siyo Wamarekani na Wazungu tu, fikiria na Wachina ambao ndiyo wawekezaji wakubwa wa dunia hii.