Contributions by Hon. Hamad Hassan Chande (15 total)
Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2021/2022 pamoja na Mapendekezo ya Muongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2021/2022
MHE. HAMAD HASSAN CHANDE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii ya kuwa mtu wa awali katika wachangiaji kwa jioni hii ya leo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, namshukuru Mwenyezi Mungu Subhanah-wataala ambaye ametuwezesha sisi kufika katika jengo hili na ametujalia kuwa na rasilimali ya uhai ambayo ndiyo inatoa thamani ya ubinadamu. Maana yake bila rasilimali ya uhai, basi binadamu anakosa thamani ya ubinadamu. Ushahidi wa hilo, moja kati ya sisi akipoteza uhai tu, basi wapenzi wake wa karibu ikiwemo familia yake, wanakaa kwa pamoja vikao tofauti kujadili wapi wanaenda kumweka na kumtoa kwenye nyumba hata kama ni nzuri aliyoijenga kwa gharama kubwa. Kwa hiyo, tumshukuru Mungu kutujalia rasilimali hii ya uhai. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu, nakishukuru sana Chama changu Cha Mapinduzi kwa kunipa nafasi hii, kuniteua tangu awali mpaka kufika hapa leo, kwa sababu ni chama makini chenye viongozi imara sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya shukurani hizo, naomba kwa ruhusa yako nianze na neno la Mungu kutoka katika Kitabu cha Qurani aya ya nane, Sura ya 102 inayosema:
Kisha kwa hakika mtaulizwa siku hiyo juu ya neema mlizopewa, mmezitumiaje? Kwa hakika tumepewa neema nyingi sana. Mungu ametujalia neema nyingi sana katika nchi yetu ya Tanzania pande zote, sisi ni wa kujivunia kwa neema hizo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu mimi ni Mbunge kutoka Jimbo la Kojani na Wakojani tunajulikana sana kwa shughuli za uvuvi, naomba tu nijielekeze huko kwenye masuala ya uvuvi. Neema hizi ambazo ametupa Mungu hasa katika suala la uvuvi baharini na hata kwenye maziwa, zipo kanuni ambazo zimewekwa na baadhi ya watendaji wetu wa Wizara ama Idara ambazo zimekuwa vikwazo vya kutumia vizuri neema hizo.
Kwa mfano, Kanuni ya 58A(1) na (2) inayomtaka mvuvi lazima atumie mtego wenye urefu wa mita 144. Hiki ni kikwazo kikubwa sana kwa wavuvi wetu, inayotaka uvue samaki wa sentimeta 26. Kwa kweli baadhi ya samaki ambao wala hatuharibu mazingira, tunawahitaji kuwapata, lakini inakuwa ni ngumu sana kwa wavuvi wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kanuni ya pili ambayo ni kikwazo kidogo ni 58A ya uvuvi wa dagaa. Inataka dagaa wanaovuliwa wawe ni wa sentimeta tano. Kwa kweli dagaa wa sentimeta tano hadi saba, unaweza ukamwita sio dagaa tena huyo, anaweza kuwa ni samaki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kanuni ya 66(1)(hh), taa za utumiaji katika uvuvi wakati wa usiku. Kanuni inataka taa ziwe ni za watts 50. Ni mwanga mdogo sana unaopatikana hasa kwa jiografia kwa baadhi ya maziwa kama vile Tanganyika au Bahari Kuu. Kuvua kwa watts 50 ni ndogo sana, samaki au dagaa hawezi kushawishika kuja katika mwanga na kuweza kumvua kwa urahisi. Kwa hiyo, ni vyema angalau iwe inafikia watts 200 au 300 kama kawaida ambavyo tunavua sisi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kanuni nyingine ambayo ni kikwazo ni ile inayomtaka mvuvi asivue wakati wa mbalamwezi, lazima avue mwezi unapokuwa giza. Sasa hizi sisi wavuvi kwa mfano wa ring net ambao tunavua usiku wote ikiwa ni wa mbalamwezi au wa giza, ukisema tuvue msimu huo, ukifika wakati wa mbalamwezi tukale wapi jamani? Au tusubiri mpaka uingie usiku mwingine wa giza, siku 15 zile, au siku 10; nadhani hiki ni kikwazo kikubwa sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ubaya wa kanuni hizi, zinawafanya wavuvi wetu kutoroka katika nchi yetu na kwenda nchi za jirani. Baya zaidi, sisi tunafuga samaki, tunawalea, wanakua, wenzetu wa jirani ndio wanavua na kutumia samaki hao. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu kwa hili ni kwamba, hizi kanuni zitakapowekwa au zitakapotungwa ni vyema kuwashirikisha na wavuvi, sio wataalam wa uvuvi peke yao ambao wanajisomea tu kwenye meza na viti. Walengwe kabisa wavuvi wenyewe kusudi washiriki kikamilifu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalo nashauri kwa kuwa ni wa mwanzo nilinde kidogo; kanuni hizi zisiwe uzi wa buibui. Nadhani unaujua; spider yule. Kanuni hizi zilikuwa zinamnasa yule mdogo tu, kama vile uzi wa buibui, akipita kurumbiza, inzi, kipepeo, wanakamatwa na ule uzi; lakini akipita njiwa tu, anaondoka nao uzi wote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakusudia kusema kwamba kanuni hizi zinapowekwa na idara zetu ni vyema ziwe zinakamata wale wakubwa na wadogo. Siyo wadogo tu ambao wanakamatwa hatimaye nyavu zao kuchomwa moto, tukasababisha watu kukataliwa majumbani kwao, tukaongeza idadi ya wajane na vijana wanaotelekezwa.
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Hamad.
MHE. HAMAD HASSAN CHANDE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru na naunga mkono hoja. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Hesabu za Serikali za Mitaa zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Awali ya yote nami nichukue fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu Rahim ambaye ametuwezesha kukutana katika Bunge hili na kujadili taarifa hizi tatu za Kamati zetu na bado anatupa thamani ya ubinadamu. Thamani ya ubinadamu ni uhai tu, ukiondoka uhai, basi tumekosa thamani ya ubinadamu na ndiyo maana tunaondolewa katika makazi ya watu na kupelekwa katika makazi maalum. Jambo la pili, naomba nimshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu Samia Suluhu Hassan, kwa namna anavyo pambana na kupigania kwa kujitoa kabisa kwa maslahi ya Taifa na wananchi wake. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naomba pia nikushukuru wewe kwa kunipa fursa hii na mimi kutoa mchango wangu katika mjadala huu, Mungu akubariki sana. Naomba niwashukuru Wenyeviti wa Kamati hizi tatu lakini na Wenyeviti wa Kamati zote, niwashukuru na niwapongeze sana Wabunge wenzangu ambao mmechangia na kwa kweli mchango unalenga kujenga Taifa letu. Michango yenu ni mizuri sana na kila mmoja ambaye amesimama hapa nilikuwa namuona anaongea, anatoa hoja kwa hisia kali sana, kwa uchungu wa nchi yake, nawashukuru na ninawapongeza sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naomba moja kwa moja nijielekeze katika hoja ambazo zimeletwa na Waheshimiwa Wabunge. Nikianza na hoja ya mwenendo wa utoaji fedha kwenda LGS siyo mzuri, ametoa mfano Mheshimiwa Mbunge, Halmashauri ya Mwanga.
Mheshimiwa Spika, mwaka 2021/2022 bajeti yao ilikuwa ni bilioni 2.31 kwa ajili ya kujenga miradi ya maendeleo ya Halmashauri hiyo ya Mwanga. Serikali ilitoa shilingi bilioni 5.07 sawa na asilimia 219 kupeleka ndani ya Halmashauri hiyo. Mwaka 2022/2023 bajeti yao ilikuwa Bilioni 5.55 hadi kufikia Oktoba tayari Serikali imeshatoa Bilioni 1.85 sawa na asilimia 33.74. Ofisi ya Msajili wa Hazina ipo katika mchakato wa kuboresha sheria ili kuonesha baadhi ya vipengele vyenye upungufu hususan utaratibu wa kutoa adhabu kwa baadhi ya viongozi wa Taasisi za Umma ambao wanakiuka taratibu na sheria.
Mheshimiwa Spika, hoja nyingine ni ya GPSA. Kwanza naomba nikiri kwamba GPSA imechelewa au imechelewesha kutoa huduma hiyo ya magari. Kwa kweli, suala hili limechangiwa na sababu mbalimbali ikiwemo UVIKO–19 pia vita vya Ukraine, hii imechangia sana ucheleweshaji wa ununuzi wa magari hayo. Serikali imelipokea hili nikuhakikishie na nilihakikishie Bunge lako Tukufu kwamba tutalichukulia hatua haraka iwezekanavyo.
Mheshimiwa Spika, ipo hoja ambayo inasema Wizara ya Fedha na Mipango iboreshe mazingira ya Internal Auditors katika Serikali za Mitaa. Wizara ya Fedha na Mipango, tayari imepitia muundo wa Idara ya Internal Auditors na Mamlaka za Serikali za Mitaa…
MHE. JERRY W. SILAA: Mheshimiwa Spika taarifa!
SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Jerry William Silaa.
T A A R I F A
MHE. JERRY W. SILAA: Mheshimiwa Spika, nimemsikiliza mchangiaji kwa makini na nimechelea kidogo. Nimemsikia akisema ziko hoja zimetolewa na Wabunge na anataka kutoa majibu, lakini hoja iliyoko mezani ni hoja ya Kamati za Bunge na Wabunge wote waliochangia wamechangia hoja ile na yeye kama mchangiaji ni vyema akachangia hoja ili tuweze kuihitimisha hoja. (Makofi)
SPIKA: Nafikiri kwa sababu hapo mwanzo alikuwa anaelezea utangulizi sasa anaenda kwenye hoja. Kwa hiyo, akishaanza hizo hoja ndiyo tutajua anazungumzia hoja za Kamati, kwa sababu pia Wabunge mmechangia humu ndani. Kwa hiyo, yeye yale yanayohusu Wizara yake ni muhimu ayatolee ufafanuzi. Kwa hiyo, mpaka tuanze kumsikia ndiyo tutajua kama ametoka nje ya hizi Kamati tatu na taarifa zake na je hilo jambo ambalo analolisema lilichangiwa humu ndani au hapana. Mheshimiwa Naibu Waziri karibu uendelee na mchango wako. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa ruhusa hii. Naomba nitoe ufafanuzi kwenye hoja iliyotolewa na Bunge kuhusu mtaji wa Benki ya Kilimo ya Tanzania. Kwanza naomba nikiri kwamba ni kweli Serikali iliahidi kutoa mtaji wa kupeleka katika Benki ya Kilimo ya Tanzania lakini mpaka sasa imetoa Bilioni 60 kutokana na uchache au uhafifu wa bajeti tuliyokuwa nayo. Serikali ipo katika juhudi mbalimbali kuhakikisha kwamba imeongeza mtaji katika benki hiyo kwa maendeleo ya benki hiyo lakini wananchi kwa ujumla.
Mheshimiwa Spika, juhudi ambazo Serikali imechukua, kwanza Serikali imechukua mkopo nafuu wa Dola za Kimarekani Milioni 92.55 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika na kuikopesha TADB. Pili, Serikali imeamua kuifutia Benki ya Kilimo mkopo wa Dola za Marekeni 92.55, takribani Bilioni 216 na kugeuza kuwa mtaji wake ndani ya benki hiyo. Tatu, Serikali imechukua mkopo nafuu wa Euro Milioni 80 takribani Shilingi 185 kutoka Benki ya Maendeleo ya Ufaransa na kuikopesha benki hiyo. Hatua nyingine ambayo imechukuliwa na Serikali, ni Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu iliipatia Benki ya Maendeleo pesa takribani Dola za Kimarekani Milioni 25 kwa ajili ya dhamana kwa wakulima wadogo kutoka IFAD. Aidha, Serikali inaendelea kuangalia vyanzo vingine vya fedha ili kuipatia benki hiyo kwa maendeleo ya benki hiyo lakini na wananchi kwa ujumla.
Mheshimiwa Spika, hoja nyingine ambayo ilizungumzwa na baadhi ya Wabunge ni kuhusu makinikia. Kwa mujibu wa taarifa ya CAG ya mwaka 2021 ukurasa wa 63, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alibainisha kuwa baadhi ya mashauri ya kodi hususan yanayohusiana na sakata la makinikia yaliondolewa katika Mahakama za Rufaa za Kodi ili kushughulikiwa kwa utaratibu wa majadiliano kati ya Serikali na Kampuni za Madini. Katika majadiliano hayo Serikali ilijenga hoja na kufanikiwa kupata mafanikio haya yafuatayo: -
(i) Kulipwa Dola za Marekani Milioni 300, takribani Shilingi za Kitanzania Bilioni 700.
(ii) Kampuni ya Barrick kukubali kufuta kesi ya madai ya fidia kwa Serikali Dola za Marekani Bilioni 2.7.
(iii) Pia, kupewa umiliki wa asilimia 16 kwenye migodi ya kampuni hiyo ambapo imeunda kampuni mpya inayojulikana kwa jila la Twiga Mineral Cooperation. Barrick wao wana asilimia 84 na Serikali ina asilimia 16 katika hisa iyo.
(iv) Serikali imepokea jumla ya gawio la Dola za Marekani Milioni 36 na kupokea gawio kutokana na marekebisho ya mkopo kwa wanahisa. Dola za Marekani Milioni 16 kwa kipindi cha 2020/2021 na Barrick imekubali kutenga kiasi cha Dola za Marekani Sita kwa kila wakia kwa dhahabu zote ambayo itauzwa kwa ajili ya shughuli za kijamii.
Mheshimiwa Spika, kwa msingi huo, sakata la madai ya kodi ya Shilingi Trilioni 360 lilihitimishwa kwa Serikali kuridhia makubaliano haya kama ilivoainishwa katika maelezo ambayo ameyatowa Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango katika Bunge lililopita.
Mheshimiwa Spika, hoja nyingine ilikuwa ni malimbikizo ya madeni hasa TANROADS. Serikali imechukua juhudi kubwa sana, kwa sababu madeni haya Serikali ya Awamu ya Sita imeyarithi, lakini imechukuwa juhudi kubwa sana katika kulipa madeni hayo yaliyokuwepo na tunaendelea. Nilihakikishie Bunge lako Tukufu kwamba tutaendelea kulipa na miradi yote ambayo imeandaliwa na Serikali ya kimkakati basi itatekelezwa na tutalipa certificates hizo zikishaletwa kwa wakati kabisa.
Mheshimiwa Spika, ilikuwepo hoja ambayo imezungumzwa kuhusu utaratibu wa kufuta madeni chechefu katika benki zetu za TIB na TCB. Serikali imeshaanza kuchukua hatua za kuondoa madeni chechefu katika benki za TIB na TCB ambapo taratibu zinaendelea kuhakikisha madeni hayo yanaondolewa kwenye vitabu vya benki.
Mheshimiwa Spika, ipo hoja ambayo imezungumzwa kuhusu kukosekana kwa bodi kunasababisha mashirika kukosa umakini wa kufanya kazi. Serikali imeendelea kuweka juhudi katika kuhakikisha Taasisi na Mashirika ya Umma yanakuwa na Bodi za Wakurugenzi hai. Kwa sasa Serikali imeshafanya uteuzi wa Bodi za Wakurugenzi zipatazo 23 kati ya Bodi 31 ambazo zimesalia Bodi Nane na hizo Serikali inachukuliwa hatua katika kipindi kifupi kabisa Serikali itakuwa imefanya uteuzi wa Bodi hizo.
SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri hebu rejea hapo kwenye takwimu za Bodi.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuweka juhudi katika kuhakikisha Taasisi na Mashirika ya Umma yanakuwa na na Bodi za Wakurugenzi hai, kwa sasa Serikali imeshafanya uteuzi wa Bodi za Wakurugenzi zipatazo 23 kati ya Bodi 31 ambazo zilikuwa hazina Bodi. Serikali inakamilisha utaratibu wa kuteua Bodi za Taasisi Nane zilizosalia…
MHE. TABASAM H. MWAGAO: Mheshimiwa Spika, taarifa.
SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Tabasam.
T A A R I F A
MHE. TABASAM H. MWAGAO: Mheshimiwa Spika, nataka kumpa taarifa Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba Bodi anazosema Serikali iko katika mpango wa kuteua Wajumbe wake kwa taarifa ya CAG, Bodi zingine zipo toka mwaka 2015, Serikali bado tu inaendeleaa na utaratibu wa Wakurugenzi wameshakuwa wamiliki wa hizo kampuni. Ahsante.(Makofi)
SPIKA: Mheshimiwa Hamadi Chande unapokea taarifa hiyo. (Kicheko)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, nina ukakasi kidogo wa kupokea hiyo taarifa, lakini mimi niseme tu kwamba takwimu ambazo tunazo ni hizi 31 na 23 tumeshafanya uteuzi wa bodi, zilizosalia ni nane. Nadhani tuna asilimia zaidi ya 70, kwa hiyo awe na subira tu Mheshimiwa Mbunge ataona matokeo hivi karibuni, bodi zilizobakia tunateua. (Makofi)
SPIKA: Sasa Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa sababu kwenye taarifa ya Kamati walitaja Bodi zaidi na ni sehemu ya maazimio ya Kamati. Mwenyekiti wa Kamati ambayo inazungumzia hizi Bodi ili tutakapofika kwenye maazimio tusianze tena kurejea nyuma. Mwenyekiti wa Kamati zile takwimu ulizonazo na hizi Bodi anazozitaja Mheshimiwa Naibu Waziri ni tofauti ni hizi au hili ni jambo jipya.
MHE. JERRY W. SILAA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA: Mheshimiwa Spika, kuna tofauti kubwa sana. Taarifa tulizonazo kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina mpaka kufikia tarehe 31 Oktoba, jumla ya mashirika 23 hayana Bodi za Wakurugenzi. Kuna mashirika 12 ambayo tayari Mheshimiwa Rais ameshateua Wenyeviti wa Bodi lakini bado Wajumbe hawajateuliwa. Kwa hiyo, jumla ni mashirika 35 mpaka kufikia tarehe 31 Oktoba wakati tunaandaa taarifa hii mashirika hayo hayana Bodi.
SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, hizi takwimu anazosema Mwenyekiti zipo sawasawa? Nataka tu kwenye takwimu ili wakati wa Azimio tusije tukaazimia na yale ambayo Serikali imeshayafanyia kazi.
Mheshimiwa Naibu Waziri, Mheshimiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma anasema Bodi 23 kufikia mwishoni mwa Oktoba zilikuwa hazina Wajumbe wala hazina Wenyeviti, Bodi 12 zina Wenyeviti ambao Rais ameshawateua lakini Wajumbe wale wanaoteuliwa na vyombo vingine ama na Mawaziri bado. Hizi takwimu zipo sawasawa?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa swali hilo. Suala hili la Bodi ambazo tuko na uhakika nazo ni Bodi 23 ambazo Wajumbe wake wameshateuliwa na zimeshakamilka. Hizi nyingine labda zipo kwa upande wa Taasisi nyingine ama Wizara nyingine lakini mimi nazungumzia ambazo ziko ndani ya Wizara ya Fedha.
SPIKA: Hivi Treasury Register anaripoti wapi? Mheshimiwa Mwenyekiti Treasury Register anaripoti wapi? (Makofi)
SPIKA: Mwenyekiti, Treasurer Registrar anaripoti wapi?
MHE. JERRY W. SILAA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA: Mheshimiwa Spika, Msajili wa Hazina anaripoti Wizara ya Fedha na Mipango. (Makofi)
SPIKA: sawa. Mheshimiwa Naibu Waziri, mimi nimekuelewa hoja yako. Ni kwamba hizi taasisi zinaweza kuwepo lakini kwa sasa hivi hapo hauna takwimu nazo, kwa hiyo sisi tutaendelea na azimio letu kuhusu hizi taasisi. Mheshimiwa Waziri wa Nchi anataka kutoa ufafanuzi.
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, kwa heshima kubwa sana ya kikao chako hiki cha Bunge, kwa spirit ambayo ameingia nayo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, na hasa baada ya kukuta tatizo hili la teuzi za bodi kwamba ni tatizo ambalo limekuwa likijitokeza sana Serikalini; Mheshimiwa Rais alishatoa maelekezo na Chief Secretary na taasisi zinazohusika walishapewa kazi ya kusimamia.
Mheshimiwa Spika, itakuwa ni kumtendea haki Mheshimiwa Rais na kazi nzuri ambayo imekwishakufanywa kwani katika kipindi hiki…
MHE. TABASAM H. MWAGAO: Taarifa.
SPIKA: Mheshimiwa Tabasam ngoja nijaribu kuelewa hoja kwanza kabla hujatoa taarifa yako, maana hajaanza bado kutoa hoja. Mheshimiwa Waziri wa Nchi.
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Nadhani itakuwa ni vizuri kama katika kipindi hiki ambacho tunaelekea kuhitimisha hoja hii tukapata fursa ya kupata taarifa ambazo ziko kamili. Ninaheshimu taarifa za Mwenyekiti ambazo zimeishia mwezi Oktoba, lakini tangu mwezi Oktoba, mpaka sasa tunaweza kuwa na taarifa ambazo ni current.
Mheshimiwa Spika, kwa heshima kubwa sana, kama utaridhia, tuweze kupata taarifa hizo ambazo tunaweza kuzipata sasa hivi kutoka kwa Treasurer Registrar ili azimio letu tukishalipitisha hapa liwe ni azimio ambalo limebeba dhana kamili ya idadi kamili ambayo inatakiwa kuwasilishwa. (Makofi)
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, taarifa.
SPIKA: Sasa, kulikuwa na taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Tabasam, sijajua taarifa nyingine inatoka wapi. Sasa ngoja, kwa sababu mtapata fursa ya kuchangia, Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI nawe ni kuhusu Bodi pengine zilizokuwa chini yako ambazo umezifanyia kazi kati ya huo muda. Sawa, Mheshimiwa Tabasam.
T A A R I F A
MHE. TABASAM H. MWAGAO: Mheshimiwa Spika, leo tupo serious na tumeamka vibaya, na ninaomba kabisa Waheshimiwa Mawaziri waje na nidhamu kabisa kwa siku ya leo, kwa sababu suala la vetting liko chini ya Ofisi ya Rais ambapo Waziri anayekuja kuzungumza maneno haya vetting iko kwake, na yeye ndiye sehemu ya ucheleweshaji wa vitu hivi. Tusubiri tufike mwisho leo. (Makofi)
SPIKA: Mwenyekiti nimekuona. Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI, naona ulisimama.
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, nami nilitaka kutoa tu taarifa; kwamba katika bodi tatu, sijajua taarifa ya Mwenyekiti wa Hesabu za Mashirika ya Umma au Uwekezaji katika Mashirika ya Umma kama na za kwetu zimo. Endapo zimo, kwa Bodi ya DART tayari imeshaundwa, kwa Bodi ya Masoko ya Kariakoo tayari imeshaundwa, na Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa pia nayo tayari tumeshaiunda, kwa hiyo kwa upande wangu wa TAMISEMI bodi zote tatu zipo.
SPIKA: Haya, ahsante sana. Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, naona ulikuwa umesimama.
MHE. JERRY W. SILAA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA: Mheshimiwa Spika, naomba nitoe maelezo madogo kutokana na taarifa zilizotolewa hapa, na kwa kuwa jina la Mheshimiwa Rais limetajwa, naomba ninukuu Hotuba ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, aliyoitoa tarehe 30, Machi 2022, nanukuu; “CAG umeeleza kuwa, mwenendo wa Mashirika ya Umma ambayo umebainisha Mashirika 38 ya Umma yanaendeshwa bila kuwa na Bodi. Hii inashangaza kwa miaka kadhaa mashirika yanaendeshwa hakuna Bodi za Wakurugenzi. Mimi nakumbuka nilipoingia nilipata mtiririko wa maombi ya bodi na yote nimeshayatoa. Sasa kama Waziri ana mashirika, bado anaendesha mashirika yasiyo na bodi, siwezi kumuelewa na sijui tatizo ni nini.” (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nimesema niyaseme haya kwa sababu kuna mashirika ama kuna Wizara wakati mwingine zinatupa mzigo wa uteuzi kwa Mheshimiwa Rais, lakini Mheshimiwa Rais alishasema hadharani kwamba yeye anateua bodi kwa wakati, la kwanza.
Mheshimiwa Spika, lakini la pili, Ofisi ya Msajili wa Hazina inao mfumo ambao unatoa taarifa kwa Wizara miezi tisa kabla bodi haijamaliza muda wake ili mchakato na urasimu wote wa vetting ukamilike kwa wakati. Kwa hiyo tunaporipoti hapa, tunaripoti mambo ambayo tunauhakika nayo na yamethibitshwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na yako sahihi, na kwa nyongeza, tarehe 30, Oktoba ni siku nne kuanzia sasa ndiyo taarifa yetu imetoka.
SPIKA: Haya, ahsante sana. Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, malizia mchango wako.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia tena fursa hii. Nimalizie mchango wangu kwa hoja iliyokuwa inazungumzia Sheria ya Manunuzi kwamba ina upungufu.
Mheshimiwa Spika, hili nikiri kwamba sheria hii ina upungufu; na kama alivyoeleza Mwanasheria Mkuu wa Serikali hatua ambayo imefikiwa kwa sasa ya kufanya marekebisho ya sheria hiyo iko katika ngazi ya maamuzi na karibuni hivi itaingia Bungeni kwa ajili ya kupata mapendekezo na maoni kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge. kwa hiyo niwatoe wasiwasi Waheshimiwa Wabunge kwamba suala la Sheria ya Manunuzi na sura 410 lipo katika hatua ya maamuzi kwa sasa.
Mheshimiwa Spika, wapo wachangiaji wengi ambao walichangia kuhusu manunuzi. Kwamba kuna upotevu mkubwa sana wa fedha katika manunuzi. Naweza kusema kwamba zaidi ya asilimia 70 ya fedha za bajeti za Serikali zipo katika manunuzi. Kwa hiyo hii ni sehemu moja nyeti na muhimu sana na Serikali imeichukulia hatua sehemu hii kwa kiasi kikubwa sana. Kutokana na mapungufu yaliyokuwepo pale, Serikali imeamua kuanzisha mfumo mpya wa manunuzi ambao unaitwa NEST ili kuepuka changamoto ambazo zinajitokeza wakati wa kufanya manunuzi.
Mheshimiwa Spika, na hii yote ni kwa sababu ya mfumo tulio nao si rafiki kwa matumizi ya watumiaji na pia utoaji wa taarifa sahihi. Kwa hiyo tumeamua Serikali kuanzisha mfumo huu, na faida ambazo zinaweza kupatikana kutokana na mfumo wa sasa wa NEST ni nyingi sana. Kwa mfano, itaongeza uwazi (transparency) kwa sababu mfumo uliokuwepo usiri ulikuwa ni mkubwa sana ambao unaweza kupelekea mianya ya rushwa. Mfumo huu utakuwa uko wazi na watumiaji wote watakuwa wana-access.
Mheshimiwa Spika, jambo lingine, utaongeza uwajibikaji; kutakuwa na uwajibikaji mkubwa sana katika mfumo huu. Faida nyingine ambayo inaweza kupatikana katika mfumo huu ni kuweka ukomo wa bei za bidhaa, yaani kuweka bei kikomo au bei elekezi, kwamba bidhaa hii bei yake ni hii hapa ili kusudi kuepuka manunuzi holela. Maana inawezekana bidhaa moja hii mfano ya kalamu kwa idara tofauti zikawa na bei tofauti kutokana na mfumo ambao ulikuwepo, lakini kwa sasa mfumo huu unaenda kujenga na kutuweka wazi. Na huu ndiyo mwarobaini pekee wa ku-save fedha za Watanzania.
MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Spika, taarifa.
SPIKA: Kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Deus Sangu, Mheshimiwa Naibu Waziri.
T A A R I F A
MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana; naomba kumpa taarifa mzungumzaji. Mfumo huu wa TANEPS ambao upo sasa ni mfumo ambao umewekwa hivi karibuni, mwaka 2020 ndio ulikuwa mandatory kwa taasisi zote za umma na umegharimu mabilioni ya fedha za Watanzania. Leo hii ndani ya miaka miwili Serikali yenyewe iliyoweka huo mfumo inatuambia kwamba ni redundant na hauna maana, na wanatuambia wanakuja na mfumo wa NEST ambao uta- address matatizo haya. Hivi kweli huu sio ufisadi mwingine? (Makofi)
SPIKA: Mheshimiwa Sangu kwa kawaida taarifa huwa haina maswali lakini, Mheshimiwa Naibu Waziri wa fedha na mipango unaipokea taarifa hiyo?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, hii taarifa siipokei kwa sababu unaweza kuishi na mke hata kwa siku tatu tu; bila kujali gharama ya mahari uliyotoa; ukaona kwa mwenendo huu sasa huyu hanifai tena. Kwa hiyo unaweza kuacha. Hata kama umetumia siku tatu, achilia miaka miwili. Kwa hiyo taarifa hii mimi siipokei.
Mheshimiwa Spika, mfumo huu tunaotarajia kuutumia endapo utatumika, kwa utafiti mdogo ambao tumeufanya, utakoa zaidi ya shilingi trilioni mbili. Pia mfumo huu utawezesha Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali angalau kuwa na matokeo mazuri badala ya kuwa na matokeo hasi siku zote, kwa sababu tunakwenda kujadili na kuona wapi kuna mwanya au kuna viashiria vya upotevu wa fedha kabla mradi haujaanza, tofauti na mfumo ambao ulikuwepo.
Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii kutoa wito kwa taasisi zote za Serikali kujiunga na mfumo huu ambao utasaidia matumizi halali. Ahsate sana. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti ahsante sana kwa kunipa nafasi hii nami kuwa sehemu ya wachangiaji katika hoja iliyoko mbele yetu. Awali ya yote, ningependa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi hii ya uzima wa afya ambayo ametujalia, tumekaa hapa, hatimaye tunaenda kufikia ukingoni kwa hoja hii iliyopo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, naomba sana nimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumpongeza sana. Mheshimiwa Rais, mbeba maono wa Taifa hili, mwenye macho haambiwi tazama. Mbeba maono maana yake siyo tu kwamba anahamisha sera kutoka kwenye makaratasi na kuzipeleka kwenye vitendo, bali hata salamu mama anaipeleka kwenye vitendo ana uwezo mkubwa sana wa kutafsiri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuliposema Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Kazi Iendelee, hiyo ni salamu. Tumeona leo dhahiri kabisa salamu hii imetafsiriwa kwa vitendo, hakuna Wilaya, hakuna Halmashauri ambayo hakuna maendeleo au mradi wa maendeleo ambao unafanyika kule. Miradi yote mikubwa tuliyonayo inatekelezwa kama SGR, umeme mpaka vijijini, Bwawa la Mwalimu Nyerere, mama ameenda kulitekeleza kwa vitendo. Waheshimiwa Wabunge wote ni mashahidi na hii haikuja burebure. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais yeye ni neema na ni baraka kutoka kwa Mungu. Kwani ukiniruhusu naweza toa tafsiri kwa ufupi tu. Jina la Mama anaitwa Samia Suluhu Hassan, utanisamehe naenda kwenye kiarabu kidogo, watu wa nahau wanasema “inna samian suluhuun hassanaah” kwa hakika Mama huyu ni msikivu wa kusikiliza changamoto za wananchi wake na kuzipatia ufumbuzi mzuri hiyo ndiyo tafsiri yake. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wilaya zote leo lipo vumbi linapeperuka kwa sababu ya ujenzi wa barabara, ujenzi wa vituo vya afya, zahanati, lakini ujenzi wa madarasa, kila kitu. Hii kwa sababu ya tafsiri la jina lake haikuwa bure bure, hii ni neema. Kwa hakika Mama ni msikivu ambaye anasikiliza changamoto za wananchi wake na kuzipatia ufumbuzi ulio mwema. Siku ukiwa na muda mzuri tunaweza kutia irabu kwamba inna ni nini, samian ni nini? na suluhu ni nini? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais ni mbeba maono kweli kweli. Nimpongeze sana na kumshukuru sana Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini Mheshimiwa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Waziri Mkuu. Viongozi wetu hawa wanasimama imara kutuelekeza na kusimama imara katika kujenga maendeleo ya Taifa letu hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaambie Waheshimiwa Wabunge wenzangu, Wahenga hunena: “kijua ni hiki tusipouanika tutaula mbichi.”
Mheshimiwa Mwenyekiti na Waheshimiwa Wabunge wenzangu, nikisema hivyo mnanifahamu? Huu ndiyo wakati, huu wakati wa leo, sasa ndiyo wa kujenga maendeleo yetu, ndiyo wa kuchagiza maendeleo ya nchi hii. Ni wakati huu na siyo wakati mwingine, ndiyo maana unasema kijua ni hiki usipouanika utaula mbichi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimshukuru sana na nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri wangu, Dkt. Mwigulu Nchemba, mentor wangu, bosi wangu, kwa kiasi anavyonikuza kisiasa lakini na kikazi. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Mungu akubariki sana. Wewe ni mtu mwema sana, ni mtu wa kipekee, nakushukuru sana na nakuhaidi kwamba nitaendelea kushirikiana na wewe katika utendaji wa kazi pamoja na wataalam wetu wote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue fursa hii pia kuwashukuru na kuwapongeza sana Wabunge, Waheshimiwa Wabunge nawashukuru sana kwa namna wanavyotushauri, kutuelekeza lakini hata kutoa mapendekezo yao, hongera sana kwa Waheshimiwa Wabunge. Kwa nini nawapongeza Waheshimiwa Wabunge? Waheshimiwa Wabunge wanaishi katika maneno ya hekima yaliyosemwa kwamba aliyekufanyia wema, basi mlipe mithili ya wema aliyokutendea, kama huwezi kufanya vile basi mwombee dua, mwombee kwa Mungu. Waheshimiwa Wabunge wanaishi katika hekima hizi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, haya maneno yalisemwa kwa Kiarabu; “Tatamanswana maarufa alaykum au manswanaa alaykum maarufa fakatiuhu,” maana yake aliyekufanyieni wema mlipeni “fainlam tajiduu” mtakapokuwa hamuwezi basi “swallu alaiy, mwombeeni dua. Waheshimiwa Wabunge nyinyi mnaishi katika hekima hii, kila Mbunge aliyenyanyuka alimshukuru na kumpongeza na kumwombea dua Mama yetu, kila Mheshimiwa Mbunge. Wabunge wote mnaishi katika hili, Mungu awabariki sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaambie Waheshimiwa Wabunge, nasikia, huko mitandaoni, nasikia, toba sikio. Wako wanaosema kwamba wanabeza Bunge, wanabeza Bunge hili, wako wanaobeza Bunge hili, lakini niwaambie Wabunge taingia katika historia maalum, ya wakati maalum, ya siku maalum na kwa tukio maalum. Majina yenu yataandikwa kwa wino mahususi, wino wa dhahabu, kwa sababu wamechapa kazi sana, nani ambaye haoni leo Waheshimiwa Wabunge wanavyopambana? Ni Wabunge wangapi leo siku zote maana yake ukiamka tu asubuhi simu wanadai maendeleo ya Majimbo yao. Waheshimiwa Wabunge hongereni sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niwapongeze wataalam wetu wakiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Natu Mwamba na Manaibu Katibu wakuu na Wataalam wote nawapongeze sana, kwani usiku na mchana hawa wanafanya kazi. Wanafanya kazi mpaka usiku wa manane na asubuhi mapema kabisa wameshafika ofisini, nisiwe mchoyo wa fadhila, niwashukuru sana wataalam wetu hawa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya salamu hizo, naomba tu niseme kwamba ushauri wote ambao umetolewa na Waheshimiwa Wabunge, mapendekezo na maoni tumeyapokea na tunawahakikishia tunaenda kuyafanyia kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, miongoni wa dondoo ndogondogo ndiyo hoja ambazo zimetajwa na Waheshimiwa Wabunge niwapongeze sana Waheshimiwa Wabunge. Walipokuwa wanachangia wengi wametoa hoja kwa njia ya ushauri, wametumia hekima kubwa sana, hongera sana Waheshimiwa Wabunge. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja moja ambayo ilizungumzwa Serikali ihakikishe kwamba inafuatilia au inatafuta mikopo ya gharama nafuu. Serikali imekuwa ikifanya juhudi za makusudi kuhakikisha kwamba mikopo yote ambayo inaingia Serikali ni ile yenye masharti nafuu na tunawahakikishia kabisa mikopo hii inaenda kutumiwa katika zile sehemu ambazo ni vipaumbele vya Taifa hili ya mwaka 2021/2022 hadi 2025/2026. Vipaumbele vya Taifa hili ambavyo tumeviweka ndiyo mkopo huu unaenda kutumika, hautotumika tofauti na vipaumbele ambavyo tungeweka ili kusudi kupunguza gharama ambazo siyo za lazima.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ipo hoja imesemwa kwamba Serikali iboreshe mikakati na ikusanye mapato ya ndani ili kuhakikisha sehemu kubwa ya bajeti inagharamiwa na mapato ya ndani. Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, kuongeza wigo wa mapato kwa kusajili biashara na walipa kodi wapya. Niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge kwamba tutaandaa mikakati maalum, tutaendelea kuitumia mikakati ambayo imeandaliwa na Serikali kuhakikisha kwamba tunapata ongezeko kubwa sana la mapato.
Mheshimiwa Mwenyekiti, matarajio yetu ambayo tumeweka, ni kupata mapato ya ndani kwa asilimia 70.7 ikilinganishwa na bajeti iliyopita au ambayo tuko nayo leo ya kupata asilimia 67.5. Niwahakikishie kwamba tutapambana, tutajitahidi kutumia maarifa yetu yote, tuone kwamba ongezeko la mapato limepatikana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaombe Waheshimiwa Wabunge wenzangu sisi wote tuwe mabalozi wa kuwa na utamaduni mwema. Tuwe na utamaduni wa kudai risiti na kutoa risiti kwa wale wafanyabiashara. Tufanye kama utamaduni wetu, kama vile ukiamka asubuhi unaenda kukosha uso, kupiga mswaki na kukoga, basi tufanye hivyo, kila unapokwenda dukani kutafuta bidhaa yoyote, basi dai risiti na wale wanaofanya biashara watoe risiti jambo hili litatusaidia sana. Hakuna mtu anayetoka mbali kuja kujenga maendeleo yetu kama siyo sisi wenyewe. Kilio kina mwenyewe, wewe mwenyewe ndiyo unajua uchungu wa nchi yako. Kwa hiyo niwaombe sana Waheshimiwa Wabunge tuwe mabalozi wa kujitahidi kudai risiti na pia nakutoa risiti kwa wale wafanyabiashara. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wapo Waheshimiwa Wabunge wametoa hoja ya wakandarasi kwamba kuna madeni mengi sana ya wakandarasi. Tulikuwa tunateta hapa na Mheshimiwa Waziri. Niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge kwamba wakandarasi hao ambao certificate zao tayari zimeshawiva, mapema mwaka ujao wataenda kulipwa bila wasiwasi wowote. Serikali yetu iko tayari kuwalipa wakandarasi hao hasa hasa wale wakandarasi wadogo ambao tukiwaachia muda mrefu hawajalipwa wanaweza kufilisiwa kama walivyosema Wabunge. Hilo halitotokea katika Taifa hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, nimalizie kwa kusema kwamba, Waheshimiwa Wabunge baadhi yao wapo wamezungumzia hoja ya kujengewa ofisi za TRA au Forodha mipakani. Niwahakikishie, kwa mfano kama Loliondo, Iramba kwa bosi wangu, Mkalama, Itilima na kwingine ofisi hizi zitaenda kujengwa hivi karibuni, mwaka wa fedha unaofuata. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme naunga mkono hoja. Wale waliosema mama apewe maua yake mimi naongezea siyo tu maua, mama apewe maua yake na matunda yake yale yaliyo mema. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa nafasi hii ya kutoa mawili, matatu kwa zile hoja ambazo zimetolewa na Waheshimiwa Wabunge. Pia niwashukuru sana wale wote waliochangia katika mada hizi mbili, suala la Muungano na Mazingira kwenye Ofisi yetu. Nawashukuru sana kwa michango yenu mizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa muda siyo rafiki, naomba kwa ruhusa yako niende tu moja kwa moja kwa baadhi ya hoja ambazo zimetolewa na Wabunge, hasa kuhusu Muungano.
Mheshimiwa Spika, hoja ya kwanza ambayo imetolewa na Mheshimiwa Khadija Hassan Aboud; Muungano umetimiza miaka 57. Pongezi zimepokelewa. Aidha, Serikali ya SMZ na Serikali ya SMT zinaendelea na jitihada za kutatua changamoto kumi za Muungano zilizobakia ambazo 15 tayari zimeshapatiwa ufumbuzi.
Mheshimiwa Spika, hoja yake ya pili ni ushauri; ametoa ushauri kuhusu kuimarisha na kudumisha Muungano. Ushauri umepokelewa. Aidha, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Awamu ya Nane ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi, zimeweka masuala hayo ya Muungano kwa nia moja vipaumbele vyake hivyo ni Serikali zote mbili kushirikiana katika kuzipatia ufumbuzi hizi kumi zilizobakia. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, hoja ambayo ameitoa Mheshimiwa Bakar Hamad Bakar kwamba kuenzi Muungano ni pamoja na kuwezesha viongozi wa Muungano huu, mfano Dkt. Omar Ali Juma; maoni yamepokelewa. Aidha, Serikali italifanyia kazi suala hili.
Mheshimiwa Spika, hoja nyingine ambayo ameitoa Mheshimiwa Kassim Hassan Haji ni kuhusu Muungano wa Taasisi zetu za Zanzibar na zile za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama vile TBS na ZBS kule Zanzibar. Suala hili ushauri huu tumeuchukua kwa mikono miwili na hatua zimeanza huko nyuma kwasababu mwenyewe nilikuwepo ZBS, tumeshakaa vikao tofauti, mbalimbali kujadili suala hili hapa. Kwa hiyo, ushauri umechukuliwa na tutaufanyia kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, pia ipo hoja ya Mheshimiwa Mwanakhamis Kassim Said ambaye hoja yake alikuwa anatoa pongezi, pongezi hizo zimechukuliwa na zimezingatiwa na tutazifanyia kazi kwa kadri inavyowezekana.
Hoja nyingine ya Mheshimiwa Mwanakhamis, haikuwa zaidi nayo ni pongezi tu kwa Jamhuri ya Muungano na kudumisha Muungano wetu wa Tanzania.
Mheshimiwa Asia Abdukarimu Halamga, Mbunge Viti Maalum, pongezi zimepokelewa na tutazifanyia kazi. Suala linaloshughulikiwa na kamati ya pamoja ya SMZ na ya SMT zinashughulikiwa masuala ya muungano baada ya kukamilika Serikali itatoa taarifa kuhusu jambo hilo.
Mheshimiwa Spika, ipo hoja ya Mheshimiwa Omar Ali Omar Hafidh, yeye amesema tu Elimu ya Juu, sana sana alizungumzia suala la mitaala kwamba hakuna mlingano mzuri kati ya mtaaala unaotumika Zanzibar na ambao unatumika Tanzania Bara. Suala hili tumelichukua na tutalifanyia kazi, tutafuatilia kwa kadri inavyowezekana ili tuweze kulinganisha mitaala yetu hiyo, ili kusudi tija na mafanikio ya wanafunzi wetu yawe yanalingana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, baada ya summary hiyo ambayo imetolewa na Waheshimiwa Wabunge katika Bunge lako hili Tukufu naomba tu niseme zipo changamoto kumi na tano ambazo zimeshapatiwa ufumbuzi na zimebakia changamoto kumi nazo kwa hakika karibuni kadri vikao vitakavyokaliwa na Serikali ufumbuzi wake utapatikana moja baada ya nyingine.
Mheshimiwa Spika, naomba nizungumze mambo mawili kuhusu muungano. Katika kipindi ambacho muungano unahitajiwa ama unahitajika zaidi Tanzania ni kipindi hiki. Hii ni kwasababu wapo maadui wengi wenye macho mabaya na makali wanaoutazama vibaya Muungano wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hiyo, kipindi ambacho kinahitajika ni hiki, kwasababu hata wahenga wanasema Umoja ni Nguvu na Utengano ni Dhaifu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, na siku zote mbwa mwitu hula nyama ya kondoo aliyejitenga. Lakini jambo la pili, tuachane na wale watu ambao wana mawazo mgando ama fikra mgando kuhusu suala la muungano. Kwani hata ingekuwa ile tarehe 26 Aprili,1964 wangeulizwa kuhusu Muungano basi wangejibu hayo hayo kwamba kwao Muungano usingefaa.
Mheshimiwa Spika, naomba niombe kwa Waheshimiwa Wabunge na Wananchi kwa jumla, mambo mawili tu; jambo la kwanza, kwa kuwa wapo watu wenye ujauzito wa mawazo kuhusu Muungano naomba tuwe madaktari wazuri sana wakuwafanyia tiba, upasuaji, taratibu kabisa ili wajifungue salama, wawe wanajua nini dhana ya muungano. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini jambo la pili, ambalo naomba ni wale watu wenye degree zao, maarifa yao makubwa ambayo maarifa hayo tunatarajia yabakie ndani ya ubongo wao lakini kwa bahati mbaya maarifa hayo wanayahamisha na kuyapeleka kwenye matumbo yao. Ili kusudi kubomoa mwelekeo wa Jamhuri ya Muungano. Naomba watu hawa tuwaelimishe na naamini wataelimika inshallah.
Mheshimiwa Spika, baada ya hayo naomba nitoe shukrani kubwa kwa familia yangu, ambayo tulikesha pamoja katika kuandaa haya. Lakini pili nitoe shukrani kubwa sana kwa wapiga kura wangu wa Jimbo la Kojani kwa kuniwezesha kufika hapa leo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ahsante sana, naunga mkono hoja. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii lakini awali ya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu Rahimu ambaye amepitisha mjadala huu katika hali nzuri na usimamizi wako mzuri kabisa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, niungane na wenzangu kushukuru sana kwa kuchaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Niwapongeze pia watoa hoja wenyeviti wote wawili ambao yaani Mwenyekiti wa bajeti na mwenyekiti wa PAC ambao wamewasilisha ripoti zao hapa au taarifa zao ziko vizuri niwapongeze sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kupunguza mzigo kwa wananchi wake wa Tanzania, dhamira hiyo inaendelea katika kuonekana utekelezaji wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hasa katika suala ambalo hoja imezungumzwa ama maoni yametolewa na kamati ya bajeti kuhusu riba. Naomba niongelee hapo kwamba Serikali inachukua hatua mbalimbali katika kupunguza mzigo kwa wananchi wake hasa wale wakopaji. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuagiza sekta ya bank na taasisi ya fedha kuweka mikakati ya kupunguza gharama za uendeshaji ikiwemo kuhamasisha matumizi ya teknolojia katika kutoa huduma za fedha kwa lengo la kupunguzia mzigo mteja na kuhakikisha viwango vya riba vinashuka kufikia tarakimu moja tu yaani single digit.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kupitia benki kuu inatoa taaluma kwa wateja mbalimbali au kwa wananchi mbalimbali ili kududi wawe na maamuzi sahihi wakati wa kuingia katika mikopo hiyo. Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kutatua changamoto na miongoni mwa hatua hizo mwezi Julai, 2021 hatua kadhaa zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kutoa unafuu wa kisheria katika kiasi cha amana ambacho bank na taasisi ya fedha zinatakiwa kuweka benki.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pili kurekebisha kauli za usajili wakala wa benki kwa kuondoa sharti la kuwa na uzoefu wa miezi 18 katika eneo la biashara, jambo la tatu kupunguza kiwango cha riba kinachotolewa kinachotolewa katika account za wateja watoa huduma za fedha kwa njia za simu za mkononi. Lakini benki imechukua hatua ya kuhakikisha benki kuu imeanzisha mfuko maalum wa shilingi trioni moja kwa riba ya asilimia 3 kwa mwaka. Benki Kuu imepunguza kiwango cha mtaji kinachotakiwa kuweka na benki za biashara kwa ajili ya kuweza kutoa mikopo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhakikisha kuwa uwiano wa gharama za uwendeshaji na mapato ya benki kuzidi asilimia 55 na mikopo chechefu isiyozidi asilimia 5, kushirikiana na umoja wa mabenki katika kusimamia maadili ya watendaji, kushirikiana mabenki pamoja na taasisi ya fedha, kufanya ukaguzi maalumu kwa wastaafu yote haya ni matarajio yetu kwa muendelezo huo zote hizi zitasaidia kuendelea kupungua kwa riba za mikopo nchini. Hivi karibuni tumeshuhudia benki kubwa za kibiashara zikipunguza riba kutoka asilimia 20 hadi asilimia 9 katika sekta ya kilimo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu pendekezo la kuanzisha Ofisi ya kupokea malalamiko ya kodi mapendekezo haya pia tumeyachukua kwa sababu pendekezo la muundo wa Taasisi ya kanuni za uwendeshaji zimeandaliwa tayari na zimekwisha andaliwa na kupelekwa kwa ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala bora kwa evening, tunatarajia hivi karibu kabla ya kumalizika mwaka huu wa fedha itakuwa idhini hiyo tumeshaipa na muundo utaanza kutekelezwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tu nijielekeze katika hoja ya pili ambayo imetokewa na Kamati ya PIC ambayo inazungumzia miradi kutokamilika kwa wakati. Serikali inatekeleza bajeti kama ilivyoidhinishwa na Bunge hadi kufikia mwezi Disemba, 2021 kiasi cha shilingi bilioni 585.1 zimetolea kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo sawa na asilimia 86.2 ya lengo nunu mwaka.
Mheshimiwa Naibu Spika, fedha za maendeleo zilizotolewa zinajumuisha shilingi bilioni 5194.3 na fedha za ndani ni shilingi bilioni 167.1 fedha za nje. Aidha shilingi bilioni 443.7 ni fedha za washirika wa maendeleo zilizopelekwa moja kwa moja ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana na awali ya yote nami niungane na wenzangu katika jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu Rahim, Mwenyezi Mungu ambaye ametujaalia rasilimali ya uhai hadi sasa tunaendelea nayo, kwani ndiyo thamani peke yake ya binadamu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili napenda kumshukuru sana na kumpongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa ambayo naifanya katika nchi yetu hii. Nawapongeza sana Wenyeviti ambao wamewasilisha leo taarifa zao. Kwa kweli wamewasilisha kwa ufanisi na weledi mkubwa sana. Nawapongeza sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, nawapongeza Wajumbe wa Kamati hizo pamoja na Wabunge wenzangu kwa namna wanavyochangia hoja katika kujenga Taifa hili. Ni Wabunge wengi ambao wamechangia katika hoja tofautitofauti ambazo ni hoja nzuri na za msingi kabisa. Miongoni mwa hoja hizo zimegusa kwa njia moja ama nyingine Wizara ya Fedha. So, niseme kwamba hoja zote ambazo zimetolewa, maoni na ushauri ambao umetolewa tumezipokea kama Serikali na tunaenda kuzifanyia kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa uchache kabisa kwa sababu ya muda, naomba nijielekeze tu moja kwa moja kwenye suala zima la miundombinu ya barabara ambayo imetajwa na Wabunge wengi katika Taasisi yetu ya TARURA.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali iliahidi kuongeza bajeti kwa kiasi cha shilingi bilioni 350 ili kutatua changamoto za miundombinu ya barabara katika halmashauri zetu zote nchini. Kwa sasa, Serikali kupitia TARURA ipo kwenye hatua za ununuzi ili miradi hiyo iweze kutekelezwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa miradi ya barabara inatekelezwa kwa kipindi cha miezi sita hadi miezi 18 (mwaka mmoja na nusu). Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, itahakikisha fedha za malipo ya awali (advance payment) inalipwa kwa wakati unaostahiki mara tu baada ya mikataba hiyo kusainiwa. Hivyo, naomba nikuhakikishie na nilihakikishie Bunge lako Tukufu pamoja na Waheshimiwa Wabunge kwamba, fedha hiyo ya miradi hiyo ambayo imetajwa, kiasi cha shilingi bilioni 350 zitatekelezwa kama ilivyopangwa na ilivyoahidiwa na Serikali. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba nirudie kukuhakikishia kwamba, Wabunge waondoe shaka katika hili. Fedha hiyo itatolewa kwa wakati kabisa ili kutekeleza miradi hiyo. Ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Fedha na Mipango
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa hii na mimi kuchangia katika mjadala huu. Awali ya yote naomba kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba mbingu na ardhi ambaye ametuwezesha kubakia hapa leo na kujadili bajeti ya Mapato ya Wizara ya Fedha na Mipango. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini jambo la pili naomba kumshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuniamini kuwepo katika Wizara hii ya Fedha na Mipango. Mheshimiwa Rais anafanya kazi kubwa sana wote sisi hapa ni mashahidi. Uwezo wake mkubwa sana wa kutafsiri sera kutoka kwenye makaratasi na kuja kwenye vitendo. Wote ni mashahidi na mwenye macho haambiwi tazama. Tunampongeza sana Mheshimiwa Rais na tuna muomba Mheshimiwa Rais aendelee kuchapa kazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, haya maneno ambayo baadhi labda yanaweza kutokea tokea na watu kukosoa kosoa basi ndiyo ada ya binadamu kusema. Hata wahenga husema, “Mwenda hidimani ndiye mkosa.” Unapokuwa unafanya kazi vizuri basi lazima kutatokea maelekezo kwa nia safi tu na kukosoa kosoa.
Mheshimiwa Naibu Spika, na mfano wa hili pengine labda inawezekana wengine nimewaacha kwamba mwenda hidimani ndiye mkosa ni pale kwa mfano upande wa michezo anaweza kusema hapa Mheshimiwa Waziri kwamba pale Mayele bora angepiga shuti badala ya kutoa pasi, lakini kwa kuwa amefanya kazi nzuri ndiyo amepata kukosoa lile. Lakini mwingine anaweza kusema Chama alikuwa asitoe pasi badala yake apige. Kwa hiyo ndiyo mwenda hidimani ndiye mkosa. Tuendelee kufanya kazi na ninaamini kabisa mafanikio ya kazi hii itapatikana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini niwapongeze sana na kuwashukuru sana Kamati ya Bajeti, kuanzia Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti, ninawapongeza sana na ninawashukuru sana. Kamati ya Bajeti wanafanya kazi nzuri na kubwa sana ya kiuzalendo. Na kwa ushahidi wa hilo Kamati ya Bajeti inakosa hata muda wa kailula, muda wote wao wapo kazini ni kwa sababu ya uzalendo wao. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nawapongeza sana Waheshimiwa Wabunge wenzangu kwa namna wanavyotupa ushirikiano mkubwa sana. Lakini si kwa umuhimu, naomba nimpongeze sana na nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango, kwa kiasi kikubwa anatupa maelekezo na kunishauri vizuri. Ahsante sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naomba niende kwenye hoja kwa maslahi ya muda.
Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na hoja ya Mheshimiwa Kilumbe. Mheshimiwa Kilumbe amezungumzia kwamba asilimia 70 ya fedha zilizopo Tanzania ziko mikononi kwa watu na haziko katika mifumo rasmi ya kifedha zikiwemo benki na ametoa pendekezo kabisa kwamba kwa kuwa suala hili lipo basi Wizara ya Fedha ichukue majukumu au jukumu lake la kutoa elimu. Ninacho mhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba Wizara ya Fedha inatoa elimu siku hadi siku kupitia vyombo vya habari vyote nchini lakini hata kwa mtu mmoja mmoja. Nimuombe Mheshimiwa Mbunge na Waheshimiwa Wabunge wenzangu wote kuchukua fursa hii ya kutoa taaluma kwa wananchi wetu kuwahimiza na kuwashajiisha waweke fedha zao katika mikono salama ambazo ni benki zetu na mifumo rasmi ya kifedha au ya sekta ya fedha ambazo zipo. Huko kwenye benki zetu kuweka fedha ni salama zaidi kuliko kuziweka kwenye nyumba zetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia nijielekeze kwenye hoja ya ndugu yangu kaka yangu Mheshimiwa Hassan King. Hoja ya kwanza mahususi amesema kwamba watumishi wazee wetu ambao wamestaafu kwa bahati mbaya sana wanachelewa kupewa fedha yao ambayo ni haki yao ya msingi. Mimi nimhakikishie Mheshimiwa kwamba suala hili tumelichukua na tunaenda kulifanyia kazi. Lakini nimuombe tu ile hoja mahususi ya watu mahususi ambao amewataja pale naomba tukimaliza tu hii bajeti basi tuonane anikabidhi yale majina. Nimhakikishie kabisa, mimi niko na Mheshimiwa Waziri, tutayafanyia kazi haraka iwezekanavyo. Kwa sababu amenitisha kidogo ametumia msamiati mkubwa sana kwamba wazee hawa wanadhulumiwa. Na jambo ambalo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linamkosesha raha na kumnyima usingizi ni suala la…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa hii. Nianze kwa kuunga mkono hoja. Katika hayo yote, naomba kuwapongeza sana Waheshimiwa Wabunge ambao wamesimama kuchangia na wale ambao labda wanachangia kwa maandishi. Nawaahidi kwamba michango yao tumeichukua na tunaenda kuifanyia kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge kila mmoja ambaye amesimama hapa leo na jana walikuwa wanazungumzia na kutoa ushuhuda wa kazi nzuri ambayo inafanywa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mheshimiwa Rais amefanya mengi na kila mmoja ni shahidi kwamba utumishi wake ni ule utumishi uliotukuka. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu ya muda, nitazungumza na kutoa ufafanuzi katika maeneo machache ambayo Waheshimiwa Wabunge wenzangu wameyasemea kwa uchungu kabisa. Kila Mbunge aliyesimama alikuwa anaonekana anazungumza kwa uchungu kabisa hasa katika masuala ya barabara na miundombinu mingine kama vile madaraja. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Wabunge walio wengi wamezungumzia kuhusu fedha ya dharura ya TARURA. Ninachotaka kusema ni kwamba Serikali inaendelea kufanya tathmini juu ya uharibifu huo mkubwa ambao umetokea katika wilaya na halmashauri zetu wa barabara ikiwemo barabara na madaraja.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninataka kusema kwamba Serikali imechukua hatua kubwa sana kwa kuingiza au kutuma au kuweka shilingi bilioni 61.3 kwa upande wa TARURA na shilingi bilioni 74.9 kwa upande wa TANROADS. Fedha hii itaendelea kutolewa siku hadi siku mpaka tuhakikishe kwamba miundombinu hiyo imerudi katika uhalisia wake. Naomba niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge kwamba fedha hii itaenda kutolewa kwa wakati kabla ya mwaka huu wa fedha kumalizika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, Waheshimiwa Wabunge wamehitaji ufafanuzi kuhusu ununuzi wa kazi zilizotekelezwa na bajeti ya nyongeza ya shilingi bilioni 350. Suala hili Wizara ya Fedha tumekaa na wenzetu wa Ofisi ya Rais, TAMISEMI na tumekubaliana kwamba mchakato wa manunuzi uanze ndani ya robo hii ya mwaka. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mchakato wake wa utekelezaji wa suala hili la shilingi bilioni 350 utaanza robo ya kwanza ya mwaka 2024/2025, yaani nakusudia kusema kuanzia Julai. Kwa hiyo, nawahakikishia Waheshimiwa Wabunge kwamba fedha hii ipo na itaendelea kutolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miundombinu yetu ya barabara na madaraja kama ilivyopangwa na sekta inayohusika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge wote ambao wametoa hoja zao, Serikali imezipokea na tutaenda kuzifanyia kazi. Ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Fedha na Mipango
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii na mimi kuchangia katika hoja iliyopo mezani.
Mheshimiwa Spika, awali ya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu, Rahim, kwa kutuwezesha kujadili hapa katika hali ya uzima na afya, lakini pili nimshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuniamini kuendelea kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini tatu, naomba nikushukuru wewe Spika na nikupongeze sana kwa kazi nzuri ambayo unaifanya, na hili, wote ni mashahidi na tunaamini kwamba, kwa mujibu wa tafiti wanawake wanapopewa nafasi ama wanapokuwa na nafasi hawajawahi kushindwa, kwa hiyo, nawapongeza sana, lakini pili wanakuwa ni waaminifu sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini naomba nimpongeze na nimshukuru pia Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Makamu wake na Wajumbe wenzangu wote kwa namna walivyotupa ushirikiano mkubwa katika suala letu hili, lakini niwashukuru pia Wabunge wenzangu kwa ushirikiano wao wote na michango yenu yote ambayo mmeitoa. Ni michango yenye afya, yenye dhamira ya kujenga Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, namshukuru pia Waziri wangu, Waziri wa Fedha na Mipango, kaka yangu Mheshimiwa Dkt. Mwigulu, yeye kwangu huyu ni mentor yaani ni kocha mzuri ambaye anatupa maelekezo na tunaenda vizuri na kufanya kazi kwa pamoja. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, niwashukuru pia watendaji wenzangu wa Wizara ya Fedha na Mipango kwa kiasi kikubwa sana ambapo wanatupa ushirikiano katika kazi zetu za siku hadi siku wakiongozwa na Katibu Mkuu, Naibu Makatibu Wakuu, Makamishna na watendaji wote.
Mheshimiwa Spika, nijielekeze tu moja kwa moja katika mjadala ama hoja ambazo zimejadiliwa hapa leo na nianze na maoni ya Kamati; Kamati iliona kwamba tuna uhaba mkubwa wa wafanyakazi ama watumishi wa TRA.
Mheshimiwa Spika, hili nikiri ni kweli kwamba TRA watumishi wetu bado ni haba, lakini Serikali imechukua juhudi mbalimbali za kuongeza watumishi hao. Ndani ya mwaka huu Serikali imedhamiria kuajiri vijana 2,100 na tayari vijana 1,443 wamesharipoti kazi na wameshapatiwa mafunzo ya kiutendaji na 657 wamo katika mchakato wa kupatiwa ajira ndani ya mwaka huu wa fedha.
Mheshimiwa Spika, ipo hoja imezungumzwa kuhusu mali chakavu au vyuma chakavu. Baadhi ya watu wanaziita mali kachara. Ni kweli zipo na mchakato ule unaonekana ipo haja ya kufanyiwa mapitio. Hili tumelichukua na tutalifanyia mapitio ili kusudi mauzo ya mali kachara ama vyuma chakavu vile yaende kwa haraka sana katika mchakato wake.
Mheshimiwa Spika, lakini pia naomba nizungumzie suala la forodha ambalo amezungumza ama ametoa maoni Mheshimiwa Mbunda, jirani yangu pale kwamba ipo haja ya kufungua ama kuweka Ofisi za Forodha katika mipaka yetu.
Mheshimiwa Spika, hili tumelichukua na tayari limeanza kufanyiwa kazi na Serikali. Sasa hivi Serikali, iko timu maalum ambayo imeundwa inafanya tathmini ya sehemu kwa mfano kama vile Momba na sehemu nyingine kuona kwamba kama ipo haja ya kufungua Ofosi za Forodha latika mpaka fulani, basi Serikali haitasita na ipo tayari kutufua Ofisi za TRA katika mipaka yetu hiyo.
Mheshimiwa Spika, lakini pia nizungumzie suala la ukusanyaji wa mapato ambayo Mheshimiwa Tarimba kwa kiasi fulani amegusa kidogo kwamba ipo haja ya kutanua wigo nalo hilo pia limechukuliwa na Serikali na Serikali imefanya juhudi hizo hata kama alivyosema yeye mwenyewe vijana 360 wamechukuliwa kuwekwa kwa muda, siyo waajiriwa lakini wanasaidia ukusanyaji wa fedha na kutoa taaluma kwa wafanyabiashara wetu.
Mheshimiwa Spika, kwa hayo machache naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Kudhibiti Utakatishaji wa Fedha Haramu wa Mwaka 2022
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii ili niweke neno katika michango ya Muswada huu. Awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu Rahhim ambaye ametuwezesha kukutana hapa na kufanya mjadala huu tukiwa katika hali ya uzima na afya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, kwa dhati kabisa naomba kuishukuru sana Kamati ya Bajeti, sana kwa sababu, nimejifunza mengi. Vile vile nawashukuru sana Wabunge wenzangu kwa mijadala yao ya kujenga. Kila mmoja ambaye ametoa maoni yake yalikuwa ni maoni mazuri ambayo yanajenga katika maendeleo ya Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naomba nimshukuru sana Waziri wa Fedha na Mipango, kwa ushirikiano wake wa karibu sana nami katika utendaji na utumishi wa Serikali yetu. Namshukuru pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa michango yake na ushirikiano wake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba niende tu moja kwa moja sasa kwenye baadhi ya michango ambayo imetolewa na Wabunge. Baadhi ya Wabunge wamechangia suala zima la kutoa elimu kwa wadau kuhusu Muswada huu. Kwa kweli hili niliseme kwa niaba ya Waziri kwamba tunalichukua na tutajitahidi kutoa taaluma kwa wadau wote ambao wanahusika na tunaahidi kwamba elimu hii itafika mpaka chini kwa wananchi wote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, Mheshimiwa Kakunda ametoa maoni, amesema kwamba tuwe na kampeni maalum ya kuongeza uelewa kwa wananchi nalo hili pia tumelichukua. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaombe Waheshimiwa Wabunge wote tuwe Walimu wa kutoa taaluma kwa wananchi wetu juu ya sheria hii endapo itapitishwa, kwa sababu, madhara ya utakatishaji wa fedha haramu ni makubwa sana na ni hatari kabisa kwa maendeleo ya Taifa letu. Nawaomba sana Wabunge wenzangu, tuwe mstari wa mbele katika kutoa taaluma. Mwisho kabisa nawaomba Wabunge kupitisha Muswada huu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa fusa hii. Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu Rahim, mwingi wa rehema, mwenye kurehemu kwa kutuwezesha kuwepo katika Bunge hili na mijadala yetu tukiwa katika hali ya uzima na afya. Pili, nikushukuru wewe kwa kunipa fursa hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, niwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote waliochangia, wametoa ushauri mzuri, wametoa hoja njema za kujenga, lakini sitoweza kujibu moja baada ya nyingine, naomba uniruhusu niweze kutoa maelezo kwa hoja chache.
Mheshimiwa Naibu Spika, ipo hoja kwanza ambayo imetolewa na Ndugu yetu Mheshimiwa Kilumbe, katika hoja yake anashauri kwamba, wakandarasi na wazabuni Serikali iwalipe kwa wakati, tunalitambua hilo na Serikali inaendelea kulipa madeni ya wakandarasi na wazabuni siku hadi siku. Hivi ninavyoongea sasa hivi mpaka kufika leo tayari bilioni 882.5 zimeshalipwa kwa wakandarasi. Hivyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Wabunge wengine kwamba kadri fedha zitakavyopatikana, basi madeni hayo yatalipwa kwa wakandarasi wote.
Mheshimiwa Naibu Spika, hoja ya pili ilikuwa ni hoja ya Mheshimiwa Kilumbe, anasema kwamba PPRA waimarishe mfumo wa NeST. Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Wabunge wenzangu kwamba Mfumo wa NeST uko vizuri sana, ni mfumo wa kizalendo, ni mfumo ambao taarifa zetu ziko salama ikilinganishwa na mfumo uliokuwepo nyuma TANePS, kwamba taarifa zetu zilikuwa zipo nje ya mawanda yetu, leo kupitia NeST taarifa zetu zipo salama na bahati nzuri wanaosimamia mfumo ule ni wazalendo yaani ni wananchi wa Tanzania wenyewe, hakuna mtu mgeni ambaye anausimamia mfumo ule. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba mfumo huu utaendelea kutoa mafunzo mazuri kwa wazabuni wote nchini, hivi ninavyozungumza sasa wazabuni 2,170 tayari wameshapatiwa mafunzo na milango iko wazi. Katika hili nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tumpongeze sana Mheshimiwa Rais, kwa fedha nyingi ambayo ameiweka pale kwa ajili ya utekelezaji na ujenzi wa mfumo huu. Hapa Mkurugenzi Mkuu, Ndugu yetu Maswi apewe maua yake kwa usimamizi mzuri wa PPRA. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hoja nyingine imetolewa na Mheshimiwa Mariam Nyoka, kwamba fedha bilioni moja itolewe kwa ndugu zetu wenye ulemavu, fedha hii tayari imeshatolewa na imeshafika kunapohusika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hoja ya mwisho ambayo nitazungumza ni hoja ya Mheshimiwa Innocent Bilakwate, anasema kwamba Serikali iendelee kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kudai risiti wakati wa manunuzi. Kwa kweli suala hili ni changamoto, naomba niwaombe Wabunge wenzangu na wananchi wote, tuwe na utamaduni wa kudai risiti tunaponunua na wale wafanyabiashara wawe na utamaduni wa kutoa risiti, yaani iwe kama ni utamaduni wetu kama vile mtu akiamka asubuhi anatafuta maji kuosha uso ama kuoga basi akifanya manunuzi lazima atoe risiti na mteja adai risiti.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunayo kaulimbiu inayosema tuwajibike. Ni lazima tuwajibike, suala la ukusanyaji wa kodi lisiwe ni suala la Serikali na TRA peke yake, suala hili liwe ni wajibu na jukumu la kila mtu hapa nchini kwa sababu maendeleo yetu yanahitaji makusanyo yetu ya fedha. Leo kila Mbunge tunatoa hoja kwamba barabara yangu imefanya hivi, barabara yangu imebomoka zinahitajika fedha, kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge tuwajibike.
Mheshimiwa Naibu Spika, hapa tumetengeneza kwamba mteja wajibu wake ni kudai risiti halisi na thamani ya kile alichokinunua, lakini mfanyabiashara wajibu wake ni kutoa risiti, tena risiti halisi na thamani ya kile ambacho amekiuza. Nini wajibu wa TRA? TRA wajibu wake ni kukusanya kodi kwa ufanisi, kwa uhalisia bila kutumia nguvu na fedha hiyo kuirudisha Serikalini na wajibu wa Serikali unaonekana ni kupeleka maendeleo kila sehemu, kujenga miradi ya maendeleo na mwenye macho haambiwi tazama. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kila jimbo, kila wilaya inaonekana miradi ya maendeleo iliyofanyika kama siyo afya, basi miradi ya elimu kama siyo elimu basi miradi ya barabara. Niwaombe Waheshimiwa Wabunge, kwa yale ambayo hatujayajibu, basi tunayachukua na tutajibu kwa maandishi na tunaenda kuyafanyia kazi. Ahsante sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali za Fedha wa Mwaka 2022
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Awali ya yote naomba nimshukuru Mwenyezi Mungu Rahimu ambaye ametuwezesha kuwepo hapa tangu asubuhi hadi sasa tukiwa katika hali ya uzima na afya pamoja na amani.
Mheshimiwa Spika, pili naomba nikushukuru sana kwa kunipa fursa hii nami kuwa sehemu ya wachangiaji katika hoja hii iliyoko mezani.
Mheshimiwa Spika, nimshukuru pia Waziri wangu, Waziri wa Fedha na Mipango kwa namna anavyonisaidia na kunielekeza. Lakini pili nimshukuru Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti pamoja na makamu wake na wajumbe wote wa kamati husika nawashukuru sana kwa ushirikiano, maoni na maelekezo yao. Kwa ujumla niwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote kwa usharikiano wao wanaotuonesha ndani ya Bunge hili Tukufu.
Mheshimiwa Spika, mimi niende tu moja kwa moja katika mambo mawili ambayo kwa ujumla ni maoni ambayo yametolewa na Waheshimiwa Wabunge. Maoni haya yote yapo kwa lengo la kujenga Taifa letu na kwa maslahi ya Serikali yetu na wananchi kwa ujumla.
Mheshimiwa Spika, maoni ambayo yametolewa na Kamati pamoja na wachingiaji moja ni usimamizi na ufuatiliaji wa matumizi ya Serikali. Hili niseme kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango tumelipokea na tutalifanyia kazi kwa maslahi ya wananchi wetu.
Mheshimiwa Spika, jambo la pili ni kufanya tathmini ya kina katika misamaha yote ambayo inatolewa na Serikali kwa miradi mahiri. Nalo hili tunalichukua na tunaahidi kwamba Serikali italifanyia kazi kwa nguvu zake zote.
Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii. (Makofi)
Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2023 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa fursa hii. Awali ya yote na mimi naungana na wenzangu, namshukuru Mwenyezi Mungu, Rahim, ambaye ametuwezesha kukutana hapa katika kikao hiki na hatimaye kuhitimisha Bajeti hii Kuu ya Serikali.
Mheshimiwa Spika, jambo la pili, naomba kumshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye ni mbeba maono ya Watanzania. Mheshimiwa Rais kwa uwezo wake mkubwa sana, ubingwa na ukinara wa kutafsiri sera kutoka kwenye makaratasi na kuwa kwa vitendo. Mara kadhaa tumekuwa na ndoto, sisi Watanzania, ya kuwa na miradi mikubwa kama SGR na mengineyo, lakini tumekuwa na ndoto ya kupeleka wanafunzi kwa mkupuo mmoja tu, siyo kwa awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu, hilo limekamilika. Hii ni kwa sababu ya uwezo mkubwa sana wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kutafsiri sera kwa vitendo, lakini nimezoea kusema kwamba, sifa moja ya Mama aliyokuwanayo ni uwezo mkubwa sana wa kutafsiri chozi la watoto wetu au watoto wenu kwa vitendo kabisa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ni watu wachache sana, sisi wakina baba sawa lakini uwezo huu mkubwa sana mnao ninyi wakina mama, mnajua kwamba sasa hivi kilio hiki mtoto anahitaji nini? Mnajua mtoto kilio hiki nini kinamsumbua. Kwa hiyo, tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, pili, naomba nikushukuru sana wewe kwa malezi yako. Wewe umekuwa mlezi mzuri kwetu na ninavyokuambia hivi sasa hivi Wana-Kojani wanaku-miss sana. Siku umewatembelea wanatamani mara nyingine itokee utembelee Kojani kule. Wewe ni mlezi mzuri na tunashukuru kwa malezi yako. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, pia, niwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge, kwa kweli michango yenu ni mizuri sana na ushauri wenu ni mkubwa na tumeupokea kwa mikono miwili. Hii ni kwa sababu huko nyuma wapo walionena aah! Kwamba Bunge hili la siku hizi lakini hili Bunge la Kumi na Mbili ndiyo ambalo limetoa Rais wa Mabara yote ulimwenguni. Rais wa ulimwengu ametoka ndani ya Bunge la Kumi na Mbili. Kwa hiyo, tuna kila sababu ya kujivuna Waheshimiwa Wabunge. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naomba nimpongeze na kumshukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha, kaka yangu Mheshimiwa Dkt. Mwigulu, yeye ni mentor kwangu na ni mwalimu mzuri kwangu. Kwa hiyo, nasema kwamba huyu ni bingwa na ni miongoni mwa Mawaziri bingwa ambao wanatufunza na kutuelekeza vizuri. Mheshimiwa Waziri nikuambie tu mengine ambayo yanatokea katika jamii, ndiyo ulimwengu na ndiyo maisha. Maana yake hata washairi wameandika na wanasema kwamba;
“Wamaani nakupa neno siwate,
Ya waneni sikiapo sitete,
Duniani mtu hapendwi na wote.” (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naomba niendelee pia kwa kuwashukuru sana Katibu Mkuu na Watendaji wote wa Wizara ya Fedha, pamoja na Wizara zote za Serikali kwa kweli wanatusaidia vizuri na wanaisaidia Serikali yao kwa juhudi kubwa sana na uzalendo mkubwa sana. Kutokana na muda lakini pia nisisahau kumshukuru care taker wangu hapa Mheshimiwa Profesa Mkumbo, yeye alikuwa anafundisha vyuoni lakini hata hapa sisi wengine tunajifunza kutoka kwake. Tunakushukuru sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nimshukuru Mheshimiwa Rais, pia kwa kutuongezea company hapa na wewe kuturuhusu kuwa na company. Mwaka jana na mwaka juzi tulikuwa wawili tu hapa lakini leo tuna company hapa unaona naongea kidogo. Tunakushukuru sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naomba hasa nijielekeze moja kwa moja kwa hoja chache ambazo nimechagua kuzielezea kwa sababu hoja ni nyingi lakini nyingi zilikuwa ni ushauri na nilithibitishie Bunge lako Tukufu kwamba hoja ambazo wametoa, ushauri ambao wametoa tumeuzingatia na tumeubeba kwa meno ya magego kabisa na tunaenda kuufanyia kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, upo ushauri Kamati ya Bajeti wameshauri kwamba Serikali ihakikishe mikopo ambayo inakopwa na Serikali inaelekezwa katika sekta za uzalishaji pamoja na miundombinu. Niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge kwamba mikopo yote ambayo imekopwa na Serikali imekuwa ikielekezwa kwenye miradi ya maendeleo hususani kwenye miundombinu ya barabara, maji, reli na umeme, kwa kuzingatia Dira ya Maendeleo ya 2025. Kwa hiyo, niwahakikishie kwamba mikopo yote ambayo itaendelea kukopwa na Serikali itaelekezwa kwenye sekta za uzalishaji ama miundombinu mbalimbali ya barabara. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Serikali ilishauriwa kulipa madeni ya wazabuni wa dawa, kwa kipindi cha Julai, 2023 hadi Mei, 2024 Serikali imeshalipa jumla ya shilingi bilioni 256 kwa ajili ya kulipa madai ya wazabuni waliosambaza dawa na vifaa tiba. Aidha, mwaka ujao wa fedha Serikali imetenga shilingi bilioni 200 kwa ajili ya kulipa wazabuni ambao wamesambaza dawa na vifaa tiba.
Mheshimiwa Spika, nimeona hapo imeshaanza kuwaka lakini naomba nimalizie hili. Niwahakikishie tu Waheshimiwa Wabunge kwamba ule ushauri ambao umetoka na Wabunge basi ushauri huo umechukuliwa na Serikali. Mwisho kabisa, yupo mchangiaji mmoja Mheshimiwa Mbunge alisema kwamba kikokotoo hiki ambacho mmeongeza asilimia saba hadi kufika 40% mmefanya jambo lakini isionekane kwamba mmefanya jambo kubwa.
Mheshimiwa Spika, mimi nikuambie nyongeza hii ya asilimia saba ni kitu kikubwa sana kutoka 33% hadi 40% ni kikubwa sana. Hata ingekuwa asilimia moja tu basi ingekuwa ni hatua kubwa sana, kwa sababu wahenga wanasema; “Jicho hutaraji haja kila namna na penye moja na moja si moja tena.” Kwa hiyo, hata ingekuwa moja tu ingekuwa inatosha. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naomba nimalizie kwa kusema kwamba wafanyakazi walio wengi wameshukuru sana na Waheshimiwa Wabunge wapo ambao wametoa shukurani kuhusu jambo hili na ndiyo ulimwengu. Nimalizie kwa kusema kwamba wahenga wanasema; “Asiyeshukuru kwa yai basi na jogoo hachinjiwi.” Ahsante. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia Baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Mwaka 2023
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa fursa hii uliyonipa ili kuwa sehemu ya wachangiaji katika Muswada huu. Naomba awali ya yote kumshukuru Mwenyezi Mungu Rahim muumba wa mbingu na ardhi kwa kutujalia kuwepo hapa katika kujadili masuala ya maendeleo ya nchi yetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia niwapongeze sana Kamati ya bajeti, Kamati ambayo muda wote inafanya kazi kwa umakini mkubwa na uadilifu mkubwa. Naomba nimpongeze pia Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango kwa namna anavyonielekeza na kunishauri katika utendaji wa kazi zetu za kila siku. Pia naomba kumpongeza Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa namna alivyoshiriki na kutusaidia katika kupitisha Muswada huu.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hayo yote, naomba niende tu kwenye michango ambayo wametoa Waheshimiwa Wabunge na maendekezo yao. Kwanza Serikali imepokea michango na maoni ambayo yametolewa na Kamati na Wabunge wote, kwani Wabunge wamechangia kwa uzuri kabisa na kwa ufanisi mkubwa sana. Serikali tayari imepokea mapendekezo ya Kamati ambayo tayari hadi sasa imeshaanza kufanya utekelezaji wa kutoa Waraka Na.7 wa Hazina wa mwaka 2021 kwa Maafisa Masuuli kuhusu utekelezaji wa miradi kwa utaratibu wa PPP kwa kuhakikisha kwamba wanatenga fedha mahususi katika bajeti zao kwa ajili ya kutekeleza miradi hii ya PPP.
Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, miongoni mwa mapendekezo ya Kamati ni kutoa taaluma kwa umma. Niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge wenzangu kwamba, taaluma hii inaendelea kutolewa na Serikali siku hadi siku kwa njia zote zinazojulikana katika kutoa taaluma. Kupitia kwako niwaombe Wabunge wenzangu na wao wawe sehemu ya kutoa taaluma kwani Wabunge walio wengi au Wabunge wote wana weledi mzuri na uelewa mzuri kuhusu umuhimu wa PPP.
Mheshimiwa Naibu Spika, niwaombe kwa fursa hii wote tuchukue nafasi hii kutoa taaluma.
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)
The Finance Bill, 2022
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimia Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii nami nichangie. Awali ya yote, naomba nimshukuru Mwenyezi Mungu Rahim ambaye ametujaalia rasilimali ya uhai hadi sasa, ambayo ndiyo thamani ya ubinadamu. Maana yake ikiondoka rasilimali ya uhai, basi thamani ya ubinadamu nayo imeondoka. Ushahidi wa hilo ni kwamba mtu huyo huchukuliwa na kupelekwa mbali kabisa na siyo katika makazi ya wanadamu wa kawaida.
Mheshimia Spika, kipekee naomba nimshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kiasi kikubwa anavyosikiliza kilio na machozi ya wananchi wake ambao ni watoto wake. Ushahidi wa hili nilisema juzi hapo kwamba mama ana upeo mkubwa sana wa kutafsiri chozi la watoto wake kwa vitendo. Nadhani Wabunge wenzangu wote ni mashahidi juu ya hilo. (Makofi)
Mheshimia Spika, kipekee naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwako kwa kiasi unavyoendesha vizuri na kwa ufanisi majadiliano ya Muswada huu na mengine ambayo yalipita.
Mheshimia Spika, napenda pia kumshukuru Waziri wetu wa Fedha na Mipango, kwa kiasi kikubwa anavyotoa maelekezo kwangu na kufanya kazi kwa ufanisi kwa pamoja. Mashirikiano yake nimeyakubali sana. (Makofi)
Mheshimia Spika, vile vile nawashukuru sana Kamati yako ya Bajeti, iko vizuri na inafanya kazi kwa ufanisi wakati wote. Saa 24 wako tayari kushirikiana nasi, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Sillo na Makamu wake Mheshimiwa Kigua, na Wajumbe wenzangu wote. Pia nawashukuru Wabunge wenzangu, tangu jana tulipoanza mjadala huu, mijadala yao ni ya kujenga tu. Kwa hiyo, niwahakikishie kwamba ushauri wao, mawazo yao, mapendekezo yao, Serikali imeyachukua na itayafanyia kazi kwa ufanisi mkubwa.
Mheshimia Spika, nitazungumza tu kwa ujumla hoja chache. Hoja ya kwanza Waheshimiwa Wabunge wametoa hoja ama wamependekeza Serikali iendelee kutoa elimu juu ya umuhimu wa Bima ikiwa ni pamoja na kuanza kukata Bima kwenye mali zake kama vile magari. Ushauri huu umechukuliwa na tumeuzingatia na tutaufanyia kazi na tutatoa elimu kwa taasisi zote za Serikali, magari yao yote yawe na Bima pamoja wao wenyewe. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, hoja ya pili ambayo imetolewa ni kwamba Serikali ifanye tathmini ya kina ya upungufu na mafanikio yaliyopatikana kutokana na utolewaji wa mikopo husika. Aidha, upungufu utakaobainika ufanyiwe marekebisho. Serikali imelichukua na itafanya tathmini ya kina sana hatua kwa hatua. Tunaelekeza Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani kufanyia kazi suala hili, tathmini hiyo na ripoti yake ipatikane haraka iwezekanavyo. (Makofi)
Mheshimia Spika, kwa hayo, naomba kuwasilisha. (Makofi)