Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia kwa maandishi. Napongeza hotuba nzuri ya Wizara ya Maji ikiongozwa na Mheshimiwa Kamwelwe na timu yake. Naunga mkono hoja.
Mheshimiwa Naibu Spika, shukrani kwa Mkoa wa Mtwara kutengewa kiasi cha shilingi bilioni 12.9 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji vijijini (mwaka 2018/2019). Katika miradi ya kimkakati Wilaya ya Tandahimba imetengewa shilingi bilioni moja. Kutengewa ni jambo moja na kupewa ni hambo lingine. Nasema hivi kwa sababu mwaka 2017/ 2018 Serikali ilitenga shilingi bilioni 2.3 kwa ajili ya Mradi wa Mkwiti Group Water Supply Scheme ambao utahudumia wananchi zaidi ya 36,000 katika Wilaya ya Tandahimba. Cha kushangaza hakuna fedha ambayo imetolewa hadi sasa. Wilaya ya Tandahimba ina wakazi takribani 243,000 lakini upatikanaji wa maji ni asilimia 24 tu.
Mheshimiwa Naibu Spika, maombi, mkandarasi ameshaandaa vifaa viko katika eneo la mradi kwa asilimia 80. Kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa ameomba advance ya shilingi milioni 400 lakini hajapewa hadi sasa. Ameomba shilingi bilioni moja kwani amekidhi certificate, lakini hajapewa. Tafadhali mkandarasi apewe fedha hii ili aweze kufukia mabomba na kukamilisha phase one vinginevyo mabomba yataibiwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, ili Halmashauri inaomba kibali cha kupata shilingi bilioni 8.5 zote ili watekeleze phase zote nne za Mradi wa Mkwiti.
Mheshimiwa Naibu Spika, tatu, Halmashauri ipate kibali cha kuanzisha Mamlaka ya Maji ya Tandahimba.