Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
2
Ministries
nil
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii. Kwa vile nina dakika tano tu, naomba niende straight kwenye points zangu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niseme ukweli kwamba namheshimu sana Waziri Mheshimiwa Profesa Mbarawa, Waziri wa Wizara hii ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Naomba tu kuongezea facts ambazo alitoa Mheshimiwa Kitandula, Mbunge wa Mkinga alipoanza kuzungumzia juu ya barabara ya Same – Kisiwani - Mkomazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Mbarawa ajue kwamba barabara hii ina umuhimu wa kipekee. Kwanza ilikuwa barabara ambayo iko kwenye Great North Road ikafanyiwa magumashi ikabadilishwa kwa sababu ambazo sitazitaja hapa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, upande huu wa Same Mashariki una hazina kubwa sana ya utajiri mkubwa sana wa maji, mvua, mazao na barabara hii inatumiwa na wakazi wa Korogwe Vijijini akiwepo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali anakaa sehemu hiyo; inatumiwa na wenzetu Jimbo la Mkinga aliko Mheshimiwa Kitandula; inatumiwa na wakazi wa Mlalo, Jimbo la Mheshimiwa Shangazi; inatumiwa na Same Magharibi kwa Mheshimiwa Mathayo; na inatumiwa na Same Mashariki kwa Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa haya yote Mheshimiwa Waziri ajue ana National Park ambayo Faru mweusi alitolewa kutoka Czech akaletwa akawekwa pale Mkomazi National Park ili watu wengi waweze kwenda kumwona. Akumbuke kwamba kuna mradi mkubwa unajengwa na LAPF ambapo tangawizi yake itatoka kwenye haya Majimbo yote ya hawa Waheshimiwa niliowataja. Akumbuke kwamba nilishasema hapa na Mheshimiwa Spika aka-join akisema katika Mkoa wa Kilimanjaro ni Jimbo la Same Mashariki tu ambalo halina barabara ya lami iliyokamilika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mradi mkubwa ambao UNCDF - Capital Development Fund wanakuja kuwekeza katika kupandikiza samaki ambapo kuna bwawa ambalo lilitengenezwa tangu Wakoloni walipohamisha wananchi kutoka Mkomazi National Park, wakawatengenezea hili bwawa ambalo lina ukubwa wa 24 square kilometers.
Mheshimiwa Mwenyekiti, UN Secretary General anaye-deal na UNCDF Deputy ali-fly kutoka New York alikuja KIA kuangalia sehemu ule mradi utakapowekwa, akatia tick. Akasema huu utakuwa ni mradi mzuri sana ambao utapandikiza samaki wa kisasa kutoka South America ambao wataweza kuwa ndio kitovu cha kusaidia Tanzania kupata samaki wa hali ya juu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hayo mafupi namwomba Profesa Mbarawa, ametengea Jimbo hili au barabara hii Sh.265,000,000 kwa kilomita 96.5, lakini hapo hapo upembuzi yakinifu uliofanywa mwaka 2015/2016 ulitumia Sh.595,000,000 kufanya huu upembuzi yakinifu. Mwaka 2016/2017 ulishafanywa tena upembuzi yakinifu; Mwaka 2017/2018 nimeambiwa juzi na Meneja wa TANROADS kwamba pia walipita kufanya upembuzi yakinifu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sikuwa napiga kelele hapa kwa ajili ya barabara hii nikijua Mheshimiwa Mbarawa anajua umuhimu wa hii barabara ndiyo maana mara tatu unafanyiwa upembuzi yakinifu, ambapo najua gharama zake zitakuwa imefika shilingi bilioni moja. Sasa kama anafanyia barabara, upembuzi yakinifu na upembuzi wa kina kwa kutumia zaidi ya shilingi bilioni moja, lakini atoe shilingi milioni 200 na kitu, kweli hii?