Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Hon. Anastazia James Wambura

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampa hongera kwa kazi nzuri Waziri wa TAMISEMI, Mheshimiwa Jafo, pamoja na Naibu Mawaziri. Pia naunga mkono hoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri; Ripoti ya CAG inaonesha hati safi kwa zaidi ya asilimia 90 ya halmashauri zote nchini. Jambo hili lisitufanye kudhani kwamba hata miradi inakwenda vizuri kwa zaidi ya asilimia 90. Hii ni kwa sababu mimi nikiwa Mjumbe wa Kamati ya LAAC nimeshuhudia miradi iliyoripotiwa na Ofisi ya CAG kwamba imekamilika na inatumika sivyo ilivyo, kwani haitumiki kutokana na kutokamilika ipasavyo. Kimsingi miradi yote miwili ya maji tuliyoikagua Mkoani Tabora ilikuwa haitumiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu ni kwamba Wakurugenzi na watendaji wahimizwe na wawezeshwe kutembelea miradi ya maendeleo vijijini na katika maeneo yao ya utawala ili kusimamia miradi kwa ufanisi. Vilevile, Ofisi ya CAG iwezeshwe kwa upande wa rasilimali fedha na rasilimali watu ili waweze kufanya performance audit ambayo itaonesha kama mradi kweli ina tija.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo inabidi hata Kamati ya LAAC iwezeshwe kufika maeneo mengi zaidi ili kuthibitisha taarifa ya CAG, hivyo, ni vyema ipewe muda wa kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika utafiti uliofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu mwaka 2009 kuhusu umuhimu wa VRTs katika kuhamasisha maendeleo ndani ya mfumo wa Serikali za Mitaa, ilipendekezwa kwamba VRTs wajengewe uwezo waenezwe katika halmashauri zote, wapewe vitendea kazi na usafiri; vilevile uwepo mpango na miongozo sahihi kwa ajili ya kufuatilia utendaji wao. Katika kuhitimisha hoja, ningependa kupata maelezo ni nini kimefanyika kuhusiana na VRTs tangu mapendekezo hayo yametolewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti suala la lishe katika halmashauri zetu litiliwe mkazo kwa kuajiri Maafisa Lishe na kusisitiza elimu ya lishe kwa jamii, pia kuhimiza agenda ya lishe katika RCC, DCC na Mabaraza ya Madiwani. Hii itapunguza gharama na bajeti katika Sekta ya Afya.