Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Madini

Hon. Janeth Maurice Massaburi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Madini

MHE. JANETH M. MASABURI: Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue fursa hii kwa kipekee kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kazi na juhudi kubwa anayoifanya ya kusimamia na kulinda rasilimali za nchi yetu ya Tanzania. Kwa kipindi cha miezi michache ya utekelezaji matokeo mazuri yameonekana. Hongera sana Mheshimiwa Rais, Mwenyezi Mungu akulinde wewe na Serikali yako.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumpongeza Waziri wa Madini, Naibu Mawaziri, Katibu Mkuu, taasisi zote zilizo katika sekta hii ya madini na watendaji wote wa Wizara hii ambao wameshiriki katika kufanikisha kazi nzuri. Kipekee, niwapongeze Mheshimiwa Waziri wa Madini na Manaibu wake wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii na kufuatilia kwa ukaribu sana maeneo mengi ya migodi na kutatua changamoto zilizoko katika sekta hii ya madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na pongezi hizo, naomba nichangie mambo au maoni machache kama ifuatavyo:-

(i) Serikali itafute uwezekano wa kuainisha aina zote za madini zinazopatikana hapa nchini na ionyeshe faida zake na masoko yake nje ya nchi. Pia kuwe na maonesho ya mara kwa mara ya uelewa na kuweza kuchukua fursa ambazo zinaweza kutoa ajira nyingi zaidi kwa vijana kwa kuuza vito na madini mengine ya ujenzi na malighafi na kadhalika.

(ii) Naomba Serikali itoe mafunzo ya vitendo kwa wachimbaji wadogo wadogo na wa kati ili waweze kuongeza ujuzi wa kuchenjua madini ya aina mbalimbali.

(iii) STAMICO ijengewe uwezo kwa kupatiwa fedha za kutosha ili iweze kujiendesha kwa ufanisi na tija.

(iv) Ufanyike uhakiki/sensa kwa wachimbaji wote wadogo wadogo ili Serikali na Shirikisho la FEMATA waweze kuwatambua kwa kuwapatia vitambulisho maalum. Hii itasaidia kuzuia watu wasio Watanzania kuvamia migodi yetu bila utaratibu wa kisheria na wakati mwingine baadhi yao hufanya uhalifu na kukimbilia nchi jirani bila kujulikana.

(v) Madini ya ujenzi kama kokoto, gypsum, madini ya kutengeneza marumaru (tiles), changa na kadhalika. Migodi ya aina hii inapaswa kusimamiwa kwa ukamilifu kama yalivyo madini mengine ikizingatiwa matumizi yake ni makubwa mno. Migodi hii hupoteza kiasi kikubwa cha fedha za Serikali kwa kutokuwa na utaratibu mzuri wa uchimbaji na usimamizi pia hata utozaji wa ushuru katika madini hayo.

(vi) Viongozi wa ngazi za aina zote wawe na lugha zinazoleta au kuashiria utaifa kuliko kutumia lugha kibaguzi kwa kutumia madini, mazao, vitega uchumi na kadhalika. Mara nyingine baadhi ya viongozi hutoa lugha ya kusema madini haya ni ya mkoa fulani hayawezi kuuzwa mkoa fulani au mazao fulani yauzwe kupitia bandari fulani. Lugha hizi zinabomoa nchi na ni hatari sana kwa kizazi kijacho.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja 100%.