Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchukua fursa hii kukushukuru wewe binafsi kwa kutupatia fursa hii ya kuchangia katika hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Pili, napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa pamoja na Watendaji wote wa Wizara yake kwa kuandaa na kuiwasilisha hotuba yake kwa ufasaha na umakini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ni Mfuko wenye madhumuni ya kuwapunguzia wananchi makali ya kiuchumi. Naipongeza Serikali sana kwa mfuko huo na naomba uendelee zaidi. Hata hivyo, imeonekana kuwa bado kuna matatizo katika utambuzi wa kaya zinazohusika, kuna udanganyifu katika kuwatambua walemavu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu katika hili, Serikali iwashirikishe Walemavu, Wabunge katika zoezi la kutambua kaya husika ili kuondoa mkanganyiko huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Mfuko wa Rais wa Kujitegemea, Mfuko huu ni mzuri sana, nachukua fursa hii kuipongeza Serikali kwa kuanzisha Mfuko huu. Bado hakuna uwiano wa kiwango cha wahitimu wanaomaliza shule za VETA. Kiwango cha wanaomaliza shule za VETA ambao ni miongoni mwa walemavu ni mkubwa kuliko kiwango cha fedha zinazotolewa kwa mkopo. Ushauri wangu ni kwamba Serikali iongeze kiwango cha fedha za mikopo kwa Mfuko huu ili dhamira ya Mfuko huu iweze kufikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nichukue fursa hii kuchangia katika hotuba ya Waziri wa TAMISEMI. Nampongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na watendaji wake wote kwa umahiri wanaoonesha katika kuongoza Wizara hii nyeti katika nchi hii. Katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mfuko wa Afya ya Jamii; katika ulimwengu wote afya ni jambo muhimu sana kwa mwanadamu. Naipongeza Wizara kwa kuanzisha utaratibu mzuri wa Mfuko wa Afya ya Jamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu katika utaratibu huu ni kuongeza kasi ya kuwapatia kadi za afya wananchi husika. Bado idadi ya wanachama 12,278,406 ni ndogo sana ukilinganisha na idadi ya wananchi wa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi ya maendeleo; naipongeza Wizara kwa ubunifu wanaoonesha kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo lakini bado inaonekana kuna utegemezi mkubwa wa fedha katika utekelezaji wa baadhi ya miradi, bado Serikali inategemea misaada kutoka taasisi za nje. Ushauri wangu ni kwamba Serikali iongeze speed ya kutafuta vyanzo vya mapato ili tuweze kuendesha miradi yetu kwa fedha zetu za ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja zote mbili. Ahsante sana.