Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

Hon. Fakharia Shomar Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, sina budi kumshukuru na kumpongeza Mheshimiwa Mama Ummy Mwalimu, Waziri, Naibu Waziri wake pamoja na watendaji wake wote, Katibu Mkuu na Wakurugenzi kwa kitabu kizuri walichotuletea ambapo wameelezea utekelezaji wa nyuma na utekelezaji kwa mwaka 2018/2019 sasa unalinganisha na unaiona faraja katika utekelezaji wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nizungumzie na pia kutoa pongezi nyingine juu ya kinga ya saratani. Kwa kweli, hii kinga ya vijana wetu wale wa miaka tisa mpaka 14 ni nzuri, lakini hii kinga inayotolewa je, vijana wetu wamepewa elimu? Unakwenda kumpeleka kwenye kinga anapata kinga yeye anajua ana kinga, lakini hizo kinga unazompa umpe na elimu namna ya kuweza kujikinga na ile kinga aliyokuwa nayo na elimu hii bado sijaiona na hata kwenye hiki kitabu chako sijaiona, ningeomba hili mliangalie.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo lingine ni la ugonjwa wa fistula. Fistula anapata wa mjini, anapata wa vijijini na ukiangalia utakuta hospitali inayoshughulikia siyo hospitali ya Serikali, ni hospitali ambayo imekubali kujitolea na kutoa huduma za bure kwa anayetibiwa hata kama yuko kijijini, nauli mpaka anaweza kufika akatibiwa. Sasa mimi ninashangaa kwa nini Serikali na ninyi msingeingia hamu mkaona hili jambo muweze kulitekeleza kama Serikali, mkapeleka vituo katika Mikoa. Kumtoa mtu kijijini kuja mjini kutibiwa ndiyo mtakuta baadhi ya wananchi hawawezi kuja hawezi kuiacha familia yake akaja huku wakati anajua anakuja kupata matibabu, lakini kama na Mikoani mngeweka vituo ambavyo vikaweza kutibu fistula ambayo inatibika, ingekuwa vizuri zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakuja kwenye suala lingine ambalo lilikuwa linazungumzwa mara nyingi na kwenye hiki kitabu sijaona. Walikuwa wanazungumza kuna kit bag ina vifaa au zana mama anapokwenda kuzaa anakuwa navyo. Hata Dar es Salaam wakati wa pasaka Mheshimiwa Makonda alivitumia kama yeye alitoa msaada kwa akina mama na ambapo ilisemekana vinauzwa, sikumbuki kama ile kit bag moja ni shilingi 20,000 au kiasi gani.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini msingefanya vikawa bure mkaviweka hospitali kwa anayekwenda kujifungua akifika ana uhakika kwamba atapata zana za kutosha ambazo zimetolewa na Serikali.

Kwa hiyo, inavyoonesha hizi kit bags syo mbaya, mimi naona hata mtakapokuwa katika ushirikiano baina ya Bara na Visiwani ingawa Visiwani kule inatolewa matibabu ni bure, ni Sera ya Zanzibar, lakini na ninyi pia mngeipeleka hii elimu wa kuwa na kit bags kama zile wakaweza kuwawekea akina mama wakati wanakwenda kujifungua wakapata wepesi na kuwa na uhakika kuna kitu kinaweza kunisaidia.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika ukurasa wa 21, namba 23 ilikuwa inaelezea ujenzi wa vituo vya afya ambapo ilikuwa TAMISEMI ishirikiane na Wizara ya Afya muweze kujenga vituo vya afya vya vijiji, Wilaya na Kata, lakini hadi hii leo mnazungumzia tu mnaboresha vya zamani vya zamani tunajua vipo, tunataka vipya vijengwe na ni muda mrefu havijajengwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja na haya mengine yaliyobakia nitayaleta kwa maandishi. Ahsante sana.