Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Hawa Mchafu Chakoma (29 total)

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2015, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa baraka zake tele.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuchangia hotuba hii ya bajeti ya Serikali ningependa kuanza kwa kumpongeza Waziri na Naibu wake kwa kazi nzuri ambayo wanaifanya. Pia kwa niaba ya wafanyakazi wote nchini nipende kuishukuru Serikali, Serikali zote mbili iliyokuwa ya Awamu ya Nne na Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwa wasikivu na kusikiliza kilio cha wafanyakazi cha muda mrefu.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ya Awamu ya Nne wafanyakazi wote nchini tunaishukuru sana kwa kukubali kuanzisha Sheria ya Mfuko wa Fidia (Workers Compensation Fund) Sheria Na. 8 ya mwaka 2008 na kuachana na ile Sura Na. 263 kwa Private na Public Service Act Na.19 kwa upande wa wafanyakazi wa utumishi wa umma kutumika kufidia once wanapoumia ama kupata ulemavu mahali pa kazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ya Awamu ya Tano tunaishukuru kwa kukubali kuwasilisha michango ya mwajiri ya 0.5 percent ya mshahara katika Mfuko huu wa Fidia ili itakapofika tarehe Mosi Julai, mwaka huu wafanyakazi wote watakaoumia ama kupata ulemavu kazini wataenda kufidiwa na Mfuko huu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, narudia tena kwa niaba ya wafanyakazi wote nchini, tunaishukuru sana Serikali tena sana kwa kuja na jambo hili jema la kuanzisha huu Mfuko. Nipende tu kusema kwa kuanzisha Mfuko huu automatically tunaongeza muda mrefu wa wafanyakazi kuwepo kazini, lakini pia tunaongeza uzalishaji, kitu ambacho kitaenda kuchochea ukuaji wa uchumi wetu na hali kadhalika pato la Taifa letu litakua. Ni ukweli usiopingika Serikali inapata kodi yake ya uhakika pasipo kusuasua kutoka katika kundi hili la wafanyakazi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pia nipende kuipongeza Serikali kwa kupunguza kodi ya Pay As You Earn hadi kufika single digit kwa wafanyakazi wa kima cha chini. Napenda kuiomba Serikali na niliuliza hapa swali katika Bunge lako Tukufu kwamba, je, Serikali ina mpango wowote ama ina mpango gani kwenda sasa kupunguza hii kodi ya Pay As You Earn kwa wafanyakazi wa kima cha juu wanaokatwa 30%.
Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana ya wafanyakazi au watumishi wa nchi hii Mheshimiwa Angellah Kairuki alitupa majibu mazuri sana kwamba tayari Workers Task Force imeshaundwa na inayafanyia kazi haya mapendekezo na tayari yamepelekwa kwenye Baraza la Majadiliano la Utumishi wa Umma wanayafanyia kazi na muda wowote wataturudishia feedback, naamini feedback itakuwa njema.
Mheshimiwa Naibu Spika, niombe tu Serikali kwa mwaka 2017/2018, ione sasa umuhimu wa kuwapunguzia kodi hawa watumishi wa umma ama wafanyakazi wanaokatwa kima cha juu ili kuwapunguzia makali ya maisha na kama nilivyozungumza hili ndilo eneo ambalo Serikali inapata kodi yake ya uhakika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mchango wangu wa tatu ni kuhusiana na afya ama vituo vya afya katika Halmashauri zetu. Kiukweli uwezo ama hali ya Halmashauri zetu katika ujenzi wa hivi vituo vya afya, zahanati ama niseme majengo ya wazazi hali yao haiko vizuri, wanatumia own source na yenyewe wanaipata kwa kuhangaikahangaika. Kwa hiyo, naomba sana Mheshimiwa Waziri atakapokuja hapa ku-windup aweze kutueleza kiukweli kabisa kwa sababu hizi Halmashauri zinajaribu kuingia kwenye huu ujenzi wa hivi vituo vya afya ama majengo ya wazazi wanafikia usawa wa lenta, kupaua wanashindwa, yale majengo yanabakia kama magofu.
Mheshimiwa Naibu Spika, nikitolea mfano katika Halmashauri yangu ya Wilaya ya Kibaha katika Kata ya Magindu kuna jengo la wazazi pale tangu mwaka 2012 mpaka leo hii 2016 ninavyoongea halijakamilika na wala halina dalili ya kukamilika. Tunahitaji shilingi milioni 26 tu ili kuweza kulikamilisha jengo lile, wanawake wa Kata ya Gwata na Kata ya Magindu waweze kutimiza haki yao ya msingi ya kuleta watoto hapa duniani. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda sana kumwomba Mheshimiwa Waziri alione hilo, tunazihitaji hizo shilingi milioni 26 ili tuweze kuwasaidia wanawake hawa ambao ni wapiga kura wetu lakini hali kadhalika niseme ni walezi wa watoto wa Taifa hili. Hii shilingi milioni 26 kwa ajili ya kumalizia hiki kituo tumeanza kuiomba tangu mwaka wa bajeti 2014/2015 hakuna kitu, 2015/2016 hakuna kitu, 2016/2017 nimechungulia hakuna kitu. Nimwombe sana Mheshimiwa Waziri atufikirie na atuonee huruma na hili suala lifike mwisho. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mchango wangu mwingine uko katika hili suala zima la private number. Hapa pengine Mheshimiwa Waziri atakuja anipe shule lakini nikiangalia kwa uelewa tu wa kawaida sasa hivi katika gari yangu nimeandika Mchafu nalipa shilingi milioni tano, lakini anasema kwamba anatutoa kwenye shilingi milioni tano anatupeleka kwenye shilingi milioni 10. Katika hali tu ya kawaida ambayo wala haihitaji akili nyingi, mimi nasema tunaenda kupunguza mapato na siyo kwamba tunaenda kuongeza mapato. Kwa sababu ni hiari ya mtu, naweza nikaamua kuacha jina langu Mchafu na nikaenda nikarudi kwenye Na. T302 BZZ.
Mheshimiwa Naibu Spika, hapo nitapenda Mheshimiwa Waziri atakapokuja anifundishe kutoka kwenye hii shilingi milioni tano kwenda kwenye shilingi milioni 10 anaongezaje mapato ilhali hili jambo ni hiari na siyo lazima. Mheshimiwa Waziri atakapokuja kuzungumza nitaomba aje anifafanulie suala hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini suala lingine ni kuhusiana na suala zima la kuongeza tozo ama kuweka tozo kwa bidhaa za mitumba. Nilitoka kuuliza swali hapa asubuhi Watanzania milioni 12 ni maskini wa kutupwa, kila mwaka vijana takribani laki nane wanaingia kwenye soko la ajira, je, Serikali kwa mwaka inatengeneza ajira ngapi?
Mheshimiwa Naibu Spika, tuna vijana wengi ambao ni hawa tunawaita Machinga, wanafanya kazi ya kutembeza hizi nguo za mitumba ili waweze kupata riziki na familia zao. Leo ukiweka tozo kwa lengo la kuizuia hii mitumba, niulize hivi viwanda vitakavyotengeneza nguo kutuvalisha Watanzania viko wapi? Kwa hiyo, nimwombe sana Mheshimiwa Waziri jambo hili alifikirie mara mbili, je, tupo tayari kuongeza hizi tozo kwenye mitumba hivyo viwanda viko tayari? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini suala lingine ni kuhusiana na CAG, wengi wamesema na mimi lazima nilizungumzie hili. Halmashauri zetu uaminifu wao ni wa kulegalega, CAG ndiye mkombozi mkubwa ambaye ameweza kutusaidia, CAG ndio jicho ambalo limeweza ku-penetrate na kuweza kuona kuna watu wanalipwa mishahara hewa, nimuombe sana Mheshimiwa Waziri na niungane na wenzangu wote waliosimama hapa kuzungumzia suala zima la CAG kuongezewa pesa, hebu akae afikirie mara mbili mbili.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunasema bajeti yetu ni shilingi trilioni 29 na hela hizo hatuna in cash, ndiyo tunataka twende tukazikusanye sasa kama CAG tunamwekea hela kidogo namna hiyo atakwenda kufanya kazi gani? Kwa hiyo, nimwombe sana Mheshimiwa Waziri afikirie tena na tena kuhusiana na suala zima la CAG, aone namna bora ya kuweza kumuongezea pesa ili aweze kufanya kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sitaki unigongee kengele, napenda kusema nakushukuru sana na naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitaanza kwa kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano lakini pia kumpongeza Mheshimiwa Waziri na Naibu wake kwa kazi nzuri ambayo wanaifanya. Kiukweli Wizara hii ya Afya ina mambo mengi sana na wenzetu Waziri na Naibu wake wanafanya kazi kubwa sana, lakini mwisho wa siku tukubaliane tu hizi changamoto za afya hazitakaa zije ziishe kwa ukamilifu wake, hata zikiisha bado zitazaliwa zingine kutokana na vyakula tunayokula, life style tunayoishi na mabadaliko ya tabianchi. Kwa hiyo, kila siku kwenye Wizara ya Afya changamoto zitakuwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa dakika ni tano itoshe kuwapongeza wenzetu kwa kazi nzuri wanayoifanya Serikali ya Awamu ya Tano hasa kwa kujitahidi ama kuweza kuokoa fedha kwa wagonjwa walikuwa wanaenda kupata matibabu ya moyo nje ya nchi. Ukiangalia hapa kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri inasema wameweza kupunguza ilikuwa kutoka wagonjwa 43 mpaka wagonjwa 12 kwa mwaka 2016/2017; hiyo ni pongezi kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine ninachopenda kuwapongeza kwa lile la kuanzisha chanjo ya saratani kwa mabinti wa miaka 14, wamefanya kazi kubwa sana. Pengine hapa nataka niiombe Serikali yangu iangalie sasa mabinti above 14 yaani huo umri wa wao ambao wameuchukua sasa wanaozidi umri huo, Serikali ina mkakati nao gani? Nilikuwa tu napenda kusaidiwa katika hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine ambacho ningependa kukizungumzia kwenye dakika hizi tano, napenda kuiomba Serikali na niliwahi kuuliza swali juu ya sera ya matibabu bure kwa wajawazito, hili bado naliona kama kidogo tuna changamoto nalo, pengine Serikali sasa ione namna bora ya kufanya mapitio upya ya hii sera, kama itabidi vipo baadhi ya vitu tutahitajika kuvitolea ufafanuzi. Hivi bure kwa wajawazito kwenye kila kitu au kuna baadhi ya vitu bure na kuna baadhi ya vitu vingine wananchi inabidi wachangie?

Mheshimiwa Naibu Spika, ni vema hii tungeiweka vizuri kwa sababu hofu yangu wapiga kura na wananchi wetu wengi wanalalamikia kwamba once wako wajawazito wanapoenda hospitalini wanatozwa ama kuwa-charged. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe tu mfano, vidoge vile vya uchungu wanaviita ama dripu, yenyewe ile, nikijitolea mfano hata mimi mwenyewe binafsi, nililipia kwa cash ingawaje nina kadi ya NHIF ni kadi ya Bunge ambayo naamini katika kadi ambazo ziko vizuri ni kadi za NHIF za Wabunge, lakini ilikuwa hai-cover vidonge tu vya uchungu. Kwa hiyo, mimi naiomba sana Serikali ikae iangalie vizuri sera, ipitie upya Sera ya Matibabu Bure kwa Wajawazito. Pia utakuta mama mjamzito ambaye anapata miscarriage anasafishwa kwa kati ya shilingi 300,000 mpaka 500,000. Kwa hiyo, nafikiri tunahitaji kuifafanua vizuri zaidi hii sera ili isituchonganishe na wananchi kipi ni bure, kipi tunatakiwa kukilipia.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine ambacho ninapenda kukizungumza kiko kwenye ukurasa wa 17, juu ya afya ya uzazi, mama na mtoto. Kiukweli Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu na Naibu wake wanajitahidi kwa kiasi kikubwa sana kupambana kupunguza vifo vya mama na mtoto. Ila kuna kitu kimoja kinanisumbua siyo peke yangu, naona tuko watu wengi tu, pengine leo mngetusaidia kukitolea ufafanuzi ili kiweze kutusaidia.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwanamama anapokuwa mjamzito anapo-attend kliniki ni lazima, sijui kama ni lazima ama ni utaratibu wa kuwa anafanya ultra sound ili kuangalia maendeleo ya mtoto. Nikikumbuka mwenyewe aliyekuwa akinifanyia alikuwa anasema unaona mtoto wako huyu anaendelea vizuri, mapigo ya moyo, vidole vyake hivi vitano, hana mgongowazi, walikuwa wanasema hivyo. Ila kuna tatizo, wanashindwa kuangalia kama nitakosea kitaalamu mtanirekebisha, Mheshimiwa Dkt. Ummy na Mheshimiwa Dkt. Ndugulile, kuna kitu kinaitwa coding ama wanasema kitanzi, sijui kwa nini lile linashindwa kuangaliwa kipindi kile mama anapo-attend kliniki, kiasi kwamba…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha muda wa Mzungumzaji)

MHE. HAWA M. CHAKOMA:Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ili na mimi niweze kuchangia hoja iliyopo mbele yetu.
Awali ya yote, nipende kumshukuru Mwenye Mungu, mwingi wa rehema na mwenye kurehemu, lakini pia nipende kuwashukuru wanawake wa Mkoa wa Pwani kwa kuniamini niweze kuja kuwawakilisha. Sambamba na hilo, napenda niwashukuru wanawake wa CCM Taifa na Chama changu cha Mapinduzi kwa kuniteua Mbunge wa Viti Maalum. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, wakati naelekea kuchangia hotuba ya Waziri Mkuu, napenda kutoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na timu yake ya Baraza la Mawaziri inayoongozwa na Jemedari Mkuu, Waziri wetu Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa kwa kazi nzuri wanayoifanya ambayo inavutia moyoni mwa Watanzania, kwa kazi nzuri wanayoifanya ambayo inaleta furaha katika macho ya Watanzania. Hakika Mungu mbariki Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza lake la Mawaziri. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuchangia hotuba ya Waziri Mkuu kwa kuanza ukurasa wa saba. Katika ukurasa wa saba hotuba hii inajielekeza katika namna ya kuchukua hatua kuhakikisha wanaongeza mapato na wanabana mianya ya ukwepaji kodi. Mimi nipende kuunga mkono jitihada hizi, ni jambo jema sana na I believe for sure kama tuna uwezo wa kukusanya hata zaidi ya shilingi trilioni 1.3 endapo TRA itajizatiti kweli kweli lakini pia kila Mtanzania atimize wajibu wake, anayepaswa kulipa kodi alipe kodi, tudai risiti tunapofanya manunuzi.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuelekea kuongeza mapato kama ambavyo Serikali imedhamiria tuna shida moja, EFD mashine bado kuzungumkuti. Suala zima la EFD mashine ni tatizo. Nimeshashuhudia nimepata risiti za aina tatu tofauti pale unapofanya manunuzi. Kuna risiti ambayo unakuta ina maelezo ambayo kwa mtazamo wangu mimi naweza kusema yamejitosheleza. Kuna TIN namba pale, utakuta jina la ile kampuni ama kile kituo cha kufanyia biashara, kuna VRN pale lakini pia utakuta jumla ya amount uliyonunua, muda, tarehe pamoja na ile amount inayokuwa deducted kwenda Serikalini, lakini zipo risiti nyingine zinazotoka katika hii mashine unakuta zina lack hizo details. Kwa hiyo, naomba sana hili suala la EFD mashine tuliangalie vizuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia baadhi ya wafanya biashara hawana hizi mashine, wanaendelea kutumia risiti za kuandika. Niseme kwamba hizi risiti siyo afya sana katika ongezeka la ukusanyaji wa mapato.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia nimewahi kwenda petrol station kuweka mafuta, nimeweka saa tatu asubuhi lakini risiti inaniandikia nimeweka saa tano usiku. Kwa hiyo, inaonekana kwamba hizi mashine watu wanaweza kucheza nazo. Kwa sababu hiyo, nasisitiza tena tuziangalie mashine hizi.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia kwenye petrol station kuna matatizo makubwa sana ndiyo maana nasisitiza TRA inabidi ijizatiti au ifanye kazi kweli kwenye hili suala la ongezeko la mapato. Utakuta kuna visima viwili, cha dizeli na petroli, vya dizeli viwili na vya petroli viwili, kimoja ni cha risiti ya kuandika na kingine ni cha risiti ya TRA. Kwa hiyo, naomba sana katika suala hilo mnaohusika mliangalie kwa ukaribu.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini mchango wangu mwingine uko katika ukurasa wa 16 ambao unazungumzia shilingi milioni 50 katika kila kijiji lakini pia umeelezea maandalizi ya namna fedha hizi zitakavyowafikia walengwa ikiwa ni pamoja na kuanzisha vikundi vya kiuchumi vinavyokidhi vigezo. Hii ni ahadi ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi ambayo unaikuta katika Ibara ya 57(d) kwa ruhusa yako naomba nikisome na kinasema; “kutenga kiasi cha shilingi milioni 50 katika kila kijiji kama mfuko wa mzunguko (revolving fund) kwa ajili ya kukopesha vikundi vya wajasiriamali kupitia ushirika wa kuweka na kukopa (SACCOS) katika vijiji husika.” (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi cha kampeni kilichokuwa kinawavuta Watanzania wengi ni pamoja na kifungu hiki cha 57(d) cha shilingi milioni 50 katika kila kijiji. Ukiangalia muktadha wa hiki kifungu hizi shilingi milioni 50 siyo kwamba watu watagawiwa, watakopeshwa then watarudisha. Wakati wa ziara yangu ya kushukuru wapiga kura wa Mkoa wa Pwani nilipata maswali kutokana na kifungu hiki, wazee wanauliza wao watanufaika vipi na kifungu hiki.
Mheshimiwa Naibu Spika, kimsingi wazee ambao wameshafika umri wa kushindwa hata kufanya kazi huoni moja kwa moja kama kinaweza kuwanufaisha. Isipokuwa naomba Serikali masuala mazima ya mapendekezo ya universal pension, pension kwa wazee wote yaweze kufanyiwa kazi kwa haraka ili yaende sambamba na hii shilingi milioni 50. Wakati watu wenye nguvu zao wananufaika na hii shilingi milioni 50 kukopa na kufanya biashara ama ujasiriamali basi wazee waweze kunufaika na pension ya wazee wote.
Mheshimiwa Naibu Spika, mchango wangu mwingine uko ukurasa wa 23 ambao unazungumzia suala zima la kazi na hifadhi ya jamii. Katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ambayo inaelezea mwelekeo wa shughuli za Serikali, nilitarajia kuuona hapa Mfuko wa Fidia (Workers Compensation Fund – WCF). Sikukuu ya Mei Mosi mwaka jana kati ya mambo ambayo Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Nne na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi alifafanua na kueleza kwamba kati ya mafanikio ya Serikali yake basi ni pamoja na kuanzishwa kwa Workers Compensation Fund.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nipende kusema na niwe mkweli na utakubaliana na mimi kabisa kati ya kitu ambacho Serikali ya Awamu ya Nne imefanya kwa wafanyakazi wa Taifa hili basi ni pamoja na kuanzisha Mfuko wa Fidia Kazini. Ikumbukwe hapo awali ilikuwa inatumika sheria ya zamani, Sheria ya Fidia, Sura Na.263 ambapo mtumishi akiumia kazini, akipoteza kiungo alikuwa analipwa shilingi 108,000 kwa upande wa wafanyakazi wa private lakini kwa upande wa wafanyakazi wa public sector ilikuwa inatumia Sheria ya Public Service Act ambayo mtumishi akiumia ama akipoteza kiungo ama ulemavu wa maisha alikuwa anapewa shilingi milioni 12 na yenyewe ilikuwa inatolewa once.
Kwa hiyo, naomba sana Waziri Mkuu na Waziri mwenye dhamana ya kazi na hifadhi ya jamii kuuangalia mfuko huu kwani umeelezea namna njema ya kuwafidia wafanyakazi wetu wanapoumia ama kupoteza viungo sehemu yao ya kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nitapenda tena kujikita ukurasa wa tano wa hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ambao unazungumzia uwajibikaji na maadili ya viongozi wa utumishi wa umma. Baadhi ya watumishi wa umma walifika mahali walijisahau sana, lakini pia baadhi ya watumishi wa umma wasiokuwa waadilifu hao ndiyo walikuwa wameigharimu Serikali ya Chama cha Mapinduzi. Hata hivyo, Serikali yetu ya Awamu ya Tano imeamua kuchukua hatua ku-deal na hawa watu ambao walikuwa hawana uadilifu wametumia madaraka yao vibaya ama wametumia nafasi zao vibaya.
Mheshimiwa Naibu Spika, cha kushangaza wenzetu hawa hawa waliokuwa wanapigia kelele kwamba Serikali ya Chama cha Mapinduzi inachelewa kuchukua hatua leo wamekuwa mstari wa mbele kutetea wabadhirifu, wamekuwa mstari wa mbele kutetea mafisadi, wamekuwa mstari wa mbele kutetea watumishi ambao hawana maadili. Wamekuwa vigeugeu, ni wao ndiyo waliokuwa wanasema tunaenda taratibu, sasa tunaondoka na supersonic speed, wanatoka tena mbele na kuanza kuwatetea wale watu.
Mheshimiwa Naibu Spika, mchango wangu mwingine…
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Naibu Spika, Taarifa...
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Hawa Chakoma naomba ukae, Mheshimiwa Cecilia Paresso...
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nilisema kwamba taarifa yake siipokei nimei-shred, lakini pia nipende kumkumbusha anaweza akaenda YouTube akaona Mwenyekiti wao Mbowe analalamika watumishi wa umma ambao wanasimamishwa anataka wahojiwe kwanza, tayari TAKUKURU imeshatoa ushahidi, anahojiwa kitu gani? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naenda ukurasa wa tisa unaozungumzia kukua na kuimarika kwa demokrasia. Nchini Tanzania demokrasia imekuwa na ndiyo maana kuna uwepo wa vyama vingi. Pia niseme tunatambua uwepo wa upinzani nchini, tunatambua uwepo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na tunatambua chama kikuu cha upinzani. Wakati tunaelekea kwenye mustakabali wa kuwafanya Watanzania wawe na maisha bora, ukiacha kazi nzuri inayofanywa na Chama Tawala ama na Serikali, pia tunahitaji mchango makini kutoka kwa chama cha upinzani ama Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Kama tunakuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ambayo kwanza haiko makini, mbili inaendeshwa na mihemko, tatu inaendeshwa na sintofahamu, hatuwezi kufika mahali kokote.
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Hawa Chakoma umemaliza muda wako.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuchangia hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa kuonesha masikitiko yangu kwa mgogoro wa wakulima na wafugaji katika Kata ya Magindu na Gwata Mkoani Pwani katika Jimbo la Kibaha Vijijini.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika ziara yangu ya kushukuru wapiga kura wa Mkoa wa Pwani hususani Kata ya Gwata na Magindu nimepokea malalamiko toka kwa wananchi juu ya mgogoro unaoendelea kati ya wakulima na wafugaji. Mfano katika Kata ya Magindu, Kijiji cha Mizuguni mgogoro huo umeota mizizi kwani wafugaji (Masai) na mifugo yao huvamia mashamba ya wakulima na kula mazao yao suala linalopelekea mapigano baina ya jamii hizo mbili. Mgogoro ambao hata Kamati ya Kijiji cha Mizuguni imeshindwa kuutatua. Hata wakulima walivyokimbilia Mahakamani bado wamekuwa wakishindwa kesi hizo (za kuharibiwa mazao yao kila siku) kwa kuwa wafugaji jamii ya Kimasai huhonga Mahakimu na hatimaye wanashinda kesi hizo. Hali hiyo pia imejitokeza katika Kata ya Gwata, Kijiji cha Mlalazi, mifugo (ng‟ombe) wanamaliza mahindi ya wakulima.
Mheshimiwa Naibu Spika, kikubwa zaidi hapa Mheshimiwa Waziri, wafugaji hawa walishatengewa eneo la kwenda ambako ni Vinyenze, kijiji hiki kiliwekwa ama kutengwa mahsusi kwa ajili ya wafugaji ili kunusuru mazao ya wakulima lakini hadi leo hii ninavyoongea wafugaji hao wamegoma kwenda Vinyeze hali ambayo inaendeleza migogoro baina yao na wakulima.
Mheshimiwa Naibu Spika, niombe sana hili suala si la kuchukulia mzaha kwa kweli maana huu mgogoro unafukuta chini kwa chini, siku ukija kulipuka hapatatosha. Hivi ninavyoongea katika Kata ya Gwata wakulima hawaoani na wafugaji lakini pia wanapigana mapanga na kuumizana ilhali hapo awali walioleana.
Mheshishimiwa Spika, naomba sana Serikali kuingilia kati kunusuru jamii hizi mbili kuacha kupigana na kuhatarishiana maisha. Pia Serikali iingilie kati ili wafugaji ambao wanasemekana ni matajiri waache kuwaonea wakulima wanaosemekana ni wanyonge. Kesi inapokuwa Mahakamani wafugaji wanakimbilia kuhonga halafu mwisho wa siku Mahakimu huwapa ushindi huo wafugaji only because wamepokea hongo.
Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, nimeamua kuchangia hoja hii moja tu mwanzo mwisho kwa sababu ya umuhimu na upekee wake. Nikuombe sana Mheshimiwa Waziri baada ya Bunge hili la bajeti katika ziara zako za kikazi Mkoa wa Pwani uwe kwenye orodha kwa kuipa kipaumbele Kata ya Gwata na Magidu.
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa nafasi hii, naomba kuunga mkono hoja. Niwatakie kila la kheri Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri katika kutimiza majukumu ya kilimo, uvuvi na ufugaji kwa maslahi ya Taifa letu.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kutoa mchango wangu katika Wizara hii ya Maliasili na Utalii kwa kujikita katika suala moja.
Kwanza, napenda kuanza kwa kuunga mkono hoja katika Wizara hii ngumu, hususani upande majangili namna yanavyoipa wakati mgumu sekta hii ya maliasili na utalii, kitu ambacho kinapelekea kukosekana kwa watalii na ukosefu wa mapato kwa uchumi wa nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania leo tunazungumzia kukua kwa utalii kwa kuwa na watalii milioni mbili, wenzetu South Africa wanazungumzia watalii milioni 12. Hivyo basi, ni kwa Serikali yetu (Wizara) kuhakikisha inaboresha miundombinu ya maeneo yetu ya watalii. Kwa mfano, utalii wa Mlima Kilimanjaro miundombinu ya majitaka siyo mizuri kabisa hususan upande wa vyoo, vyoo ni vichafu. Mbaya zaidi vyoo ambavyo wanatumia wananchi/wafanyakazi wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ndiyo hivyo hivyo vinatumiwa na wageni wetu (watalii). Hii si sawa kabisa na ni moja ya sababu ya kufukuza watalii katika chanzo hicho cha Mlima Kilimanjaro. Sote tunafahamu wazungu/wageni ni waungwana na wasafi sana ukilinganisha na Watanzania wa maeneo yale. Hivyo basi, niitake Wizara kuhakikisha inajenga choo mahsusi kwa wageni wetu (watalii) na siyo kuwachanganya na wenyeji. Usafi ni sehemu ya kutangaza utalii wa nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho ni kuhusiana na mjusi aliyepelekwa nchini Ujerumani. Wabunge walio wengi wanahitaji mjusi huyo kurudishwa nchini, mimi naomba nitofautiane nao kidogo katika maana ya kwamba kuna gharama kubwa sana katika kumtunza, mjusi huyo aendelee kuwepo na kuingiza faida ya nchi. Kwanza ni mkubwa sana, hivyo anahitaji eneo kubwa sana, ni sawa na viwanja vinne vya mpira, lakini pia anahitaji muda wote kuwepo kwenye AC ili asiweze kuharibika/kuoza. Hivyo basi, kuliko kutaka arejeshwe sasa ilhali hatujajipanga, nipende kuishauri Serikali (Wizara) ni bora tuone utaratibu wa kuweza kupata royalty (mrahaba). Ni vyema Serikali yetu ya Tanzania ione utaratibu bora wa kuitaka Serikali ya Ujerumani kutupatia gawio linalotokana na utalii wa mjusi huyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, mchango wangu ni huo. Naomba kuunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa Ijumaa Tukufu na nianze kwa kuunga mkono hoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu wa kwanza uko kwenye ukurasa wa 14 juu ya suala zima la uwezeshaji wananchi kiuchumi. Napenda kuipongeza Serikali kwa kutenga fedha za Mfuko wa Maendeleo kwa ajili ya uwezeshaji wananchi kiuchumi, lakini niseme bado kuna changamoto kubwa kwa sababu hela inayotengwa haijaweza kuwanufaisha wananchi waliokuwa wengi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe Serikali iwe na jicho pana zaidi juu ya huu Mfuko wa Maendeleo kuhusiana na hii asilimia 10 kwa maana asilimia nne vijana, asilimia nne wanawake na asilimia mbili walemavu. Changamoto kubwa hapa asilimia 10 hii upatikanaji wake tunategemea vyanzo vya ndani vya Halmashauri zetu na Halmashauri nyingi zina changamoto kubwa mara baada ya kupokonywa baadhi ya vyanzo vyao kwenda Serikali Kuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kumekuwa na changamoto ya matamko ama maagizo ya Waheshimiwa Mawaziri pengine asubuhi ama wakisimama hapa Bungeni kwa kuagiza mambo kadha wa kadha, Halmashauri zifanye pasipo kuwatengea bajeti. Kwa hiyo, hilo ni tatizo kwani ile dhana nzima iyotafutwa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kama hili jambo halijaangaliwa vizuri, haitakaa ifikiwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiendelea hapohapo, tunawaambia Wakurugenzi kwamba wahahikishe wanatenga hizi hela ama baada ya kupokonywa hivi vyanzo tunawaambia wawe wabunifu, lakini wanapokuwa wabunifu wakianzisha vyanzo vipya Serikali Kuu mnawanyang’anya. Kwa hiyo, hili ni tatizo lazima Serikali tuliangalie kwa jicho pana kabisa. Pia, so long hii asilimia 10 hatujaiwekea utaratibu wa kisheria itakuwa kila siku ni hivihivi tunapiga dilly-dally hizi hela hazitakaa zitoke kwa ukamilifu wake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiendelea kwenye ukurasa huohuo wa 14, hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu inaendelea kwa kusema kwamba, uwezeshaji wa wananchi wakiwemo vijana, wanawake na wazee. Hapa nitaomba kusaidiwa, nashindwa kufahamu Mfuko wa moja kwa moja ambao uko kwa ajili ya uwezeshaji wa wazee, nitaomba nije nisaidiwe ni Mfuko gani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo niseme sioni namna wazee wanavyoweza kushiriki kwenye mchakato huu wa VICOBA, SACCOS ama huu Mfuko wa Maendeleo ambao tayari umeshajipambanua ni kwa ajili ya vijana, wanawake pamoja na watu wenye ulemavu. Kwa wazee napenda kuishauri Serikali, pengine muda umefika sasa ule mchakato wa universal pension (pensheni kwa wazee) mje nao ili tuweze kuwasaidia wazee wa Taifa hili. Sitaki kuzungumza sana, ni wazi tunafahamu mchango wa wazee kwenye Taifa letu. Kwa hiyo, nipende kuiambia Serikali…

T A A R I F A . . .

MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Napenda tu kuishauri Serikali iangalie namna bora ya kuanzisha mchakato wa universal pension (pensheni kwa wazee wote) ili tuweze kuwasidia wazee wa Taifa letu kwa mchango wao mkubwa kwa Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu wa pili uko kwenye ukurasa wa 18 kuhusiana na suala zima la ajira. Nipende kuipongeza Serikali kwa kuanzisha miradi mikubwa ukiwemo wa Standard Gauge, Stiegler’s Gorge, bomba la mafuta, ujenzi wa viwanja vya ndege pamoja na ujenzi wa meli pamoja na vivuko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni wazi kwamba uanzishwaji wa miradi hii inaenda sambamba na upatikanaji wa ajira. Ninachopenda kuishauri Wizara isikae ikaishia ku-count kwamba Standard Gauge imetoa ajira ngapi, Stiegler’s Gorge itatoa ajira ngapi, napenda twende mbele zaidi ihakikishe inafuatilia huku kwenye hii miradi watu ama wananchi wanapata ajira zenye staha na job security. Kwa nini nasema hivyo? Ni kwa sababu mikataba inayoingiwa kwa wananchi ambao wanapata ajira kwenye miradi hii imekuwa ina ukakasi ama imekuwa ikiwaminya wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitatoa mfano kwenye ujenzi wa feri ile ya Kigongo - Busisi, tulienda pale tumekuta ujenzi wa feri unaendelea, Watanzania wengi wako pale wameajiriwa, lakini changamoto inayojitokeza pale mikataba inakiukwa, ile mikataba ambayo imeingiwa haifuatwi. Kwa hiyo, nawaomba msiishie tu kuhesabu ajira zilizopatikana mwende mbele zaidi mkaangalie ajira hizi kama zina staha, mikataba inafuatwa na kama job security iko ya kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu mwingine uko ukurasa wa 44 kuhusiana na barabara. Asubuhi hapa wakati Mbunge wa Singida anauliza swali Wabunge wengi walisimama hapa kuhusiana na suala zima la barabara. Sote tutakubaliana Mikoa, Wilaya ama Majimbo ambayo yamepata ujenzi wa kuunganishwa kwa barabara ya lami uchumi wao unaenda haraka ukilinganisha na yale maeneno mengine. Tunakubaliana kabisa upatikanaji wa barabara ya lami kuunganisha mkoa mmoja na mkoa mwingine unapeleka maendeleo ya kiuchumi haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hapa nataka niiombe Serikali ikae chini na iangalie jambo moja. Kiukweli ujenzi wa barabara una gharama kubwa mno, kilometa mbili tu unakuta ni billions of money. Sitaki kuamini kama kwenye Wizara kuna kushindanishwa kwamba Wizara gani imekusanya kwa kiasi gani kwa sababu nature ya Wizara zingine ziko kwa ajili ya kutoa huduma tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nasema hivyo? Kwa sababu kwenye ujenzi wa barabara kumekuwa kuna tozo nyingi sana. Ukiacha hii ya fidia (compensation) ambayo hiyo kwa namna moja ama nyingine itakuwepo tu kuna hii fidia ya mrabaha au royalty ambayo barabara zetu zinajengwa kwa kutumia changarawe, kokoto, mawe, mchanga, maji, chokaa na kadhalika. Mradi wowote wa barabara huwa unai-include hivi vitu pamoja na hizi tozo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, vumbi la kokoto kwenye ujenzi wa barabara kwa mita moja ya ujazo Wizara ya Nishati na Madini inatoza Sh.25,000, mawe inatoza Sh.16,000 lakini kokoto kwa mita moja ya ujazo inatoza Sh.80,000, kuna tozo nyingi ambazo zinaingia inapelekea miradi ya barabara kuwa ya gharama sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuishauri Serikali ama kuiomba hebu wakae chini waangalie kwamba endapo wakiondoa hizi tozo watakuwa wamepunguza gharama ya barabara kwa asilimia ngapi ama wamepunguza kwa kiasi gani, pengine inaweza ikasaidia. Niwaombe wakafanye hiyo analysis waone kama itaweza kuwa na mchango tukijaribu kuziondoa hizi tozo. Kwa sababu kuna ile Sheria ya Ardhi wanasema kwamba Serikali inapotwaa ardhi yake haiwezi kulipa, sasa inakuwaje hapa Wizara ya Ujenzi inaenda inalipa hela nyingi kwenye Wizara ya Madini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri kwa sababu kila Wilaya, kila Jimbo na kila Mkoa unasuburi kuunganishwa kwa barabara ya lami, ni vema sasa wakapitia sheria hii kama kuna uwezekano wa kupunguza hizi tozo zikapunguzwe ili suala zima la ujenzi wa barabara liende haraka haraka ili ziweze ku-boost uchumi wa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunavyozungumzia barabara kuna Kisiwa Mafia. Kisiwa kile ili uweze kufika kwenye Makao Makuu ya Mkoa wa Pwani hakuna usafiri zaidi ya maji na kwa wale waliojaliwa ndege, lakini wananchi wengi wanasafiri kwa njia ya maji. Hatuna kivuko cha kuwavusha wananchi kutoka Mafia kuja Makao Makuu ya Mkoa wa Pwani ambayo ni Kibaha Maili Moja. Sisi kule hatuhitaji barabara, tunahitaji kivuko. Kwa hiyo, niombe Serikali iwasaidie wananchi wa Mafia ili kuweza kupata kivuko. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu wa mwisho utakuwa kwenye ukurasa wa 44 kuhusiana na TARURA. TARURA ina changamoto kwamba kile kiasi cha 30% ambacho wanapewa hapohapo kinatumika kwa administration cost lakini nyingine kwa ajili ya maendeleo. Kwa hiyo, kile kiasi cha 30% kiongezwe ifike angalau 50%.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nasema hivyo? Ni kwa sababu tuna barabara ya Vigwaza – Kwala – Dutumi - Kimalamasale ambayo inaunganisha Wilaya tatu za Mkoa wa Pwani, Bagamoyo, Kisarawe na Kibaha Vijijini. Tuna barabara pale ambapo unapita mradi wa bandari kavu, barabara ile TARURA wanasema hawana uwezo nayo, TANROADS wanasema iko kwa TARURA, wamekuwa wanatupiana mpira kati ya TARURA na TANROADS. Naamini kama TARURA wataongezewa hela ya kutosha pengine wanaweza wakaijenga barabara ile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe tu Serikali tusisubiri mpaka ule mradi wa bandari kavu ukamilike ndipo tuweze kuipitisha ile barabara ya lami. Nadhani ni vema tungeitengeneza sasa hata kuvutia wawekezaji waende wakajenge kule hoteli. Pia wakati mradi unaendelea vifaa vinavyotumika kujengea mradi ule wa bandari kavu viweze kupita kwenye barabara ambayo inapitika vizuri. Kwa sasa hivi ile barabara haipitiki vizuri. Kwa hiyo, niiombe sana Serikali iangalie namna bora aidha, kuichukua hiyo barabara kwa upande wa TANROADS…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na naunga mkono hoja.
Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2021/2022 pamoja na Mapendekezo ya Muongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2021/2022
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia Mpango wa Maendeleo. Awali ya yote nipende kumshukuru Mwenyekiti Mungu aliyenijalia kusimama katika Bunge lako Tukufu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiusoma Mpango wa Maendeleo, ukichukua Ilani ya Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi na ukiangalia hotuba za Mheshimiwa Rais, nyaraka zote hizi zinajielekeza katika kukuza uchumi wa nchi yetu, kupunguza umaskini na kuondoa ukosefu wa ajira nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutakubaliana sote hapa Serikali ya Awamu ya Tano imejizatiti katika kukuza uchumi wa nchi yetu na hili linajidhihirisha pale Serikali ya Awamu ya Tano ilipoamua kwa makusudi kuanzisha miradi ama kujenga miradi ya kimkakati ikiwemo Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi ule ambao unaenda kutupa megawatt 2,115 nini tafsiri yake? Tafsiri yake ni kwamba viwanda vilivyopo na viwanda vitakavyojengwa vinaenda kupata umeme wa uhakika, vinaenda kupata ambao hauna kusuasua katika suala zima la kuchakata, kusindika, kuzalisha bidhaa na kupeleka sokoni, jambo ambalo linaenda kuleta mzunguko wa fedha. Bidhaa zinazozalishwa ni kwa ajili ya soko la ndani na zile zinazozalishwa kwa ajili ya kupelekwa nje exportation, jambo ambalo litatuletea forex, ni kitu ama ni chachu inayochochea ama inayochagiza uchumi wa nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ujenzi wa reli iendayo kasi, ujenzi wa miundombinu ya barabara na ununuzi wa ndege mpya 11 vyote hivi kwa pamoja vinachagiza, vinachochea ukuaji wa uchumi wa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiuangalia Mpango, nitapenda kujielekeza jicho langu litaenda katika Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Uwekezaji pamoja na Wizara ya Mifugo. Nikianza na Wizara ya pacha, Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Wizara ya Uwekezaji, ndani ya Mkoa wetu wa Pwani, lipo eneo linajulikana kama Kata ya Kwala, ama linajulikana Kwala. Kwala ni potential sana katika ukuaji wa uchumi wa nchi yetu, ninapoizungumza Kwala ndio kule ambapo kuna biggest dry port, tuna bandari kavu kule, lakini pia tukiizungumzia Kwala, kuna sub-station kubwa ya umeme inayotoka Stigler’s kuelekea Chalinze. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia i ukiizungumzia Kwala umepita pale Mto Ruvu, tunapoizungumzia Kwala kuna reli ya TAZARA pale, tunapoizungumzia Kata ya Kwala kuna central railway line ama SGR na measuring yard. Tutakubaliana halipo eneo katika Tanzania hii linalofana na Kata ya Kwala ndani ya Mkoa wa Pwani, lina vitu vyote, lina vichocheo vyote ambavyo mwekezaji yeyote akifika ndani ya nchi yetu leo hatashindwa kuwekeza pale kwa sababu lina vitu vyote ambavyo vinatakiwa ama niseme mwekezaji anavihitaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda sana kuwaomba Waziri mwenye dhamana ya viwanda na biashara na Waziri mwenye dhamana ya uwekezaji, kuhakikisha wanatenga eneo katika Kata ya Kwala kwa ajili ya ujenzi wa viwanda. EPZA niwaombe sana tuache kuhangaika na maeneo ambayo yanahitaji fidia kwa wananchi, tunapozungumzia Kata ya Kwala pale wala hamuhitaji fidia, lile eneo lipo chini ya Serikali ambayo iko chini ya Wizara ya Mifugo, kwa hiyo Wizara ya Mifugo, Wizara ya Uwekezaji pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara ni watoto wa baba mmoja, wakae chini wazungumze waone namna bora ya kutenga eneo kwa ajili ya viwanda pale. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaombe sana tena sana Mawaziri niliowataja waangalie namna gani wanahakikisha wanalitangaza eneo la Kwala kwa sababu lina kila kitu ambacho leo mwekezaji akija anapata kwa mara moja, maji yapo, umeme upo, barabara ipo, kila kitu kipo, kwa hiyo, nataka niwaombe sana tuliangalie eneo hili kwa sababu linaenda kuleta uchumi wa haraka sana, matokeo ya uchumi tutayaona haraka sana litachochea ongezeko la uchumi na kupunguza umaskini kwa nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa bahati nzuri, Waziri mwenye dhamana ya uwekezaji, Jimbo lake ni Ubungo ambapo kimsingi akienda jimboni lazima atakatisha Mkoa wa Pwani na Waziri mwenye dhamana ya Viwanda na Biashara, Jimbo lake Masasi kimsingi akienda jimboni lazima atakatisha Mkoa wa Pwani. Kwa hiyo, niwaombe sana wakati wanaelekea jimboni wakatishe pale kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani awapatie hiki kitu Pwani Regional Investment Guideline, ambayo imeeleza kwa undani, thamani na ubora na jinsi gani Kwala itakavyoenda ku-boost uchumi wa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Wizara ya Mifugo ambayo kimsingi nimesema eneo kubwa la Kwala liko chini yao, nidhahiri Wizara ya mifugo wamehodhi eneo kubwa pale. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu ameshatoa maelekezo kwamba na sisi kama Mkoa wa Pwani tumeshaandika barua kuomba ekari 4,000 kwa ajili ya kuweka maeneo wezeshi kwa kupokea wawekezaji na kupokea viwanda. Tunahitaji hilo eneo la ekari 4000 kwa ajili ya ujenzi wa hoteli, benki pamoja na maeneo ya huduma za kijamii. Lengo na tija hapa kwamba once viwanda vinapokuja au wawekezaji wanapokuja wakute kila kitu kiko tayari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu mwingine upo katika Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere. Kama ambavyo nimetangulia kusema kwamba Mradi huu unakwenda ku-boost uchumi wa nchi yetu na nipende kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa uthubutu, umahiri na ujasiri, kimsingi hapa tuliwekewa vikwazo vingi kwamba kuna environment impact assessment na vikwazo vinavyofanana na hivyo kuhusiana na ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere lakini leo hii Mheshimiwa Rais wetu amefanikisha, hivi tunavyozungumza overall ya Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere kwa upande wa nishati wameshafika asilimia 30. Nampongeza sana Waziri Dkt. Kalemani, lakini pia nampongeza Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hapa lipo jambo ambalo tunataka kuzungumza kama Taifa, Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere unaenda sambamba na miradi mingine mingine katika Wizara zingine. Nitazungumzia mfano mradi wa kupump maji, Wizara ya Maji hatujasikia chochote mpaka dakika hii katika mradi ule wamefikia wapi na wamefikia hatua gani. Pia Wizara yenye dhamana na kilimo tunazungumzia suala zima la kilimo cha umwagiliaji kwamba ndiyo maana nasema Wizara ya Maji kwa kupitia mradi ule wakiya-pump yale maji inamaana yataenda kuwanufaisha watu wa Kibiti, Rufiji, Mkuranga, Kisarawe na majirani zetu Dar es Salaam. Kwa hiyo, tunapenda tusikie status, mpango ukoje kwa Wizara ya Maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Wizara ya Kilimo, tunasema kilimo cha umwagiliaji. Imezungumzwa na Wabunge wengi humu ndani kwamba viwanda vinahitaji malighafi sasa kama watu wako tayari kwa ajili ya kilimo kikubwa cha umwangiliaji na mradi wa Mwalimu Nyerere unaenda sambamba na masuala mazima ya kilimo cha umwangiliaji, nini kauli ya Serikali mmefikia wapi katika ule mradi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara yenye dhamana na Ujenzi na Uchukuzi, mradi ule unaenda sambamba na ujenzi wa barabara ya Kibiti - Mloka yenye kilometa 97. Vilevile mradi ule unaenda sambamba na barabara ya Kisarawe - Vikuruti ambayo ina kilometa 167 (The Great Nyerere Road).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara yenye zamana na Maliasili na Utalii, Wizara zote ambazo kimsingi kwa namna moja ama nyingine ziko katika Mradi wa Ujenzi wa wa Bwawa la Mwalimu Nyerere tungependa kusikia kauli na mipango kwa sababu mradi ule wa nishati utakapokamilika uende sambamba na hii miradi mingine. Tumesema itakuwa kazi bure kama tutakuwa na viwanda, tutazalisha tutachakata, halafu tutakosa miundombinu ama barabara ya kubeba bidhaa hizo na kuzipeleka sokoni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho ni shukurani, napenda sana kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa namna alivyotusaidia katika Kisiwa chetu cha Mafia kuhakikisha tunapata gati pamoja na kivuko maana ilikuwa adha kwa wafanyabiashara na kwa watu ambao wanachangia uchumi maeneo ya Mafia. Kwa sasa wamepata usafiri wa uhakika, kwa hiyo, wana nafasi nzuri ya kuchangia uchumi wa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, nipenda kutoa shukrani zangu kwa Chama cha Mapinduzi kwa kunipendekeza kuwa Mbunge wa Viti Maalumu kwenye Bunge lako la Kumi na Mbili pamoja na kuwashukuru wanaweke wa Mkoa wa Pwani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, ahsante sana kwa kunipa nafasi, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Tutakubaliana wote hapa kwamba afya ndiyo msingi wa maisha ya binadamu licha ya kwamba kumekuwa na ongezeko la magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza ambayo yanasababisha vifo vya wapendwa wetu. Sekta ya afya ndiyo mahususi kutoa huduma kwa jamii, lakini imekuwa na changamoto kadha wa kadha zikiwemo upungufu wa watumishi na vifaa tiba pamoja na uhaba wa dawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Mkoa wa Pwani tuna uhaba wa watumishi takribani asilimia 52, watumishi wa sekta hii ya afya tulionao kwa sasa ni asilimia 48 tu ambayo kimsingi ni ndogo, hawatoshi kutoa huduma iliyokuwa bora.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Mkoa wetu wa Pwani halmashauri inayoongoza kwa uhaba wa watumishi wa sekta ya afya ni Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji yenye upungufu wa watumishi wa sekta ya afya takribani asilimia 75, ikifuatwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti yenye upungufu wa watumishi wa afya kwa asilimia 71 pamoja na Halmashauri ya Mafia ambayo ina watumishi wa afya asilimia 78 tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sana Mheshimiwa Waziri aziangalie kwa macho matatu halmashauri hizi tatu, tuone namna bora ya kuwaongezea watumishi hawa wa sekta ya afya, hususan Halmashauri ya Wilaya ya Mafia ambayo kimsingi ni kisiwa, watumishi wakipelekwa kule huwa hawakai.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo naomba kuishauri Serikali tuangalie tuje na mpango kabambe wa kuhakikisha tunaandaa motisha. Tutoe motisha ya makusudi kwa hawa watumishi ambao wanafanya kazi katika mazingira magumu; maeneo ya visiwa, maeneo ya Delta na maeneo ya kule ndani ndani (remote/interior). Serikali ikitoa motisha kwa watumishi wetu hawa tutawafanya wavutiwe kubaki katika hayo maeneo, lakini sambamba na hilo, kutoa huduma iliyokuwa bora.

Mheshimiwa Naibu Spika, haikubaliki watumishi wa sekta ya afya Kinondoni na Ilala na wale watumishi wa sekta ya Afya kule Jibondo, Mafia ama wale wanaotoka kule Delta, Kibiti, wote kulipa sawasawa. Hiyo siyo sawasawa. Tena tunaambiwa kwa hawa watumishi waliokuwa Kinondoni na Ilala wenyewe wana motisha ya overtime kwa kuwa wanaona wagonjwa wengi, lakini tumewafikiria hao wanaotoka humo pembezoni. Usafiri mpaka kufika huku mjini kupata zile huduma za kijamii wanapanda kivuko, wanashuka, wanapanda bodaboda wanashuka, wanapanda magari wanashuka na bado wanatembea umbali mrefu. Mishahara yao yote inaishia kwenye nauli. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo Serikali kama ambavyo busara na taratibu waliotumia kuwaongeza watumishi wa mijini kwa kuwa wanaona wagonjwa wengi, busara hiyo hiyo itumike kwa watumishi ambao wanatoka kwenye visiwa, delta na remote areas. Kwa hiyo naomba ushauri huo Serikali iuchukue na iufanyie kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Bagamoyo, Halmashauri ya Chalinze; tunaishukuru sana Serikali mmetupatia gari la wagonjwa (ambulance), lakini TANROADS ikisimamiwa na Wizara ya Afya wanao mradi wa kujenga huduma za majengo ya dharura katika barabara kuu. Kituo cha Afya Chalinze ni miongoni mwa vituo vilivyokuwa barabara kuu lakini pia ni miongoni mwa vituo ambavyo vimepatiwa mradi huu. Sasa naomba Mheshimiwa Waziri wakati anakuja ku-wind up atuambie mradi huu umeishia wapi? Unaonekana kusuasua, hatujui status yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, huu mradi ni muhimu sana kwa sababu hii leo ukipata ajali katika maeneo ya Chalinze pale Kibaha ina maana kupata huduma za dharura wewe mpaka ukimbizwe Mloganzila ama Muhimbili. Kama tungekuwa na huduma za dharura ama hapa Chalinze ama pale kwenye Hospitali ya Mkoa Tumbi, ina maana tungeweza kuokoa maisha ya Watanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, bado tuna changamoto ya foleni sisi, maana foleni ile tuliyoi-clear pale Ubungo ile barabara nane yote inatapikia Kibaha. Kwa maana hiyo tunaomba sana Serikali waje na majibu, watujibu, maana Wanapwani na Watanzania kwa ujumla ambao wanaitumia ile barabara kuu tunataka kujua mradi wa ujenzi wa majengo ya huduma ya dharura umekwamia wapi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri, alifanya ziara yake katika Hospitali ya Mkoa pale Tumbi; majengo yalishaanza kujengwa, yamechakaa na kuchakaa. Kwa hiyo nitaomba atuambie kwamba ule mradi gharama zake ni kiasi gani na wana mpango gani na mradi huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu huu mradi utatusaidia Wabunge tunaoishi Mkoa wa Pwani, Wabunge wa Dar es Salaam, Wabunge wa Lindi, Wabunge wa Mtwara, Wabunge wa Ruvuma pamoja na Wabunge kutoka Zanzibar. Sisi ndio wasafiri wakuu kuja Dodoma kwenye vikao na kurudi majimboni. Mungu aepushie mbali, lakini once tukipata ajali kusema tukimbizwe mpaka Mloganzila ama Muhimbili, ama hakika mradi huu utakwenda kuokoa maisha ya Watanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, imezungumzwa na Dkt. Thea hapa kuhusiana na masuala ya ukeketaji, lakini pia naomba niseme jambo moja; wanaume wa nchi hii wanapenda sana kujadili mpira na wanapenda sana kujadili siasa kuliko ambavyo wangeweza kujadili masuala ya kuhamasishwa kwenda kupima Virusi Vya UKIMWI. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, yaani ukiwakuta kwenye mijadala ya mpira, mijadala ya ukewenza pamoja na mijadala ya masuala mazima haya ya siasa; wangetumia effort hiyo kuhamasishana kwenda kupima Virusi Vya UKIMWI leo hii tungesaidia akinamama. Maana wanaume hawa kwenda kupima UKIMWI wanasubiri mwanamke ashike ujauzito akapime ndiyo wao wapate majibu yao na wakati kila mtu ana immunity yake, kila mtu ana kinga zake. Kwa hiyo nataka niwaombe sana kaka zangu, baba zangu na marafiki zangu, ile nguvu wanayotumia kujadili Simba na Yanga, ile nguvu wanayotumia kujadili siasa na ile nguvu wanayotumia kujadili ukewenza ihamisheni ipelekeni kwenye masuala ya kupima UKIMWI na Virusi Vya UKIMWI. (Makofi/ Kicheko)

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Dkt. Thea kule amezungumza kuhusiana…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Hawa Mchafu, kuna taarifa, sijajua ni Mbunge gani aliomba kutoa taarifa.

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Sawa, Mheshimiwa Twaha Mpembenwe.

T A A R I F A

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimpe taarifa tu mzungumzaji kwamba asilimia 99 ya wanaume ambao ni Wabunge katika Bunge hili la Kumi na Mbili, taarifa zilizopo ni kwamba wamepima UKIMWI. Ahsante. (Kicheko)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Twaha, naona hata wenyewe wanakushangaa maana hawajapima na kama wamepima hawajachukua majibu. (Kicheko)

Mheshimiwa Hawa Mchafu.

MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru; siipokei taarifa ya Mheshimiwa Twaha kwa sababu kama anasema kweli, hicho anachokisema wakihamishe sasa kwenye majimbo yao wakawatangazie na wananchi wao ili waweze kufanya hivyo hivyo, kwamba tukipata asilimia 90 ya wananchi wanaume kwenye jimbo lake wamepima, sina shaka Tanzania tutakuwa tuko vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, bado niko hapohapo kwa wanaume wa nchi hii, kwamba tumeambiwa madhara ya ukeketaji, lakini wanaume hawa ndio watu wa kutusaidia sisi. Wakitoka huko nje wakasema aliyekeketwa na ambaye hakukeketwa nani yuko vizuri, lakini wanaume hawa wakisema kwamba hawa waliokeketwa hawatawaoa, sina shaka itakuwa ni njia, itakuwa ni mwarobaini wa kusaidia kupunguza ukeketaji. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, natoka sasa hapo kwa wanaume, mchango wangu mwingine ni kuhusu suala zima alilozungumza Mheshimiwa Askofu Gwajima kuhusiana na chanjo ya Corona na madhara yake. Nikiwa kama Mjumbe wa Kamati ya Masuala ya UKIMWI tulipata fursa ya kutembelewa na watu wenye hii dawa inaitwa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na naunga mkono hoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Dakika moja, hebu elezea dawa gani. (Makofi)

MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Nilikuwa nataka kuizungumzia hii dawa Phyt Exponent. Imeonekana kusaidia watu wengi sana kwenye masuala ya Corona. Kwa bahati nzuri Mkemia Mkuu ameicheki na amethibitisha kwamba inafaa kuwa ni medicine, lakini inatambulika kama supplementary na inauzwa ghali, shilingi 150,000. Ili kuwasaidia Watanzania waweze kuipata hii dawa, ikianza kufahamika kama ni medicine, madaktari wakiweza kui-prescribe ina maana itauzwa madukani kwa bei rahisi, tutaweza kusaidia watu wetu na janga zima la Corona. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo nikushukuru sana kwa kunipa nafasi. Naunga mkono hoja. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia Bajeti Kuu ya Serikali. Napenda kumpongeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kwa kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nipende kuipongeza Serikali yake kwa kuja na bajeti nzuri ambayo ina mguso kwa Watanzania wote. Katika bajeti ya kwanza kabisa ya Rais Samia Suluhu Hassain imefanikiwa kugusa makundi yote katika jamii.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikianza na kundi la wakulima; zipo tozo pamoja na ushuru ambazo zimeondolewa katika mapendekezo haya ya bajeti. Nia, lengo na kusudi ni kuwawezesha wakulima wetu waweze kulima kilimo chenye tija. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia ukisoma mapendekezo ya bajeti, unakuta kuna lengo ama dhamira ya kuongeza tija kwa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi. Sambamba na hilo pia wanakusudia kutafuta masoko kwa ajili ya mazao hayo ya wakulima yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nikiangalizia kundi lingine ambalo ni kundi muhimu sana, ni kundi la wafanyakazi ama watumishi. Tutakubaliana sote hapa Serikali inapata kodi yake ya uhakika katika vyanzo vyake vyote vya kodi, kodi ya uhakika inatoka kwenye kundi la wafanyakazi. Ni kodi ambayo haina kuvutana mashati, ni kodi ambayo haina kuifukuzia, yaani ipo inapatikana kiurahisi kabisa. Tunampongeza sana Mheshimiwa Rais Samia kwa kuona umuhimu wa kupunguza kodi ya pay as you earn kwa watumishi wa Taifa hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kwa muda mrefu sana takribani miaka mitano ama miaka sita, watumishi wa Taifa hili wamekuwa wakinungunika juu ya masuala mazima ya kupanda daraja ama ya kupanda vyeo. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia katika bajeti yake ya kwanza kabisa kukusudia kutenga bilioni 449 kwa ajili ya kupandisha vyeo watumishi 92,619.

Mheshimiwa Naibu Spika, tutakubaliana ni haki ya msingi ya watumishi kupanda madaraja ama kupanda vyeo na unapokuwa unawapandisha vyeo watumishi tafsiri yake ni kwamba …

T A A R I F A

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Getere natumaini unataka kutoa taarifa na siyo kuchangia, Mheshimiwa Getere.

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli nataka kutoa taarifa kumpa mzungumzaji anayeongea. Alipozungumza ile malipo ya pay as you earn, nataka kujua tu anapoendelea kwenye mchango wake majibu yake yaje yapatikane kwamba asilimia iliyotolewa ni ipi, kuna watu wa kundi la kwanza ambao wanamshahara wa 270 mpaka 540 ambao wana asilimia 9.0, wanakwenda
mpaka asilimia 10...

NAIBU SPIKA: Sasa hebu ngoja tuelewane hiyo ni taarifa au unamuuliza swali? Kwa sababu yeye hana uwezo wa kukujibu wewe.

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kuchangia tu, watakavyompa majibu watuambie kwamba...

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Hawa Mchafu, endelea na mchango wako.

Waheshimiwa Wabunge, Mbunge akiwa anaenda na mchango wake hivi, ukimkatisha njia yaani ile namna anavyoenda unamchelewesha. Kwa hiyo usimame kutoa taarifa kama hasa unataka kuongeza kwenye jambo ambalo unaona yeye hajamaliza vizuri pengine hoja yake. Sasa yuko katikati ya jambo, wewe umeingia hapo hata point yake hajamaliza bado.

Mheshimiwa Hawa Mchafu.

MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naendelea kwa kusema kwamba tunampongeza Mheshimiwa Rais kwa kutenga hizo bilioni 449 kwa ajili ya kupandisha vyeo watumishi wa Taifa hili. Nilikuwa nasisitiza kwa kusema kwamba mtumishi yoyote ambaye ana haki anastahili kupanda cheo, unapompandisha cheo unampa moraly na ari ya kufanya kazi kwa ufanisi, jambo ambalo litaenda kuchochea na kuchagiza kodi iweze kupatikana zaidi kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kubwa zaidi ambalo Rais Mheshimiwa Samia amelifanya na limenigusa kwa namna moja ama nyingine nilikuwa mtumishi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Kwenye Bunge lililopita nilikuwa nikiwakilisha wafanyakazi. Rais, Mheshimiwa Samia amefanya jambo kubwa sana kudhamiria kulipa madeni ya hifadhi ya jamii.

Mheshimiwa Naibu Spika, hiki alichokuja nacho hapa ni mwarobaini wa kuhakikisha tunatenga fedha za bajeti na zinaenda kutumika katika utaratibu wa hati fungani ili kwenda kulipa madeni ya hifadhi ya jamii. Hii nini maana yake? Ni kwamba hifadhi ya jamii ilikuwa na madeni ya muda mrefu sana na madeni ambayo yalikuwa yakienda yakikua katika mifuko yetu ile mitano.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kama Serikali imeamua na kudhamiria kufanya hivyo, wakitenga fedha kwenye bajeti na kupeleka kwenye hati fungani na baadaye kulipa kulipa madeni kwa Mfuko tuliokuwa nao sasa wa PSSSF, tafsiri yake ule Mfuko unaenda kukuwa, Mfuko ule unaenda kuwa na ukomavu, sasa kile kilio cha wastaafu kinaenda kumaliza na mapendekezo haya. Ile kauli mbiu ya Mfuko wa LAPF iliyokuwa ikisema mstaafu wa leo analipwa kesho, kwa huu mwarobaini aliokuja nao mama Samia ndiyo inaenda kutekelezeka kwa vitendo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo hili lilikuwa likipigiwa kelele sana na ndugu yangu Ester Bulaya pamoja na Mheshimiwa Halima Mdee kwenye Bunge lililoisha na Bunge hili. Hivyo nitawaomba sana mapendekezo haya yakipita tutakapofika kupiga kura siyo dhambi wakapiga kura ya ndiyo kumpongeza Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassain kwa sababu ametii kiu yao ya muda mrefu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitaomba sana Mheshimiwa Mwigulu akija atufafanulie jambo moja, kulikuwa na watumishi waliokuwa wanafanya kazi Serikali Kuu ambao kimsingi walistaafu kabla ya mwaka 1999, watumishi wale Serikali ilisema walipwe mafao yao na Mfuko wa PSSSF. Sasa wale walilipwa lakini lile deni halikulipwa ambalo linajulikana kama pre-1999 na muda wote ulikuwa tukijadili madeni ya hifadhi ya jamii pre-1999 tulikuwa tunaijadili separate. Kwa hiyo nataka kujua kwenye hii dhamira waliyoileta ya kutaka kutenga hii hati fungani kulipa madeni ya hifadhi ya jamii na pre- 1999 iko included. Kama watakuwa wamefanya hivyo Mheshimiwa mama Samia atakuwa amemaliza kabisa kilio cha Trade Union, cha wafanyakazi, cha watumishi, pamoja na wastaafu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kundi lingine ambalo linaguswa katika bajeti hii ni kundi la vijana na akinamama. Bajeti inakusudia kwenda kuboresha uwezeshaji wa wananchi kiuchumi. Tunaposema kuwawezesha wananchi kiuchumi ni kundi linalokusudiwa hapa ni akinamama pamoja na vijana na juzi alivyotuita wanawake wa Taifa hili alizungumza ana dhamira ya kuhakikisha anataka kuhakikisha haya majukwaa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi. Kwa maana hiyo hapa wanawake watanufaika na vijana watanufaika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kundi lingine ambalo linanufaika kwenye bajeti hii ni kundi la wafanyabiashara, kundi la wawekezaji hususani wenye viwanda, ukiangalia bajeti kwamba Mheshimiwa Waziri anakusudia kuondoa sharti la kuweka dhamana la asilimia 15 ya ziada ya ushuru wa forodha iliyorejeshwa kwenye sukari ya matumizi ya viwandani.

Mheshimiwa Naibu Spika, hili ni jambo kubwa sana, wakati tupo hapa Bunge lako linaendelea walikuja wadau wa viwanda chini ya mwavuli wa CTI. Katika mambo waliyokuwa wanayalalamikia, liko hili la kuondoa hii tozo asilimia 15, lakini lipo lile la kuondoa ama kupunguza tozo ya mabango ambayo kimsingi nadhani imependekezwa ishuke kutoka asilimia 15 mpaka asilimia 10, if I am not mistaken. Napenda sana kuipongeza Serikali na kama hivyo ndivyo basi kazi imebaki kwao wenzetu wenye viwanda kuhakikisha wanaongeza uzalishaji, wanaongeza ajira, lakini pia wanalipa kodi stahiki kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naomba nimwonyeshe Mheshimiwa Waziri Sehemu ambayo kimsingi hajatolea jicho, pale tunaweza tukapata mapato ama tukapata kodi. Tukizungumzia uvuvi wa wa Bahari Kuu, tukizungumzia kule deep sea, sisi kama nchi hatuna meli itakayoweza kwenda kuvua kule, lakini sisi kama nchi hatuna bandari ya uvuvi kwa utaratibu meli kubwa kutoka nje zinalipa tozo kidogo kwa Wizara wanapewa kibali wanaenda wanavua. Wanavua tones and tones za samaki ambazo zinapatikana katika eneo la Jamhuri ya Muungano, ambayo ni bidhaa ya Jamhuri ya Muungano.

Mheshimiwa Naibu Spika, kimsingi bidhaa ile inayopatikana katika mipaka ya bahari ya Jamhuri ya Muungano haikatwi kodi. Kwa hiyo nimwombe sana Mheshimiwa Waziri, TRA waone namna bora ya kufanya makadirio ili tuweze kutoza kodi zile tozo tunazotoza ili kuwapa kibali wakavue, ni maduhuli tu yale madogo madogo, lakini tuweke utaratibu wa kisheria ili tuweze kutoza kodi hao samaki wanaoweza kwenda kuuzwa huko duniani.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, ukiangalia katika ukurasa wa 41(e) cha hotuba ya Mheshimiwa Waziri anasema anakusudia kuongeza ushuru wa forodha kutoka asilimia 25 mpaka 35 kwenye bidhaa ya marumaru. Bidhaa za marumaru…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimalizie kidogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimalizie kidogo. Kwa bidhaa hizo za marumaru zinazotoka nje, Mheshimiwa Waziri kuongeza tozo ni sahihi kabisa, kwa sababu anakusudia kulinda viwanda vyetu vya ndani. Tunapozungumzia suala zima la viwanda, mkoa unaoongoza kwa viwanda ni Mkoa wa Pwani; na ukizungumzia masuala mazima ya viwanda vya tyles, unavikuta Mkuranga, Mkiu, Chalinze, Bagamoyo na Kisarawe. Kwa kufanya hivyo, atavilinda viwanda hivi, wataweza kuzalisha, kulipa kodi na kutoa ajira kwa Watanzania.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana.

MHE. HAWA M. CHAKOMA Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuipongeza Serikali kwa miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea katika nchi hii. Licha ya pongezi hizo, kumekuwa na changamoto nyingi mno zinazoikabili Wizara hii nazo ni kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa bandari hususani Bandari ya Dar es Salaam ina changamoto kubwa ya ujenzi wa magati na kina kirefu cha maji. Yapata miaka kumi na zaidi Serikali inahangaikia changamoto ya upanuzi wa gati hizo (gati namba 7 hadi 13). Licha ya changamoto ya gati na changamoto zote zinazoikabili Bandari yetu ya Dar es Salaam kushindwa kushindana na bandari jirani, ni vema Serikali ikajitathmini upya miaka 10 au 20 baadae hii bandari itaelemewa kupita kiasi hivyo muda umefika sasa kuigeukia Bandari ya Bagamoyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Bandari ya Bagamoyo ni bandari ya kimkakati, ni mbadala mzuri kabisa wa Bandari ya Dar es Salaam. Mchakato wa bandari hii ulianza muda mrefu sana tangu mwaka 2012 - 2018 haujakamilishwa hususani wa fidia kwa wananchi wa Kata ya Zinga. Mwekezaji yupo tayari kuanza kulipa fidia wananchi wa kata hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna minong’ono kwamba mwekezaji atakuwa tayari kuchukua na kufidia ndani ya hekta 3,000 ila Serikali inahitaji mwekezaji achukue hekta 9,000. Yeye ameshajipambanua atakuwa na uwezo wa hekta 3,000 sasa hekta 9,000 hazihitaji hizo zote ni nyingi mno yeye anahitaji hekta 3,000 aendelee na kazi hii habari ya hekta 9,000 tunaweka mkwamo usiokuwa na msingi. Mnakwamisha zoezi kwa kung’ang’ania hekta 9,000 badala ya hekta 3,000 alizozihitaji mwekezaji. Serikali ifike mahali imruhusu mwekezaji a-develop hekta 3,000 kama alivyoomba ili kurahisisha eneo la bandari kuwa wazi na wananchi kuanza kulipwa fidia zao haraka na miundombinu ya kijamii ihamishwe haraka kama shule na zahanati.

Mheshimiwa Naibu Spika, nipende kutoa masikitiko yangu kwa Serikali. Inasikitisha sana watu hawajaondoka, hawajafidiwa, bado wanaishi pale lakini Serikali inaondoa wahudumu kwenye shule na zahanati ikiwa ni njia ya kushinikiza wananchi wapishe eneo la bandari. Watapisha vipi ilhali bado hawajafidiwa?Kibaya zaidi hiyo shule na zahanati zimejengwa kwa nguvu za wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kampuni ya Mawasiliano ya Simu (TTCL) ni Shirika la Umma ambalo linaushindani na mashirika ya simu ya binafsi (Tigo, Voda, Halotel na kadhalika). Shirika letu la umma lina madeni makubwa linadai taasisi na mashirika ya umma kitu kinachopelekea kushindwa kujiendesha na kushindana na mashirika binafsi. Hivyo ni vema wakalipwa madeni hayo ili wafanye kazi vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, watumishi wa TAZARA wana madai ya muda mrefu ya malimbikizo ya mishahara, overtime na marupurupu yao. Ni vema Serikali izingatie suala la ulipaji madeni ya watumishi ili wafanye kazi kwa ufanisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, mbali na hilo deni la mishahara ya watumishi, pia TAZARA imekuwa inakabiliwa na changamoto ya sheria yake kupitwa na wakati na kutoenda na wakati ulipo. Suala la CEO wa TAZARA kwa sheria ya sasa ni lazima atoke Zambia jambo ambalo sio sawa kwa maendeleo ya reli yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia kwa mapungufu makubwa ya sheria hiyo hiyo kumekuwa hakuna condition juu ya masuala ya fedha, kitu ambacho mwaka huu wa fedha unaisha Serikali zote mbili Tanzania na Zambia tumetenga fedha za maendeleo shilingi bilioni 26; shilingi bilioni 16 toka vyanzo vya ndani vya TAZARA na shilingi bilioni 10 kutoka Serikali Kuu. Kwa upande wa Tanzania fedha hizo shilingi bilioni 10 tayari zimeshatolewa ila kwa wenzetu wa Zambia hadi hivi tunavyozungumza bado hazijatolewa. Sasa hapa tunaongelea maendeleo ya reli ya TAZARA, je, yanaafikiwaje kama upande wa Muungano mwingine wa reli hawatengi fedha hizo?

Mheshimiwa Naibu Spika, niombe sana Serikali ilete mabadiliko ya sheria, sheria hiyo ya TAZARA ifanyiwe marekebisho na viwekwe vifungu vinavyoweza kuweka masharti juu ya masuala ya fedha kwa maendeleo ya reli yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchangia katika hotuba hii ya Mheshimiwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, nianze kwa kuunga mkono hoja iliyopo mezani, sambamba na kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kazi nzuri ya kuendeleza sekta ya elimu nchini na hili linathibitishwa na masuala yafuatayo:

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa ni masuala ya elimu bure kwa watoto kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne. Serikali kila mwaka imekuwa ikitenga karibu shilingi bilioni 263.6 kwa ajili ya kuhudumia elimu ya watoto wa Kitanzania, ni budi kuipongeza Serikali kwa hatua hii kwani ni Serikali chache duniani zinatoa au kupatia wananchi wake elimu bure.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ambalo ni kubwa ambalo Serikali ya Awamu ya Tano inafanya kwenye sekta hii ya elimu ni pamoja na mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini. Kila mwaka Serikali imekuwa ikitenga karibia 483 bilioni kwa mwaka kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi, hili ni jambo la kuungwa mkono maana karibia wanafunzi laki moja wamekuwa wakinufaika na mikopo hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, licha ya pongezi hizo, pia nijikite kwenye changamoto zinazoikabili sekta hii ya elimu nchini nazo ni kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, utitiri wa nyaraka zinazokinzana katika kusimamia elimu ya msingi, sambamba na Sheria ya Elimu kutokukidhi mahitaji ya wakati uliopo. Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 (Na. 25) imepitwa na wakati, haiendani na mahitaji ya sasa na hili lilijitokeza baada ya mabadiliko ya Sera ya Elimu mwaka 2014. Aidha, kumekuwa na utitiri wa nyaraka unaotumika kusimamia utoaji wa elimu nchini ambazo kimsingi kwa sehemu kubwa zinakinzana. Ninapenda kuishauri Serikali ione umuhimu wa kufanya marekebisho ya Sheria ya Elimu Namba 25 ya mwaka 1978, ifanyiwe marekebisho ya haraka ili iweze kuendana na Sera mpya ya Elimu ili iweze kuendana na wakati uliopo au mahitaji ya sasa. Pia Serikali iangalie namna ya kuifanyia marekebisho kupitia upya nyaraka na miongozo inayokinzana na kufanyiwa marekebisho ili kukidhi mahitaji ya wakati uliopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto ya pili ni mfumo wa ufundishaji wetu hasa kwa masomo ya kiingereza na kiswahili kwa shule zetu za awali hadi msingi hususani darasa la pili. Tafiti za kisayansi zinaonesha ufundishwaji wa lugha kwa binadamu huweza kujifunza vizuri na kwa urahisi lugha yoyote akiwa katika umri mdogo. Hivyo ni vema misingi ya ufundishaji wa lugha ikajengwa kimfumo ili kuwawezesha watoto kumudu lugha hizo kuanzia madarasa ya awali. Wakati sera inatambua kiswahili na kiingereza kuwa ni lugha rasmi zinazotumika katika ngazi mbalimbali za elimu nchini, bado ufundishaji wake haujajengwa kimkakati kuanzia elimu ya awali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ilivyo sasa kwenye mfumo wa ufundishaji wanafunzi wanaosoma shule zinazotumia kiswahili kama lugha ya kufundishia kuanzia elimu ya awali, hawasomi somo la kiingereza hadi wafike darasa la tatu na kwa wale wanaosoma shule zinazotumia kiingereza kama lugha ya kufundishia, hawatakiwi kusoma kiswahili hadi wafike darasa la tatu ingawaje wote wanatarajiwa kufanya mitihani inayofanana kwa masomo hayo wafikapo darasa la nne.

Mheshimiwa Mwneyekiti, jambo hili kama litaachwa liendelee litakuwa na madhara makubwa kwa vijana wetu maana makundi yote wanakosa umahiri wa lugha nyingine kwa kukosa misingi yake kuanzia hatua za awali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika changamoto hii ya mfumo wa ufundishaji katika lugha, ninapenda kuishauri Serikali iangalie upya juu ya suala hili hususani masomo ya lugha ya kiingereza na kiswahili, yafundishwe sambamba kuanzia elimu ya awali ili kuwajengea msingi unaofanana na mzuri vijana wetu na hivyo waweze kumudu vema masomo yao katika ngazi ya sekondari na elimu ya juu. Ni vema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali iongeze uwekezaji hasa katika ufundishaji fasaha wa somo la kiingereza ambalo ndilo linalotumika kuanzia elimu ya sekondari kwa shule zote hadi elimu ya juu nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto ya mihula na siku za masomo kwa shule za awali, msingi na sekondari nchini inayochochewa na changamoto kubwa ya usafiri nchini hasa kwa watoto wadogo wa shule za awali na msingi huhitaji kusoma kwa muda mfupi na kupumzika. Hivyo, nashauri Serikali iruhusu utaratibu wa kuwa na mihula mitatu kwa shule za msingi, awali na sekondari nchini kama inavyofanywa na nchi nyingi za Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naunga mkono hoja.
Makadilio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Awali ya yote nipende kumpongeza Mheshimiwa Waziri na Naibu wake wanafanya kazi vizuri sana na nipende kusema Waziri na Naibu wake ni wasikivu na wanyenyekevu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninachotaka kukuomba Mheshimiwa Waziri ile speed uliyoanza nayo wakati unateuliwa naamini umejipumzisha kidogo mara baada ya kutoka hapa ukaendelee nayo ile ile dhidi ya haya malalamiko yanayotolewa hapa ya askari wako kuuwa watu na kuliza watu, nikuombe sana Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kitu kingine ambacho nataka kusema tunapozungumzia utalii ni international business ni biashara ya kimataifa. Tuna vivutio vingi tunachangamoto ya miundombinu. Niliuliza swali last week linalohusiana na urithi wa malikale kule Kilwa Kisiwani hapaendeki hakuna kivuko cha uhakika hakuna miundombinu ya kueleweka. Kwa hiyo, niombe sana hii changamoto ya ufinyu wa bajeti ama huku kupunguzwa kwa bajeti kwa asilimia 22 ni tatizo, tuwaongezee bajeti kwa bahati nzuri tunapozungumzia Wizara ya Maliasili na Utalii kuna mashirika ya kimataifa ambayo yana-support wizara hii au sekta hii lakini pia tuiombe Serikali suala zima la miundombinu ya maeneo husika liko kwenye mikono yenu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kitu kingine nilichotaka kusema kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri ukurasa wake wa tano alisema malengo ya Wizara yanaendeshwa kupitia sheria, kanuni, taratibu na mikakati. Baadhi ya sheria kwenye wizara hii zimepitwa na wakati. Nikuombe sana Mheshimiwa Waziri uangalie namna bora ya kwenda kuzifanyia marekebisho Sheria ya Malikale lakini pia Sheria ya Masuala mazima ya Utalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine sambamba na hilo ni kuhusiana na suala zima la Sera. Sera ya utalii ya mwaka 1999, Sera ya Malikale na Sera ya Utamaduni hebu tuziangalie hizi sera tuone kama tunaenda nazo vile ambavyo zilivyoandikwa. Sera zinasema katika kila Mkoa na kila Wilaya tuwe na cultural centre, lakini katika uhalisia hivyo vitu havipo. Kwa hiyo tuangalie matakwa ya sera hii kama bado tunaenda nayo na kama yako vinginevyo basi tuende tukazifanye kuzipitia upya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kingine Serikali imehamia Dodoma. Dodoma sasa hizi ni Jiji na hatuna museum hapa Dodoma na tutapokea wageni wengi sana kutoka mataifa mbalimbali na wenzetu kati ya vitu ambavyo wanavipendelea mara baada ya kazi ni kujifunza tamaduni mbalimbali ama kujifunza historia ya eneo husika. Kwa hiyo, niishauri Serikali ione umuhimu wa kuanzisha museum hapa Dodoma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala lingine twende Pwani kidogo, Mheshimiwa Dau jana alizungumza kwa masikitiko ya hali ya juu kuhusiana na viboko wanaouwa watu. Lakini pia kule Kisarawe kuna mamba wanaokula watu. Niombe sana Wizara ya Maliasili na Utalii muende mkavune mamba wale, muende mkavune viboko wale kwa sababu itakuwa ni wazuri kwa masuala ya utalii. Kule waliko Kisarawe Mafidhi na kule waliko Mafia wanasababisha madhara makubwa sana.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu ya muda naomba tumalizie na maporomoko ya Mto Njombe. Maporomoko ya Mto Njombe…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2018
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia ripoti ya Kamati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nipende kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunisimamisha mbele ya Bunge lako tukufu, lakini pia nipende kuipongeza Serikali katika mwaka wake wa fedha 2018/2019 imeweza kutenga kiasi cha shilingi trilioni 4.2 kwa ajili ya sekta ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwenendo huu wa bajeti unakwenda vizuri kwani katika sekta hii ya uchukuzi na mawasiliano ina miradi mikubwa na mingi sana hivyo nipende kuipongeza Serikali…

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, Mheshimiwa Hawa Mchafu ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, msikilizeni atoe vipande sasa. (Makofi)

MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo nipende kuipongeza sana Serikali na niseme tu nipende kuishauri Serikali sambamba na ushauri tulioutoa kwenye Kamati kuhakikisha bajeti inatolewa kwa wakati ili miradi yote ya maendeleo iweze kutekelezeka kwa wakati ikiwa ni ishara ya kupunguza madeni lakini pia kuipeleka nchi yetu kwa kasi iliyokuwa kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kuchangia mchango wangu wa kwanza katika Shirika la Ndege la ATCL, nipende sana kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ndani ya kipindi kifupi ameweza kununua ndege sita na ndege zingine ziko njiani zinakuja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia niseme, hii imewezesha kurahisisha huduma ya usafiri wa anga lakini pia imeongeza idadi ya safari na miruko kitu ambacho kinakwenda kuchochea ongezeko la ajira, ongezeko la watalii nchini lakini pia mapato yanakwenda kuongezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nipende kutaarifu Bunge lako tukufu, mnamo mwaka jana mwezi wa nane, Shirika la ATCL lilizindua safari ya kwenda Entebbe - Uganda, lakini Bujumbura-Burundi. Niseme mwezi wa pili mwaka huu tunakwenda kuzindua safari ya kwenda Johannesburg -South Africa, Harare pamoja na Lusaka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya ni maendeleo makubwa, lakini nipende tu kuishauri Serikali, tumenunua Ndege zetu kwasababu ya safari za ndani, safari za kikanda na safari za kimataifa. Ushauri wangu kwa Serikali ni kwamba mharakishe mchakato uliokuwepo kati ya TCAA ya Tanzania na CAA ya nchini China ikiwezekana hata mtumie Balozi zetu watupe majibu sasa ni lini mchakato unakamilika ili tuanze safari za kwenda Bombay. Sambamba na hilo pia nipende kuitaka Serikali kuharakisha mchakato uliopo baina ya nchi ya China na Tanzania ili kuhakikisha safari ya Guangzhou inaanza haraka iwezekanavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu mwingine upo katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Mwalimu Nyerere. Kumekuwa na changamoto kubwa ya ucheleweshaji kwa malipo ya treasury voucher, hii inapelekea mzigo kukaa muda mrefu bandarini. Hivyo itakumbukwa kwamba gharama za kuhifadhi mzigo bandarini wakati mwingine zinazidi hata ile gharama ya kilichonunuliwa zile bidhaa ama ile mizigo gharama yake inakuwa ni kubwa zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vitu vyote ambavyo vina exemption kutoka kwake ni lazima taratibu wa GN zikamilike. Huwezi kutoa vitu vyenye exemption ya VAT kama GN haijakamilika na ukisema unatoa kwa utaratibu huo unakuwa umevunja sheria. Sasa ninataka niwaombe TRA maana hatuna sababu leo hii tuliuliza kwa nini viti vya uwanja wa ndege vya terminal three mpaka leo havijafungwa? Lakini kwa nini lift ya uwanja wa ndege wa terminal three mpaka leo haijafungwa? Ni kwa sababu tunaambiwa masuala haya ya GN hayajakamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiri, kwa kuwa mnafahamu TRA ule mzigo uko exempted, lakini ule mzigo pia unatakiwa ufike katika terminal three, vyombo vya usalama vipo. Ushauri wetu tunashauri TRA sambamba na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ikibidi hata muwa-escort mfike mpaka eneo husika wakati vinafungwa mpo, mnashuhudia kwamba kweli huu mzigo ama hizi bidhaa ni kwa sababu ya terminal three. Hatuna sababu ya kuchelewa kwa sababu ya masuala ya GN, wakati sisi huku tunaendelea na hizo process za GN huku zinaendelea. Kwa kufanya hivi tutaharakisha ama tunahatarisha process ya mkandarasi kuongezeka anapata muda, muda wa mradi unakuwa ni muda mrefu zaidi muda ule wa kukamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu mwingine uko kwa Shirika la Posta Tanzania, Shirika la Posta lina changamoto kubwa ya kulipa pension ya wafanyakazi. Mpaka mwezi Juni, 2018 imelipa tayari shilingi bilioni 4.9 pasipo Serikali kuwarejeshea lakini wakati huo huo TRA inawadai Shirika la Posta deni la shilingi bilioni sita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, deni hili limetokana na kipindi kile Posta inashindwa kujiendesha ama inashindwa kufanya biashara vizuri. Kilichopo hapa baba anamdai mtoto na mtoto anamdai baba. Kwa kuwa Shirika letu la Posta limeanza kuimarika na kwa kuwa Shirika letu la Posta liko kwa ajili ya kufanya biashara kushindana na akina DHL, kushindana na wakina Forex, ushauri hapa tunaoutoaWizara ya Fedha na Mipango ikae chini na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Miundombinu waangalie namna bora aidha ya kuwaondoshea hili deni ama kama siyo kuwaondoshea hili kuwapounguzia hili deni kwa sababu Shirika la Posta linaidai Serikali na Serikali inaidai Shirika la Posta. Kwa hiyo, naomba sana Serikali iliangalie hilo ili tuweze kusaidia Shirika la Posta lisimame vizuri na liweze ku-compete na Mashirika mengine ya Kimataifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu mwingine utakuwa kwa Shirika la Kampuni ya Meli (MSCL), nipende kuipongeza sana Serikali katika mwaka wake wa fedha 2017/ 2018 ilitenga takribani shilingi 24,496,000,000 kwa ajili ya ununuzi wa meli mbili mpya. Tuna kila sababu ya kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa jinsi anavyoikimbiza nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, shilingi bilioni 24 tayari zimeshatolewa na kilichokwenda kufanyika mpaka sasa tumeshalipia ama imeshalipiwa advance payment kwa sababu ya chelezo. Lakini pia nyingine niseme wamelipa advance payment ya kuanza kujenga meli mpya na advance payment nyingine imetolewa kwa ajili ya ukarabati wa MV Victoria na MV Butiama kwa ajili ya Ziwa Victoria. Kwa hiyo, haya ni mapinduzi makubwa sana tuna kila sababu ya kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kikubwa kile anachokifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru sana, naunga mkono hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge na Utawala na Serikali za Mitaa pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuchangia taarifa za Kamati zilizopo mbele yetu. Kwa dakika tano ulizonipatia nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa namna anavyotekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Pwani ndiyo mfano mzuri sana kwa namna gani Mheshimiwa Rais ameweza kutekeleza Ilani. Nasema hivyo nikiainisha miradi mitano ya kimkakati ama miradi mitano ya Kitaifa yote inaonekana ama inapatikana ndani ya Mkoa wa Pwani. Tuna mradi wa kufua umeme Bwawa la Mwalimu Nyerere, unapatikana Rufiji Mkoa wa Pwani, tunao mradi wa njia nane ambao unapatikana Kibaha Mkoa wa Pwani, tunao mradi wa ujenzi wa bandari kavu inapatikana Kibaha Mkoa wa Pwani, tuna mradi wa reli iendayo kwa haraka standard gauge ambayo kimsingi pia inapita Mkoa wa Pwani na pia tunao ujenzi wa viwanda unaoendelea takribani kwenye mikoa yote ya Pwani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, sina budi kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa hili kubwa analolifanya. Sambamba na hilo, napenda sana kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa ununuzi wa ndege. Napenda tu kusema kwamba muda siyo mrefu, ndani ya mwaka huu tunatarajia kwenye kupokea ndege nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri hapa watu wanashindwa kufungamanisha maisha ya watu pamoja na aspects za uchumi. Wanaposema wananchi hawataki ndege ni kwamba wanashindwa kuainisha ni kwa namna gani ndege zinaweza kuingizia nchi yetu mapato ambayo kimsingi mapato yale yakikusanywa yakiingia kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina, ndiyo yanaenda kulipa Elimu Bila Malipo, ndiyo yanaenda kwenye miradi ya maji na elimu ya juu. Kwa hiyo, sijajua wenzetu wanafeli wapi? Ila nafikiri wanashindwa kuoainisha hivi vitu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ninalopenda kusema, kazi kubwa ambayo Mheshimiwa Rais anafanya na hatuna budi kumpongeza na bado nikuchukulia mfano wa Mkoa huo wa Pwani, ametupatia miradi mbalimbali kwenye Wilaya mbalimbali za Mkoa wetu wa Pwani ya ujenzi za Ofisi za Halmashauri. Tuna ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri Kibiti, ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri Kibaha, ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri Mafia na ujenzi wa Ofisi za Halmashauri Kibaha Vijijini. Kwa sababu hiyo, Mheshimiwa Rais anafanya mambo makubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile ujenzi wa Hospitali za Wilaya, Mheshimiwa Rais ametoa shilingi 1,500,000,000/= kwa ujenzi wa Hospitali za Wilaya karibia kwenye Wilaya nne za Mkoa wa Pwani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hayo yote na mengine mengi yanayofanywa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli hatuna sababu ya kushindwa ifikapo Oktoba, 2020. (Makofi/Vigelegele)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yamekuwepo hapa malalamiko juu ya uhamasishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, kwamba inasemekana daftari limekuja mwishoni. Daftari hili lilianza nyuma kidogo, liko linaendelea kutoka Mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine. Mkoani kwetu linatarajia kuingia muda siyo mrefu mnamo tarehe 14 mpaka tarehe 20. Serikali imefanya kazi kubwa ya uhamasishaji, lakini suala la uhamsishaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura lina mahusiano ya karibu na ushikaji wa dola. Kwa maana hiyo, kama unataka Serikali ndiyo ikuhamasishie, hakika itakapifika hapo kesho kutwa tutakapoenda kupata ushindi wa kishindo, bado mtabaki kulalamika na Wakurugenzi, bado mtabaki kulalamika na kuibiwa kura, lakini dola inatafutwa, dola inaandaliwa, dola inachakarikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mziki wa Mheshimiwa Magufuli sioni wa kumuingia mpaka sasa. Kuna mambo makubwa ambayo yamefanywa na Mheshimiwa Rais na pengine wenzetu walikuwa wanadhani pengine Mheshimiwa Rais ana-bip, lakini kwa matokeo ya Serikali za Vijiji na Vitongoji, walipoona mziki umekaa vibaya, ndipo walipoona ngoma ngumu na kuomba maridhiano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Naunga mkono taarifa zote tatu. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushuru kwa kunipa nafasi. Awali ya yote, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu. Nianze kwa kusema naunga mkono hoja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kujielekeza kuchangia hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujikita zaidi katika Kamati ya Masuala ya UKIMWI. Sote hapa tutakubaliana kwa namna moja ama nyingine kila mmoja ameguswa na janga hili la UKIMWI, kama siyo yeye mwenye basi ndugu yake, jirani yake ama rafiki yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, takwimu nchini Tanzania zinaonesha kila siku iendayo kwa Mungu watu 200 wanaambukizwa UKIMWI na Virusi vya UKIMWI, watu 6,000 kwa mwezi na watu 72,000 ndani ya mwaka. Bado tukiziangazia takwimu, Mkoa wa Njombe ndiyo mkoa nchini Tanzania unaoongoza kwa maambukizi ya makubwa kwa asilimia 11.4, ukifuatiwa na Mkoa wa Iringa wenye asilimia 11.3, ukifuatiwa na Mkoa wa Mbeya wenye asilimia 9.3. Hii ndio mikoa top three nchini Tanzania inayoongoza kwa maambukizi ya UKIMWI na Virusi vya UKIMWI. Hivyo, ni kuonyesha ni kwa namna gani UKIMWI bado ni janga la Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na takwimu hizo na hali ya maambukizi nchini, napenda kuipongeza Serikali kupitia Tume ya Kudhibiti UKIMWI yaani TACAIDS kwa namna inavyopambana na kudhibiti UKIMWI na Virusi vya UKIMWI. Hili linadhihirishwa na survey iliyofanywa mwaka 2013, kiwango cha maambukizi kilikuwa asilimia 5.1 ukilinganisha na survey iliyofanywa mwaka 2017 kiwango hicho cha maambukizi kilishuka mpaka asilimia 4.7. Kwa hiyo, hii ni kusema kwamba maambukizi ya UKIMWI yamekuwa yakipungua. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hali hiyo ya kupungua kwa maambukizi ya UKIMWI na Virusi vya UKIMWI nchini, inachagizwa na jitihada nzuri zilizofanywa na Serikali kufikia zile 90, 90, 90. Sasa tunabakiwa na jukumu moja kubwa ya kufikia malengo tarajiwa ya mkakati wa Kitaifa kwamba mpaka kufikia mwaka 2025 tuhakikishe tumefika zile 95, 95, 95 kwa maana maana 95 ya kwanza asilimia 95 ya Watanzania tuwe tumepima virusi vya UKIMWI, lakini asilimia 95 ya Watanzania ambao wanaishi na virusi vya UKIMWI wawe wanatumia dawa na asilimia 95 ambao wako kwenye kutumia dawa wahakikishe hawawi watoro kwenye kufuata dawa hizo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tutaweza kuzifikia hizi 95 tatu ifikapo 2025 ama hizi sifuri tatu ifikapo mwaka 2030, endapo Serikali itaendelea kujidhatiti katika masuala mazima ya kuhakikisha tunatenga bajeti kwa kutumia fedha zetu ndani. Kwa kiasi kikubwa bajeti ya UKIMWI hususan kwenye upande wa miradi ya maendeleo tumekuwa tukitegemea wahisani. Kama tutaendelea kutegemea wahisani, siku wakijitoa au wafadhili wakiacha kutupatia fedha hizi ina maana lile lengo tulilolikusudia kama Taifa ifikapo 2030 tufike zile sifuri tatu itabaki kuwa historia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitaomba katika kulidhihirisha hili kwa namna gani tupambane kufikia 95 tatu ama kufika 0 tatu kwa kuangalia mwenendo wa bajeti hii tunayoenda nayo. Tume yetu ya Kudhibiti UKIMWI yaani TACAIDS kwenye bajeti hii tunayoenda nayo iliidhinishiwa shilingi bilioni 4.9, kama fedha za miradi ya maendeleo ambapo shilingi bilioni 1 ndiyo fedha ndani, zilizobaki ukitoa katika bilioni 4.9 ni fedha kutoka kwa wa hisani. Nini tafsiri yake? Asilimia 76.6 ya fedha ya masuala ya UKIMWI zinatokana na wahisani. Fedha zinazotokana na wahisani sio vyanzo endelevu, lakini pia niseme kutenga bajeti ya masuala haya ambayo bado ni janga la Kitaifa, maambukizi ni kwa asilimia 4.1, kwa kutegemea wafadhili kama Taifa tunakuwa hatuendi sawasawa. Rai yangu kwa Serikali tujitahidi tuhakikishe kwamba asilimia 75 ya fedha za miradi ya maendeleo katika masuala mazima ya UKIMWI yatokane na fedha zetu za ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hapa pengine niishauri Serikali, tunazo taasisi, NGO lakini pia tunazo zile Asasi ambazo kimsingi ziko chini ya TACAIDS au ambazo zinaangaliwa na TACAIDS hasahasa zile zinazopewa technical supports na TACAIDS, Serikali sasa wakati umefika wa kuangalia namna bora ili taasisi hizi kupitia maandiko yao watenge sehemu ya mchango angalau percent fulani ili iweze kuingia kwenye Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI. Tukifanya hivi, tutakuwa tumepata chanzo endelevu katika kutafuta afua hizi za UKIMWI. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nikigeukia upande wa Mfuko huu wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI (Aids Trust Fund) ambao wenyewe umetengewa shilingi bilioni 1. Pesa hizi ni za juzi juzi tu kwa msaada wa Mheshimiwa Spika baada ya kuitisha Kamati ya Uongozi na Kamati yetu ya Masuala ya UKIMWI kulibeba jambo hili kama jambo mahsusi ndipo Serikali ambapo mmetoa shilingi milioni 500. Kwa hiyo, nachopenda kuishauri Serikali tutoe hizi fedha kwa wakati. Hizi shilingi milioni hizi 500 mlizozitoa ambazo ni nusu ya bajeti, napenda sana kuiomba na kuisisitiza Serikali mpaka kufika Juni, 2021 mhakikishe mmemaliza sehemu iliyobaki ili afua za UKIMWI ziweze kupatikana kwa unafuu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mchango wangu wa mwisho nitajielekeza kwenye masuala ya madawa ya kulevya. Tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Mamlaka imekuwa haitengewi fedha za miradi ya maendeleo. Kama hatutatenga fedha za miradi ya maendeleo, changamoto ya kwanza ni ile iliyosemwa na Kamati kwamba tutakuwa uhaba wa Vituo vya Waraibu wa Madawa ya Kulevya ambao wanapatiwa ile dawa ya methadone. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama Taifa tunapambana na pia kupitia wadhamini ama wafadhili wanaotusaidia kupambana na masuala ya UKIMWI pamoja na madawa ya kulevya, tunahangaika kuwasaidia vijana wetu kuwapatia afua za UKIMWI na methadone ili watoke kwenye ule uzombi warudi katika hali ya kawaida, lakini hatuna miradi ya maendeleo. Wanaporudi katika hali yao ya kawaida, tukikosa kuwajengea uwezo, wakikosa shughuli za kufanya, it’s obvious watarudia tena kule kwenye kuvuta haya madawa ya kulevya. Ndiyo maana tunaitaka Serikali kutenga miradi ya maendeleo ili kuweza kusadia kundi hili na hususan wengi wake ni vijana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati tunafanya ziara ya ukaguzi wa miradi, tumetembelea hizi sober house, unakutana na wale waraibu wa madawa ya kulevya, ambao tayari wameshapewa dawa ile ya methadone wamerudi kwenye hali ya kawaida, wanasema wakirudi mtaani hawana cha kufanya, wakienda kwenye familia wananyanyapaliwa, kwa hiyo wanajikuta wanarejea tena kwenye uvutaji wa madawa ya kulevya. Kwa hiyo, nachopenda kukisisitiza hapa, tutenge fedha za miradi ya maendeleo ili tuweze kuokoa nguvu kazi ya vijana wa Taifa letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema haya, naunga mkono hoja, nakushukuru. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi. Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu. Sambamba na hilo, nampongeza sana Mheshimiwa Waziri Jafo kwa uwasilishaji wake mzuri.

Mheshimiwa Spika, mchango wangu nitapenda kujikita kwenye upande wa mazingira. Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama tulioridhia wa Mkataba wa Minamata kuhusiana na kemikali za zebaki. Ukisoma mkataba wa Minamata katika Ibara ya 13 imeainisha vyanzo na utaratibu wa upatikanaji wa rasilimali fedha ili kuweza kutekeleza mkataba huo. Baadhi ama sehemu ya vyanzo hivyo ni pamoja na kutenga bajeti ya Serikali, kutumia Mfuko wa Dunia wa Mazingira, washirika wa maendeleo pamoja na sekta binafsi.

Mheshimiwa Spika, nimesikiliza hotuba ya Mheshimiwa Waziri, sijang’amua kinagaubaga ni kwa namna gani tumetenga fedha za bajeti ya Serikali ili kutekeleza masuala yaliyomo kwenye mkataba wa Minamata. Tunaambiwa tunayo fursa kama nchi wanachama kuweza kupata fedha kutoka Mfuko wa Dunia wa Mazingira ili kuweza ku-deal na matumizi ya kemikali ya zebaki ambayo ni hatari sana na ni sumu kwa maisha ya binadamu. Mheshimiwa Spika, hivyo, nitataka kujua, sisi kama nchi tumeitumiaje fursa hiyo ya kuweza kupata fedha kutoka katika Mfuko huo wa Mazingira ili kuweza kuwajengea uelewa watu wetu sambamba na kupunguza athari ama madhara yanayotokana na kemikali ya zebaki.

Mheshimiwa Spika, ninapoizungumzia zebaki ninapenda Bunge lako lifahamu kwamba hii ni kemikali hatari sana na ni sumu kubwa inayosababisha maradhi kwa binadamu ikiwemo ugonjwa katika mifumo ya nerve za fahamu, uzazi, upumuaji, magonjwa ya figo, moyo na saratani, lakini inadhoofisha viumbe hai majini pamoja na athari za kimazingira. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kemikali hii ya zebaki nimetangulia kusema kwamba ina madhara makubwa sana, nasi kama binadamu tunadhurika na kemikali hii kwa kuishika hususan pale tunapochenjua dhahabu, tunapovuta mvuke wenye zebaki, tunapokunywa au kula vyakula vyenye viambata vya zebaki.

Mheshimiwa Spika, hivyo ni vyema sasa Serikali yako ikatambua na kuona namna bora ya kushughulika na kupunguza matumizi ya kemikali hii. Nitaomba Bunge lako lijue kwamba jamii ya wachimbaji wadogo hususan wenzetu wanaotokea ukanda wa ziwa, hawa ndiyo waathirika wakubwa wa matumizi ya kemikali hii ya zebaki. Wanapofanya shughuli za uchenjuaji wa dhahabu maji yale yanayotiririshwa kwenda kwenye vyanzo vya maji hususan mito na maziwa kuelekea…

MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Taarifa. Endelea tu wewe mwenye taarifa. Nimeshakuona sasa.

T A A R I F A

MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Spika, naomba nimpe taarifa mzungumzaji kwamba miongoni mwa waathirika wakubwa sana wa kemikali ya zebaki ni pamoja na wanawake ambao wanashughulika katika shughuli za uchimbaji mdogo wa madini katika migodi yetu hususan Kanda ya Ziwa. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Hawa Mchafu, unapokea taarifa hiyo?

MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Ninaipokea Taarifa hiyo. Ni kweli kabisa jamii ya wachimbaji wadogo pamoja na watu wanaotokea Ukanda wa Ziwa ndio wanaoathirika na matumizi ya kemikali hiyo ya zebaki.

Mheshimiwa Spika, nimeshasema, wakati wa shughuli ya kuchenjua dhahabu, yale maji yanayotiririka kwenda kwenye vyanzo vya maji, mito na maziwa ndipo pale maji yale yanapokuwa contaminated na kemikali hii ya zebaki…

SPIKA: Kumbe ndiyo maana akina Musukuma hawanenepi, zebaki tupu! (Kicheko)

Endelea Mheshimiwa Hawa. (Kicheko)

MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Spika, ndiyo Ndugu zetu hawa wa Ukanda wa Ziwa, hawa Wanyamwezi, Wasukuma watani zangu, wajuu zangu wanapojiweka katika hatari kubwa ya kupata maradhi ambayo nimeyataja hususan maradhi hayo ya saratani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ipo shaka; na research ambayo siyo rasmi ni kwamba leo ukienda katika Taasisi…

SPIKA: Mheshimiwa umesimama eh! Endelea Mheshimiwa Hawa.

MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Spika, ipo shaka ama hofu na niseme kwamba hii ni research lakini siyo rasmi kwamba leo ukienda katika Taasisi yetu ya saratani, pale Ocean Road, wagonjwa wengi na Ndugu wa wagonjwa wengi wa pale, lugha na lafudhi inayozungumzwa pale, ni watani zangu Wasukuma.

Kwa maana hiyo, ni dhahiri shahiri, kufuatia shughuli hii, wenzetu wamejaaliwa kupata madini, lakini athari yake au madhara yake ni kujiweka kwenye hatari ya kupata maradhi ambayo nimeshayataja.

SPIKA: Yaani Mheshimiwa Hawa anasema, ukifika Ocean Road pale utasikia tu titiri titiri, unajua hao hao! (Kicheko)

MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Spika, unasikia tu ng’wadila, ng’wadila, wanakandamiza. Asilimia kubwa ya wagonjwa wa pale ni hawa watani wangu. Tafiti zinaonesha vifo vinavyotokana na ugonjwa wa saratani vimefikia asilimia 15. Asilimia 15 ya vifo, siyo vidogo katika nchi yetu. Hivyo nina mambo mawili ya kuishauri Serikali.

Mheshimiwa Spika, jambo la kwanza ninapenda kuishauri Serikali kwamba wakati umefika sasa kuja na njia mbadala ya kuchenjulia dhahabu na kuachana na hii kemikali ya zebaki.

Mheshimiwa Spika, ninaomba…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Malizia…

MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Spika, naomba kumalizia kwamba tunayo teknolojia ama njia mpya ya uchenjuaji dhahabu inayoitwa cyanide. Kwa hiyo, Ndugu zangu na Serikali naomba sana tuanze kutumia hii njia mpya, tuachane na zebaki ambayo ina madhara makubwa kwa Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo. Ninashukuru, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Rais wa Awamu ya Sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan wakati anawaapisha Mawaziri katika hotuba yake alisema haya maneno, naomba ninukuu. ‘Competitiveness ya TTCL iangaliwe vizuri kwa sababu hili ndilo shirika letu na tunategemea lishindane na mashirika mengine ya private sector. Kwa hiyo, competitiveness hiyo ikoje? Tuangalie vizuri tutoe nini, tuache nini, turekebishe ndani ya TTCL ili shirika lisimame vizuri’. Mwisho wa kunukuu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiiangalia nukuu hii ina maana nzito na kubwa sana katika mustakabali wa maendeleo pamoja na ushindani wa Shirika letu la TTCL. Imesemwa hapa na baadhi wa Wabunge kwamba kila mwaka mashirika binafsi ama mashirika shindani na TTCL yanawekeza kati ya milioni 100 dola mpaka milioni 150. Lakini, shirika letu la TTCL linawekeza sifuri. Halafu tunategemea hapa uwepo ushindani ama uwepo ufanisi wa biashara katika shirika letu hili la TTCL na mashirika haya mengine shindani ya simu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, imagine shirika giant kama Vodacom kila mwaka linawekeza milioni 100 lakini kashirika ketu ka-dwarf kanawekeza sifuri. Kwa hiyo, hapa ule ushindani tunaoutafuta hatuwezi kuupata. Imesemwa hapa teknolojia inakua kila leo na inakua kwa kasi kubwa sana. Kwa maana hiyo, tunapozungumzia teknolojia uwekezaji wake unahitaji fedha nyingi na unahitaji fedha ya kutosha. Sasa tunaambiwa Shirika letu la TTCL ndani ya miaka 10 halijawahi kufanya huo uwekezaji. Mara ya mwisho shirika hili liliwekeza mwaka 2001. Sasa tuangalie kutoka mwaka 2001 mpaka leo 2021 hapa katikati teknolojia ime-change kwa kasi na kiasi gani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesisitiza tena, akina Vodacom wanawekeza kiasi kikubwa lakini sisi ndani ya miaka 10 mfululizo tumewekeza sifuri, sifuri. Sasa kwa kuwa sasa hivi Tanzania tumekuwa tunaelewa sana masuala ya mpira hapo ukifanya ulinganifu yaani uichukue ndondo cup iende ikacheza kule Barcelona. Ama uichukue Simba iende ikacheze na Arsenal. Juzi wamecheza na Kaiza wamefungwa goli nne, sasa pata picha iende ikacheze na Barcelona, majibu na matokeo hapa wote tunayo kwamba itachezea kipigo cha mbwa koko. Kwa hiyo, ninatoa mfano huu kujaribu kuonesha kwamba Arsenal ndiyo giant hawa Vodacom halafu Simba ndiyo hii ndondo cup ninayotolea mfano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ama hakika hatuwezi kupata tija inayotafutwa. Kwa hiyo ushauri wangu kwa Serikali, Serikali toeni mtaji ipeni TTCL. Malalamiko yote yanayolalamikiwa hapa na pia katika hotuba ya Mheshimiwa Rais ilisema kwamba wawekezaji binafsi wanawekeza
sehemu zenye mvuto wa kibiashara. Kule ndani ndani, interior wenyewe huwa hawawekezi, ni shughuli yetu Serikali kuwekeza. Kwa sababu hiyo, tuna kila sababu Serikali kuipatia mtaji TTCL ili iweze kuwekeza kwa ufanisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili TTCL iweze kusimama, mtaji wake wa awali tu inahitaji bilioni 800 za Kitanzania, huo ni uwekezaji wa awali wa mwanzoni kabisa. Inawezekana kwamba fedha hizi zinaonekana kuwa nyingi kwa sababu tunazo huduma muhimu za kijamii kama afya, elimu na maji pengine sasa Serikali inapata ugumu na ukakasi kupeleka fedha hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanini tusiwaruhusu sasa waende wakakope? Kwa muda mrefu nikiwa mjumbe wa hii Kamati, ushauri tuliokuwa tunaishauri Serikali iruhusuni TTCL iende ikakope concession loan, mkopo wa gharama na masharti nafuu ili iweze kuwekeza ifanye kazi shindani na kazi yenye tija kama ambavyo tayari imeshatanguliwa kusemwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wamesema hapa Waheshimiwa Wabunge kwamba TTCL inaidai Serikali na Wizara fedha nyingi tu za kutosha na ukiangalia ripoti ya CAG ya mwaka 2019/20 katika ukurasa wake wa 337 inasema kwamba TTCL ilipaswa ilipwe zaidi ya shilingi bilioni 15. Hii ni kutokana na huduma ya mkongo. Lakini ripoti ya Kamati imetuambia mpaka hivi leo tayari imeshafika dola za Kimarekani milioni 68. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maana hiyo, tunaweza tukaona ni fedha kiasi gani ambayo TTCL wanaitafuta, Serikali mko mmeishikilia. Kinachoumiza hapa, TTCL inatoa mapato yake ya ndani kwa ajili ya kuendesha na kuhudumia mkonge ambapo taasisi binafsi zinatoa hizi huduma za simu kwa kupitia mkongo huo. Niseme kuwa wanalipa, lakini kile kinacholipwa kinaenda kwenye Wizara, sasa tunamkamua ng’ombe huyu TTCL pasipo kumlisha majani. Kwa maana hiyo, Serikali muda umefika wa kuhakikisha mnatoa hela mnawapa TTCL ili waweze kufanya kazi yenye tija.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia ukiangalia ripoti hiyo hiyo ya CAG inasema TTCL inadai Serikali madeni ya huko nyuma ya miaka 10 karibu bilioni 40. Kwa hiyo, kuna hizi milioni 68, kuna hizi bilioni 40, zote hizi tukiwapatia TTCL angalau watakuwa na sehemu ya kuanzia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia imesemwa hapa naomba nisisitize kwamba taasisi ama mashirika ya umma yanapata huduma kutoka katika shirika letu hili la TTCL lakini kimsingi hawalipi. Wanapata huduma ya Internet, wanapata huduma ya data, wanapata huduma ya simu, hawalipi! Sasa tukitegemea kwamba eti siku moja TTCL ije ifanye maajabu hii TTCL itakuwa tu kama zombie, ilikuwepo, inakufa, tukaifufua kwa sheria tena mpya sijui 2017 tulifanya marekebisho ya sheria, leo tunajaribu kushauri ten ana tena lakini bado Serikali haitaki kupokea ushauri wetu. Ama hakika, hili shirika litakufa tena halafu tutegemee litakuja litafufuka tena huko mbele ya safari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sheria ya manunuzi, Sheria ya Manunuzi ya Umma tunaiona ni kwa jinsi gani ambavyo ina mchakato mrefu na mgumu. Kwa mashirika kama TTCL na yanayofanana na hayo kama ATCL, hebu sasa Serikali ifike wakati, ifike mahali mtengeneze kanuni mahsusi kwa ajili ya mashirika haya ya umma yanayofanya kazi kibiashara, kwa sababu leo Vodacom wakitaka kununua mitambo mipya, wakikaa tu ile Bodi, wakijadili wakiamua ikionekana inafaa, kesho wanaenda kununua. Lakini, TTCL, ni mchakato utachukua mwezi mzima hata mitatu ili waweze kukidhi mahitaji ya Sheria ya Manunuzi ya Umma ili waweze kununua hiyo mitambo, wafunge mitambo kwa ajili ya kuweza kutoa huduma stahiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho nimalizie na Mkoa wangu wa Pwani. Maeneo mengi ndani ya Mkoa wetu wa Pwani kumekuwa na kusuasua kwa mawasiliano. Ukichukua kwa mfano katika Wilaya ya Mkuranga maeneo ya Sotele, Chamgoni, Kibuyuni pamoja na Mbezi, huku mawasiliano ya simu imekuwa ni changamoto. Lakini pia kwa upande wa wilaya ya Kibiti, maeneo ya kule Delta, Msala kule, Kihomboloni, changamoto kubwa ya mawasiliano. Pia ukichukua kwa upande wa Mafia, visiwa vya Jibondo na visiwa vya Chole, mawasiliano yamekuwa yakisuasua. Hata kule kwa Mheshimiwa Jaffo, maeneo ya Mafizi, maeneo ya Manyani, vikumburu, mawasiliano yamekuwa ya kusuasua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, nakushukuru sana, tunamuomba Mheshimiwa Waziri aje na majibu, pasipo hivyo, jioni tunakusudia kushika shilingi. Naunga mkono hoja. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo kwa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia hotuba iliyopo mbele yetu. Awali ya yote nipende kumshukuru Mwenyezi Mungu, nikushukuru wewe pia kwa kunipa nafasi. Nipende kwa kuanza kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa wasilisho lake zuri, na mchango wangu wa kwanza nitapenda kuanza kuangazia deni la Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hotuba zote mbili zilizowasilishwa katika Bunge lako tukufu, ile ya Kamati ya Bajeti pamoja na ya Mheshimiwa Waziri zinatuambia kwamba deni la Taifa limekuwa likiendelea kukua ama likiongezeka hadi kufikia trilioni 71.56 kutoka ile 64.50. Hili ni sawa na ongezeko la asilimia 11.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa tunaambiwa deni hili ni himilivu kwa viwango vya Kimataifa, ni vema sasa tuka-focus na tukapigia jicho zaidi kwenye miradi ya kimaendeleo na miradi ya kimkakati. Lengo ni kufanya miradi hii iweze kurudisha return ya haraka kwa mkopo huu wa shilingi trilioni 71.56.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi hii mikubwa ni miradi itakayosaidia kusimamisha uchumi wa nchi. Kwa hiyo, tukiacha sababu zile ambazo ziko dhahiri shahiri zinaonekana, lakini tuondokane na sababu za hapa na pale zinazopelekea kuchelewesha miradi hii ama sababu zinazopelekea miradi hii kwenda kuongezeka thamani ya fedha ukilinganisha na hile thamani ya mwanzo tuliyongia katika mikataba hii pale awali. Kwa kufanya hivyo tutaweza kukuza uchumi, tutaweza kukuza pato la Taifa na pia tutaweza kukuza ajira na fedha za kigeni. Haya yote kwa pamoja yatafanya uchumi wetu uweze kuwa stable zaidi, jambo ambalo litatusaidia sasa kupanga na kubajeti masuala mazima ya elimu, afya pamoja na kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu wa pili upo katika eneo la mfumuko wa bei. Ukisoma hotuba ya Mheshimiwa Waziri katika ukurasa wake wa nne, ameelezea kwa namna gani mfumuko wa bei umekuwa ukiongezeka hususan kwenye bei za bidhaa ya chakula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na ongezeko kubwa, tena kubwa sana, kutokea asilimia 3.6 mpaka asilimia 7.8; kilo ya mchele imeongezeka, kilo ya unga na mahindi imeongezeka; hivyo ni vyema sasa tukajikita kwenye mpango huu tunavyopanga mpango huu wa maendeleo, tukaangazia zaidi eneo hili kwani ndiyo eneo linalowagusa Watanzania wengi. Mtanzania wa leo anahitaji unga, maharage na mchele, lakini ndiyo sehemu ambayo bei imekuwa ikiongezeka kwa kasi. Kwa maana hiyo, hapa Mheshimiwa Waziri ni lazima afuate ushauri uliotolewa na Kamati juu ya suala zima la kuanza kutumia gesi asilia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine namwomba Mheshimiwa Waziri, hebu atusaidie na alisaidie Taifa, tunampongeza sana Mheshimiwa Rais, kila mwezi anatoa ruzuku ya Shilingi bilioni 100 ili kwenda kuongezea kwenye bidhaa za nishati pamoja na fuel. Jambo la kusikitisha hapa, na kimsingi ni kwamba uongezwaji huu wa hii Shilingi bilioni 100 kila mwezi, ili iende ikapunguze usafirishaji pamoja na uzalishaji, jambo ambalo litasaidia bidhaa sokoni angalau zishuke bei. Cha ajabu bei ndiyo zimekuwa ziki-shoot kwa hali ya juu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziri akija atuambie nini faida ya hii Shilingi bilion 100 anayoitoa Mheshimiwa Rais kila mwisho wa mwezi kwa ajili ya kwenda kupunguza makali kwenye nishati na kwenye fuel ilhali bei za bidhaa ya chakula inapanda kila leo? Kwa hiyo, atakapokuja hapa, naomba anipatie hayo majibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni kuhusiana na mikopo ya sekta binafsi. Tunakubaliana sote hapa kwamba sekta binafsi ni kichocheo kikubwa na kichocheo kizuri cha uchumi wa nchi yetu. Tunashukuru kuona kwamba mikopo kwenye sekta binafsi imekuwa ikiendelea kukua kutoka Shilingi trilioni 20 mpaka Shilingi trilioni 24. Ila ukija kwa upande wa riba, riba tunashukuru inapungua, lakini inapungua kwa kiasi kidogo, asilimia 0.19. Sasa kwa mipango na maendeleo tunayotaka kupanga ya nchi yetu, kwa upunguaji huu wa riba tutasababisha kukosa wawekezaji wa kutosha na wakopaji wa kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tulikuwa tunaiomba Benki Kuu na mabenki kukaa na kuangazia tena namna bora ya kuendelea kupunguza kiwango cha riba ili tupate wakopaji na wawekezaji wengi. Nia na madhumuni ni ku- boost uchumi wa nchi yetu, ajira zipatikane kwa wingi, kuingiza fedha za kigeni na katika yote tuweze kulisaidia Taifa hili kuweza kuwa na uchumi stable katika kupanga maendeleo endelevu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchangia kuhusu Bandari ya Bagamoyo. Sote tunafahamu kwamba bandarai ndio lango kubwa la uchumi na upanuzi unaofanywa kwenye Bandari ya Dar es Salaam imeishafika mahali, wanasema point of no return. Kwamba mbadala wa Bandari ya Dar es Salaam ni Bandari ya Bagamoyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa SGR unaoendelea unahitaji Bandari ya Bagamoyo. Uchimbaji wa Makaa ya Liganga na Mchuchuma utahitaji Bandari ya Bagamoyo, ukuaji wa uchumi wa nchi yetu unahitaji Bandari ya Bagamoyo, yaani ni Bandari ya Bagamoyo, Bandari ya Bagamoyo. Tukilala Bandari ya Bagamoyo, tukiamka Bandari ya Bagamoyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nakuomba Mheshimiwa Waziri, nimepitia Mpango nimeona tu nyota nyota. Nataka uje uniambie Mpango unasemaje kuhusiana na masuala mazima ya Bandari ya Bagamoyo? Vilevile nataka uje uniambie kuhusiana na kulipa fidia ya watu wa Bagamoyo ili tukawekeze kwenye Bandari ya Bagamoyo. Naomba unipe majibu, kwa sababu mradi huu wa Bandari ya Bagamoyo tayari kulishakuwa timu, tayari kulishakuwa na kikosi kazi na makubaliano, nitapenda uje uliambie Taifa, ile timu ya negotiation iliishia wapi? Tunataka tupate maelezo ya kina kuhusiana na Mradi wa Bandari hii Bagamoyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi wa Bagamoyo utaenda uta-boost uchumi wa hii nchi, utateka masoko ya Jirani na utafungua ajira pamoja na kufanya tupate fedha za kigeni za kutosha. Tukiimarika hapo, hatutakuwa tunajenga madarasa halafu tunashindwa kuwaboreshea walimu stahiki zao. Ili tuweze kuwa na elimu bora, tunapaswa tujenge madarasa, mishahara ya walimu tuiboreshe, ndivyo tutakapoweza kupata elimu bora. Suluhisho ni huu mradi wa Bagamoyo utakaotuletea uchumi kukua kwa kasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutaenda na vyote; tunajenga zahanati, tunapata vifaa tiba na at the same time stahiki za watumishi zinaboreshwa, lakini tukiwa tunafanya mipango yetu, eti tunajenga tu zahanati halafu vifaa tiba hatuna, work done is equal to zero. Tukiwa tunafanya mipango yetu, tunajenga madarasa halafu walimu hakuna, work done is equal to zero. Kwa hiyo, lazima mipango hii iende sambamba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kumalizia napenda sana kuipongeza Serikali na kuiomba ipokee ushauri huu ambao tunaweza kuipatia ili kuweza kusongesha maendeleo ya Taifa letu mbele. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, nakushuru, ahsante sana. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Awali ya yote nipende kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu, lakini pia nikushukuru wewe kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia ripoti za Kamati zilizoletwa mbele yetu. Nitapenda kujielekeza kwenye ripoti ya Kamati ya Masuala ya UKIMWI, Kifua Kikuu, Madawa ya Kulevya na Magonjwa yasiyoambukiza.

Mheshimiwa Naibu Spika, nipende sana kuipongeza Serikali, Wizara na taasisi kwa namna zinavyopambana na masuala haya ya UKIMWI; lakini pia nipende kuwapongeza wadau kwa kushirikiana na Serikali kwa namna wanavyopambana na kutokomeza haya masuala ya UKIMWI kwa kufanya tafiti, kutoa huduma, kutoa vifaa tiba na kuwezesha matumizi ya takwimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, mchango wangu wa pili ni juu ya miradi inayoendelea kutekelezwa na Serikali ukiwemo ule Mradi wa Fikia Plus, Mradi wa Timiza Malengo na Mradi wa THIS (Tanzania HIV Impact Survey). Miradi hii ni mizuri na ina malengo mazuri kwa Taifa letu kwa kuwa ina dhamira njema ya kupambana na kutokomeza masuala ya UKIMWI, lakini pia inataka kuja na data na takwimu sahihi kabisa. Vilevile wanahitaji kuibua wanaohitaji tiba ya methadone kwa upande waraibu pamoja na matibabu ya UKIMWI na Virusi vya UKIMWI kwa watu walioathirika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo nimetangulia kusema miradi hii ni mizuri isipokuwa kuna changamoto kubwa kwenye Mradi wa THIS. Tama unavyojieleza ni Tanzania HIV Impact Survey kwamba una lengo la ku - survey masuala haya ya UKIMWI. Changamoto iliyokuwepo kwenye mradi huu, mradi hauwatambui watoto wenye umri chini ya miaka 15 ilhali tunafahamu sasa hivi kumekuwa na hatari kubwa kwa watoto wetu. Tunafahamu kuna maambukizi ya UKIMWI toka kwa mama kwenda kwa mtoto, kumekuwa na vitendo vikubwa vya ubakaji kwa watoto. Kumekuwa na vitendo vikubwa vya ulawiti kwa Watoto, lakini pia kumekuwa na tabia ama wimbi limezuka la watoto kufanya mapenzi ya jinsia moja halafu Serikali inafanya mradi kabambe ya masuala ya UKIMWI wanawaacha watoto wenye umri chini ya miaka 15. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa maana hiyo hapa niseme kwamba haijafikiriwa ama haijawekwa sawa sawa…

WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Taarifa.

T A A R I F A

WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninamshukuru sana Mheshimiwa Hawa Mchafu kwa mchango wake mzuri, hususan kuhusu kupunguza maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Nataka tu kumthibitishia Mheshimiwa Mbunge kwamba juzi Mawaziri wa nchi 12 za Afrika tumekubaliana kwa vitendo kwamba tutaweka program maalum za kupunguza maambukizi ya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto hususan watoto wenye umri wa miaka 18. Kwa hiyo, hili tunalifanyia kazi na Tanzania ndiyo nchi ya kwanza Barani Afrika ambayo imekubali kufanyiwa tathmini na nchi zote duniani katika mpango huu wa kupunguza maambukizi ya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Hawa taarifa hiyo.

MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa ninaipokea. Ninachokisema Dada yangu Ummy, Mheshimiwa Waziri, mradi unaoendelea wa THIS ambao ni 2022/2023 unaelekea mwisho. Mradi hauwatambui watoto kwa maana hiyo sasa tutakuwa sasa tumeshafanya mradi kwa lengo la kutafuta data na takwimu za UKIMWI tunaacha kundi muhimu la watoto halafu tunasema tuje kufanya tena mradi mwingine? Hebu tuangalie kama tunaenda sawa sawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ninaipongeza miradi hii ni mizuri ina nia nzuri ila tunachopaswa, hata huo mradi unaokuja tuzingatie na tuangalie watoto kwa sababu wimbi la ubakaji, wimbi la ulawiti na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kwa watoto wetu, watoto wamekuwa ni kundi la hatari sana. Watoto wapo kwenye kundi hatarishi. Kwa hiyo nitaomba sana na mradi mwingine na mwingine uweze kuzingatia hilo. Nimeipokea taarifa na nakushukuru Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mchango mwingine ni kuhusiana na masuala ya UKIMWI na Virusi vya UKIMWI kwenye maeneo ya visiwani. Hapa najumuisha visiwa vyote na nikizungumza kwa maeneo ya mialo ama visiwani kule Mwanza. Mkoa wa Mwanza hususan kwenye maeneo yake ya visiwa, maeneo mengi yanaongoza ya wagonjwa kutokufikiwa na huduma ya 953 kwa sababu ya nature ya jiografia ya mazingira yale.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali wana mpango kwamba ifikapo 2030, kuwa na maambukizi sifuri.

Kwa hiyo nataka tuangalie kama kwa namna hivi tunavyoenda, maeneo ya visiwani, matibabu ya huduma ya afya hayapo sawasawa. Utakuta tunacho kituo cha afya lakini idadi ya Madaktari hawatoshi ama vifaatiba havitoshi ama niseme kwamba wataalam hawatoshi kwa hiyo tunajikuta tunapambana ifikapo 2030 kufikia maambukizi sifuri, lakini kwenye maeneo kama hayo unakuta bado hatujafanya ama hatujayafikia sawasawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, mchango wangu mwingine ni kuhusiana na magonjwa yasiyoambukiza. Nataka kusema kama kuna kitu muhimu Watanzania tunakihitaji ni bima ya afya kwa wote. Tunahitaji bima ya afya kwa wote kuliko kitu kingine chochote. Watanzania tuache masihara na afya zetu, tunahitaji bima ya afya kwa wote. Nitakupa mfano, mgonjwa mwenye Virusi ya UKIMWI ama mwenye UKIMWI. Tunashukuru kwa mgonjwa huyu ambaye anapata matibabu ama niseme dawa bure kutoka Serikalini lakini ni vipi akipata magonjwa nyemelezi na hana bima ya afya?

Mheshimiwa Naibu Spika, matibabu yamekuwa ghali sana, kwa maana hiyo kama hauna bima ya afya, mgonjwa anaumwa UKIMWI ama ana Virusi vya UKIMWI halafu ana diabetes, mgonjwa ana UKIMWI ama ana Virusi vya UKIMWI ana hypertension, mgonjwa mwenye UKIMWI ama ana Virusi vya UKIMWI ana hepatitis B ama C. Hebu angalia mgonjwa huyu atakuwa yuko katika hali gani. Ama hakika atakuwa yuko katika hali ya hatari sana kwa sababu magonjwa ya sukari, presha ni sehemu ya magonjwa yanayochukua bajeti kubwa ya Serikali kwa ajili ya kuwatibu Watanzania. Kwa hiyo naomba sana hili jambo Watanzania na Serikali tuliangalie ili tuweze kuharakisha jambo hili la bima ya afya kwa wote.

Mheshimiwa Naibu Spika, niendelee kuwapongeza Serikali kwa kazi nzuri wanayoifanya na dhamira yao njema ya kutaka kuhakikisha wanafikia maambukizi sifuri ifikapo 2030, lakini nitapenda kujua, Serikali ina mpango gani, ina mkakati gani na imejipanga vipi kuondokana na maambukizi mapya na tusifikie maambukizi sifuri ikifika mwaka 2030 kwa kuyafikia makundi yafuatayo: -

(a) Wanaojidunga;

(b) Wanaojiuza; na

(c) Wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunasema maambukizi sifuri 2030 lakini leo tuko 2023 na bado ipo changamoto kubwa kuyafikia makundi haya. Kwa hiyo nitapenda kusikia kauli ya Serikali mpango mkakati tumejipangaje kuweza kuyafikia makundi haya matatu ili kutimiza dhamira njema ya kufikia maambukizi sifuri ifikapo 2030.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, nashukuru kwa kunipa nafasi na naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya TAMISEMI. Awali ya yote nipende sana kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunisimamisha mbele ya Bunge lake tukufu, pia napenda kuwapongeza Mheshimiwa Waziri, Angellah Kairuki na Manaibu wake Dkt. Festo Dugange pamoja na Deo Ndejembi kwa kazi nzuri wanayoifanya na kwa uwasilishaji wao wa hotuba hii yenye kurasa takribani 286, napenda kuwapongeza sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa ni miongoni mwa Mawaziri ambao wanatoa ushirikiano, wanapokea simu na wanajibu meseji pindi unapowapa changamoto za watu wetu huko Majimboni, kwa hiyo napenda kuwapongeza sana na muendelee kumsaidia Mheshimiwa Rais kwa kasi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu wa kwanza nitakwenda kwa kuanza kumpongeza Dkt. Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya nchini Tanzania. Nimesoma bajeti mbili zilizopita za Rais Samia kwa upande wa miradi ya maendeleo kwa Mkoa wetu wa Pwani namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwani Halmashauri zote Tisa za Mkoa wa Pwani zimepata miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza na miradi ya sekta za afya. Kwa upande wa Mkoa wa Pwani tumepata Hospitali mpya za Wilaya Tatu na siyo Tatu niseme Nne ikiwepo Hospitali ya Wilaya ya Kibiti, Kibaha DC, Kibaha Mji pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, kilichokuwa Kituo cha Afya Msoga tumepatiwa fedha nyingi sana na tumejenga majengo na kimeshapandishwa hadhi na sasa na yenyewe imekuwa hospitali ya Wilaya. Kwa kusema hivyo ni kwamba tunazo Hospitali mpya 4 ndani ya Mkoa wetu wa Pwani. Tunayo kila sababu ya kumpongeza Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kusema hapa ni kwamba Mheshimiwa Rais amesogeza huduma ya afya karibu kabisa na wananchi wake na kimsingi kama ambavyo tunafahamu afya ni jambo muhimu sana kwenye maisha ya binadamu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa ninachotaka kukisisitiza ni kwamba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametimiza wajibu wake, ametupa Mabilioni lakini ametupa hospitali ya Wilaya. Jukumu na kazi iliyobaki hapa ni kwa Wizara na nitaomba Mheshimiwa Waziri na Naibu Mawaziri wako muweze kunisikiliza. Mheshimiwa Waziri tunayo changamoto kubwa ya upungufu wa Watumishi, haitakuwa na maana na haitakuwa na afya, Rais katoa Mabilioni ya fedha, tumejenga Hospitali ya Wilaya, lakini tunakosa Watumishi, wananchi wetu wanaenda pale wanakosa kupata huduma kwa sababu watoa huduma hawapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndani ya Mkoa wa Pwani tuna watumishi wa kada hii ya afya asilimia 48 tu kwa kusema hivyo tunakuwa na upungufu wa watumishi wa kada ya afya kwa asilimia 52. Nitaomba ili u ende kuliandika na peni yako ya kijani. Katika zile ajira 21,200 zilizotolewa na Mheshimiwa Rais, nitaomba Pwani uiangalie kwa jicho la dharura ili tuweze kupata watumishi wa Kada ya Afya, tuweze kupunguza hii asilimia 52 kwani imekuwa ni kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ambalo Mheshimiwa Waziri naomba uende kuandika kwa peni yako ya kijani ni suala la upungufu wa vifaatiba. Tunashukuru tumepata hospitali Nne za Wilaya lakini tunakosa vifaatiba. Katika hili Mheshimiwa Waziri umelisema katika hotuba yako ukurasa wa 150, kwamba umetenga Bilioni 15 point au niseme Bilioni 16 kwa ajili ya ununuzi wa vifaatiba. Kwa hiyo ombi langu hapa ni lilelile kwa hiyo niangaliwe kwa jicho la huruma, ili tuweze kupatiwa vifaatiba katika Hospitali zetu hizo za Wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu ambalo Mheshimiwa Waziri na lenyewe nenda kaliandike na kalamu yako ya kijani, ni kuhusiana na suala zima la hospitali kongwe. Kama nilivyotangulia kusema katika Halmashauri zetu Tisa Halmashauri Nne mmetupa Hospitali za Wilaya tunawashukuru sana. Halmashauri Tano zimebaki ni hospitali kongwe ambapo kimsingi majengo yake pamoja na mifumo ya kutolea huduma imekuwa chakavu sana inahitahi ukarabati, amezungumza kwenye hotuba yake kwenye ukurasa wa 149 kwamba umetenga Shilingi Bilioni 27.9 kwa ajili ya ukarabati wa hospitali kongwe. Nikuombe sana usizisahau Halmashauri za Mkoa wa Pwani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri, jambo la nne ninaloomba ukaliandike kwa peni ya kijani, ni vizuri sana kukawa kuna mawasialiano kati ya zahanati, kituo cha afya na hospitali ya Wilaya. Ndani ya Mkoa wa Pwani tunao upungufu wa magari ya wagonjwa, kwa hiyo nimetoa mambo haya manne ambayo nimekuomba na kukusisitiza yaandikwe kwa peni ya kijani kwa sababu nitaomba uyahifadhi na uyafanyie kazi pindi tunapokuja hapa mwakani kwa ajili ya Bajeti.

MWENYEKITI: Ahsante sana, Mheshimiwa Hawa Mchafu kwa mchango wako.

MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru ahsante naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Afya
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Ningependa kuanza kuwapongeza Dkt. Ummy na Dkt. Mollel kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya na nikope maneno yake kwamba Mawaziri hawa wako very loyal na very committed nawapongeza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa nianze kwa kumpongeza Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya. Rais Samia anaendelea kuboresha na kuimarisha Sekta hii ya Afya Nchini. Hivi tunavyozungumza tayari takribani bilioni 290 zimeshatumika kwa ajili ya kukarabati ama kuboresha hospitali za kanda, hospitali za mikoa na hospitali ya Taifa. Sambamba na hilo Mheshimiwa Rais Samia ameweza kusaidia kupunguza rufaa takribani kwa asilimia 97 za kwenda kutibwa nje ya nchi. Tunampongeza sana Dkt. Samia Suluhu Hassan. Pia tunaona nchi za jirani sasa ni zamu yao kuja Tanzania kufuata matibabu kama ambavyo zamani ilikuwa sisi tunatoka kwenda kufuata matibabu Kenya, India na nchi zingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, juzi nimeona Madaktari saba wa Tanzania wakienda Malawi kwa ajili ya kwenda kutoa tiba, lakini pia kufanya uchunguzi pamoja na ukaguzi kwa wagonjwa ambao kimsingi walitakiwa waje kutibiwa Tanzania. Madaktari wetu hawa wakaenda kuwatibia kule kule Malawi. Hongera sana kwa Mama yetu kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya kwa wananchi wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, nitapenda kumpongeza sana Waziri Ummy na timu yake kwa kuja na wazo la kufikiria sasa Hospitali ya Taifa ya Mirembe kuipandisha hadhi kuwa Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili. Napenda sana kuwapongeza kwa hili, kwani hapo awali hospitali hii ya Mirembe imepewa majina mengi ikiwemo hospitali ya vichaa, jambo ambalo mtu kama unahitaji huduma kwa hospitali ile inakuwa ni changamoto kwa namna vile ilivyokuwa ikiitwa. Kwa hiyo hongera sana kwa Wizara kwa namna ambavyo wameipandisha hadhi na kuweza kuiita Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi tunaambiwa karibu Watanzania wengi tunazo dalili za magonjwa ya afya ya akili, kucheka kupitiliza tunaambiwa ni dalili ya afya ya akili, kukasirika kupita kiasi, tunaambiwa hizi ni dalili za magonjwa ya afya ya akili, wivu uliokithiri na uliopitiliza tunaambiwa ni dalili ya magonjwa ya afya ya akili, lakini pia uwoga uliopitiliza, zote hizi tunaambiwa ni dalili za magonjwa ya afya ya akili. Kama hivyo ndivyo, mimi nitapenda kuuliza Serikali haya maswali yafuatayo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la kwanza, je, Serikali inaifahamu changamoto hii kwa ukubwa gani? Swali la pili ambalo ningependa Waziri Ummy aje atujibu sasa, je, Serikali wamejiandaa vipi sasa kukabiliana na tatizo hili, maana inaonekana karibia kila Mtanzania anayo dalili ya ugonjwa huu wa afya ya akili? Kwa hiyo ningependa kujua mipango na mikakati ambayo wamejipanga nayo na kama wana takwimu sahihi kabisa za wagonjwa hawa na hawa walionyesha dalili za magonjwa ya afya ya akili.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala langu la pili, lilikuwa ni kuhusiana na Toto Afya Card, kwa sababu ya muda ningependa Mheshimiwa Waziri achukue ushauri na maoni yaliyotolewa na Kamati hii ya Afya pamoja na Masuala ya UKIMWI, wamelichambua vizuri na wameshauri vyema. Kwa hiyo kwa kutunza muda ningependekeza wachukue ushauri huo uliotolewa na Kamati.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na MSD; amesema vizuri Mheshimiwa Mwenyekiti wa Kamati hii. Niliwahi kuuliza swali hapa ama niliwahi kuchangia hapa kwamba MSD sasa hivi kazi yake imekuwa inachukua ama inapokea hela ya Kituo cha Afya Mlandizi, inaenda inanunua dawa ya kituo kingine. MSD inapokea hela za Hospitali ya Wilaya ya Kibiti inaenda inanua dawa za Hospitali za Wilaya ya Mkuranga. Kwa maana hiyo imekuwa inachukua hela huku inaenda inanunua dawa kule, wamesema kwamba tuwaongezee mtaji, ifike mahali wapewe mtaji ili waweze kufanya kazi iliyokusudiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, lengo la MSD ni Bohari ya Madawa, tunatakiwa tuwe na stoo ya madawa pindi zahanati, hospitali ya wilaya ama hospitali ya mkoa inapopeleka mapendekezo ama inapopeleka fedha kwa ajili ya kupatiwa dawa, basi dawa ziwepo stand by pamoja na vifaa tiba, lakini tusikuchue hela za dawa za huku na kwenda kununua dawa kule. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ambalo nililokuwa nataka kulizungumzia ni kuhusiana na suala zima la bima ya afya kwa wote. Hili nilishalizungumza na leo narudia tena, Watanzania tumefika mahali tunahitaji bima ya afya kwa wote na hususan kwa upande wa magonjwa yasiyoambukiza. Magonjwa haya yamekuwa yanachukua kiasi kikubwa sana cha bajeti ya Serikali. Kwa hiyo muda umefika, kama suala tunaambiwa 360,000 kwa mwaka ni kubwa, basi tuiangalie tena na tena lakini kwa mwendo huu tunaoenda nao tutawapoteza Watanzania wengi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuchangia Hotuba ya Wizara ya Elimu. Nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri na Naibu wake kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya. Tunampongeza sana Mheshimiwa Rais kwani wizara hii tayari imeishapokea asilimia 70.2 ya bajeti kufanya kubakia asilimia 29.8 ambapo kimsingi tunaamini mpaka mwisho wa bajeti hii tunayoenda nayo mtakuwa mmeishakamilisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile pia niendelee kumpongeza Mheshimiwa Rais, kwani bajeti ya sekta ya elimu imeongezeka kwa asilimia 18 sisi wote tumekuwa mashuhuda fedha takribani bilioni 300 ambazo zimeenda kwenye miundombinu ya ujenzi wa madarasa ya UVIKO hivyo kufanya kupata madarasa 12,000 tunawapongeza sana kwa kazi kubwa na nzuri mnayoifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuzungumzia ubora wa elimu na tunapozungumzia ubora wa elimu Mheshimiwa Waziri penda usipende, taka usitake lazima tutalizungumzia ama utalisikia suala zima la upungufu wa walimu katika shule za msingi na sekondari ambayo takribani ni 160,000. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Husna, amesema hapa kwamba suala zima la walimu wa kujitolea kwamba majibu ambayo umetujibu ndani ya Bunge ni kwamba hakuna miongozo. Swali lingine ambalo Mheshimiwa Waziri, nikuulize inatohali nini? Au inatutaka nini kuweza kupata hii miongozo kama suala la miongozo tunaamini kwamba walimu wa kujitolea ni kweli linasaidia watoto wetu, linasaidia wanafunzi wetu sasa kwa nini msilete hiyo miongozo? Ama kwanini msitoe hiyo miongozo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu Mheshimiwa Waziri hapa ulipokaa unafahamu kwamba kwenye shule zetu walimu wa kujitolea wapo, wanapeleka maombi, walimu wakuu wanawapokea na wanalipwa posho na inategemea Serikali za vijiji. Serikali za vijiji ambazo zina mapato mazuri ndiyo hawa wanatoa fedha kulipa posho walimu hawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa wakati tunasubiri mpango wa muda mrefu kuhakikisha walimu laki tatu wote tuweze kuajiri siyo jambo la miaka miwili, miaka mitatu inatuchukua hata miaka mitano hata miaka sita. Kwa hiyo, wakati tunasubiri kwenda kwenye jambo la muda mrefu, embu tuje namkakati wa muda mfupi, tuje na jambo la muda mfupi kama tutafanya ile ya kuingia mikataba sawa, kama tutaendelea hili la kusema kwamba Serikali za vijiji lakini mwisho wa siku ni vijiji vingapi vyenye uwezo? Hili kama tunalibariki bado linatakiwa kuja huko wizarani. (Makofi)

Mheshimiwa Mweyekiti, kama sote tunakubali walimu wanaojitolea ni msaada kwa wanafunzi wetu. Kwa hiyo, hatuwezi kuzungumzia ubora wa elimu kama hatuna walimu, hatuna madarasa, hatuna matundu ya vyoo, hatuna madawati, hatuna nyumba za walimu. Kwa hiyo, suala zima la ubora wa elimu ni lazima tuangalie miundombinu lakini pamoja na walimu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo mbali na hilo suala zima la elimu msingi ni lazima Sera itamke wazi wazi kwamba elimu ya msingi ianzie elimu ya awali. Suala hilo Mheshimiwa Waziri, nakusikiliza na nakufatilia sana huwa unalitamka kwamba elimu ya awali na yenyewe ni elimu msingi. Lakini tukija kwenye Sera aijitabanaishi, haijasemwa popote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, elimu ya awali ni iwe elimu ya lazima. Kwa sababu hali ilivyo sasa ni kwamba wengine wanaona ni lazima lakini wengine wanafanya hiyari, na ndiyo hii sasa unakuta katika shule zetu masomo ya kujifunza wakati kwenye shule ya awali a for apple b for ball and c for chair. Watoto wa private wanajifunza kwenye shule za awali lakini watoto wetu sisi wa Serikali wanaenda kujifunza kwenye shule za msingi na ndiyo matokeo yake wakimaliza darasa la saba kwenye mitihani wanaandika mazombi hawajui kuandika majina yao, wakimaliza hawajui kusoma na kuandika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, wakati umefika wa elimu ya awali kuwa elimu ya lazima ili tuweze kuwa na msawazo mzuri kati ya vijijini pamoja na mijini na isiwe kwamba kwa ambae anaejisikia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalo nataka kulizungumzia kwamba tunapo zungumzia ubora wa elimu na tuna zungumza suala zima la udhibiti wa ubora wa shule. Sasa tunao mradi mzuri, niwapongezeni kwa huu mradi wa strengthen school quality assurance. Mheshimiwa Waziri umeutengea takribani bilioni moja lakini mpaka tunavyo zungumza mwezi Februari hakuna hata senti kipande ambayo imeenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi una nia njema, una nia nzuri ya kuweza kusaidia suala zima tunaloliita ubora wa elimu. Tunakuomba kwenye kipindi kilichobaki hebu wapeni fedha ili waanze na mchakato wa huu mradi wa strengthen school quality assurance. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wamesema watu hapa wadhibiti ubora kwamba wadhibiti ubora tunataka kuwalinganisha na CAG katika masuala mazima ya elimu. Sote tunafahamu kazi nzuri inayofanywa na CAG katika masuala ya fedha lakini kama tunasema wadhibiti ubora ndiyo CAG kwa upande wa walimu. Mheshimiwa Waziri muda umefika sasa wadhibiti ubora kuwaanzishia ama kuanzisha taasisi ya udhibiti ubora, wasiishie kuwa kwenye kurugenzi ama kwenye idara kwa sababu kazi wanayoifanya ndio tunataka kusaidia watoto wetu..

Mheshimiwa Mwenyekiti, dunia inaenda kasi sana, mambo yanaenda kasi sana. Kwa hiyo kama hatutakuwa na elimu iliyokuwa bora kwa watoto wetu, tutashindwa Kwenda kushindana huko duniani. Kwa hiyo muda umefika wa kuanzisha taasisi ya udhibiti ubora, muwapatie bajeti yao, muwapatie vote ya kwao ili waweze kufanya kazi bora na nzuri ya elimu hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nakushukuru sana, kubwa la kwangu nililokuwa nataka kulizungumzia ni hilo. Ifike mahala tuwe na elimu iliyokuwa bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo nakushukuru sana. Naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia hotuba ya bajeti iliyokuwa mbele yetu.

Awali ya yote nipende kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia kusimama mbele ya Bunge lako tukufu, lakini naomba uniruhusu nimpongeze Mheshimiwa Waziri kwa uwasilishaji wake mzuri wa bajeti. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niliwahi kuuliza swali hapa Bungeni kuhusiana na mgogoro uliopo Kijiji cha Tondoroni, Kata ya Kiluvya, Wilaya ya Kisarawe, Mkoani Pwani na majibu ya Mheshimiwa Waziri yalikuwa kama ifuatavyo kwamba; “tayari imeshaundwa task force kwa ajili ya kupitia migogoro yote iliyopo baina ya wananchi pamoja na Jeshi letu la Wananchi.” (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama hivyo ndivyo nitapenda kujua sasa status ikoje ya mgogoro unaoendelea wa Kijiji cha Tondoroni, Kata ya Kiluvya, Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani na Jeshi letu task force inasemaje? Nini hatma ya wananchi wa eneo hilo la Tondoroni? Mara ya mwisho katika eneo lile Serikali ililipa fidia lakini kile kilicholipwa kilikuwa kiduchu (kidogo), wananchi wakagoma kuondoka kwa ajili ya kupata nyongeza ama mapunjo ya madai yao. Lakini kilichofuata ni kwamba nyongeza hawakupewa na wananchi hawakuruhusiwa kuyaendeleza yale maeneo. Walipolima, walipojenga Jeshi lilikuwa linaingia usiku linabomoa na asubuhi linazua taharuki kubwa kuharibu mali za watu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nitapenda sana kupata majibu Mheshimiwa Waziri ukija ku-wind up ni nini majibu ya hiyo task force kuhusiana na wananchi wale?

Mheshimiwa Spika, mchango wangu wa pili na wa mwisho ni kuhusiana na suala hilo hilo la migogoro kati ya wananchi pamoja na Jeshi letu la Wananchi. Kwa sasa tunaangazia eneo la Kata ya Kazimzumbwi, Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wetu wa Pwani. Kuna mgogoro mkubwa unaoendelea kati ya wananchi wa Kata ya Kazimzumbwi pamoja na Jeshi Kikosi Na. 191KJ Kisarawe. Hali sio shwari kiasi kwamba kuna malalamiko na masikitiko ambayo tayari yameshawasilishwa katika Ofisi ya CCM Wilaya, juu ya wananchi kupigwa, kuvunjiwa mali zao, nyumba zao pamoja na mashamba yao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, itakumbukwa katika eneo lile la Kazimzumbwi Jeshi lilikuja likaomba nafasi ama likaomba eneo tukaweza kuwapatia eneo, lakini baadaye walirudi wakaomba waongezewe eneo la ukubwa wa mita 200. Serikali ya Kijiji iliwajibu kwamba hakuna hilo eneo, lakini Jeshi lilikaa kimya kwa muda na baadaye likafika likaanza kupiga watu, likaanza kudhuru watu na hatimaye wakatwaa hilo eneo la mita 200 na wakaongeza mita nyingine 300 kufika mita 500. Ni kwa nini Jeshi linatumia nguvu kubwa hivi, hivi imekosekana njia ya namna ya kutumika ili kama hilo eneo linahitajika kwa sababu za kiusalama na bado wananchi wakaendelea kupata haki zao? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa sababu hii migogoro ni ya tangu na tangu tangu enzi ya Mkuu wa Mkoa akiwa Mwantumu Mahiza mpaka sasa RC wetu ni RC Kunenge bado majibu hayajapatikana. Watu hawa wanapata shida sana.

Mheshimiwa Spika, nimeonelea nizungumzie hoja hizi mbili za maeneo haya mawili kwa sababu haya ni maeneo yao kutoka kwa mababu zao. Kama Serikali mnataka lipeni fidi kwa wananchi, mnawaweka wananchi wetu katika hali tatatishi.

Kwa hiyo, nitakuomba Mheshimiwa Waziri utakapokuja kujibu nipate majibu ya kina ya hoja na haja wana Kisarawe wanataka kusikia juu ya hatma yao na haki yao ya ardhi yao ya maeneo mawili niliyoyataja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia. Awali yayote nipende kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia kusimama mbele ya Bunge lako tukufu.

Mheshimiwa Spika, naomba nimpongeze Mheshimiwa Waziri Dada yangu Pindi Chana pamoja na Naibu wake Waziri Mary Masanja, Katibu Mkuu wa Wizara hii Dkt. Francis Michael na Naibu wake Juma Mkomi kwa kazi nzuri na kubwa wanayoifanya.

Mheshimiwa Spika, nitapenda kuanza mchango wangu kwa kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama yetu Samia Suluhu Hassan juu ya suala zima la Royal Tour. Royal Tour imeifungua na kuitangaza zaidi nchi yetu, vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini lakini pia sambamba na hilo Royal Tour imeweza kuongeza fursa za uwekezaji na utalii hapa nchini kwetu. Hivyo ni muhimu sana Royal Tour ifanyike kwa kasi kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, matokeo ya Royal Tour leo tumeweza kuongeza watalii wengi zaidi, tunaambiwa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkoa wa Arusha na Mkoa wa Kilimanjaro kwa miezi mitatu ijayo hoteli zipo full booked kwa ajili ya kupokea watalii kuingia nchini. Lakini kwa upande wa ndege wameongeza flight mfano, Emirates kutoka tatu kwa wiki mpaka saba kwa wiki, Qatar kutoka saba kwa wiki mpaka 15 kwa wiki. Hii ni hatua kubwa sana ama ni matokeo makubwa sana ya Royal Tour. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ingawa lengo la Royal Tour si kuongeza tu watalii pia tunahitaji investment pamoja na biashara ili kukidhi mahitaji ya watalii wetu hapa nchini. Kama hivyo ndivyo watalii wetu hapa nchini watahitaji hoteli nzuri, rest house, vivutio vya huduma muhimu, barabara nzuri, usafiri wa ndege wa uhakika, wahudumu wazuri interms of customer care. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni vema Bunge lako likafahamu utalii ama Wizara hii ya Utalii can’t stand alone ili kuweza kufikia mkakati sawasawa wa masuala mazima ya utalii hapa nchini. Hivyo basi Wizara kama Miundombinu, Wizara ya Ardhi, Wizara ya Mawasiliano na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ni lazima zizungumze lugha moja ili tuweze kufikia malengo tarajiwa ya sekta nzima ya utalii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais Mama yetu Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa na kazi nzuri sana ya kuhakikisha milango ya utalii inafunguka na imefunguka kwelikweli. Tumeona kwenye filamu ya Royal Tour kupitia hapo kisiwa chetu cha Zanzibar kimeweza kupata watalii wa kutosha.

Mheshimiwa Spika, alternative ya utalii hapa nchini ukiacha Kisiwa cha Zanzibar ni Kisiwa cha Mafia Mkoani Pwani, Kisiwa cha Mafia Mashallah Mwenyezi Mungu amekijalia kina beach ama fukwe nzuri sana, lakini pia kuna samaki yule wa ajabu mwenye madoido anaitwa whale shark ama papa potwe ambaye wazungu wanampenda sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia kuna sport fishing, nikisema nielezee vivutio vilivyopo katika kisiwa chetu cha Mafia nitapoteza ama nitachukua muda mwingi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, isipokuwa kwa masikitiko makubwa kabisa as we are speaking here over 90 percent ya ardhi ya Kisiwa cha Mafia hakijapimwa. Leo tunazungumzia suala la uwekezaji, tunazungumzia suala la biashara; ni mfanyabiashara gani, ni mwekezaji gani atakuja kuwekeza kwenye ardhi ambayo haijapimwa. Tunajua wazi hakuna mwekezaji wa namna hiyo, wenzetu wanavyotaka kuwekeza wanahitaji wawe na title, sasa kama hatuna title, kama eneo hatujapima tusifikiri kama tunaweza kupata hao wawekezaji.

Kwa hiyo, mimi nataka niwaombe sana Serikali hususani Wizara ya Ardhi iangalie namna ya kupima maeneo haya mahususi kama vile Kisiwa cha Mafia ili tuweze kukifungua kwa upande wa utalii. Hakuna biashara ya utalii isiyoendana na hoteli, migahawa pamoja na fukwe nzuri za beach. Sasa kama hatujapima ardhi yetu itakuwa tunapoteza wakati na ndiyo maana nikasema ni vema Wizara hizi zikazungumza lugha moja ili tuweze kuufungua utalii pamoja kisiwa chetu cha Mafia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tukizungumza habari ama biashara ya utalii mimi nitaomba Serikali ikija inieleze mipango na mkakati wa kuhakikisha inakipanua kiwanja cha ndege cha Mafia. Kiwanja cha ndege cha Mafia ni kidogo chenye runway ya mita 800 kimsingi ndege kubwa haziwezi kutua pale na tunafahamu watalii wanapotoka eneo la utalii wanataka waende straight kwenye destination na wakitoka hapo waongoze moja kwa moja kwenda eneo wanalotaka kwenda kutalii. Wazungu hawapendi mambo ya transit, kwa msingi huo tunaweza tukapoteza baadhi ya watalii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, mimi nataka niombe sana Serikali ije na mipango ya kuhakikisha kwamba inapanua kiwanja hiki cha ndege, lakini pia tuweze kujenga barabara ya lami iliyokuwa kule Mafia ya Ras Mkumbi kilometa 55. Mtalii anapoingia, ametua kwenye ndege anapoingia kwenye gari kuelekea hotelini barabarani vumbi tupu. Kwa hiyo, lazima tujenge miundombinu yetu ili tuweze kuifungua sekta hii ya utalii. Lakini kisiwa cha Mafia kina visiwa vidogo vidogo kama Chole, Jibondo na vinginevyo, kwa hiyo, mtalii kutoka kisiwa kimoja mpaka kwenda kisiwa kingine tunahitaji tupate vyombo vya kuwachukua kama speed boat. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwahiyo, nitaomba sana Serikali ije na majibu ya kujibu hizi changamoto ya namna gani tunakifungua kisiwa cha Mafia kwa ajili ya kuchochea utalii. Niombe sana kwamba Royal Tour inaendelea, episode ya pili ama season ya pili, nataka kuomba sana ipige jicho lake kwenye kisiwa chetu cha Mafia ili na yenyewe iweze ku-appear kwenye hii filamu ya Royal Tour.

Mheshimiwa Spika, nikushukuru sana kwa kunipa nafasi mwisho nimalizie na ombi ama ushauri kwa Serikali. Royal Tour kwa ushauri wangu mimi ni vema ikakabidhiwa ama ikawa chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii na si kule Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo licha ya kwamba Serikali ni moja tunakubali, lakini ili iweze kusimama vizuri ni vema ikawa mikononi mwa Wizara ya Maliasili na Utalii na si kwenye michezo.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nakushukuru kwa kunipa nafasi, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na naunga mkono hoja na niwaombe Wabunge wenzangu wote tuunge mkono hoja ya Wizara yetu hii muhimu kwa usalama wa nchi yetu, sote tunalala na tunaishi kwa amani kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka jana nilisimama hapa Mheshimiwa Waziri, nikamwambia hivi Kikosi Namba 191 cha kule Kazimzumbwi, Kisarawe walifika katika Ofisi ya Serikali ya Kijiji kwa ajili ya kuomba eneo lenye mita 202 na kwa sababu tunafahamu jeshi na tunafahamu kwamba ardhi ni mali ya umma ambaye msimamizi wake mkuu ni Rais, sisi tukasema sawa kabisa walete barua ama maombi ya eneo hilo la mita 200.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuwakubalia na kuwaletea barua wakati wanakuja kupima hizo mita 202, wakaenda zaidi wakachukua zaidi ya mita 202 na hapo ndipo sintomfahamu ilipoanza kati ya Wananchi wa Kazimzumbwi pamoja na Jeshi Kikosi Namba 191 kule Kisarawe.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikamwambia Mheshimiwa Waziri kwamba baada ya ile mivutano ikafika mahali tukakubaliana mtatulipa fidia, lakini tangu mwaka 2011 na leo tunazungumza mwaka 2024 fidia hiyo takribani miaka 13 bado hamjatulipa. Mheshimiwa Waziri nitaomba utakapokuwa unakuja kujibu hapa katika shilingi bilioni 11 ulizozisema katika hotuba yako, Kisarawe Kazimzumbwi na kule Tondoroni tupo mahali gani au tuna kiasi gani za kulipiwa fidia ya maeneo yetu? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya sisi kuridhia kabisa mchukue hili eneo kwa sababu tunafahamu umuhimu wa jeshi, tunafahamu kazi ya jeshi, kilichofuata ni kwamba kuna ambush, mnatukataza tusiendeleze, kujenga, kulima mnatukataza na mmeweka pale mabango kwamba hili ni eneo la jeshi huruhusiwi kufanya kitu chochote. Kama hivyo ndivyo, tunaomba mtuambie fidia yetu mnatupatia na mtatupatia lini? Mheshimiwa Waziri mimi nitakuomba kama nimetangulia kusema tunaunga mkono bajeti yako na Wabunge wote wa Bunge hili tunaomba tuunge mkono kwa uzito wa Wizara hii, lakini nikuomba sana mara baada ya Bunge hili, tunakuomba uje Kisarawe, uzungumze na wananchi wa Tondoroni pamoja na wananchi wa Kazimzumbwi. Tunakuomba sana Mheshimiwa Waziri kwa unyenyekevu wa hali ya juu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la mwisho kabisa Mheshimiwa Waziri mimi nitakuomba ukija kujibu uje utuambie kwa sababu watu wa kutoka Wizarani kwako walivyofika wao wakasema wanafanya utambuzi, sisi hatuelewi utambuzi ni kitu gani, sisi tunaelewa tathmini.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili tuweze kufidiwa maeneo yetu tunachokijua sisi tunatakiwa kufanyiwa tathmini na sio utambuzi kwa sababu hatujapigwa picha na wala wale wananchi hawajajaza fomu wale wananchi. Sasa utakapokuja kutoa majibu hapa utuelezee kwamba huo utambuzi ndiyo tathmini na tutaenda kulipwa kwa minajili ipi ili hali fomu hatujajaza na wala picha hatujapigwa, tunaenda kulipwaje lipwaje? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, atakapokuja kujibu Mheshimiwa Waziri anaomba atuambie shilingi bilioni 11 ni kiasi gani inaenda kwa wananchi wa Kisarawe, Kata ya Kazimzumbwi, Kijiji cha Kazimzubwi pamoja na Kijiji cha Tondoroni.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nipende sana kumpongeza sana tena sana Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, lakini pia nakupongeza wewe Mheshimiwa Waziri ninyi ni wanawake na nusu. Mnafanya kazi kubwa sana wamama ninyi, Taifa letu lipo limetulia kabisa, nchi yetu ipo imetulia kabisa chini ya wanawake mahiri na madhubuti. Kwa hiyo mimi nipende kuwapongeza sana kwani ulinzi wa nchi yetu upo imara. Kwa hiyo, nitaomba sana utakapokuja hapa utupatie majibu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi, naunga mkono hoja na ahsnate sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na naunga mkono hoja na niwaombe Wabunge wenzangu wote tuunge mkono hoja ya Wizara yetu hii muhimu kwa usalama wa nchi yetu, sote tunalala na tunaishi kwa amani kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka jana nilisimama hapa Mheshimiwa Waziri, nikamwambia hivi Kikosi Namba 191 cha kule Kazimzumbwi, Kisarawe walifika katika Ofisi ya Serikali ya Kijiji kwa ajili ya kuomba eneo lenye mita 202 na kwa sababu tunafahamu jeshi na tunafahamu kwamba ardhi ni mali ya umma ambaye msimamizi wake mkuu ni Rais, sisi tukasema sawa kabisa walete barua ama maombi ya eneo hilo la mita 200.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuwakubalia na kuwaletea barua wakati wanakuja kupima hizo mita 202, wakaenda zaidi wakachukua zaidi ya mita 202 na hapo ndipo sintomfahamu ilipoanza kati ya Wananchi wa Kazimzumbwi pamoja na Jeshi Kikosi Namba 191 kule Kisarawe.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikamwambia Mheshimiwa Waziri kwamba baada ya ile mivutano ikafika mahali tukakubaliana mtatulipa fidia, lakini tangu mwaka 2011 na leo tunazungumza mwaka 2024 fidia hiyo takribani miaka 13 bado hamjatulipa. Mheshimiwa Waziri nitaomba utakapokuwa unakuja kujibu hapa katika shilingi bilioni 11 ulizozisema katika hotuba yako, Kisarawe Kazimzumbwi na kule Tondoroni tupo mahali gani au tuna kiasi gani za kulipiwa fidia ya maeneo yetu? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya sisi kuridhia kabisa mchukue hili eneo kwa sababu tunafahamu umuhimu wa jeshi, tunafahamu kazi ya jeshi, kilichofuata ni kwamba kuna ambush, mnatukataza tusiendeleze, kujenga, kulima mnatukataza na mmeweka pale mabango kwamba hili ni eneo la jeshi huruhusiwi kufanya kitu chochote. Kama hivyo ndivyo, tunaomba mtuambie fidia yetu mnatupatia na mtatupatia lini? Mheshimiwa Waziri mimi nitakuomba kama nimetangulia kusema tunaunga mkono bajeti yako na Wabunge wote wa Bunge hili tunaomba tuunge mkono kwa uzito wa Wizara hii, lakini nikuomba sana mara baada ya Bunge hili, tunakuomba uje Kisarawe, uzungumze na wananchi wa Tondoroni pamoja na wananchi wa Kazimzumbwi. Tunakuomba sana Mheshimiwa Waziri kwa unyenyekevu wa hali ya juu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la mwisho kabisa Mheshimiwa Waziri mimi nitakuomba ukija kujibu uje utuambie kwa sababu watu wa kutoka Wizarani kwako walivyofika wao wakasema wanafanya utambuzi, sisi hatuelewi utambuzi ni kitu gani, sisi tunaelewa tathmini.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili tuweze kufidiwa maeneo yetu tunachokijua sisi tunatakiwa kufanyiwa tathmini na sio utambuzi kwa sababu hatujapigwa picha na wala wale wananchi hawajajaza fomu wale wananchi. Sasa utakapokuja kutoa majibu hapa utuelezee kwamba huo utambuzi ndiyo tathmini na tutaenda kulipwa kwa minajili ipi ili hali fomu hatujajaza na wala picha hatujapigwa, tunaenda kulipwaje lipwaje? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, atakapokuja kujibu Mheshimiwa Waziri anaomba atuambie shilingi bilioni 11 ni kiasi gani inaenda kwa wananchi wa Kisarawe, Kata ya Kazimzumbwi, Kijiji cha Kazimzubwi pamoja na Kijiji cha Tondoroni.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nipende sana kumpongeza sana tena sana Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, lakini pia nakupongeza wewe Mheshimiwa Waziri ninyi ni wanawake na nusu. Mnafanya kazi kubwa sana wamama ninyi, Taifa letu lipo limetulia kabisa, nchi yetu ipo imetulia kabisa chini ya wanawake mahiri na madhubuti. Kwa hiyo mimi nipende kuwapongeza sana kwani ulinzi wa nchi yetu upo imara. Kwa hiyo, nitaomba sana utakapokuja hapa utupatie majibu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi, naunga mkono hoja na ahsnate sana. (Makofi)
The Written Laws (Miscellaneous Amendment) (No.2) Bill, 2016
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Napenda kuipongeza Serikali kwa kuja na huu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na.2 ya mwaka 2016. Kikubwa zaidi napenda kuipongeza Serikali kwa kutuletea mapendekezo na maboresho ya kuongeza kifungu kipya cha 45 (a) katika sheria ya Taasisi za Kazi Sura namba 300.
Mheshimiwa Naibu Spika, kimsingi sina matatizo na uwepo wa hiki kifungu kwa sababu kinaenda kuwasaidia wafanyakazi wa Taifa hili. Kimsingi kifungu hiki kinaenda kuwabana wale waajiri ambao kwa makusudi wanaamua kukanyaga sheria za kazi ikiwemo na hili la kutokupeleka michango ya hifadhi ya jamii. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ambacho sikubaliani katika kifungu hiki, ni ile faini ama tozo iliyowekwa kwa mwajiria mbaye kwa makusudi atakiuka Sheria za Kazi kwamba atatozwa kiasi cha shilingi 100,000/=. Ninasema hivyo kwa sababu nimekaa kwenye Vyama vya Wafanyakazi na nimekaa kwenye Mamlaka ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, nina uzoefu na hawa waajiri. Hizi faini ndogo ndogo, wao wameshafika mahali wamezizoea. Wao imeshafika mahali wanaona ni wanazimudu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ambacho napendekeza, twende tukaifute hii shilingi 100,000/= na twende tukaweke shilingi 500,000/= iwe “not less than TShs. 500,000/=.” Tukiweka hii shilingi 100,000/= ama tunavyosema not less than TShs.100,000/=, mwisho wa siku ile tija ambayo tunaitafuta nia njema Serikali ambayo mnataka kuwasaidia wafanyakazi wa Taifa hii hatutakaa tuipate. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda tu kutoa mfano katika hili suala zima la ucheleweshaji wa michango ya hifadhi ya jamii. Ukienda kwenye sheria zote za mifuko ya hifadhi ya jamii, ama niseme Mifuko ya Pensheni, kuna kifungu ambacho kinasema, “mwajiri yeyote atakayechelewesha michango ya mwanachama katika mifuko ya hifadhi ya jamii, ataenda kutozwa asilimia tano.” Leo hii kuna ucheleweshaji mkubwa wa michango ya hifadhi ya jamii katika mifuko ya hifadhi ya jamii. Ndiyo maana nasema, kwa kuwawekea hiki kiwango kidogo, haitatuletea tija ile ambayo sisi tunaitafuta. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, bado nipo hapo hapo katika hiki kifungu kipya cha 45 (a). Kimsingi hiki kifungu kinampa mamlaka Afisa Kazi (Labour Officer) kuweza kuwatoza faini hawa waajiri ambao wanakiuka sheria za kazi ikiwemo na hili la kutokupeleka michango ya hifadhi ya jamii. Sina tatizo na Labour Officer kusimamia hao waajiri ambao wanakiuka hizi sheria za kazi, sina tatizo, isipokuwa wasiwasi wangu upo kwa huyu anayeitwa Labour Officer kupatiwa jukumu la kumtoza faini mwajiri ambaye hakupeleka michango ya hifadhi ya jamii.
Mheshimiwa Naibu Spika, wasiwasi wangu ni kwamba Labour Officer scope yake ya kazi ni kubwa, ana-deal na mambo mengi sana likiwemo hilo la kusimamia hizi sheria za kazi; ana mambo ya OSHA, Vyama vya Wafanyakazi na mambo mengine mengi. Kwa hiyo, kuchukua hiki kipengele cha kutokupeleka michango ya hifadhi ya jamii, kipengele mahususi hiki kumkabidhi yeye naona kwamba impact yake itakuwa ndogo. Kwa nini tunampa Labour Officer na wakati mamlaka ama taasisi mahsusi inayo-deal na hifadhi ya jamii ipo? Kwa nini tusipeleke mamlaka haya ama kazi hii kwa mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, yaani SSRA?
Mheshimiwa Naibu Spika, ukiliacha hilo la kwamba Afisa Kazi, scope yake ya kazi ipo kubwa sana na hili suala la kutokupeleka michango ya hifadhi ya jamii linaweza likaleta ucheleweshaji, lakini pia SSRA tayari wamesha-advance katika mifumo yao. Wana kitengo cha compliance ambacho kimsingi kipindi niko pale nikifanya kazi, kuanzia asubuhi mpaka jioni wanachama wanamiminika na complain yao kubwa ni kwamba michango yao ya hifadhi ya jamii haijafika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda ieleweke, kwa mujibu wa hizo sheria ni kwamba mtu kuweza ku-qualify kupata pension ukiacha ile umeshafikisha umri miaka 55 kwa hiari na 60 kwa lazima, lakini pia kuna kifungu kinachosema, uwe umechangia miaka 15. Kwa maana hiyo, kama imepelea miezi minne ama mitano hukupeleka michango yako, hu-qualify wewe kupata pension.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tukienda tukasema tunampa huyu, tukaacha kumpa SSRA, ninahofu na wasiwasi kwamba dhamira njema Serikali mnayoitafuta hatutakaa tuipate.
Mheshimiwa Naibu Spika, kingine tena, SSRA wana instrument, wana database management guideline ambayo inawawezesha wao kwa kupitia hii mifuko kuweza kupata details ama taarifa za mwanachama, namba ya mwanachama, majina yake, michango yake nakadhalika. Kwa hiyo, nadhani tukimkabidhi SSRA, itakuwa ni nyepesi sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kingine, wakati naondoka pale SSRA niliacha wanaandaa program ya wao ku-connect mifumo yao na TRA ili waweze kuwajua waajiri wote, walipakodi nchini. Kwa hiyo, kama unawafahamu waajiri wote wanaolipa kodi nchi hii, ni rahisi ni rahisi kama kuna mwajiri analipa kodi kwa kiasi kikubwa, huyo atakuwa na wafanyakazi. Kwa hiyo, ni rahisi ku-trace kwamba kama analipa kodi: Je, wafanyakazi wake amewaandikisha kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii? Je, michango ya hifadhi ya jamii imepalekwa? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nilikuwa naona tukimpa SSRA itakuwa ni rahisi sana. Pengine kama Serikali itapata ugumu wa moja kwa moja kulipeleka kwa SSRA katika maana kwamba hii kazi apewe SSRA, basi naomba huyu Labour Officer afanye kazi hii kwa kushirikiana na SSRA. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kukushukuru sana, lakini pia naungana na wale wenzangu wote waliokuwa wakizungumzia Sheria ya Elimu. Adhabu ya miaka 30 ni mahsusi kabisa, inawatosha kwa wale wote ambao wanaenda kuwakwamisha watoto wa kike wasitimize ndoto zao ambazo wamekuwa wakizifikiria. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naungana na wale wote waliozungumzia marekebisho, I mean kupongeza kifungu hicho, nami niungana nao mkono.
Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, nachukua nafasi hii kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufanya uteuzi wake wa ma-DC. Kikubwa zaidi, kumekuwa na ma-DC vijana wengi sana. Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuonesha imani kwetu vijana. Nawaomba vijana wenzangu walioteuliwa u-DC waende wakafanye kazi. Kimsingi tunasema, Hapa Kazi Tu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru.
Muswada wa Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma wa Mwaka 2017
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuchangia Muswada uliopo mbele yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya uchache wa muda, niende moja kwa moja kwenye Ibara ya 29 ambayo imeweka orodha ya mafao pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuiomba Serikali yangu ione sasa umuhimu ili iweze kuja na amendment iongeze fao la elimu. Kwa mujibu wa ILO, minimum standard ya haya mafao ni tisa, sisi hapa tuna saba, haitakuwa mbaya sana tukiongeza fao la elimu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tukiacha hivyo, Serikali ya Awamu ya Tano ya Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli, tayari inatoa elimu bila malipo kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne. Kwa hiyo, itapendeza kama mfuko utatoa fao la elimu ili kuweza kusaidia kwa Kidato cha tano na cha sita, mwanafunzi huyu akimaliza, anakutana na Bodi ya Mkopo kuweza kupata mkopo kuendelea na elimu yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu wa pili uko hapo hapo kwenye Ibara ya 29 kuhusiana na unemployment benefit. Naipongeza sana Serikali kwa kuona umuhimu wa kuja na fao hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa muda mrefu sana nchini kwetu kumekuwa na taharuki au sintofahamu ya withdrawal benefit. Kwa hiyo, naipongeza sana Serikali kwa kuliona hili. Ukichukua ripoti ya Upinzani ambapo katika ukurasa wake wa 12, wao wanavyoona, fao la kujitoa linaenda kuchukua nafasi ya withdrawal benefits. Hivi ni vitu viwili tofauti, unapuzungumzia withdrawal benefit ama fao la kujitoa kwanza kwa mujibu wa ILO, hakuna fao la kujitoa au hakuna withdrawal benefit. Kwa wao hilo siyo fao, ukienda kwenye orodha ya mafao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, unapozungumzia withdrawal benefit, tafsiri au maana yake mwanachama aliyechangia kwa muda wa miaka nane akaja akapata janga la kupoteza ajira, maana yake anaenda kwenye ule mfuko anatoa yale mafao yake. Baada ya mwaka mmoja au miaka miwili, akipata ajira anaenda tena kuanza sifuri ama kuanza moja. Sasa hapo tunamsaidia mwanachama ama tunamuumiza huyu mwanachama? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuja na hili fao la unemployment benefit litaenda kuwasaidia wenzetu ambao katikati ya ajra yake amepata bahati mbaya ya kupoteza ajira.

TAARIFA . . .

MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, siipokei taarifa yake, achukue ripoti yake, sitaki kupoteza muda, dakika ni saba. Asome mstari wa mwisho. Imeandikwa tu kwa kiswahili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, najaribu kuwapa elimu ya withdrawal benefit. Unapoenda kumwambia mtu aka- withdraw mafao yake unaenda kumuumiza huyu mwanachama. Kwa sababu ili u-qualify kupata pension ni miaka 15. Kwa hiyo, kama leo ana-withdraw mafao yake, akija baada ya miaka miwili akipata ajira, tafsiri yake anaanza sifuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza sana Serikali kwa kuja na unemployment benefit, maana huyu mwanachama ikitokea bahati mbaya amepoteza ajira, kutokana na fao hili, ataenda atalipwa asilimia 33.3 ya michango yake kwa muda wa miezi sita. Ikipita miezi sita ikitokea hajapata ajira, atahamishwa kutoka kwenye mandatory scheme atapelekwa kwenye supplementary au voluntary scheme. Ataendelea kupewa michango yake kwa muda wa miezi 18 tukiamini baada ya hiyo miaka miwili atakuwa amepata ajira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali yangu sasa iboreshe tu hapa kwa kuangalia baada ya ile miezi sita na ile miezi 18 ambayo amehamishiwa kwenye voluntary scheme, ikitokea amepata ajira, je, tutamrudisha tena kule kwenye mandatory? Tukimrudisha, tunaanzaje kuhesabu? Kwa hiyo, naiomba Serikali yangu ikiweke hicho kifungu kizuri kabisa cha unemployment benefit ili kuweza kuwasaidia watumishi wa Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye Ibara ya 35. Ibara hii pia inazungumzia suala hili la unemployment benefit. Ili tukae vizuri kabisa na tuondokane na hizi kelele za withdraw, naona kile kifungu cha 35(2)(e) ambacho kinasema; “proves to the Director General that he has not secure, another employment.” Ni ngumu sana kuli-prove hili kwmaba sijapata ajira. Hili limekaaje? Naomba Mheshimiwa Waziri atakapokuja ku-windup, alitolee ufafanuzi hili ili kuondoa huo ukakasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tuzungumze kuhusiana na suala la formula kuwepo kwenye muswada huu. Suala la kutumia moja chini ya 520 ama moja chini ya 540 ama 580 hatukurupuki tu kwa utashi wa kiasiasa na tukasema twende tutumie hii. Ni lazima tukafanye actuarial report, hii ndiyo itatuongoza tunaenda na mtindo gani ambapo tutaangalia namba ya wachangiaji, namba ya wastaafu, namba ya uwekezaji na kadhalika. Hiyo ndiyo itakayosema tunaenda kwenye formula ipi? Siyo tu mtu unaamka unataka ile formula ambayo unaitaka wewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kile kinachosemekana kana kwamba Serikali imekuja na merging as if haijafanya actuarial report, no, Serikali imefanya. Pengine labda mwende mkasome, mkatafute. Tukienda na hii 100 chini ya 540 maana yake, contribution rate iende ikapande mpaka asilimia 35?

Sasa are we ready kwa wafanyakazi wetu wachangie kutoka asilimia 20 mpaka…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Mwaka 2018
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili na mimi niweze kuchangia muswada huu wa ubia kati ya sekta binafsi na sekta ya umma. Awali ya yote napenda kuipongeza Serikali kwa kuona umuhimu wa kuleta marekebisho haya ndani ya Bunge lako tukufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimejaribu kusoma tafsiri ama maana tofauti ya hili neno PPP lakini pia ukiangalia madhumuni ya mapendekezo ya sheria hii, huoni moja kwa moja ni kwa namna gani mradi wa Daraja la Kigamboni kwamba ni mradi wa PPP. Pia mabasi yaendayo kasi ukiangalia hasa tafsiri ya PPP huioni moja kwa moja. Ukija pia kwenye ule mradi uliokuwa mwanzoni uanzie Kigamboni uje Ubungo mpaka Mlandizi - Chalinze lakini kwa sasa kwa namna inavyoenda pia haijieweki waziwazi kama ni mradi wa PPP. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niruhusu nisome madhumuni au kusudio la kuletwa marekebisho haya. Nikianzia hapa inasema kwamba juu ya madhumuni mengine, lakini hapa anasema; “Aidha, muswada huu unakusudia kumpa Waziri mwenye dhamana na masuala ya PPP mamlaka ya kisheria ya kuidhinisha miradi ya ubia kati ya sekta binafsi na sekta ya umma kwa lengo la kuimarisha utekelezaji wa miradi ya PPP.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa napenda sana kuipongeza Serikali kwa kusudio hili. Kiukweli tuna miradi mingi sana na mikubwa sana nchini kwetu ambayo kimsingi Serikali ikisema ifanye miradi hii yote kwa pesa yake yenyewe binafsi hatutakaa tumalize ama tutaimaliza kwa kuchelewa sana ukilinganisha na nchi nyingine duniani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna mradi kwa mfano wa reli ya kati wenye kilometa takribani 2,700 ukijumlisha na matawi yake ambayo kimsingi tunajenga kwa fedha za ndani. Pia tuna mradi wa reli ya kwenda Kusini na Kaskazini, upanuzi wa viwanja vya ndege, upanuzi wa bandari, ujenzi wa vivuko na ujenzi wa meli. Kwa hiyo, ukichukua miradi hii yote ukisema tusubiri Serikali itekeleze kwa fedha yake binafsi tutachelewa na tutaachwa na wenzetu ambao kimsingi hapo awali wao tuliwaacha nyuma, sisi tulikuwa mbele, lakini kwa sasa wametuacha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia nchi kama South Africa, India, Brazil na China wenyewe ukiangalia uchumi wao na muonekano wa nchi zao wametuacha mbali sana. Kwa hiyo, naipongeza Serikali kwa kuona huo umuhimu wa kuweza kuleta marekebisho haya ya sheria. Umuhimu wa suala hili na hata tukiangalia kwa upande wetu wa bajeti, haitakaa ituathiri kibajeti. Kwa sababu gani nasema hivyo? Kuliko kutenga bilioni kadhaa at once kwa mradi mmoja, ni vema mradi huo tukauingiza kwenye masuala ya PPP. Halafu kitu tutakachokifanya, kila mwaka wa bajeti tuwe tunatenga fedha ile kidogo kidogo mpaka kufikia ile miaka aidha, 20 ama 30 tuliyokubaliana ya utekelezaji wa mradi ule. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunajikuta kwamba mambo yetu mengine ambayo yanawavutia wawekezaji tunayafanya na yale mambo ambayo wawekezaji hawapendi kupeleka fedha moja kwa moja, pia tunakuwa tunafanya. Kwa hiyo, masuala mazima ya PPP ni masuala muhimu sana kwa Taifa letu hapa tulipofikia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pengine napenda tu kuishauri Serikali, amesema ndugu yangu Mheshimiwa Kanyasu na mimi nitapenda kukazia hapo. Hii Sheria ya PPP tulikuwanayo miaka nane iliyopita, leo yameletwa marekebisho. Kimsingi unaona kabisa hatujawahi kufanikiwa kwenye mradi wa PPP na ndiyo maana Mheshimiwa Waziri kwenye taarifa yako mifano uliyotoa ni Kigamboni na barabara ziendazo kasi ama mabasi yaendayo kasi, huoni moja kwa moja ile maana hasa ya mradi wa PPP.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niseme tu kimsingi kwenye PPP hatukufanikiwa. Sababu ambazo zimepelekea kutofanikiwa ni pamoja na kutokuwa makini katika kuingia hii mikataba. Tumekosa umakini mzuri katika kuingia hii mikataba ndiyo maana tumejikuta tunakosea ama tunashindwa mradi, tunafanya namna ya kuingia miaka 90 ndiyo huo mradi wawekezaji watuachie sisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo kila mradi tunaweza kuingia nao kwenye PPP. Kwa mfano, tukisema miradi ya barabara, barabara life span yake ni miaka 30. Kwa hiyo, tunajengewa barabara katika tafsiri kwamba mwekezaji atoe huduma na aweze kurudisha faida yake na baada ya hapo airudishe kwa Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia kitu kama barabara, baada ya miaka 30 au 20 inakuwa tayari imeshachoka, kwa hiyo, ndicho hicho ninachozungumzia umakini katika design. Watu wetu tutakaowapa hili suala au watakaosimamia haya masuala, mbali ya kwamba watatakiwa kujengewa uelewa, pia mbali ya kuwa makini katika masuala ya mikataba, namna ya kuiingia ni muhimu kwenye suala la designing wakawa makini kweli kweli, siyo kila mradi tutakaoweza kuuingiza huko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine nililokuwa nataka kulizungumza, nakubaliana na wale wote waliosema kiukweli tumechelewa kufanya marekebisho ya sheria hii. Ni kweli tumechelewa kwa sababu uzuri wa miradi ya PPP vihatarishi vyote vinabebwa na mwekezaji. Pia tuna chance ya kuchagua namna ya ule mradi tunapenda uweje ama uonekanaje? Kwa hiyo, siyo suala la kukaa nalo mbali au siyo suala la kulala, ni suala la kulichangamkia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ukiangalia umuhimu mkubwa ambao unakuwepo hapa katika masuala mazima haya ya uwekezaji wa PPP, mwekezaji anawekeza katika lengo la kufanya biashara. Mbali ya hapo atalipa kodi kwa Serikali yetu, atatoa ajira kwa vijana wetu na baada ya miaka kadhaa atarudisha ule mradi kwa Serikali yetu, inabaki kuwa mali ya Serikali kwa asilimia 100.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hili suala cha msingi ninachozungumza hapa, hatuhitajiki kulala, tunahitajika kuwa faster katika suala hili, kwani wenzetu wametuacha mbali sana. Kikubwa zaidi hapa, lengo la mwekezaji kufanya biashara ambalo atakakuwa nalo whether kwenye mradi wowote atakaouanzisha, fedha zitarudi kwa Serikali kupitia kodi, lakini pia ukiacha masuala mazima hayo ya kodi, kama nilivyozungumza suala la ajira, suala la utoaji nafasi mbalimbali kwa...

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

Nakushukuru sana, naunga mkono hoja.