Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CUF
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. ALFREDINA A. KAHIGI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi kuongea machache. Mimi nitazungumzia kuhusu mambo ya afya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nimshukuru Mwenyekiti wangu Profesa Ibrahim Lipumba, mchumi duniani pamoja na baraza lake, naahidi sitamuangusha Mheshimiwa Lipumba. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja yangu, katika Kamati yetu ambayo tumekaa kuna Wilaya 64 ambazo zinakosa Hospitali za Wilaya, mojawapo ni Wilaya yangu ya Bukoba Vijijini hatuna Hospitali ya Wilaya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa Bukoba hawana hospitali ya wilaya, wanatembea mwendo mrefu au wanalipa gharama za kwenda kutafuta matibabu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hizo gharama ambazo wanalipa wanakuwa hawakuzipanga kusudi waweze kwenda kutibiwa huko. Kama wangekuwa na hospitali katika wilaya yao wasingepata usumbufu huo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali iwaangalie kwa jicho la huruma iwajengee Hospitali ya Wilaya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni Wilaya ya miaka mingi sana. Wilaya ya Bukoba ni Wilaya ya miaka mingi sana, Wilaya zote ambazo ziko katika mkoa wetu zimetokana na Wilaya hiyo, lakini yenyewe haina hospitali. Watu wengine kwa kukosa hela za kwenda kwenye hospitali za private wanakunywa dawa za mitishamba ambazo hazina vipimo vyovyote, wengine wanakufa, naomba Serikali iliangalie. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini namshukuru Waziri wa TAMISEMI, Mheshimiwa Jafo, lazima nimseme jina, pamoja na Naibu wake na wataalam wao, ni watu wenye moyo mkunjufu. Hili suala tumeliongelea na wameliona na wameahidi kutusaidia katika bajeti hii ambayo tutakaa waweze kutuweka katika list hiyo, nawashukuru sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikitoka huko, kwa kuwa, dakika ni kidogo niizungumzie Ofisi ya Utumishi. Ninamuunga mkono Rais wangu Mheshimiwa Dkt. Magufuli, kazi aliyofanya siidharau ya kutumbua, kazi ya kutumbua na iwe endelevu, ni kazi nzuri sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo ninawasikitikia madereva ambao walitumbuliwa. Madereva mimi najua ujuzi wao, leseni zao, kama wanajua kusoma na kuandika, hivyo ndivyo vinavyowafanya wawe na kazi lakini maskini ya Mungu wametumbuliwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Wizara hiyo iwaangalie sana watakaokuwa wanaajriwa wawaangalie wasiwe wanawafukuza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hayo machache naunga mkono hoja. Ahsante.